Kashfa ya Ufisadi Bandari ya Dar

Kule kwenye FORUM yako umeanzisha thread unasema Dr DAU apelekwe Bandari kwa kudai hivi:

SOURCE HAPA:
Dr. Dau kupelekwa Bandari kuiokoa? - Page 2 - MwanaKijiji.COM


mwanakijiji huu ni UNAFIKI wa highest order!
wewe huyo huyo miezi michache iliyopita ulikuwa na kampeni Dr DAU afukuzwe na hafai all along leo ghafla Dr Dau anafaa? au ndio njama Dr Dau asikamilishe malengo ya NSSF ya kumaliza University Dodoma ambako watoto wa walalahoi wanasoma na Daraja la Kigamboni kuwakomboa wasio na pesa za kuishi Detroit kama wewe mwanakijiji? Kinachowaudhi hasa ni nini? hutaki NSSF chini ya Dau iache landmark ya miaka ijayo? maana inavyoelekea hilo ndilo msilolitaka.Wapo watanzania wengi tuuu AMBAO WANGEWEZA KWENDA BANDARI na wakaisort out . Jamani DR DAU SI MWARUBAINI!


Nadhani tatizo lako unakaa sana nje na kupiga makelele bila kujua hali halisi ilivyo on the ground hivi ushaona wanachokifanya NSSF kule Dodoma au ushaona walivyo wafanya polisi pale Keko?

Kila mtu anajua matatizo ya Bandari kwa kiasi kikubwa yanatokana na TRA mbona husemi Dr Dau apelekwe TRA akakusort out au basi tuu?

Lakini Game kwani hayo ni maneno ya Mwanakijiji au ni maneno ya mnukuliwa (chanzo)? Au sijaelewa vizuri hiyo nukuu uliyoiwekea rangi nyekundu?
 
Akheri mimi nakesha nyumbani kuliko wewe unayekesha kufunga vidonda vya walevi....ndio umetoka shift yako nini?

Nyani Ngabu;

Hakika mnasikitisha sana, watu wazima kama ninyi kukashifiana hapa jamvini si vema, sisi wenzenu tunataka kujua kinachoendelea pale bandarini ninyi mnaleta mzaha, be carefull na yale mnayoyabandika hapa,

Nyani Ngabu; siku zote huwa naona kama michango yako imekwenda shule sasa pale unapoanza kutoa lugha chafu, mnaifanya forum hii ionekane kama likijiwe la wahuni furani.
 
Nyani Ngabu;

Hakika mnasikitisha sana, watu wazima kama ninyi kukashifiana hapa jamvini si vema, sisi wenzenu tunataka kujua kinachoendelea pale bandarini ninyi mnaleta mzaha, be carefull na yale mnayoyabandika hapa,

Nyani Ngabu; siku zote huwa naona kama michango yako imekwenda shule sasa pale unapoanza kutoa lugha chafu, mnaifanya forum hii ionekane kama likijiwe la wahuni furani.

Niwie radhi ndugu IsayaMwita.
 
Makontena kujaa pale bandarini ni ulaji wa hali ya juu wakuu wanajua na CCM wanapata mgao. Makontena yanayojaza yard ya bandari mengi ni yale ya transit ambayo huwezi kwenda kuyaweka kwenye yard ya nje ya bandari( amabayo hayakustahili kushushwa pale). Ila kwa kuwa haka kamchezo kanachezwa na wenye kampuni za meli, TICS na CCM ndo maana kameota mizizi. Dar Port sio transit port!!
Kwa kuwa kuna mizigo mingi ya ya kwenda ulaya, hasa madini toka DRC na Kahawa ya Burundi, meli zenye makontena ambayo yanakenda port zaidi ya Dar wanapunguza gharama kwa kuyashusha hapo Bandarini ili yaje yapakiwe na meli zingine yafikishwe kule yanakokwenda, then wao wanapakia mzigo ya kutoka DRC, Burundi na baadhi yetu sisi, kama Pamba, mbao, magogo nk. hivyo wanatengeneza kaela ka kueleweka kwa kuwa wanarudi na mzigo. Sasa hayo makontena kwa kuwa yanakuwa yanasubiri meli za kuyafikisha kule yanakokwenda, hayawezi kuondolewa pale yard Bandarini mpaka pale yatakapopata meli. Wakati huohuo wenye kampuni za meli wanakuwa wako tayari kulipa charge za kuyaweka pale hayo makontena na hii pesa wanayokula bila wasiawasi kwa kuwa haiko ndani ya mkataba.
Sasa meli zinazokuja zinakosa nafasi kwa kuwa kunakuwa hakuna mahali pa kuyapakulia, kwa lugha ingine yard inakuwa imejaa makontena ya transit.
 
Lawama inabidi pia ziende serikalini, kwa sababu hao waliotajwa hapo juu, mbali na udhaifu wao lakini pia nafikiri hawana hela za kununua cranes, hawana uwezo wa kujenga magati mengine, hawana uwezo wa kufuta mkataba wa TICTS, maamuzi mengi sana yamelazimishwa tu kutoka wizarani kwa manufaa binafsi ya mawaziri na watendaji wao, akina Mgawe mimi sometimes naona wanabeba lawama kwa sababu tu ni uso wa shirika, ni sawasawa na kumfokea fundi wa umeme wa TANESCO kwa umeme kukatika katika. Tutakuwa tunapeleka hasira zetu sehemu isiyostahili.
 
Lakini Game kwani hayo ni maneno ya Mwanakijiji au ni maneno ya mnukuliwa (chanzo)? Au sijaelewa vizuri hiyo nukuu uliyoiwekea rangi nyekundu?

NN - mimi hayo matatizo ya bandari sikuyajua kabla ya wiki mbili zilizopita. Sikuhitaji kwenda bandari ya Dar kujua matatizo hayo.

Hadi hivi sasa vyanzo vya ndani kabisa vinasema Dr. Dau ni front runner wa kwenda Bandari.
 
MKJJ .......Dr. Dau anakitaka hicho cheo au watu wanampendekeza...? !!!

Mwanakijj viulizwe vyanzo vyako kuwa kwani hakuna MTz mwingine anaeweza pewa nafasi hio akaimudu?...ktk List ya Viongozi wanaofaa ulionao hakuna anae wafaa ktk nafasi hio?

Ninaochohofia wana JF tunapoelekea ni kuwa wapambe wa baadhi ya Viongozi either kwa kujua au kutokujua.
 
Kati ya watanzania milioni 40 yaani Dau peke yake ndiye anayeweza kutatua THA?

acheni uhuni hapa.

mbona mnapenda kuleta issues zisizo husiana? why not anza na BODI NZIMA ya THA?


Halafu mbona chama kikuu cha upinzani kama CHADEMA na DR SLAA,ZITTO et al wako kimya kuhusu huu ufisadi au kwa sababu hii haiwapi sifa wanazozitaka?
 
al muhimu ni kuwa nilituma Kontena mwezi wa 11 toka Hanoi mwishoni mwa mwezi wa 11 na kilichotokea ni kuwa mpaka leo naambiwa bado meli haijapewa nafasi ya kuingia...to be fair wanaotuma magari dogo wao meli zao zinapata nafasi hivyo kama kuchelewa ni miezi miwili

Hivi unaweza kuamini kuna watu waliagizia miti ya krismass na mpaka leo kontena zao haizija teremshwa? Kisa Bandari imejaa


Unajua LUHIGO japo alikuwa ni mshenzi mshenzi na mla rushwa enzi zake lakini JAMAA KAZI ALIKUWA NAFANYA....i am not gonna knock him him down

sasa kwa taarifa yako niliagiza 40ft container nyingine wakati huo huo lakini ilikuwa inatokea Ghuanzhou na ilichukua only 1 month na niliteremshia Mombasa ambako it only took 24 hrs contena likawa lishapita kule border HORO HORO...sipendi ku confess lakini kwanza nililipa less,pili sikusumbuliwa na TRA kama ambavyo ningesumbuliwa Dar na mzigo ushakwisha


Inaniumz akuwa serikali imekosa pesa nyingi toka kwangu kwa sababu ya uzembe wa hao niliowataja kwa sababu wanaogopa kuwaambia TICS kuwa wamebreach contract yao na kazi wameshindwa WHY ? kwasababu zaidi wanamwogopa ROSTAM na kampuni yake...jambo ambalo Jakaya hana kinyongo in the wake of huu ufisadi left and right


Suggestion yangu ni kuwa mindhali KIMEI wa CRDB au jule bosi wa TRA wanafanya kazi nzuri tuuu kwa nini JK asimuapoint mmojawao kwenda kuisort out THA? maana Mgawe na GENGE lake la MAFISANI naona wameshindwa kazi na evidence wee pila SALENDA bridge utaona meli zilivyo jazana kule baharini
GT huo ndo uwezo wa muungwana katika kupanga safu ya wasaidizi wake. kwa kweli hyu dk kawambwa simwelewi kabisaaaaaaa. jk anambeba kwa kuwa sijui ni ndugu au ndo mtandao ila jamaa umanager HAWEZI. halafu amempatia wizara muhimu na yenye masilahi makubwa kwa taifa kama reli, bandari, ndege, barabara nk.

nasikia magufuli mkulu alikuwa anamwonea donge sanaa wakati wa ben alivyokuwa anapawezea na kumwagiwa sifa na boss wake. adhabu alompa nikumpeleka kwenye VITOWEO ambako gafla jamaa amepatia kuna uhai kwa sasa.

jamani mapato ya bandari tuuu kwa faida tuliyo nayo kijiografia kazi ikafanyika kwa asilimia 75 yaani ufanisi itachangia ya 50 pasent ya pato la taifa. dar, tanga na mtwara zikifanya kazi kwa ufanisi huo.

huyu kawambwa ataweka uswahili hapooooooooooooo na mambo yatakuwa hivyoooooo basi twaendeleaaa kuumia.

ni dk wa namna gani hata decision level yake inakuwa chini namna hiyoooooooooooooooooooo. huenda nisisomee phd kama ndo hivyoooooooooo
 
Labda Dau anapendekezwa kwa sababu aliishafanya kazi THA miaka ya nyuma. Raphael Mollel anahusika vipi na hii ishu?
 
Nadhani bosI wa TRA angefaa zaidi kule THA na JK is seriuosly considering kumbadilisha on a flipside ni kweli Mataka naye anaitaka sana hiyo post
 
GT, unafikiri Dr. Dau hawezi kuimudu na kuirudisha katika nidhamu Bandari?


kwani tatizo la bandari ni nidhamu ya Meneja na bodi au?


pili Dau unayemzungumzia ni yupi,yule yule aliyekuwa ukisema kashindwa kazi NSSF? sasa kama alishafeli NSSF (kutokana na maelezo yako siku za nyuma)iweje apelekwe Bandari ambako tayari alishapita?

Pili kwa sababu tatizo la bandari kwa ukubwa linatokana na TRA huoni kama kuna mabadiliko ya kufanya basi yafanywe TRA?
 
CHADEMA mbona wamekuwa kimya sana kwenye hili sakata la bandari au hili halina political capital?
 
CHADEMA mbona wamekuwa kimya sana kwenye hili sakata la bandari au hili halina political capital?
Kuna TLP,CUF,NCCR Mageuzi etc,etc...Why just CHADEMA!!?May be wakawa hawana facts za kutosha kuhusu hili suala,je ungependa wajitwishe hivyohivyo??
 
Kuna TLP,CUF,NCCR Mageuzi etc,etc...Why just CHADEMA!!?May be wakawa hawana facts za kutosha kuhusu hili suala,je ungependa wajitwishe hivyohivyo??

CHADEMA kwa sabau ndicho cham pekee amabo kina credibility na uwezao wa kuongelea mambo yenye maslahi ya taifa...surely huwezi kukilinganisha na CUF,NCCR,TLP na wengineo

Hilo la kutokuwa na facts zishani kama linanguvu kwa sababu wanaye shadow minister wa hiyo wizara ya SHUKURU KAWAMBWA na hili suala la bandari ya Dar kuwa na huduma hafifu halikuanza kuongelewa leo wala jana na sidhani kama kila kitu lazima akiseme Dr Slaa

Unless CHADEMA hili hawana interest nalo na kama ikiwa wao hawaoni umuhimu nalo then tumekwisha maana sidhani kama Lipumba na maalim Sefu wana nia ya kuzungumzia mambo kama haya zaidi ya kutaka wapewe ruzuku wagombee tena urais mwakani
 
kwani tatizo la bandari ni nidhamu ya Meneja na bodi au?


pili Dau unayemzungumzia ni yupi,yule yule aliyekuwa ukisema kashindwa kazi NSSF? sasa kama alishafeli NSSF (kutokana na maelezo yako siku za nyuma)iweje apelekwe Bandari ambako tayari alishapita?

Pili kwa sababu tatizo la bandari kwa ukubwa linatokana na TRA huoni kama kuna mabadiliko ya kufanya basi yafanywe TRA?

Katika suala la NSSF na vifo Tabora ulitetea uwezo mkubwa wa Dr. Dau kiutendaji. Nakupa wewe benefit of the doubt kwa sababu hata Rais inaonekana anaamini hivyo. Sasa kwa kadiri unavyomjua na kutokana na ukweli kwamba alishakuwa Bandari, unafikiri ni mtu ambaye anaweza kuleta uongozi unaohitajika sana (hii ni pamoja na kupata bodi mpya of course)?

Kama huoni yeye ana uwezo wa kuinua Bandari na kuwa ni bora aendelee kubakia NSSF unafikiri ni nani mwingine ambaye unaweza kumpendekeza kushika nafasi hiyo hasa kutokana na matatizo ya Bandari uliyoyaonesha? Ungempendekeza nani?
 
Back
Top Bottom