Kashfa ya Richmond: The FACTS

Haya yote yakiendelea, hali ya umeme inazidi kuwa mbaya. Soma hii habari ya Nipashe:

Mgao wa umeme hadi saa 4 usiku

2006-11-19 09:12:07
Na Joseph Mwendapole


Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limetangaza hali mbaya ya umeme nchini na kwamba kuanzia kesho wateja watakuwa wanakatiwa umeme kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 4:00 usiku.

Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Bw. Daniel Mshana, alisema Shirika limelazimika kufanya hivyo kutokana na hali ya uzalishaji umeme kuzidi kushuka.

"Tofauti na siku zilizopita ambapo shirika lilikuwa na uwezo kidogo wa kukidhi mahitaji hayo ya wateja yanapoongezeka usiku, hivi sasa uwezo huo haupo tena kutokana na uzalishaji kuzidi kushuka, '' alisema Bw. Mshana.

Alisema ratiba hiyo mpya itawahusu wateja wote wa majumbani na viwandani na kwamba wateja wachache nyeti, zikiwemo hospitali za mikoa, viwanja vikubwa vya ndege, vituo vya jeshi na Ikulu, havitakuwa kwenye mgao huo.

Alisema Shirika hilo linashindwa kukidhi mahitaji ya matumizi ya umeme kutokana na maji ya kuzalisha umeme kwenye mabwawa makuu ya vituo vya nguvu za maji kupungua kwa kiasi kikubwa.

Alisema TANESCO imefikia hatua hiyo kwa sababu mitambo mingi ya dharura ya kukodi, haijaanza kuzalisha umeme kama ilivyotarajiwa.

Bw. Mshana alisema wateja wote walioko kwenye mikoa iliyounganishwa na Gridi ya Taifa imewekwa kwenye makundi matatu na kwamba kila kundi litakuwa likipata umeme baada ya siku tatu.

"Makundi haya yatakatiwa umeme kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 4:00 usiku, mbali na mgao unaofanyika mchana.

Kwa hiyo umeme utakatwa kwa kila kundi, kila baada ya siku tatu," alisema.

Alisema kwa kuwa mahitaji ya wateja wa umeme yamekuwa yakiongezeka hususan wakati wa usiku kati ya saa 12 na saa nne usiku, imekuwa vigumu kutosheleza mahitaji ya wakati huu.

Alisema mitambo ya kwanza ya dharura ya kukodisha ni ile iliyowekwa na kampuni ya Aggreko ya Uarabuni ambayo tayari inatoa megawat 40 za umeme, unaoingia kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa.

Bw. Mshana alisema mitambo ya pili ya kukodi ya kampuni ya Richmond Development ya Marekani ambayo ina uwezo wa kuzalisha Megawat 100 za umeme haijawasili yote isipokuwa yenye uwezo wa kuzalisha megawat 22 tu.

Hata hivyo alisema hiyo iliyowasili haijaanza kuzalisha umeme na huenda ikaanza kabla ya mwezi Desemba mwaka huu.

Alisema mitambo iliyobaki ya megawat 80 itafungwa na kuanza kazi kabla ya mwisho wa mwezi wa kwanza mwakani.

Kwa mujibu wa Bw. Mshana, mitambio mingine italetwa na kampuni ya Alstom Power Rentals ya Marekani itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawat 40.

Alisema mitambo hiyo inatarajiwa kufungwa mkoani Mwanza na kuanza kazi kabla ya mwisho wa mwaka huu na kwamba mitambo ya awali ya megawat 20 inatarajiwa kuanza uzalishaji kabla ya Desemba mwaka huu.

Bw. Mshana alisema mitambo ya nne itakayojengwa na kampuni ya Wartsila ya Finland na baadae kumilikiwa na TANESCO, itakuwa na uwezo wa kuzalisha megawat 100 na itaanza kazi kabla ya mwezi Agosti mwakani.

SOURCE: Nipashe
 
quarz: hoja zako ni nzito. Lakini unategemea nini kama vijana waote mliosoma vizuri ama mnaogopa kuingia katika siasa au mnaona mlango pekee wa kuingia katika siasa ni CCM? Hii inaniumiza sana kichwa. Wewe niambie leo hii vichwa kama Mwanakijiji, Mkandara, quarz, Augustino Moshi, Kichuguu, Sam, Mzee ES n.k. vingeingia katika chama kimoja cha upinzani hasa CHADEMA, siasa zetu zingebadilika mno na tugeweza kupata mwanga katika mambo mengi yanayotusumbua. Otherwise, tutaendelea kulialia tu na wafanya maamuzi wataendelea kuwa walewale akina Nungwi. Juzi nilikutana na dada moja kutoka Ghana katika mkutano fulani London, yule dada anamjua sana JK akaniambia alishangaa aliposikia amekuwa rais. yeye anasema kama JK ameweza kuwa Rais anaamini anybody in TZ anaweza akawa president! It was really embarassing to me!
 
mwanasiasa said:
quarz: hoja zako ni nzito. Lakini unategemea nini kama vijana waote mliosoma vizuri ama mnaogopa kuingia katika siasa au mnaona mlango pekee wa kuingia katika siasa ni CCM? Hii inaniumiza sana kichwa. Wewe niambie leo hii vichwa kama Mwanakijiji, Mkandara, quarz, Augustino Moshi, Kichuguu, Sam, Mzee ES n.k. vingeingia katika chama kimoja cha upinzani hasa CHADEMA, siasa zetu zingebadilika mno na tugeweza kupata mwanga katika mambo mengi yanayotusumbua. Otherwise, tutaendelea kulialia tu na wafanya maamuzi wataendelea kuwa walewale akina Nungwi. Juzi nilikutana na dada moja kutoka Ghana katika mkutano fulani London, yule dada anamjua sana JK akaniambia alishangaa aliposikia amekuwa rais. yeye anasema kama JK ameweza kuwa Rais anaamini anybody in TZ anaweza akawa president! It was really embarassing to me!





Mwanasiasa

unajua kusema kwingi hakumfanyi mtu kuwa mwanasiasa bora na sielewi strategy yenu ya kuchagua future leaders ikoje labda ungefafanua kidogo hilo

Kuhusu huyo dada wa GHANA wewe ulikuwa huna haja ya kuwa embarassed na ungemjibu kuwa wao Ghana mbona waloimchagua MSCOTTISH awe rais wao (Jerry Rawlings),pili huyo Kuffor wa sasa hivi sio msafi kama ambavyo wanataka watu wajue kwa sababu serikali yake inanuka kwa kuliko hata serikali ya Nigeria na mfano mzuri ni mtoto wake mwenyewe huyo Kuffor kujenga hoteli katika mazingira ya utatatanishi

Na huyo mtoto wake aliopo hapa London naye si safi kama hivyo wanavyotaka kumfanya unajua kwanini PRICEWATERHOUSE COOPERS hawataki kumwachia?

hao waGhana watuachie huyo Kikwete wetu na hata kama ananuka ni bado wetu
 
HAYA WAZEE HII HOJA NI MOTOMOTO,HALI NDIO KAMA HIYO NYUMBANI,,,MAISHA BORA TUNAYAONA ,TUMWAGE FACTS HADI WASIKIE PIA NAPENDA KUWAARIFU KAMA UKIHISI HAWASIKII WAFUATE KWENYE MTANDAO WAO,UPO LIVE WA, www.kikweteshein.com
INAONEKANA JK ALIPOAHIDI AJIRA MLIONI MOJA KWA MWAKA ALIJUA KUPITIA MGAO WA USIKU VIBAKA WATAPATA AJIRA.
 
kitu kingine amabcho nimekinotice ni jinsi reginald mengi alivyolishupalia suala hili. i can smell kuwa walimwacha kwenye mgao..doesnt look good at all
 
Unajua as much as mimi huwa ni critic za serikali lakini naona humu ndani tumekuwa overzealous katika kuweka hoja zetu bayana.....sasa hebu tuliangalie suala hili kwa mitazamo tofauti maana kuna waosema kuwa Msomali alikuwa Front tu na hata huyo Msabaha kuhamishiwa East Africa ni baada ya kumhoji Lowasa...yaani inshort kumelezwa mengi amabayo naweza kuyaweka katika kabrasha ya CONSPIRACY THEORIES

Sasa kuhusu huo umeme wa Richmond

Je FACTS ni zipi ? na je hizo facts zinakuwa backed namna gani? je kuna source zipi za kuback up hizo facts? Je wanao expose hii issue walinyimwa ulaji? mbona mengine hawayaexpose kama hili?

na kama hakuna basi lets move on
 
ndugu wadanganyika hiyo richmond iliyotufikisha hapa tulipo leo lazima tukubali tumeliwa na hata kama ikikanushwa tunajua gire amepata hii deal kutoka na link na watoto wa wakubwa kabisa wa nchi hii ambao wanatoka upande wa bara.,historia itawahukumu tena bila aibu mnaendellea kujifaidisha na matatizo yetu wasaka tonge kwa kuagiza na vijijenereta vingine kwa makontena na kuwapa wahindi wawauzie,shame!!!!

haya hili la kampuni nyingine ya[alston power rental] marekani na [wartisala]finland ambayo ameongelea kwenye press conference meneja uhusiano wa tanesco naomba wana forum tuzichimbue kwa kina ili usijekua mzigo tena kama richmond

nimejaribu kuifuatilia alsto na matokeo ya mwanzo ni haya..

contact:13901 sutton park drive
[souh third floor]
32224FLORIDA
TEL +1 904 223 8488
FAX +1 904 223 8955
CONTACT PERSON: PAUL
paul.marcroft@alstompowerrentals.com
WEBSITE:www.poweralstom.com

meneja aameahidi mitambo ya hawa jamaa 40w itafungwa mwanza kabla ya mwisho wa december 06 .hembu chekecheni.

hawa wartisala nawafahamu kama walio plaay role kubwa kwenye mradi wa IPTL walikodishwa na wale wa malaysia na yule rugemarilla [VIP ENG SASA HEINEKEN MABIBO BEER] ,wao walikuwa MANAGEMENT COMPONY.. hapa kati katikati walipelekana kwenye arbitration wakamtema rugemarila[msanii mwingine]
sasa sijui wartisala bado ni wasafi namna gani,though ni kampuni serious[tutafute mkataba huu mpya tuuone]
 
Mwanasiasa,
Braza umenivuta shati hapo ulipodai kuwa tujiunge na vyama vya upinzani.
Tatizo kubwa nililokuwa nalo mimi na hizi siasa za Bongo ni MALENGO MABAYA....
Mbinu zinazotumika ni mbovu sana na mara nyingi wanashindwa kujitetea pale kiongozi wa CCM anapokuwa na sifa za kimwili.
Kama unakumbuka alipochaguliwa JK kusimama kama mgombea wa CCM, vyama vyote vilikunywa sumu. Hawakuwa na la kusema isipokuwa kukubali kuwa JK ni kiongozi bora ktk uchaguzi huo 2005... nafasi yao kuongoza imekwisha... why? hali mgonvi wetu ni CCM?
Hivi vyama vilishindwa kui-attack CCM kabisa hali wakifahamu matatizo sio JK ila vigogo walioshika kasia za kukiongoza chama CCM. Katiba mbaya, na pia nchi nzima haina Dira!...yet bado wanaendelea kuwepo ktk boti ambayo haina dira.
1. Nitarudia kusema kwamba hadi hapo vyama vyetu vitakapo simama imara na kuonyesha mabadiliko ktk Katiba, Ufafanuzi zaidi wa mwelekeo wa Kitaifa kwani sasa hivi sioni kabisa kati ya vyama vyote nchini kuwa UJAMAA na KUJITEGEMEA ni malengo ya kitaifa.

2. Kama ujuavyo, mimi ni mpinzani mkubwa wa kuwapa urithi wetu wageni. Kuwa na imani kwamba maendeleo ya nchi yetu yataletwa na wageni kwa tafsiri mbaya inayoendeshwa eti hatuna elimu na fedha kwa hiyo -TUNAUZA NCHI. Hii ni loop hole ya RUSHWA nchini na wizi wa kimachomacho.

3. Mwisho, ni mentality ya Kibongo..
Hakuna viongozi ama chama kinachosisitiza kuimarisha culture zetu zilizotufanya tuwe HURU... KUJITAWALA. Leo hii imefikia kwamba tunaamini kuwa wafanyakazi bora ni wale wanaoweza kuongea Kiingereza - Tena tunaona ufahari kuajiri wageni (Wakenya na Waganda) wanaozungumza kiingereza kuhudumia wananchi ambao asilimia 90 hawazungumzi kiingereza. Ebu nambie utaongeza vipi uzalishaji ikiwa majority ya wananchi (kimaendeleo) wako Empire sinema wakitazama sinema ya kihindi?..
Imani kama hii ndiyo ina-create kunyenyekea watu wenye rangi, wageni na kurudisha kutawaliwa - Ukoloni mambo leo, badala ya kuwatajirisha wananchi wazawa.
REALITY over PERSPECTIVE:- Nchi zote maskini sana duniani ni zile zinazotumia lugha ya kigeni over their own...Hii ni result ya watu kutoelewana.

Kwa yote hayo hakuna kiongozi ama mwanachama ambaye atakubaliana na mawazo yangu, kwa hiyo kilichobaki hapa ni kuzoza na matokeo!....
 
Mkandala: Nakubaliana nawe sana. Tatizo ni kuwa mambo uliyoongea ni makubwa sana, viongozi wengi wa vyama vya upinzani sio rahisi kuya-comprehend. Amini ndugu yangu mimi nipo huko kwa muda sasa, watu wenye uwezo ni wachache mno; ndo hao kina Lipumba, Mbowe. Zito, JJ, n.k. Ni wachache sana hawa, ndio maana wanasikika wao tu kila siku. Watu wengi wenye uwezo kisiasa bado ama pembeni au katika CCM. Ndio maana huwa natoa wito kila nikipata nafasi kwa vijana wenye upeo kama wako, Dr WHO na wengine tuingie huko. Hizo katiba unazolalamikia haziwezi kutengamaa kuwa nzuri kama wanaozipitisha ndo hao hao kina Nungwi.Tukiwa wanachama wa hivi vyama maana tunaweza kuwa wajumbe wa vikao vya maamuzi kwa hivyo tutashiriki kutoa mawazo yetu na kuweka mambo sawa inavyopaswa.

Sina cha kuongeza kuhusu lugha, maana katika hili ni kama tulilogwa; na nafikri mchawi wetu alishafariki. Yaani kiingereza kimetufanya tuwe wazimu, tukiona mtu anaongea kiingereza kizuri tunatamani tumpe hata mke. Tunashida sana ndugu yangu katika hili.

Dr WHO: Actually yule dada wa ki-Ghana nililumbana naye sana kwa kumtetea JK na nchi yangu, na nilimpa mifano kibao juu ya viongozi wa Ghana wabovu japokuwa sikuwa na huo mfano wa Kuffor. Ningekuwa nao huo ingekuwa silaha kubwa sana akatika mazungumzo yale. Hata hivyo huyo dada anamjua JK at personal level, na data zake zilinitisha mno, walivyokuwa wakikutana huyu bwana akiwa Waziri wa Foreign Affairs. This said, pamoja na utetezi wangu wote, moyo wangu ulinishuhudia kabisa kuwa kwa kweli sisi tulichemsha, na sio safari hii tu, mara nyingi sisi huchemsha katika kuchagua viongozi. Yote hii ni kwa sababu tumefunga options zote outside CCM. I fervently believe that our problems are attributable to poor leadership. We will get out of leadership mess by thinking beyond the Skinner's box; I mean by looking for political alternatives other than CCM. Otherwise, our problems are there to stay. Trying to improve our situation via CCM is like trying to service a car whose state of dilapidation is irreparable!

PS: Nungwi ni kiwakilishi cha mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikri kuliko maelezo; pale UDSM watu wa namna huu huitwa vilaza; sijui kama siku hizi wamebadilisha jina.
 
MWANASIASA

vipi umesema huyo dada wa ki ghana anamjua rais wetu saana,au jamaa alikuwa akichapa nini? maana nasikia alipokuwa foregn kuna incidence nyingi akifika ulaya alikuwa anapoteza....na kujichanganya saana...nimepita uk na marekani nimezikuta watu baadhi washenda nae sana night clubs....lakini hata rawlings na jk hawachekani tena alipofika nyumbani alijichanganya sana nights ,,maeneo ya masaki kwa siku tatu alizokaa dar
 
phillemon mikael said:
MWANASIASA

vipi umesema huyo dada wa ki ghana anamjua rais wetu saana,au jamaa alikuwa akichapa nini? maana nasikia alipokuwa foregn kuna incidence nyingi akifika ulaya alikuwa anapoteza....na kujichanganya saana...nimepita uk na marekani nimezikuta watu baadhi washenda nae sana night clubs....lakini hata rawlings na jk hawachekani tena alipofika nyumbani alijichanganya sana nights ,,maeneo ya masaki kwa siku tatu alizokaa dar

Kuna mama mmoja pale Atlanta Airport aliwahi kunipatia ujumbe wa kupeleka kwa Bilali na kwa Mkapa. Alikuwa anashangaa kusikia kuwa Mkapa ni President, hakuwa anaamini kuwa jamaa anaweza kuwa President. Alidai walikuwa marafiki sana wakati akiwa pale Washington DC l;akini hakuniambia undani wa urafiki wao.
 
Mwanasiasa,
Maneno yako nayaafiki 100 kwa 100 nadhani ipo haja ya kuwasiliana nje ya siasa maanake babu ubishi kama mimi ni rudisho nyuma la chama kama Chadema!...Navyoamini mimi watu kama Kaborou ni matokeo ya kutoelewana ndani na mwisho wake ndio huo wa kukamatana uchawi. Nimejaribu sana kuwasiliana na Free through J J Mnyika, lakini naona hatuendi popote. Watu wako Bizi bizi kuweka mkate mezani hadi hapo 2010.

Tukirudi ktk swala la generators na Umeme nchini. Jamani ya Richmond ndio hivyo tumeisha liwa kama tulivyoliwa toka 1996 baada ya report ya warioba. Ten years bob ten years na hakuna kilichofuatia zaidi ya sifa za uongozi bora toka kwa hao wazungu IMF. Rushwa kwetu ni kubomoa na kuiba kilicho ndani mwako ndio maana hata JK haelewi kuwa rushwa ya nchi za magharibi ni upokea commission au takrima ukiwa kiongozi lakini kazi imefanyika kujenga nchi.
Wanabodi inabidi niulize... Je, hakuna mtu mwenye refa huko juu tuweze kuingiza umeme wa solar nchini hata iwe mkataba mdogo wa mkoa?
 
One of the facts ni kwamba Richmond ni kampuni hewa,regardless of who owns it.Rumour has it that jenerators walizoleta ni za boeing na haziko sawasawa.
 
Mkandara umenifurahisha sana na hiyo ya watu kuwa biz biz; very true indeed! Free yupo huku UK. Yupo pale Hull; Nitakupa namba yake ya simu na email address kwenye private message umtwangia moja kwa moja badala ya kupitia kwa akina JJ.

Hilo la umeme labda turudi kwa mzee wa Karachi tumuombe atuletee wale wazungu wake tena!
 
Fact ingine ni kwamba hii kampuni imeshindwa ku-deliver kama ilivyoahidi. f'acts speak for themselves'! Hiyo evidence vipi Dr?
 
mwanasiasa said:
Fact ingine ni kwamba hii kampuni imeshindwa ku-deliver kama ilivyoahidi. f'acts speak for themselves'! Hiyo evidence vipi Dr?



Unaaman wameshindwa kudeliver hiyo mitambo au specification za huo mtambo?

Kama ni delay naweza kukubali kuwa kulitokea delay za kuudeliver na hili sijui limekuwa covered na insurance au vipi

Tatu hatujui contracts zinasemaje inawezekana ikawa hiyo delay ilitokana na upande wa serikali na hili mimi silishangai kama likitokea kwani hiyo ni kawaida kwetu

Nnne evidence inaweza ikawepo lakini ikawa circumstantial evidence hivyo tunarudi back to square 1
 
Fact 1: Kampuni hiyo haijawahi kufanya project yoyote ya power generation na wala haina mhandisi hata mmoja wa power engineering. Biashara yao kubwa ni huduma za printing.

Fact 2: Kampuni hiyo ilipata tenda ya $178m hiyo bila ushindani wowote.

Fact 3: Mwaka jana, mkurugenzi wa kampuni hiyo aliwahi kumstarehesha balozi wa Tanzania aliyeko marekani (Balozi daraja) pale Houston kwa siku kadhaa.

Fact 4: Hadi leo kampuni hiyo imeleta generator moja tu ya MW 22 na generator hiyo haijafanya kazi yoyote. Bado tunasubiri generatopr nyingine zenye jumla ya MW 78 kufikia lengo la MW 100 za mkataba. Kwa sipidi hii si vibaya ku-extrapolate kuwa itachukua zaidi ya miezi 9 kukamilisha mradi huo.

Fact 5: Hakuna uhakika kama hizo generator tumezuiwa au tumeazimwa kwa muda tu wakati jamaa wanatafuna hizi dolari milioni 178.
 
Back
Top Bottom