Kashfa ya Richmond: The FACTS

This is very stupid.

Sijawahi kuona wizara au kampuni inasukumia matatizo/uchafu wake ikulu. Hii inakuonyesha wazi ni jinsi gani raisi na wapambe wake walivyohusika. Wananchi inabidi tuamke. Hii sio amani kwani hata hiyo kodi ambayo inakusanywa kutokana na uzalishaji haipo tena. Inabidi raisi ajiuzulu na serikali yake yote. Huu uchafu hatuuwezi kabisa kwani tutaishia kuwa kama Haiti.

This is just unbelievable. We don't have leadears, we have followers.
 
Interested Observer,

Malizia msumali kwenye jeneza , please if you can post those pictures.
 
Rufiji,

Turudi Tanzania tukaanzishe gazeti linalopekenya na kutoa habari sahihi.

Hili la wasanii hao mi nimechoka. Lakini what do you guys expect?, Uchumi umempitia kando VDG wetu. Kama yule mwenzie aliyekimbilia kuoa baada ya kuingia ikulu. woote wanafuata the same path. makandara samahani ila kuna ka correlation kati ya marais waliopita kidizaini. Nadhani umeelewa.

baadaye leo nikipata muda nitakuja na uchambuzi yakinifu, naona jamaa walijaribu kurusha silaha zao hapa lakini wapi!, ngoma niliigundua mapema na kuachia Scud ikaiteketeza. Hivi kwanini msifanyie kazi maoni yetu?, kama ni mabaya yaacheni kama ni mzuri basi implement, sisi hatuchukii mtu, tunataka nchi yetu iwe na maendeleo. Na kumbuka mpaka tupo humu uje hela ya kula haitupigi chenga. Acheni kutunyamazisha kwa kurusha virus, ukirusha virus narekebisha. BTW utarushia wangapi?, nikienda kwenye cafe pia utarusha?

FD
 
Wewe umeona wapi mtu ana utalaam wa kulima mchicha unampa kazi ya kulima kahawa ataweza? Nina maana hawa Richmond wamesaini mkataba na serikali ya kujenga bomba la mafuta, na bado hawajaanza na wala hatujuwi performance yao wewe unakwenda mkuwapa mkataba (USD 172 Mil contract) to supply 100MW! Hawa jamaa walionana na Kikwete kwanza then akawaagiza vijana wake wafanye upembuzi yakinifu (evaluation). Kama unavyojua wabongo wamepiga mchanga wa macho wakazoa chao na kwenye njaa wengi ni sherehe nchi nyingi za Afrika zikipatwa matatizo zinaposaidiwa watu huiba kumbuka wakati wa njaa mwezi january na feb we acha tu.
 
Ndugu Malecela , Rostam, Jk, Lowasa,Kingunge, Makamba, Kinana , na wana CCM wengine wote na viongozi wa Serikali inayo ongozwa na Msanii JK , onen aibu na jueni Watanzania sasa wanajua mengi na kwa urahidi .Najua mtandao hapa bongo umefanikiwa kuzima habari kutoka na badala yake kumwacha JK na Lowasa wanalambwa miguu lakini sasa njia ya upashanaji habari ziko kibao .

Naungana na Tatu to call for the president to resign japokuwa naweza kushitakiwa kwa kosa la kumrushia matusi Rais ,kisa hatuna neno resign for the nation interest .JK badala ya kuhangaikia matatizo ya Nchi yeye anaanza kumwandaaa Asha Rose kwua Rais wa Tanzania .Jamani .

Lakini historia itawashitaki na iko siku tutaona viongozi wa kweli Tanzania . Slowly but sure ama upinzani ama watu ndani ya CCM watakuja kusimama na kusema no na kila muhusika atasimama kizimbani kujibu mshitaka .

Mkuu wa usalama uko humu mwenyewe ama vijana wako .Tunakupa ujumbe huu kwamba umwambie bosi wako tuna machungu na uongo wa serikali yemu kwa watu masikini wa Tanzania .
 
Chingwanji,

tatizo ni njaa tu, hata huyu mkuu wa UWT hana awezalo kufanya, Wenye uwezo ni mtandao wa CCM tu basi. Yes Rostam anaweza kufanya mabadiliko akiamua...
Usije ukauliza majibu....
FD
 
Sasa hao wafadhili wakisitisha msaada wao si ndiyo tutakwisha kabisa?

Power crisis handling disappoints donors
ABDUEL KENGE
Daily News On Saturday; Saturday,October 21, 2006 @00:09

THE donors' General Budget Support review (GBS), yesterday criticised the way the government has handled the ongoing power crisis, resolving to assess the situation before assisting the country's five-year emergency power master plan.

The GBS says that the power crisis, which started seven months ago, was scheduled to end in September through leased gas-generators, but it was 'questionably delayed because of mismanagement'.

The outgoing Chairman of the GBS, Mr Torbjorn Pettersson of Sweden, told the 'Daily News on Saturday' yesterday that the donors want to assess the issue before deciding the next step.

"We regret the mismanagement of the power problem," Mr Pettersson said after GBS wound up its five-day annual review, adding "the development partners are watching closely how the government will manage this crisis--this is all I can tell you for now."

The government had set aside about 220bn/- for leasing gas generators that were supposed to bridge the gap when Mtera Dam ceases generation of hydropower. The dam was switched off a few days ago.

A joint GBS Secretariat communique said that a small group of government officials and development partners--the World Bank, Sweden, United Kingdom and IMF--would meet in advance of the next cabinet meeting, to discuss the issue. The cabinet is scheduled to meet next Friday.

"There is need to start implementing the emergency power supply programme immediately," the summary says.

To speed up management of the power crisis, the donors also have nodded to government's intention of using emergency procurement regulations to address the problem.

The development partners support 80 per cent of the government's development budget which this year is over 800bn/-.

Commissioner for Policy Analysis at the Ministry of Finance, Mr Mugisha Kamugisha, agreed there was a delay in delivering the generators to offset the hydropower vacuum.

"The money is there on the budget but the problem is the delivery", Mr Mugisha said.

Mid this year the government hired Agreko and Richmond Development Company (RDC) to produce 40 megawatts and 100MW, respectively, but starting with 20MW each, to ease the power crisis. However, the latter failed to effect delivery on time, further worsening the power crisis.

Bank of Tanzania Governor, Mr Daudi Ballali said due to the power cuts, the economic growth would not grow as anticipated at 7.0 per cent claiming it would now grow at 5.9 per cent.

The Minister for Finance, Ms Zakia Meghji, warned during the opening of the GBS on Monday that unless the blackouts were halted, positive economic growth would be a distant dream.

The five-year Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) recovery master plan requires a capital investment of 1.3trilion/- that will also minimise TANESCO's financial losses. To mobilise the resources, the government intends to convene a donors' meeting soon.

Halafu angalia na hii...

Waziri mpya anusa hujuma Tanesco

Na Mwandishi Wetu (Mwananchi 21 Oktoba 2006)
WAZIRI wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi ameshutushwa na taarifa za kufungwa kwa bwawa la Mtera, licha ya kupewa taarifa na uongozi wa Tanesco kuwa lingeweza kuzalisha umeme kwa siku 21 zaidi.

Kutokana na hali hiyo, Karamagi ametafsiri hali hiyo kama njama za kuhujumu uchumi zinazofanywa dhidi ya serikali kutoka ndani ya shirika hilo.

Karamagi amesema jana kuwa serikali imeshtuka baada ya kusoma kutoka kwenye magazeti taarifa za kufungwa kwa bwawa hilo wakati siku moja kabla, viongozi wa Net Group na Tanesco, walishaithibitishia serikali kwamba maji katika bwawa hilo yangeweza kutosha kwa siku 21.

Karamagi alisema baada ya kuingia katika wizara hiyo Oktoba 17 mwaka huu, uongozi mpya uliitisha kikao cha watendaji wote katika shirika hilo na kutoa taarifa kuwa maji yangekuwepo kwa siku 21.

Juzi Karamagi alikaririwa akisema kuwa taarifa za kufungwa kwa bwawa la Mtera zilizoripotiwa na vyombo vya habari hazikuwa sahihi.

"Asubuhi ya tarehe 17 Oktoba wahusika wa Tanesco walitwambia kwamba maji katika bwawa la Mtera, yalikuwa yamebakiza kina cha sentimeta 21 na kwa kuwa matumizi yalikuwa sentimeta moja kila siku, walitarajia bwawa hilo lingeendelea kutoa nishati angalau kwa wiki mbili," alisema.

Lakini, alisema kuwa kesho yake yaani Oktoba 18, waliona kwenye magazeti habari za kufungwa kwa bwawa la Mtera.

"Serikali imekitafsiri kitendo hicho kama njama za kuihujumu na kuhujumu uchumi wa taifa," alisema na kuongeza:

"Kinachotushangaza katika serikali, ni kwa nini taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na ambayo ilikuwa sahihi, haikutolewa serikalini na badala yake, serikalini ikapelekwa taarifa ambayo ni ya uongo wa wazi?" alihoji.

Kwa mujibu wa Karamagi, suala nyeti la kufungwa kwa bwawa hilo lisingeweza kutangazwa kwenye vyombo vya habari bila kuiambia serikali.

"Kwa nini wanafunga bila kutueleza?" sisi katika serikali tunajiuliza hatupati jawabu," alisema Karamagi.

Waziri huyo ameshangazwa na utaratibu huo na kuhoji: "Huu ni utamaduni wa wapi? Wizara ndiyo yenye mamlaka na suala la nishati. Hawa wa Tanesco na Net-group walitaka kuniweka mimi katika mazingira ya kumwambia Rais jambo ambalo si kweli."

"Hebu fikiria kama mimi ningekwenda kumwambia Rais kwamba tunayo maji ya kutosha kwa siku 21 na bwawa linaweza kutusukuma kwa siku hizo, na Rais akalitangazia taifa kwamba bwawa la Mtera halitafungwa katika siku 21. Lakini kesho yake vyombo vya habari vikatangaza kwamba bwawa hilo limefungwa, hii ingekuwaje? Hali hii tunaitafsiri kama njama tu," alisema.

Alipoulizwa ni hatua gani serikali inachukua, Karamagi alisema serikali imekwishaanza kuchukua hatua. Hata hivyo, alisema kwa sasa suala la muhimu sana ni kuweka sawa suala la umeme nchini.

"Katika hali kama hii, huwezi kushughulikia matatizo mawili, kwanza tunahangaika na hili la nishati ndipo tutaanza kushughulikia hili la kiutawala. Lakini hatua za kiserikali tayari zimekwishaanza," alisema waziri huyo.

Wakati huo huo, Nora Damian anaripoti kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuunda tume kuchunguza suala zima la umeme kikihisi kuwa kuna baadhi ya viongozi wakubwa serikalini wanahujumu jitihada za kutatua tatizo hilo ili wajinufaishe kupitia biashara ya jenereta.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, mara baada ya kufungua mkutano wa mafunzo ya vijana wa chama hicho, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, alisema inatia hofu kuona jitihada za kutatua tatizo la umeme zinakwama mara kwa mara, jambo ambalo alisema huenda likawa na mkono wa mtu.

“Tunamuomba Rais aunde tume ya kuchunguza suala hili, inawezekana kabisa jenereta tunazoziona mitaani ni biashara ya wakubwa na ndiyo maana tatizo la umeme haliishi kila siku. Rais anapotoshwa kila siku kuhusu tatizo la umeme na hii huenda inafanywa makusudi,” alisema Dk. Slaa.

Alipoulizwa na Mwananchi kama ana ushahidi au kumjua kiongozi yoyote wa serikali anayejishughulisha na biashara ya jenereta, Dk Slaa alisema; “Inawezekana ni mpango wa viongozi wakubwa lakini siwezi kuwataja.”

Alimtaka Rais Kikwete kutoona aibu kulitangaza tatizo la umeme linalolikabili taifa kwa sasa kuwa ni janga la kitaifa.

Alisema pamoja na tatizo la umeme kuwa na athari mbaya kiuchumi, lakini pia linaathari za kijamii hasa kwa akina mama ambao alisema wapo katika hatari kubwa ya kubakwa na kupoteza maisha kwa sababu wanafanya kazi nyingi kama kutafuta mashine za kusaga usiku wakati umeme unapopatikana.

“Wanazima umeme mchana wakifikiri wanapunguza matumizi lakini matokeo yake kazi zinafanyika usiku, hii ni hatari hasa kwa wanawake kwa usalama wao kwani wanaweza kubakwa na kuporwa,” alisema.

MAONI YANGU

Nimejaribu kujiuliza na kurejea yafuatayo:
1. Tukumbuke hapo nyuma kuna kampuni inaitwa Utegi Enterprises nayo ilipewa jukumu la kuleta jenereta kwa ajili ya hapo hapo Ubungo, deadline iliwasumbua sana na almanusura wanyang'anywe tenda. Sikumbuki waliishia wapi. Mwenye kumbukumbu anisaidie kwa hili. Ninachojua ni kuwa hiyo kampuni nayo kazi yake kubwa ni "clearing and forwarding".

2. Tangu mitambo hiyo ya gesi ifungwe hapo Ubungo, imekuwa "inaharibika" mara kwa mara. Kwa nini? Ilikuwa, na ni mibovu, kwa sababu ya rushwa au hujuma?

3. Tatizo la Richmond ni nini? Hawana pesa za malipo ya awali kwa huyo mwenye jenereta? Au jenereta yenyewe ndiyo haipo? jambo ambalo haliniingii akilini. Kama JK anahusika si angeweza kumwambia dada yake Meghji awape fedha hao jamaa ili walete huo mtambo, mambo yakaisha chapchap bila yeye kuadhirika? Kama ameweza kuagiza serikali itoe milioni 500 zaidi kwa halmashauri licha ya kwamba bunge lilishapitisha kiasi cha milioni 500 tu, kwa nini kwenye hili isiwezekane?

4. Sekta ya nishati ni nyeti kwa taifa na ndiyo maana kina WB, IMF na "wahisani/wafadhili" (kwa manufaa ya nchi zao) wanaiangalia kwa karibu. Ni wao wanahusika kwa kiasi kikubwa ku-sanction nani (kampuni) afanye nini. Walilazimisha, kwa mfano, serikali iingie mkataba na Netgroup Solution na kwamba wao "wangelipa" fedha hizo ikiwa ni "mkopo" kwa serikali yetu. Wao wanafaidika vipi? Ni nia njema tu ya kusaidia?

5. Netgroup Solution (watu waliishaibatiza Netgroup Problems) inahusika vipi na sakata hili? Waziri Karamagi "kanusa" nini? (rejea hiyo habari hapo juu). Serikali ilitangaza kuwa haitaendelea na mkataba na Netgroup. Je, wamekasirika hivyo "wanatufanyizia" kabla hawajaondoka? Badala ya ku-manage wame-mismanage mitambo na mabwawa ya kuzalisha umeme kisha wanatuacha solemba?

Bado naendelea kutafakari.
 
Fikiraduni,
Chonde mkirudi nyumbani msinisahau. Mkianzisha gazeti tuwe pamoja.
 
Jasusi,

Sasa bila ya ujasusi habari tutazipataje?:) Lazima uwemo. husiwe na wasiwasi.

FD
 
Mwanasiasa,
Waandishi tutakuwa sisi. Jasusi, Fikiraduni na Yombayomba.
Utaona mambo.
 
Jasusi,
Mawazo mazuri nina matumaini tutahimiri si unajua waandishi siku hizi wamenunuliwa inasadikiwa hata BBC idhaa ya kiswahili, achilia mbali yule mwanachama mwenzetu wa zamani kwenye ile foroum (jina kapuni) Mh Kaburu. Akiwa mwenzetu alikuwa ni mpinga rushwa mkubwa lakini alivyokuja kufoji yeye na Mh Ndasa kwenye swala la Kitine na adhabu aliyopewa mimi nilikataa tamaa kabisa, sasa usije tukajikuta FD, yuko kwenye pay roll ya EL kwi kwi kwi who knows?
 
Yombayomba,

Kuwemo kwenye payroll yao siwezi. Aminia rafiki yangu. Sijui jamaa wa richmond wametoa wapi hela......

Au wanamtandao wamejikusanya au RA amewakopesha kumuokoa rafiki yake JK aliyeingizwa mjini?.

Vipi jamani bado Turbine engines zenyewe zimekuja nusu nusu huku ma bezo kibao!!!!!!!!!!

TZ bado kufa tu!

FD
 
Nitafurahi zaidi kama "mchawi"atapatikana na kuchukuliwa hatua kali na kwa uwazi...

Taasisi zachunguzwa kuhujumu umeme

na Charles Mullinda

TAASISI mbili kubwa nchini zinazohusika kwa namna moja au nyingine na usambazaji wa nishati ya umeme kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) zinatuhumiwa kula njama za pamoja na kuhujumu mpango wa kitaifa wa kutafuta nishati mbadala ili kukabiliana na tatizo la upungufu mkubwa wa umeme nchini.

Taarifa ambazo Tanzania Daima imezinasa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya serikali zinaeleza kwamba, tayari serikali imeshaanza kuzichunguza taarifa hizo, kabla hatua rasmi hazijachukuliwa dhidi ya taasisi hizo mbili (majina tunayo).

Habari zaidi zinaeleza kwamba, tayari kuwapo kwa taarifa hizo za hujuma ambazo zimeishtua serikali, zimesababisha kuzorota kwa mahusiano ya kikazi kati ya taasisi hizo mbili na viongozi wa juu wa serikali.

Kwa mujibu wa habari hizo, wasiwasi wa kuwapo kwa hujuma hizo, ulianza siku chache tu kabla hata Rais Jakaya Kikwete hajawahamisha mawaziri kadhaa, akiwamo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha ambaye sasa ni Waziri anayeshughulikia Afrika Mashariki.

Habari zaidi zinasema kwamba, eneo moja ambalo lililengwa na taasisi hizo mbili lilikuwa ni lile la kuingizwa nchini kwa majenereta yanayoendeshwa na gesi ambayo yangesaidia kuongeza kiwango cha uzalishaji wa megawati 100 za umeme.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi jana, na kumuuliza kuhusu kuwapo kwa hujuma hizo, ikiwa ni pamoja na kumtajia majina ya taasisi zinazotuhumiwa, hakuwa tayari kukanusha wala kukubali kuhusu kuwapo kwa hali hiyo.

Hata hivyo, Karamagi alisema, serikali inakusudia kuwachukulia hatua wale wote ambao kwa namna moja au nyingine watabainika kuwa walihusika katika kukwamisha jitihada za serikali za kukabiliana na tatizo la nishati ambalo limekuwa likiongeza makali ya mgawo wa umeme nchini.

“Serikali haiwezi kusema moja kwa moja kama kuna watu waliohujumu juhudi zake za kukabiliana na tatizo la umeme, lakini ni wazi wapo watendaji ambao wamehusika ama kwa kuzembea kutekeleza majukumu yao au kwa makusudi.

“Kama mambo yalipangwa vizuri, halafu baadaye yanakwenda mrama, hilo ni kosa, hapo ni lazima serikali iwachukulie hatua kali. Sio lazima serikali itangaze hatua watakazochukuliwa moja kwa moja, zinaweza kuwa za kiutawala, lakini ni lazima wachukuliwe hatua,” alisema Waziri Karamagi.

Kauli hiyo ya Karamagi imekuja siku chache tu baada ya kutoa tamko akilaumu uamuzi wa TANESCO kuzima mitambo ya Mtera kabla hawajatoa taarifa kwake na kinyume cha taarifa waliyokuwa wamempatia awali.

Katika tamko lake hilo, Karamagi alieleza kushangazwa kwa kutopelekewa taarifa za kufungwa kwa bwawa la Mtera na kwamba taarifa aliyoipokea siku mbili kabla, ilikuwa ikieleza kuwa Mtera ilikuwa na maji ya kutosha kuendesha mtambo kwa siku 21 zaidi.

Katika hatua nyingine, Waziri Karamagi jana alilieleza gazeti hili kwamba, sehemu ya mwisho ya mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 20 aina ya TM 2500 inatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa ijayo.

Alisema kuwasili kwa mitambo hiyo kutakamilisha uingizaji wa awamu ya kwanza ya mitambo hiyo inayoletwa na Kampuni ya Richmond Development ya Marekani ambayo inapaswa kuleta nchini mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100.

Waziri Karamagi alisema amepanga kutembelea eneo litakalofungwa mitambo hiyo wiki ijayo, ili kujiridhisha jinsi kazi hiyo inavyoendelea kabla ya kutoa taarifa rasmi kwa umma.

“Nimepata taarifa kuwa sehemu ya mwisho ya mitambo hiyo ambayo inaingizwa nchini kwa awamu, itawasili Ijumaa wiki hii, wameniambia kuwa wamelazimika kuisafirisha kwa ndege kutokana na ukubwa wa tatizo la umeme, hivyo kutumia meli ingechelewa kuwasili nchini.

“Kama ingesafirishwa kwa meli, ingekuja kamili, lakini ndege sio rahisi kwa sababu ni mikubwa. Mimi nimepanga kuwatembelea wiki ijayo ili kuona kazi ya ufungaji inaendeleaje na baada ya hapo nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuwataarifu Watanzania kinachoendelea kuhusu suala la umeme,” alisema Waziri Karamagi.

Alisema anatarajia kuwa baada ya kuwasili kwa sehemu hiyo ya mwisho ya mitambo, kazi ya ufungaji itaanza na itakamilika katika muda uliopangwa.

Akizungumzia nyanzo vikuu vya uzalishaji umeme katika bwawa la Mtera alisema, halitarajiwi kufunguliwa mpaka mvua zitakapoanza kunyesha.

Kuhusu bwawa la Kidatu, alisema taarifa alizopokea Jumamosi iliyopita, bwawa hilo bado lina maji kidogo na linazalisha umeme wa kati ya megawati 18 na 20. Hata hivyo alieleza kuwa linaweza kufungwa wakati wowote iwapo mvua hazitanyesha.

Wakati huo huo, makali ya mgawo wa umeme ambayo yameuma kwa zaidi ya miezi mawili, yamepungua katika kipindi cha siku chache zilizopita kwa sababu ya mvua kunyesa mkoani Tanga na kuongeza uzalishaji wa umeme katika bwawa la Pangani.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Meneja Uhusiano wa TANESCO, Daniel Mshana alisema kituo cha bwawa dogo la Pangani ambacho kinahudumia gridi ya taifa kimejaa maji kutokana na mvua hizo.

“Maji yamejaa kwa wiki nzima sasa na yameongeza uzalishaji kutoka mashine moja iliyokuwa ikitumika awali hadi mashine tatu ambazo kwa jumla zinazalisha megawati 68,” alisema Mshana.

Hata hivyo, alionya kuwa kwa vile maji yanayopatikana katika bwawa hilo yanatumika yote, makali ya mgawo yanaweza kurejea wakati wowote maji yatakapopungua.
Aidha, Mshana alieleza kuwa matukio ya kukatika kwa umeme ghafla yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, hayahusu mgawo wa umeme, bali matatizo ya kiufundi kwenye mfumo wa uzalishaji umeme.

“Jumamosi, gridi ya taifa ilipata hitilafu kwa saa mbili, hivyo umeme haukuwepo na katika siku hizo hizo za mwisho wa wiki, mashine zinazozalisha gesi za Songas nazo zilipata matatizo na kusababisha kukatika kwa umeme,” alisema Mshana.

Alisema mashine ya Songas iliyoharibika bado inafanyiwa matengenezo, lakini haitaathiri jitihada za TANESCO kusambaza umeme kwa wateja wake, hasa katika kipindi cha Sikukuu ya Idd.

“Katika siku hizi za Sikukuu ya Idd el Fitr, mzigo wa matumizi ya umeme kwenye mfumo wa usambazaji utapungua kwa kuwa viwanda vingi vitakuwa havifanyi kazi,” alisema Mshana.
Source: Tanzania Daima (24 Oktoba 2006)
 
Salaam,
I pass through and found Richmond Development Company is online, but is this the manner of saying Wanaoipakazia ni kampuni hewa wana wivu wa kisiasa?

However, katika miradi ya karibuni kwenye list yao hakuna Tanzania, je hapa tuwahukumu kwa kutokuwa wazi toka awali au tuvilaumu vyombo vyetu vya habari kwa kuwa na waandishi vihiyo! hawatafuti information, wangojea hadi waitwe maelezo kusomewa risala!

ACCOMPLISHMENTS & NEW PROJECTS
Financially Closed Projects
130 MW Power Generation Station in Gaziantep, Turkey. Project Value: $117 million.
Upstream Oil & Gas in collaboration with Major Oil Company in The Balkans. Project Value: $150 million.
Leveraged Buy Out (LBO) of an Infrastructure Development Company in The State of Michigan, USA.


Projects Currently Under Development
National Sports Stadium with seating capacity of Sixty Thousand Spectators.
1,150 km of Petroleum Product Pipeline plus Five Terminals.
Redevelopment of Multiple Civil Airports.



5825 Schumacher Houston, Texas 77057
ph (713) 952-3472
fx (713) 952-0932

© Copyright 2004 Richmond Developement Company, All Rights Reserved

...........................................
:U Can't Change The Nature:
 
Okay, Mwanakijiji, nimekupata.
Computer yangu sijafanikiwa bado kuplay podomatic yako, labda ningefaidi kupembua mengi huko.
Well, n' good, yawezekana walirejister baada ya kusikia minong'ono kibao! but where is the truth?
Bytheway, twataka umeme uwake tuu, ili bongo watu wafanyekazi mchana badala ya usiku!

.....................................
:U Can't Change The Nature:
 
Back
Top Bottom