Kashfa ya "degree ya chupi": Mkuu wa wilaya ya Korogwe kizimbani

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Korogwe jana kwa shtaka la kumkashifu Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe kuwa ana stashahada ya chupi. Katika kesi hiyo, Hakimu alikataa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumwakilisha Mkuu huyo wa wilaya katika kesi ya madai ya Shilingi Milioni 96 dhidi yake.

Katika kesi hiyo Na. 7/ 2012 mlalamikaji ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Najum Tekka anayedai kukashifiwa na Gambo wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya kwamba stashahada ya Sheria aliyopata mtumishi huyo ni ya chupi.

Awali ilidaiwa kwamba mkuu huyo wa wilaya alimwalika mlalamikaji kutoa ushauri wa kisheria kuhusu namna ya kumaliza mgogoro baina ya halmashauri ya mji na wafanyabiashara na kwamba baada ya kufanya hivyo mlalamikiwa alipinga ushauri uliotolewa na kisha kutoa kauli hiyo kwamba shahada yake ni ya chupi.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Hamis Salum, mlalamikaji huyo aliiomba mahakama imwondoe Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye aliwakilishwa Mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Rebecca Msalangi kwa kuwa hana mamlaka katika madai hayo na kamwe Ofisi yake haikuwahi kupeleka ombi maalum la kutaka kumwakilisha Gambo kwenye shauri hilo.
 
KIkwete rais wa ajabu! Yaani hajamwajibisha huyu muhuni wake? Hata kama wanajuana walivyovuana chupi na kupeana shahada, Gumbo hakupaswa kuyasema aliyosema hadharani. Je katika mchezo huu rais anafaidika vipi? Je huu si ushahidi kuwa aliridhika na mwakilishi wake kumtukana bi wa watu? Ningekuwa huyu bi mkubwa ningemshitaki Gumbo na aliyemteua under vicarious accountability and liability.
 
kwani huyu dada kasomea wapi? Tunataka kujua kama mkuu wa wilaya anaonewa ama vipi

Does that really matter? Kimsingi huyo mkuu wa wilaya alimtaka huyo mwanasheria kuzungumzia kesi ambayo tayari iko mahakamani. Lakini mwanasheria akakataa on the basis kuwa hana uwezo wa kuzungumzia kesi ambayo tayari ipo mahakamani.

Kutokana na kauli yake DC alikiuka maadili ya uongozi wa umma na kukidhalilisha kiti cha ukuu wa wilaya na kiongozi Mkuu wa nchi aliyemteua kushika wadhifa huo regardless of whether mwanasheria alisomea wapi.
 
KIkwete rais wa ajabu! Yaani hajamwajibisha huyu muhuni wake? Hata kama wanajuana walivyovuana chupi na kupeana shahada, Gumbo hakupaswa kuyasema aliyosema hadharani. Je katika mchezo huu rais anafaidika vipi? Je huu si ushahidi kuwa aliridhika na mwakilishi wake kumtukana bi wa watu? Ningekuwa huyu bi mkubwa ningemshitaki Gumbo na aliyemteua under vicarious accountability and liability.

Mkuu Presidaa aliwahi kusema watoto wa kike wa shule wanapata mimba kwa viherehere vyao.. Remember..? Unategemea wateule wake wawe tofauti...?
 
Ha ha ha degree ya Chupiiiiiiii,hizi kauli tumezizoea maana hata mkuu wa nchi huwachochea kusema,ulikwishaona kiwanda cha kutengeneza uongo?Ilibidi mkuu wa nchi nae tumshitaki.
 
Wapi alisoma haijalishi ila kwa DC kutoa maneno kama hayo ni kudhihaki kiti chake. Aliyepiga walimu wazembe mkoani Kagera alifukuzwa kazi. Nashangaa kwanini Gumbo bado yuko ofisini.
 
Mkuu wa Wilaya anapotoa kauli ya utoko, hatujali kama degree ni ya chupi ama la.

Yaani hata kama degree ni ya chupi, tunaona ile kauli ya utoko ndiyo issue kubwa zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hapa mkuu wa wilaya ata takiwa athibitishie mahakama alikuwa ana sema ukweli.

Na huyo dada ata takiwa athibitishe hiyo ni kashfa sio ukweli.

Japo kwa haraka mkuu wa wilaya ana makosa ya kumdharisha huyo dada.
 
Eti kwenye hii kesi huyo mkuu wa wilaya alikuwa na haki ya kutetewa na ofisi ya mwanasheria mkuu?
 
Back
Top Bottom