Je, ni rahisi kwa taasisi kubwa kama Tanapa kusahihisha written interview (yenye maswali 25) ya zaidi ya watu 800 kwa masaa ma 5 tu na kutoa matokeo kuwa watu 30 pekee ndo wamefaulu kuendelea na oral interview?!
ninasema hivyo kwa kuwa naona kama kuna rushwa na kujuana maana haingii akilini zaidi ya watu 800 pepa yao kusahihishwa kwa masaa ma 5 halafu eti matokeo yanawaruhusu 30 tu na wanaarifiwa the same day kuwa keshoye warudi for oral interview.
ni hivi:
tarehe 13 august kulikuwa a interview ya nafasi mbali mbali za kazi katika Tanapa.interview ilifanyikia msimbazi center saa 3 asubui mpaka saa 5 asubui.maswali 25 yalipitishwa kwa watahiniwa ili wayafanye.ilipofika saa 11 jioni majina ya watu 30 waliofaulu kuingia oral interview yakabandikwa.sio matokeo ya watahiniwa wote waliofaulu,bali ni majina tu na wala haionyeshi maksi zao.
nina wasi wasi matokeo na majina yalishapangwa kitambo na ile interview ilikuwa ni kutimiza wajibu tu..naomba vyombo vinavyohusika vilifuatilie suala hili ili kuondoa kujuana ndani ya taasisi hizi kubwa za serikali
Nafikiri kutakua na procedure ya kuappeal jaribu kufind out.