Kashfa Uingereza yasababisha Cameron kukatisha ziara, Kikwete yeye aenda kutalii

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
206
Kule Uingereza kuna skandali inayohusu gazeti la News of the World na mapolisi wa UK. Tuhuma hizo zimesababisha Cameron wazir mkuu wa UK akatishe ziara yake South Africa na kurudi kwao.

Tanzania iko kwenye tatizo zito la umeme na serikali iko kwenye tuhuma nzito za rushwa. Mkuu wa nchi yeye leo anaendelea na safari ya "KIHISTORIA"ya kwenda kutembelea kisiwa alichosotea Madiba kwa miaka 27.

Wana JF nipoozeni kwa maoni yenu kabla sija-collapse kwa msongo wa mawazo..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Unamshangaa kikwete?mshangae pinda kwa nn hajamfuta kazi jairo, na ngeleja kwann hajajihuzuru pamoja na naibu wake kwa kuingiza serkali kwenye kashfa ya rushwa na wabunge wa ccm a.k.a washangiliaji
 
Kama mnavyojua Rais Jakaya Kikwete na Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron wako ziarani Afrika ya Kusini. Hata hivyo, Cameron amekatisha ziara yake na kurudi nyumbani kutokana na kashfa kali ya phone hacking na rushwa ambayo imesababisha maafisa wa polisi wa ngazi za juu kujiuzulu. Pia Cameron amekatisha ziara ili akaongelee hili suala bungeni kesho.

Na hapa kwetu, Tanzania pamoja na ukosefu wa umeme, rushwa imeitikisa Wizara ya Nishati na Madilni na kusababisha bunge kutopitisha bajeti ya wizara hiyo. Pinda amesema alikuwa akisubiri Rais Jakaya Kikwete ili aweze "kumshtaki" Katibu Mkuu wa wizara hiyo kutokana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake.

Je, hakuna umuhimu wa Kikwete kukatiza ziara yake na kurudi nyumbani kushughulikia hili suala?
 
EMT ni ngumu sana kuielewa hii nchi na viongozi wake. Hili la umeme JK analiona la kawaida tu, so bora ana miaka 10 ya kumaliza.
Moja kati ya agenda na Cameron ni BAE, wakati kuna bilions zinaibwa na rais hashtuki. Kagoda hajui pesa zipo wapi halafu anatudanganya na BAE.

Hawa akina Jairo na Ngeleja ni sehemu ya uozo uanoendelea serikalini. Kwahiyo JK kwake ni fair.
Nchi ipo gizani miezi sasa Rais anazunguka duniani, So sad!!

Ndiyo maana nasema Lazima watanzania watoe funzo! nadharia haieleweki kwa viongozi wetu.
 
Si anaongoza wafu hivyo arudi kufanyanini wakati wafu aliowaacha wanazikana vema.Cameroon anaongoza watu ndio maana amerudi upesi.
 
Kule Uingereza kuna skandali inayohusu gazeti la News of the World na mapolisi wa UK. Tuhuma hizo zimesababisha Cameron wazir mkuu wa UK akatishe ziara yake South Africa na kurudi kwao. Tanzania iko kwenye tatizo zito la umeme na serikali iko kwenye tuhuma nzito za rushwa. Mkuu wa nchi yeye leo anaendelea na safari ya "KIHISTORIA"ya kwenda kutembelea kisiwa alichosotea Madiba kwa miaka 27. Wana JF nipoozeni kwa maoni yenu kabla sija-collapse kwa msongo wa mawazo..
kwani jk babako hadi upate msongo akiwa hayupo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom