KASHFA TANZANITE ONE YAENDELEA...? Soma...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
UJUMBE MAALUM WA KIZALENDO​


KAMPUNI YA TANZANITE ONE NA UCHIMBAJI WA MADINI

Kuna makampuni mengi yanayojihusisha na uzalishaji wa madini ya tanzanite ambapo kuna makampuni ya kizalendo kama Kilimanjaro Mines, Tanzanite Africa na wachimbaji wadogowadogo. Mbali na makampuni hayo ya kizalendo kuna kampuni kubwa ya TanzaniteOne Mining Ltd ambayo ndiyo kampuni ya kigeni inayojihusisha na uzalishaji na uuzaji wa vito vya tanzanite. Ikiwa ndiyo kampuni kubwa na ya kigeni tunategemea iwe mfano wa kuigwa kwa kampuni ndogo za ndani ili kusaidia kukuza kipato cha Watanzania na kutoa mchango kwenye mapato ya serikali kupitia kodi mbalimbali.

Kampuni ya TanzaniteOne Mining Ltd ni kampuni ambayo haina shughuli za uchimbaji wa madini mahali pengine duniani. Kitu cha kushangaza ni kuhusu mazingira yaliyopelekea kwa kampuni isiyokuwepo mahali popote duniani kupewa dhamana ya kuja kuchimba madini haya Tanzania, ambako wakiwa hawana ujuzi wowote wamepewa dhamana ya kuwa mfano kwa makampuni ya kizawa. Kwa ujanja huo huo wa kupata tenda ya kuchimba madini katika kitalu C waliamua kutumia wazawa ili kujua namna ya kuyapata na kuyachimba madini hayo adimu. Sasa kampuni tuliyotegemea iwe kielelezo bora kwa makampuni mengine imekuwa hatari kuigwa kama mambo inayofanya yakijulikana kwa watu wengine. Kampuni hii inayoonekana kuwanunua baadhi ya viongozi wa serikali imefanikiwa kuvunja sheria kwa kurubuni viongozi hao walafi na wasiokuwa na moyo wa kizalendo.

MATAZIZO NDANI YA KAMPUNI

Tatizo la kwanza la kampuni hii ni ajira. Suala la ajira kwa kampuni hii limekuwa la ajabu sana ambapo sehemu kubwa ya nafasi za juu zimekaliwa na wageni tu. Katika watu zaidi ya ishirini wenye heshima ndani ya kampuni ni Watanzania wasiozidi watatu walio kwenye nafasi za kati. Mbali na watu hao waliopewa nafasi za kiutawala lakini bado hawana nafasi za kimaamuzi katika kampuni isipokuwa wana nafasi za kisiasa ambapo hawashughulishwi kwenye maamuzi mazito. Kwa mfano hakuna kiongozi mtanzania anayeelewa juu ya usafirishaji na uuzaji wa madini hayo. Mfano mwingine ambao unagusa ajira ni wa meneja rasilimali watu ambaye hana nafasi ya kujua suala la ajira za wageni watokao nje ya nchi na wala kuwa na makabrasha yao yanayoeleza juu ya wasifu wao, uzoefu na nafasi zao ndani ya kampuni.

Kisa cha Colin Martin
Kwa sababu hiyo kumekuwa na ujio wa watu wasiokuwa na sifa kwa ajili ya nafasi ambazo zingeweza kushikwa na Watanzania. Suala la ajira za wageni zisizofuata taratibu zimesababisha kuajiriwa kwa mtu asiye na sifa ya kukanyaga ardhi ya Tanzania. Mtu huyo ajulikanaye kwa jina la Colin Martin aliwahi kufanya kazi katika kampuni hii miaka ya nyuma na mwaka 2004 akiwa kama Meneja Usalama (Security Manager) aliua mtanzania kwa risasi. Colin alishikiliwa kwa karibia mwaka mmoja kule Babati na baadae kwa kutumia ujanja na rushwa walifanikiwa kumtoa rumande ambapo alirudi kazini na kuachishwa kazi.

Hiyo ilikuwa kama kufunika kombe mwanaharamu apite, kwani mwaka 2010 Colin Martin alirudishwa tena nchini tena bila vibali vya kazi wala mkataba wa kazi. Na mwanzo wa mwezi wa tisa 2010 alifanya kosa jingine ambalo lingeweza kumtoa mtu uhai kwa kumfyatulia risasi mtanzania aliyekuwa kwenye eneo la kutupa taka za mgodini (dump site) na kumjeruhi kwenye mkono. Kwa kujua kuwa ana kesi nyingine ya kuua kwa risasi huko nyuma aliamua kumtupia kesi askari mtanzania ili ionekane yeye ndiye anayehusika. Maskini askari mtanzania aitwae Sylvester aliamua kukubali kuwa yeye ndiye mhusika wa tukio hilo hali akijua kuwa aliyemfyatulia risasi yule mtanzania ni Colin Martin.

Maaskari wa Kinepali
Waajirwa wengi kutoka nje ni mbumbumbu wasiokuwa na ujuzi wowote zaidi ya ukatili dhidi ya wazawa. Watu wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji sio wahandisi wa kweli bali ni watu waliowahi kufanya kazi za migodini na hasa kwenye eneo la baruti. Kwa sasa kuna maaskari wa Kinepali maarufu kama Ghurkhas kwa ajili ya shughuli za ulinzi. Watu hao katika kuajiriwa wanaitwa risk control officer, lakini huku ndani ya kampuni wanafanya kazi za ulinzi nafasi ambazo zingeweza kushikwa na Watanzania. Cha kushangaza sana ni kuwa Wanepali hao ni wanajeshi katika nchi zao ambao wengine wamekuwa kwenye nafasi mbalimbali. Je, kuna usalama kiasi gani kwa nchi hii kama tunaweza kuruhusu mwanajeshi wa nchi nyingine kuja kufanya shughuli za usalama ndani ya nchi yetu. Kama watu hao ni majasusi tuna usalama gani wa mipaka yetu. Na je, ni kwa kiasi gani tunailinda thamani ya shilingi yetu pale tunapoongeza mahitaji ya dola ya kimarekani huku hakuna haja ya kufanya hivyo? Kwa muono wetu ni kwamba shughuli zisizokuwa na ulazima wa wageni tunahitaji kuzifanya wenyewe badala ya kutegemea wageni. Kwa sasa kuna maaskari wa Kinepali wanaokaribia ishirini wanaopata dola za kimarekani kutoka Tanzania na kupeleka kwao Nepali.

RIPOTI YA UZALISHAJI

Kuficha kiasi kinachozalishwa ili kukwepa kodi

Jambo la pili linaloshangaza juu ya kampuni hii ni ripoti zake za uzalishaji. Kimsingi kampuni hii ambayo ina eneo kubwa kuliko makampuni yote yanayochimba tanzanite ndio kampuni inayoongoza kwa uzalishaji. Ripoti za kampuni zinazozungumzia uzalishaji wa madini hayo unatia mashaka sana kwani hauendani na kinachotoka chini ya ardhi. Siku zote watu hawa wanaficha ukweli wa kile wanachopata ili kukwepa kodi.

Kwa mfano kumekuwa na mfululizo wa uzalishaji wa tanzanite tangu kuanza mwaka huu ambapo zaidi ya kilo 1000 za madini ya tanzanite zimepatikana. Idadi hiyo kubwa inatokana na jumlisho la madini yanayouzika na yale yasiyouzika (tanzanite chafu). Tukisema madini yanayouzika yanafanya theluthi ya madini yote yaliyochimbwa tutapata kama kilo mia tatu (300) za madini yenye thamani ya kuuza. Hii inatokana na rekodi za mifuko ya uzalishaji (production bag) inayopimwa mara baada ya madini hayo kutolewa ardhini. Lakini viongozi wa kampuni hiyo wanashikilia msimamo wao wa kudanganya serikali ili kuendelea kukwepa kulipa kodi. Na wameshikilia kumbukumbu zote za uzalishaji na kukataza mtanzania kuyaona na wala kuhoji juu ya kinachoendelea.

Usafirishaji
Jambo la tatu ni juu ya usafirishaji na uuzaji. Madini hayo yakishapatikana huchujwa kwa mikono na baadae kuondolewa sehemu zilizokatika ili ibaki sehemu inayoweza kukatwa kwa ajili ya vidani. Kampuni hii ambayo inadai kuwa inauza madini ghafi kwenye soko lake huko nje ya nchi ina mtindo wa kibiashara ambapo hakuna mtanzania awaye yote mwenye ufahamu juu ya biashara hiyo isipokuwa wao tu. Madini hayo huwekewa bei hapa ndani na watendaji wa TO wenyewe na kisha kusafirishwa yakiwa hayana thamani kabisa. Kimsingi lebo zao za bei zinaonyesha kiwango cha chini cha bei ukilinganisha na bei inayonunuliwa na wanunuzi wa soko la ndani.

Kwa kuzingatia hilo ni kwa nini kampuni hiyo isitumie soko la ndani kukuza mapato yake kama inauza soko la nje kwa hasara. Hapa kuna mchezo mchafu wa kuficha mapato. Kwa mtazamo wetu ni kwamba kampuni hii ya uchimbaji ina mikono zaidi ya mitatu mmoja ukiwa ndani ya nchi. Huu ndio unaolia umaskini kila kukicha, na mwingine ni ule unaouza kwa faida na kuupa mkono wa tatu kwa ajili ya matumizi ya wajanja. Kampuni hii kwa kutumia ujanja kama ule unaofanywa na DeBeers imeweza kuunda kitu kinachoitwa site holders. Site holders ni watu wanaouziwa madini hayo ya tanzanite mara yanapopatikana. Site holders hawana mahusiano yoyote na serikali isipokuwa kampuni. Mahusiano yao yanaishia wapi sisi hatujui.

Kukwepa agizo la serikali
Serikali ilipitisha sheria ya kuzuia kusafirisha madini ya vito yenye uzani wa zaidi ya gramu moja (1g) kwenda nje ya nchi kabla ya kukatwa. Hiyo ilikuwa ni habari njema kwani ingeweza kukuza mapato ya serikali na makampuni ya ndani yanayochimba madini hayo. Na zaidi hatua hiyo ingeweza kukuza soko la ajira ndani ya nchi na hivyo kukuza mapato ya serikali kupitia kodi na gharama nyingine za kiutendaji. Cha kushangaza habari hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti na wajanja hao wa TanzaniteOne ambapo kwa kutumia mbinu zao zote wametafuta mbinu za kukwepa agizo hilo la serikali. Mchakato huo wa kuiwezesha nchi kunufaika na madini ya tanzanite na vito vingine ulipitishwa na bunge lakini serikali kwa kutumia watendaji wake walafi wameweza kupindua sheria hiyo na kuipa nafasi kampuni hiyo kusafirisha madini bila ya kuyakata.

Ikumbukwe kuwa kampuni hiyo ina mashine chache za kukata madini hayo hapa nchini lakini haitaki kuzitumia na zaidi huzitumia kwa ajili ya watendaji wa TO na marafiki zao tu. Vilevile kampuni hii imewahi kuwa na kitengo cha ukataji madini kijulikanacho kama lapidary lakini walihamishia mitambo hiyo kusikojulikana na kujitambulisha kwa umma kuwa hawafanyi kazi ya kukata madini hayo. Hapa kuna mazingira makubwa yanayoashiria kampuni kutumia rushwa na uongo mwingi ili kuhadaa watendaji wa serikali na hivyo kuwadanganya Watanzania. Mbinu ya kwanza waliyotangaza ni kuwa serikali kama itashikilia msimamo huo basi itasababisha kushusha thamani ya madini hayo na hivyo kushusha mapato kwa kampuni na serikali kwa ujumla. Mbinu ya pili waliyotumia ni kusema kuwa suala la kutaka kukata madini ya tanzanite ndani ya nchi ni njama za madalali (brokers) ili waweze kuidhoofisha kampuni kwa kununua madini yake. Hii ni chuki iliyo wazi ya watendaji wa TO dhidi ya Watanzania, kwani siku zote hawataki kuona Watanzania wanaendelea. Chuki hiyo inadhihirishwa na mtendaji mkuu wa kampuni pale anaposema watu wanataka kuona eneo hili linaenda mikononi mwa Watanzania, lakini yeye anasema kuwa hawezi kukubali kuona wao wanapoteza eneo hili mikononi mwa Watanzania.

Akizidi kusema bila hofu wala haya anasisitiza kuwa wao wakiondoka Tanzania nzima itahamia kwenye eneo hilo. Hiyo inathibitisha kuwa anafahamu kuwa thamani ya kitalu hicho ni ya kuweza kuihudumia nchi hii yote. Mbinu ya tatu waliyototumia ni kukwepa mjadala wa hadhara uliofanyika kati ya wajumbe wa wizara chini ya katibu mkuu na wadau wengine wa madini ya tanzanite ikiwemo kampuni ya TanzaniteOne. Mkurugenzi wa kampuni (sasa COO) hiyo anayejulikana kwa jina na Zane Swanepoel akishirikiana na mwenyekti wa bodi ya wakurugenzi ambaye amewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ndugu Ami Mpungwe waliomba kukutana na katibu mkuu wa wizara akiwa peke yake pasipokuwa na wajumbe wengine ili wazungumze nae.

Walikubaliwa na wakapewa ratiba ya kuonana naye Mwanza tarehe 9 ya mwezi wa nane mwaka 2010 kwa ajili ya maongezi ya siri. Bila shaka mazungumzo yao yaligubikwa na rushwa ili kufanikisha azma yao ya kukwepa kodi na kuikosesha serikali mapato yatokanayo na mauzo ya vito hivyo adimu duniani. Inavyoonyesha kuna matumaini yaliyopatikana kutokana na ziara hiyo ya wakuu mkoani Mwanza kwani baadae kidogo kuna tamko lililotolewa na mkurugenzi wa TanzaniteOne juu ya kukuza uzalishaji kwa kipindi cha miezi miwili ijayo. Chini ya mpango huo kampuni imeelekeza nguvu zake kwenye maeneo ya uzalishaji tu na kusimamisha maeneo ya utafiti ili kuisaidia kampuni kupata mawe ya tanzanite katika kipindi walichoruhusiwa kuvusha mawe hayo bila kuyakata. Jukumu la kukuza uchumi wa nchi liko mikononi mwa Watanzania kwa hiyo tukiwa kama Watanzania wenye upeo wa kuyaona haya tunayohaki ya kuyafichua na kuieleza serikali juu ya mambo yanayofanywa na watendaji wake yanayoifanya nchi kuendelea kuwa masikini.

Tunaomba ieleweke kuwa sehemu kubwa ya madini ya tanzanite hukatwa nchini India katika mji wa Jaipur. Na kuna habari kuwa mji huo mkubwa wa India unatengeneza mapato yake kwa asilimia arobaini kutokana na shughuli za biashara ya tanzanite. Kupitia kukata na kuuza vito mji wa Jaipur umekuwa ndio sehemu ya kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa madini hayo na hivyo kuutengenezea mapato yanayokaribia asilimia arobaini (40%) ukilinganisha na mapato mengine. Kuna aina nyingine za madini zinazokatwa ndani ya mji huo lakini tanzanite inakatwa kwa wingi ukilinganishwa na aina zingine ambapo theluthi moja ya vito vyote hutokana na tanzanite. Ukizingatia kuwa kuna zaidi ya aina thelathini ya vito vinavyopatikana duniani, lakini kwa tanzanite kufanya asilimia thelathini na tatu (33%) ya vito vingine inaashiria ni kwa kiasi gani madini hayo yanapelekwa kwa wingi nchini India. Je, kwa picha hiyo tuliyonayo ni manufaa gani ambayo Tanzania inayapata kutokana na kuwa nchi pekee yenye ardhi inayotoa madini ya tanzanite?

UBAGUZI WA RANGI
Tatizo jingine la kuangalia juu ya kampuni hii yenye asili ya Afrika Kusini ni juu ya tabia ya watendaji wa TO ya kuwabagua watu weusi. Hakuna haki kabisa kwa mtu mweusi kuanzia kwenye mishahara hadi kwenye huduma za msingi zinazopaswa kutolewa na kampuni kwa wazawa. Kampuni hii imeamua kuwatumia wafanyakazi wazawa kama maroboti ya uzalishaji ambapo baada ya kuzalisha mali huitwa majambazi na maadui wakubwa wa kampuni. Ikiwa hakuna uzalishaji wafanyakazi husifiwa na kupewa heshima kama watu wa muhimu kwa ajili ya kampuni, tatizo hujitokeza pale inapotokea kuwa tanzanite imepatikana, hapo ndipo ubaguzi wa wazi hujitokeza kwani mtu awaye yote ilhali akiwa na rangi nyeusi basi hatakiwi kuonekana eneo la uzalishaji hata kama ni askari wa kampuni.

Cha kushangaza ni pale ambapo hata wafanyakazi wenye nafasi za juu katika kampuni ambao hufukuzwa huku wakiitwa ni wezi wakubwa. Hali hiyo ya unyanyasaji haiishii hapo kwani wakitoka hapo baada ya kuchukua kile walichokuwa wakikitafuta huenda kusema kwa serikali kuwa uzalishaji ni mdogo kwa kuwa sehemu kubwa ya madini inaibwa na Watanzania. Hicho ni kichekesho, kwani hao Watanzania wanaosingiziwa kuiba hawaruhusiwi kufika eneo la uzalishaji mpaka hapo mtendaji anapokuwa ameridhika kuchukua kile alichokiona. Na jambo jingine la kushangaza ni pale ambapo utaratibu unaotumika kuwaingiza Watanzania kwenye eneo la kazi ambapo wakiingia hupangwa na kila mmoja kupewa msimamizi wa kumuangalia ambapo kazi hiyo hufanywa na maaskari wa Kinepali.

Watu hao huwasimamia watu kwa kuwanyanyasa ambapo akikuhisi kuwa vibaya anakufukuza eneo la kazi na pengine kuhatarisha kibarua kabisa. Kama mtu ungebahatika kuangalia picha ya jinsi kazi zinavyofanyika na jinsi watu wanavyosimamiwa usingeweza kutofautisha na zama za ukoloni. Ubaguzi mwingine unaofanywa na kampuni kwa wazawa ni wa huduma za msingi kwa wafanyakazi kama chakula. Kwa wafanyakazi wanaofanya kazi chini (underground) ni Watanzania wachache ambao hupewa huduma ya maji wawapo chini. Watanzania hao ni wale manyapara wa wenzao (supervisors) ambao hawafiki kumi na nne. Hebu fikiria kwa mtu anayeshinda chini huku akifanya kazi nzito za kutoka jasho kama maji anapelekewa vipande vya mkate bila maji. Huu ni unyanyasaji mkubwa sana kwani watu hao wanafanya kazi kuanzia saa moja mpaka saa kumi jioni.

Pamoja na hayo yote yanayofanywa na kampuni hiyo ya kigeni bado serikali inaamini juu ya ripoti zake za kuwatukana wafanyakazi Watanzania kwa kuwaita wezi wanaoiibia kampuni na kuipotezea serikali mapato kutokana na hasara inayopata kampuni. Tunapenda serikali ielewe kuwa kampuni hii imejaa wezi wakubwa wanaoiba mali za nchi na Watanzania. Kampuni hii ikiwa imejitengenezea vibaraka miongoni mwa Watanzania wenye nafasi zao za kutumikia umma imefanikiwa kuvunja sheria kadha bila hatua stahili kuchukuliwa.

Matumizi mabaya ya cheo ya Wessel Marais
Kwa mfano suala la ajira za wageni zinafanywa kwa mgongo wa mtu mmoja anyeitwa Wessel Marais ambaye awali alikuwa msaidizi wa meneja (Ass General Manager) kabla ya kuwa Risk Manager. Akiwa kwenye nafasi zote hizo amekuwa akifanya kazi zote kama meneja mwajiri (Human Resource Manager) na wakati huo huo kama meneja manunuzi (Logistic Manager). Kwa nafasi yake hiyo hutoa ajira kwa wageni bila kumshirikisha meneja mwajiri (HR) na kutengeneza vibali vya wageni hao kwa kuvunja taratibu. Kwa mfano maaskari wa Kinepali wajao nchini hujaziiwa fomu na yeye mwenyewe na kuweka saini zote yeye mwenyewe na kupeleka serikalini kwa ajili ya kuwaombea vibali vya kazi.

Mara nyingine wageni huja kufanya kazi bila hata vibali na kukaa hapa bila ruhusa huku wakichapa kazi na kulipwa mishahara. Matatizo ndani ya kampuni hii ni mengi na hayawezi kuelezeka kwa siku moja. Lakini tunahitaji serikali iweze kuchukua hatua za haraka kabla hali haijawa mbaya na kubaki historia. Katika uchunguzi wetu tuliofanya tumegundua uhai wa machimbo hayo unaweza usivuke miaka kumi kutoka sasa. Na tumeshuhudia miaka 42 ya uchimbaji wa tanzanite usiokuwa na tija kwa mtanzania huku maeneo mengi yanayozunguuka machimbo hayo yakizidi kuwa duni na Jaipur ikizidi kung'arishwa na madini hayo. Je, miaka michache iliyobaki kabla ya machimbo hayo kufungwa na Tanzania kusahaulika katika uzalishaji wa madini hayo, tumejipanga vipi katika kufaidika na mali asili hii?

Dharau dhidi ya Watanzania
Suala la mwisho kujadili kwa leo ni dharau ya watendaji wa TO dhidi ya Watanzania inayojidhihirisha kwa kauli zao kwa wafanyakazi Watanzania. Moja ni kuwaita Watanzania wezi wa tanzanite. Kila mfanyakazi mweusi anaitwa mwizi na pengine huitwa majangili kwa kiswahili. Pili ni suala la mkurugenzi wa kampuni, Zane Swanepoel kuwaita wafanyakazi kuwa ni panya pori pale walipogoma kusikiliza mafunzo ya kuchomwa mionzi. Wafanyakazi walipeleka malalamiko yao bungeni na serikali ikatoa tamko lililomzuia mwekezaji kuacha kutumia mionzi katika kuwakagua wafanyakazi wake. Tamko hilo lilifuatia kamati ya madini ya bunge kuunda tume ya wataalamu kuchunguza madhara ya mashine hizo za mionzi kisha itoe ripoti. Kabla ya ripoti kutolewa ndipo mkurugenzi akakurupuka na hiyo semina. Wafanyakazi walihoji juu ya uhalali wa mafunzo ya mionzi huku ikiwa haina kibali cha kutumika na ndipo kaburu aliwatolea maneno ya kejeli na kuwaita panya (mice).

Baada ya malalamiko ya wafanyakazi kuhusu madai yao ya kutokaguliwa kwa mionzi na suala la kutukanwa, aliulizwa kama ana kibali cha serikali kinachomruhusu kutumia mionzi katika kufanya ukaguzi na yeye akajibu kwa dharau kwamba 'the parliament does not run the mine', hiyo inaashiria wazi ni kwa kiasi gani amejijengea himaya kiasi cha kudharau bunge tukufu la Tanzania kuona kuwa halina amri juu ya shughuli zake. Kutokana na udhalili huo, wafanyakazi waliamua kumfungulia mashtaka mahakamani, kesi ambayo inazungushwa kwa takribani miezi mitano sasa. Na haikuishia hapo kwani baada ya malalamiko ya wafanyakazi kutua kwa mwenyekiti wa bodi ndugu Ami Mpungwe alikuja na kukutana na wawakilishi wa wafanyakazi ambapo kauli yake kubwa ilikuwa kuwa Zane yuko Tanzania kufanyakazi na kukaa, asiyekubaliana nae ndiye anatakiwa aache kazi kwani kampuni inamuamini.

Na alizidi kusema kuwa yeye hakuja kuzungumza na wafanyakazi kwani wao si wa hadhi yake na akawataka wakome kumsumbua mtu wao Zane ili afanye kazi zake. Alizidi kusema kuwa vurugu za wafanyakazi wa TanzaniteOne zinajulikana kuanzia ngazi ya kijiji mpaka ngazi ya taifa ambapo zimejadiliwa kwa marefu na mapana. Hiyo inadhihirisha wazi ni kiasi gani hawa watu wamejipanga kuwaumiza Watanzania kwa kutumia migongo ya Watanzania wachache.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

From Reliable Sources: MMM
 
haya mambo yanaendelea kwenye kampuni nyingi tu za madini na hata makampuni makubwa makubwa ya utalii. Makaburu ni wengi wanachokifanya hakuna na mishahara mikubwa mikubwa. I dont know who let in these pple to TZ.

Ubaguzi ni nature yao wao kubadilika ni jambo litakalochukua muda mrefu sana. They should just go to where they came from.
 
Anko Ben aliwaleta hawa jamaa wakatili, wanyanyasaji na wenye dharau.
 
Protests as govt exempts firm from raw tanzanite ban

stonepix.jpg

The Tanzanite. File Photo
By Adam Ihucha (email the author)
Your Email Message Send Cancel


Posted Monday, September 27 2010 at 19:02

Tanzania has lifted the July ban on exports of raw tanzanite for commercial mining firm TanzaniteOne much to the dismay of other players.
Minister for Energy and Minerals William Ngeleja said the ban was relaxed to allow TanzaniteOne ample time to build capacity.
Mr Ngeleja says the firm asked to be allowed to export at least 50 per cent of its stockpile of rough gems larger than five carats in size.
After consultations with key industry players, he says, the state lifted the sanctions until December 31.
"It's my hope that by December 31, the domestic processing industry will be developed to polish the entire gemstone production locally", Mr Ngeleja explained.
But key players in the gemstone industry see the London Stock Exchange-listed TanzaniteOne as trying to establish a monopoly on the $500 million tanzanite industry at the expense of local small-scale firms.
Manyara Regional Miners Association (Marema) secretary-general Abubakari Mollel said the move amounted to the government supporting TanzaniteOne to form a monopoly on the most lucrative tanzanite industry.
Mr Mollel argues that TanzaniteOne firm now will take advantage of the suspension to solidify its control over newly mined tanzanite.
"What they will do is to purchase much of the top-grade tanzanite on the secondary market from the desperate small-scale-miners and combine with their substantial production to flood the world market at the expense of poor local dealers," Mr Mollel said.
He termed the move absurd adding that it had shattered their hopes of a fair playing field in the tanzanite industry.
The Tanzania Mineral Dealers Association (Tamida) that fought for nearly eight years to have the sanction in place says the ban relaxation is unjust to local small-scale polishers.
"It is discouraging small-scale Tanzanite dealers who were keen on increasing capacity of the industry to polish raw gems locally," Tamida chairman Sammy Mollel told The EastAfrican in Arusha.
For TanzaniteOne, the temporary suspension is welcome news as it is expanding its in-house cutting and training capabilities through existing relationships with overseas experts, in addition to entering into agreements with external beneficiation companies in Tanzania.
Until a few years ago, TanzaniteOne was said to account for at least 35 per cent of the total tanzanite exports and the remainder by other exporters, mainly small and medium scale companies.
 
Kuna siku niko cassino Mwanza, jamaa walikuja nikasikia wanasema kwa sauti ya chini "This country is so good, the taxes are almost free and alot of minerals they have gold, Diamond, Tanzanite, copper and silver"

Yaani jamaa wanashangilia kila siku kuwepo hapa. Jamani tusisahau october 31, Dr Slaa for presidency.
 
Baada ya malalamiko ya wafanyakazi kuhusu madai yao ya kutokaguliwa kwa mionzi na suala la kutukanwa, aliulizwa kama ana kibali cha serikali kinachomruhusu kutumia mionzi katika kufanya ukaguzi na yeye akajibu kwa dharau kwamba 'the parliament does not run the mine', hiyo inaashiria wazi ni kwa kiasi gani amejijengea himaya kiasi cha kudharau bunge tukufu la Tanzania kuona kuwa halina amri juu ya shughuli zake. Kutokana na udhalili huo,
the parliament doesnt run the mine, HAYO NI MAJIVUNO MACHACHE yatolewayo na hawa wakezaji uchwara wanaolindwa na mfumo FISADI, ambao umelelewa na wapuuzi ndani ya serikali hii inayoendweshwa na chama cha Mapinduzi.
Inafadhaisha sana, wawekezaji ni miungu watu, hawaguswi, nakumbuka Chacha Wangwe alikua sauti yhai pekee kule migodini, alikemea, aliwapigania watu wake, tangu afariki hakuna mwingine aliejitokeza waziwazi kuwapigania.
 
Huko nyuma kampuni hiyo ikiitwa jina jingine Mkuu Wa mkoa wa Arusha wa wakati huo alidiriki kutamba kuwa kama kampuni hiyo ikiondolewa yeye yupo tayari kujiuzulu kazi ya ukuu wa Mkoa. Kipindi hicho kilikuwa cha Mkapa na njemba hii Jk aliiona inafaa sana hata akiteua Ukuu huohuo wa Mkoa na sasa hivi yuko Rukwa.

Dawa ya matatizo yetu ni kumtimua JK na CCM yake kazi na mengineyo yatafuatia
 
dawa ni kubadili uongozi. chagua serikali yenyenia ya ukombozi wa kweli (uchungu na nchi na siyo matumbo yao)
 
Kuna siku niko cassino Mwanza, jamaa walikuja nikasikia wanasema kwa sauti ya chini "This country is so good, the taxes are almost free and alot of minerals they have gold, Diamond, Tanzanite, copper and silver"

Yaani jamaa wanashangilia kila siku kuwepo hapa. Jamani tusisahau october 31, Dr Slaa for presidency.

"Educate and inform the whole mass of the people…. They are the only sure reliance for the preservation of our liberty."
 
Hii kampuni Kikwete ni mmoja ya board member..

sasa lazima alinde interest zake.... tusubiri slaa na zitto atafanyia kazi hilo..
 
Thanks MMM

its worth reminding each other kila wakati haya mambo muhimu.... we have to defend our rights and our grand children rights whose !d!ots and criminals like collins play with and molest
 
Kuna siku niko cassino Mwanza, jamaa walikuja nikasikia wanasema kwa sauti ya chini "This country is so good, the taxes are almost free and alot of minerals they have gold, Diamond, Tanzanite, copper and silver"

Yaani jamaa wanashangilia kila siku kuwepo hapa. Jamani tusisahau october 31, Dr Slaa for presidency.

kuna tetesi kuwa wafanyakazi watapunguzwa....
 
Back
Top Bottom