Kashfa nzito: Malipo hewa kwa wabunge na ubadhilifu wa pesa bungeni waanikwa na CAG

Hiyo ramani iliyochorwa na mafisadi ni pana sana! Kwanza wanatuhamisha kwenye hii inshu ya mawaziri, then tutaona inshu iko complex na hivyo tutaamua kuwa wapole kama kawaida yetu wabongo. Hapa cha kufanya ni M4C ikaze mwendo kuelimisha wananchi ila naimani kubwa kuwa baada ya CCM kuanguka kifo cha mende, kuna viongozi wengi watamalizia maisha yao jela au kufilisiwa vibaya. Time will tell!!
 
Ninachojua ni kwamba bunge lilijadili ripoti za kamati mbalimbali zilizowasilishwa Bungeni wakitumia ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali kama ushahidi wa kuhalalisha madai yaliyoko kwenye ripoti zao, LAKINI hiyo ripoti ya CAG kwenye kipengele cha Bunge huwa inawasilishwaje? Kama hili nalo likifuatiliwa kwa umakini kuna watu wanahusika na hayo mambo? siyo wabunge wote wanajua matumizi hayo ya mhili huu wa bunge, kwa harakaharaka wanaoliongoza hilo bunge ambako kuna hayo madudu watoe majibu! Tanzania itapona kweli?
 
Utoh(22).jpg
Anne%20Makinda(3).jpg

Kushoto (CAG), Ludovick Utouh Kulia Speaker Anne Makinda

Malipo hewa kwa wabunge yabainishwa

Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Ludovick Utouh, amebaini kulipwa kwa posho ya kujikimu Sh. 6,960,000 wabunge wakati hawakuwa mjini Dodoma.

Hayo yapo katika ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka jana, iliyowasilishwa katika mkutano wa saba wa Bunge. Pia alisema Sh. 20,915,126 zililipwa kwa wafanyakazi kinyume cha kanuni za Bunge na mwongozo wa utumishi.

Utouh alisema uongozi uliripoti kuwepo kwa madeni katika taarifa ya fedha ambayo ni Sh. 209, 010,235. Alisema madeni hayo ni kinyume cha mfumo wa bajeti ambayo unatumiwa na serikali.

Aidha, malipo yenye thamani ya Sh. 163,195,130.34 hayakuwa na nyaraka zinazostahili kama kanuni ya 94 (4) ya kanuni ya fedha za umma ya mwaka 2001. Pia ukaguzi huo umebaini posho za muda wa ziada wa kazi na posho nyingine zinazofikia Sh. 94,000,000 zililipwa kwa wafanyakazi wa Bunge.

Pia alisema madurufu ya safari (imprests) yenye thamani y a Sh. 65,803,144 hayakurudishwa kwa mwaka mzima kinyume na kanuni namba 103 (1) (7) ya kanuni ya fedha za umma ya mwaka 2001 ambayo inataka madurufu ya awali kurudishwa kabla ya kutoa mapya.
Aliongeza kuwa marejesho yanatakiwa kurejeshwa siku 14 tangu mfanyakazi aliporejea kutoka safari ambayo aliombea madurufu. Ripoti hiyo imeonyesha kuwa matumizi ya sh 170,858,030, vocha za malipo zilikosekana.Katika ripoti hiyo kunabainisha kuwa uongozi wa Bunge ulinunua mashine ya kuchapisha kwa gharama ya sh 370,019,894 lakini haikufanya kazi.

Hivyo, ilisababisha uongozi wa Bunge kukodisha mashine nyingine kwa malipo ya Sh. 190,480,496 kwa mwaka. Hali kadhalika uongozi wa Bunge, haukuweka kumbukumbu sahihi kama vile za orodha ya mali zisizohamishika hali inayosababisha mapungufu mbalimbali.
Alizitaja kuwa ni magari mawili yaliyosajiliwa kwa namba STK 8590 aina Toyota Land Cruiser Hardtop na STK 3039 Toyota LandCruisser hazikuwekwa katika orodha ya mali zisizohamishika. Magari hayo yalishushwa thamani ya mali kwa kuwekwa katika taarifa ya fedha.

Safi sanaaa katika orodha aliyotoa wamo Zito kabwe,Sugu,Mdee,Mbilinyi,Zambi,Makamba,Makala,hawakurudisha masurufu ya safari
 
Mkuu, hapo kwenye red, hizo ni mali zinazohamishika, labda ndo maana hazikuwekwa kwenye orodha ya mali zisizohamishika.

Nilishangaa jana wabunge katika kipindi cha kuhitimisha bunge walikuwa wapole isivyo kawaida kumbe (CAG), Ludovick Utouh kawafunga goli la tikitaki.

Kama taarifa ya CAG ilikuwa pia na ripoti dhidi ya Wabunge hapa kuna maswali mengi sana! Yaani hata Zitto hajasema lolote juu ya hili? Hapa kazi ipo!
 
Kule bungeni nako kuna madokta na maprofessor...wote ndo wale wale...wezi na wadokoaji pale inapowezekana...lakini sio kama mawaziri....mhhh

Kwani mawaziri sio wabunge? kwi kwi kwi teh teh teh!
 
1. Watajwe hao wabunge na wafanyakazi husika
2.Masurufu na si madurufu.
3.Kama mtu kapewa masurufu(imprest) na hajafanya marejesho(retirement/settlement), kwa nini inaonekana kwenye vitabu vya fedha kama madeni wakati mfumo ni kumkata yule mtumishi kwenye mshahara wake kiasi kile kile ailichopewa?Naomba kueleweshwa hapo.

Iwapo wabunge wangekuwa wamepokea hizo fedha yasingekuwa malipo hewa.

Yanaitwa malipo hewa kwa sababu kuna mtu amekaa ofisini akatengeneza orodha ya wabunge waliolipwa kisha akatia fedha mfukoni mwake. Kama wabunge wamepokea fedha wakati hawakustahili basi wanatakiwa warudishe chenji na wawajibike pia ikiwa ni pamoja na ofisi ya bunge
 
Hivi watu wanaokazana kusema wabunge wamekuwa wapole mara akina Zito, Mbowe, Mnyika etc wamo ndani. Hivi hawaelewi au makusudi kutuchelewesha kwenye m4c. Mbona hata mimi mwl wa kata nimelielewa hilo la malipo hewa?
 
DUH! WABUNGE WAMEZIBWA MIDOMO! na nawaambia subirini mtaambiwa Mbowe, Zitto wamo humo! dah! kweli HATUTAFIKA kama wananchi wakiandamana maji ya washa washa na mabou ya machozi na wabunge nao wanazimwa kama hivi! KAZI IPO Tanzania!

Ofisi ya bunge na si mbunge mmoja mmoja. Hapa unazungumzia kashilia na vijana wake inckding bi mkora.
 
Hapa ndipo tatizo lilipo CAG kesha jirekebisha anajaribu kufanya checks zake rightly, but then, the next responsible body PCCB ndio uzushi unapoanzia si jukumu la bunge tena hapa kama kumetokea namna. Kwanini hawa PCCB hawaendelezi uchunguzi na kuna hitilafu tayari, you see this is where the problems begin na katiba ya accountability inapohitajika hawa jamaa PCCB ni problem kubwa mno nao.
 
Hiyo ni taarifa ya Mkaguzi wa fedha wa serikali, taarifa hiyo imesomwa siku ya mwisho ambapo wabunge hawakupata nafasi ya kuchangia kutokana na ratibu kutoruhusu. Tusubiri bunge lijalo tuone kama wabunge watamvimbishia mishipa bila Mkola na Katibu wake.
 
Kama taarifa ya CAG ilikuwa pia na ripoti dhidi ya Wabunge hapa kuna maswali mengi sana! Yaani hata Zitto hajasema lolote juu ya hili? Hapa kazi ipo!

Kweli hata mie nashangaa hata Mbowe na Tundu Lissu hawajasema juu ya hili.
 
Back
Top Bottom