Kashfa nzito chuo cha polisi moshi hadi kifo cha askari polisi

Shujaa huyo Amefia Kazini Kama Daudi Mwakosi

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
:embarassed2:habari ambazo nimezipata toka kwa kaka yangu anayehudhuria mafunzo ya kupandishwa cheo katika chuo cha polisi moshi (ccp). Ni kuwa siku ya jana chuoni hapo ilikuwa ni majonzi makubwa kwa askari wanaohudhuria course mbalimbali chuoni hapo. Majonzi hayo na vilio vilitawala pale mwili wa askari mwenzao aliyekuwa akihudhuria mafunzo ya ngazi ya corpolo kutokea mkoani manyara. Askari huyo alifariki dunia kwa prssure na kisukari. Sasa basi kilichipelekea kuwepo na vilio vingi na lawama za hapa na pale ni kwamba: Askari huyo ambaye kwa sasa ni marehemu na mungu amlaze mahali pema, hakuhudhuria kipindi chuoni hapo kwa vile alikuwa na mapumziko aliyopewa na daktari wa chuo ( ed ). Baada ya kutafutwa wasiohudhuri vipindi ikaonekana na yeye hakuhudhuria hivyo afisa mmoja aliyetajwa kwa jina la jb ibrahim mwenye cheo cha mrakibu mwandamizi (asp), na ambaye ni adjutant hapo chuoni. Afisa huyo bila hata kumsikiliza askari huyo na bila hata kuangalia cheti toka kwa daktari kama kweli amepewa mapumziko. Pamoja na kulalamika kuwa anayo ed bila huruma na bila ubinadamu na bila kutumia busara na bila kutumia akili kama afisa wa polisi mwenye cheo na madaraka makubwa kama hayo. Afisa huyo aliamuru askari huyo awekwe mahabusu kwa kosa hilo. Kitendo cha kuwekwa mahabusu askari huyo kilipelekea afya yake kubadilika ghafla na akiwa ndani ya mahabusu hiyo ni wenzake ambao walitoa taarifa kuwa kuna mgonjwa ndani amezidiwa na ndipo askari waliokuwa zamu wakatoa taarifa na kumkimbiza hospital ambako ndiko alikotwaliwa na muumbaji na ikwa ndiyo mwisho wake.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi waliopo chuoni hapo wamehuzunika sana na baadhi yao wamesikika wakisema ni vyema mkuu wa jeshi afanye uchunguzi wa kina wa swala hilo. Inasemekana pia afisa huyo ameonyesha kutokuwa na uelewa wa maamuzi yake katika kila kona ya chuo hicho na kuonekana kama antafuta sifa au kujipendekeza kupandishwa cheo haraka. Pamoja na hayo wameomba kwamba mara mkuu wa polisi atakapofika chuoni hapo wiki hii kuhitimisha mafunzo ni vyema akaondoka na ofisa huyo na kwenda kumpa kazi nyingine huku akifanya uchunguzi wa jambo hilo. Kuendelea kuwepo hapo chuoni ni kuharibu nidhamu ya askari na jeshi zima la polisi. Kitendo cha kumuweka askari mwenzake mahabusu huku akiwa mgojwa na ugonjwa ambao tayari daktari amethibitisha ni kufundisha nini askari ambao watakwenda sasa kuwa karibu na wananchi na endapo watamkamata mwananchi ana kosa na ni mgonjwa je atasalimika. Naomba ndugu zangu hasa waandishi wa habari mlioko humu mnisaidie kupaza sauti ili tukomeshe tabia kama hizi. Huyu ni kiongozi ambaye anatoa mafunzo kwa askari wa nchi nzima. Je kuna haja ya ofisa huyo kuendelea kuwepo chuoni hapo? Tafadhalini tusaidiane.

nyani kula ya tumbili ni sawa na tumbili kula ya nyani ni sawa sasa panya kala ya nyani na tumbili ameharibu, ungejua hampendeki uraiani, basi ungekaa kimya, ujinga aliofanyiwa (wala siyo unyama)ndo ujinga NA UNYAMA mnaoufanya kwa raia. ASKARI ANAPASWA KUWA RAFIKI WA RAIA LAKINI NYIE MMEGEUKA KUWA ADUI
 
Hiyo siyo kashfa ni utii wa sheria bila shuruti
Jingine ni kwamba hata sisi mnapotushambulia kwa risasi na mabomu na kutuua huwa tunasikitika hivyo2- isiwe mkuki kwa nguruwe tu.
 
:embarassed2:Habari ambazo nimezipata toka kwa kaka yangu anayehudhuria mafunzo ya kupandishwa cheo katika Chuo Cha Polisi Moshi (CCP). Ni kuwa siku ya jana chuoni hapo ilikuwa ni majonzi makubwa kwa askari wanaohudhuria course mbalimbali chuoni hapo. Majonzi hayo na vilio vilitawala pale mwili wa askari mwenzao aliyekuwa akihudhuria mafunzo ya ngazi ya corpolo kutokea mkoani Manyara. Askari huyo alifariki dunia kwa prssure na kisukari. Sasa basi kilichipelekea kuwepo na vilio vingi na lawama za hapa na pale ni kwamba: Askari huyo ambaye kwa sasa ni marehemu na mungu amlaze mahali pema, hakuhudhuria kipindi chuoni hapo kwa vile alikuwa na mapumziko aliyopewa na daktari wa Chuo ( ED ). Baada ya kutafutwa wasiohudhuri vipindi ikaonekana na yeye hakuhudhuria hivyo Afisa mmoja aliyetajwa kwa jina la JB IBRAHIM mwenye Cheo cha Mrakibu mwandamizi (ASP), na ambaye ni Adjutant hapo Chuoni. Afisa huyo bila hata kumsikiliza askari huyo na bila hata kuangalia cheti toka kwa daktari kama kweli amepewa mapumziko. Pamoja na kulalamika kuwa anayo ED bila huruma na bila ubinadamu na bila kutumia busara na bila kutumia akili kama afisa wa polisi mwenye cheo na madaraka makubwa kama hayo. Afisa huyo aliamuru askari huyo awekwe mahabusu kwa kosa hilo. Kitendo cha kuwekwa mahabusu askari huyo kilipelekea afya yake kubadilika ghafla na akiwa ndani ya mahabusu hiyo ni wenzake ambao walitoa taarifa kuwa kuna mgonjwa ndani amezidiwa na ndipo askari waliokuwa zamu wakatoa taarifa na kumkimbiza hospital ambako ndiko alikotwaliwa na Muumbaji na ikwa ndiyo mwisho wake.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi waliopo Chuoni hapo wamehuzunika sana na baadhi yao wamesikika wakisema ni vyema mkuu wa jeshi afanye uchunguzi wa kina wa swala hilo. Inasemekana pia afisa huyo ameonyesha kutokuwa na uelewa wa maamuzi yake katika kila kona ya chuo hicho na kuonekana kama antafuta sifa au kujipendekeza kupandishwa cheo haraka. Pamoja na hayo wameomba kwamba mara mkuu wa polisi atakapofika chuoni hapo wiki hii kuhitimisha mafunzo ni vyema akaondoka na ofisa huyo na kwenda kumpa kazi nyingine huku akifanya uchunguzi wa jambo hilo. Kuendelea kuwepo hapo chuoni ni kuharibu nidhamu ya askari na jeshi zima la polisi. Kitendo cha kumuweka askari mwenzake mahabusu huku akiwa mgojwa na ugonjwa ambao tayari daktari amethibitisha ni kufundisha nini askari ambao watakwenda sasa kuwa karibu na wananchi na endapo watamkamata mwananchi ana kosa na ni mgonjwa je atasalimika. Naomba ndugu zangu hasa waandishi wa habari mlioko humu mnisaidie kupaza sauti ili tukomeshe tabia kama hizi. huyu ni kiongozi ambaye anatoa mafunzo kwa askari wa nchi nzima. je kuna haja ya ofisa huyo kuendelea kuwepo chuoni hapo? Tafadhalini tusaidiane.
Pamoja na kwamba sipendi utekelezaji kazi wa Polisi wetu bado sijaliona kosa la Adjutant huyu kijeshi. Nitamshangaa Mwema kama atalichukulia hili kisiasa kwani kijeshi hata kama askari anaumwa anatakiwa kufuata "procedure" yaani baada ya kuandikiwa hiyo uliyoiita ED (Kijeshi ni "C" I mean TPDF) alipaswa kuripoti kwenye mamlaka zilizo juu yake kwamba amepewa "Remark" hiyo, na kuruhusiwa rasmi kwenda mapumzikoni huku mamlaka ikilijua hilo fika. Kitendo cha kutafutwa na Adjutant hadi kuwekwa ndani kinadokeza hali ya uongozi kutojulishwa rasmi na kwa kweli Adjutant alifanya alichatarajiwa; haswa ikizingatiwa ni Adjutaant wa chuo kinachofundisha pia nidhamu ya kijeshi katika Jeshi la Polisi. Kama ni kifo kingemkuta hata kule ndani alikokuwa alikokuwa amelala bila ya mamlaka kujua. Kulalama ovyo namna hii ndiko kunakolifanya hilo mnaloliita Jeshi la Polisi kutoa wahitimu wa ovyo ovyo wanaoliaibisha baadae.
 
Kuna watu mmekariri mambo kama maroboti. Yule ni koplo siyo kuruta, naamini anafahamu taratibu zote, kumuumiza askari ili vita ikitokea awe mkakamavu nani kasema?b akirudi mtaani anakuwa raia tu mabia, kitimoto full kitambi.

Nadhani huyo adjutant sio kwamba hakuwa sahihi ila kuna mazingira ya kutoa adhabu na kutotoa adhabu au kuweka adhabu mbadala! Hivyo ni vitu muhimu sana. Sio kukariri tu, kazi haziendi hivyo pamoja ya kuwa yawezekana huyo koplo alikosea lakini kwa hali yake ya ugonjwa angemsikiliza! Mambo ya tekeleza amri malalamiko baadae huwa yanawacost viongozi wengi wa kijeshi, jitahidini kutumuia busara zaidi na sio kukariri PGO iliyotungwa na mkoloni.
 
:embarassed2:Habari ambazo nimezipata toka kwa kaka yangu anayehudhuria mafunzo ya kupandishwa cheo katika Chuo Cha Polisi Moshi (CCP). Ni kuwa siku ya jana chuoni hapo ilikuwa ni majonzi makubwa kwa askari wanaohudhuria course mbalimbali chuoni hapo. Majonzi hayo na vilio vilitawala pale mwili wa askari mwenzao aliyekuwa akihudhuria mafunzo ya ngazi ya corpolo kutokea mkoani Manyara. Askari huyo alifariki dunia kwa prssure na kisukari. Sasa basi kilichipelekea kuwepo na vilio vingi na lawama za hapa na pale ni kwamba: Askari huyo ambaye kwa sasa ni marehemu na mungu amlaze mahali pema, hakuhudhuria kipindi chuoni hapo kwa vile alikuwa na mapumziko aliyopewa na daktari wa Chuo ( ED ). Baada ya kutafutwa wasiohudhuri vipindi ikaonekana na yeye hakuhudhuria hivyo Afisa mmoja aliyetajwa kwa jina la JB IBRAHIM mwenye Cheo cha Mrakibu mwandamizi (ASP), na ambaye ni Adjutant hapo Chuoni. Afisa huyo bila hata kumsikiliza askari huyo na bila hata kuangalia cheti toka kwa daktari kama kweli amepewa mapumziko. Pamoja na kulalamika kuwa anayo ED bila huruma na bila ubinadamu na bila kutumia busara na bila kutumia akili kama afisa wa polisi mwenye cheo na madaraka makubwa kama hayo. Afisa huyo aliamuru askari huyo awekwe mahabusu kwa kosa hilo. Kitendo cha kuwekwa mahabusu askari huyo kilipelekea afya yake kubadilika ghafla na akiwa ndani ya mahabusu hiyo ni wenzake ambao walitoa taarifa kuwa kuna mgonjwa ndani amezidiwa na ndipo askari waliokuwa zamu wakatoa taarifa na kumkimbiza hospital ambako ndiko alikotwaliwa na Muumbaji na ikwa ndiyo mwisho wake.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi waliopo Chuoni hapo wamehuzunika sana na baadhi yao wamesikika wakisema ni vyema mkuu wa jeshi afanye uchunguzi wa kina wa swala hilo. Inasemekana pia afisa huyo ameonyesha kutokuwa na uelewa wa maamuzi yake katika kila kona ya chuo hicho na kuonekana kama antafuta sifa au kujipendekeza kupandishwa cheo haraka. Pamoja na hayo wameomba kwamba mara mkuu wa polisi atakapofika chuoni hapo wiki hii kuhitimisha mafunzo ni vyema akaondoka na ofisa huyo na kwenda kumpa kazi nyingine huku akifanya uchunguzi wa jambo hilo. Kuendelea kuwepo hapo chuoni ni kuharibu nidhamu ya askari na jeshi zima la polisi. Kitendo cha kumuweka askari mwenzake mahabusu huku akiwa mgojwa na ugonjwa ambao tayari daktari amethibitisha ni kufundisha nini askari ambao watakwenda sasa kuwa karibu na wananchi na endapo watamkamata mwananchi ana kosa na ni mgonjwa je atasalimika. Naomba ndugu zangu hasa waandishi wa habari mlioko humu mnisaidie kupaza sauti ili tukomeshe tabia kama hizi. huyu ni kiongozi ambaye anatoa mafunzo kwa askari wa nchi nzima. je kuna haja ya ofisa huyo kuendelea kuwepo chuoni hapo? Tafadhalini tusaidiane.

Mh itakuwa ngumu sana kwa hawa uliowataja, wapaze sauti kisa polisi kafa,
Nyie nyie mapolisi mlimuua mwandishi mwenzao Iringa? sidhani kama watakusupport kwa hilo.
 
na mungu amlaze mahali pema = (Mungu amlaze sehemu yoyoye anayoona inafaaa) note that please..
 
kumbe polisi nao wanalalamika pale wenzao wanapokosa ubinadamu
nlidhani wako tofauti na raia tulio mitaani
 
SASA U GREAT THINKER WA HAPA NASHINDWA KUUELEWA WENGI MKO BIASED SANA KATIKA MICHANGO YENU ESP WHEN IT COMES TO PLOLICE.sasa mnategemea tutajenga taifa la namna gani?Hivi hata CDM wakichukua nchi je tutaishi kama mbinguni.Jifikirie leo POLISI wote wagome je ndo tutakuwa na maisha bora cha msingi ni kuangalia nani kaharibu wapi na tufanye nini kama taifa.Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.Basi kama mnaona polisi wote hawafai zaeni watoto muwapeleke polisi huenda watakuwa wema.
 
Kuna watu mmekariri mambo kama maroboti. Yule ni koplo siyo kuruta, naamini anafahamu taratibu zote, kumuumiza askari ili vita ikitokea awe mkakamavu nani kasema?b akirudi mtaani anakuwa raia tu mabia, kitimoto full kitambi.

Nadhani huyo adjutant sio kwamba hakuwa sahihi ila kuna mazingira ya kutoa adhabu na kutotoa adhabu au kuweka adhabu mbadala! Hivyo ni vitu muhimu sana. Sio kukariri tu, kazi haziendi hivyo pamoja ya kuwa yawezekana huyo koplo alikosea lakini kwa hali yake ya ugonjwa angemsikiliza! Mambo ya tekeleza amri malalamiko baadae huwa yanawacost viongozi wengi wa kijeshi, jitahidini kutumuia busara zaidi na sio kukariri PGO iliyotungwa na mkoloni.

Hakuna inshu hapo mkuu,c kashfa c lolote jamaa alikuwa mgonjwa tu huyo. Nakumbuka mwingine alifia Zanzibar mwaka mmoja akiwa kozi kwa matatizo related na hayo
 
Nifahamuvyo mimi hakuna kifo kizuri, wala si ustaarabu kushabikia kifo cha mtu mwingine, maana sisi sote ni marehemu watarajiwa. Si kifo cha Mwangosi wala cha mtanzania yeyote, awe askari au mwananchi wa kawaida wa itikadi ya chama chochote.
Nina hakika kama kama kifo cha huyo askari kina mkono wa mtu yeyote, mkuu wenu wa kazi atakishughurikia na hatimaye haki itatendeka.
Hata anayetuhumiwa kumuua mwangosi yuko jela hivi tujadilipo mambo haya akisubiri kutendewa haki kutokana na matendo yake.
Pia ifahamike, kama taaluma yoyote ile, kutenda makosa wakati wa kutekeleza majukumu ya kitaaluma ni kawaida na mara zote anayefanya makosa hupewa haki yake kwa mujibu wa sheria. Hivyo basi katika taaluma mtu mmoja akikosea hatusemi wana-taaluma nzima wamekosea. Mfano daktari aliyemfanyia operation ya kichwa mgonjwa wa miguu na kumuacha mwenye tatizo la kichwa, hatukusema madaktari wote wafungwe, la hasha, bali tulisema daktari aliyehusika achukuliwe hatua za kisheria.
 
:embarassed2:Habari ambazo nimezipata toka kwa kaka yangu anayehudhuria mafunzo ya kupandishwa cheo katika Chuo Cha Polisi Moshi (CCP). Ni kuwa siku ya jana chuoni hapo ilikuwa ni majonzi makubwa kwa askari wanaohudhuria course mbalimbali chuoni hapo. Majonzi hayo na vilio vilitawala pale mwili wa askari mwenzao aliyekuwa akihudhuria mafunzo ya ngazi ya corpolo kutokea mkoani Manyara. Askari huyo alifariki dunia kwa prssure na kisukari. Sasa basi kilichipelekea kuwepo na vilio vingi na lawama za hapa na pale ni kwamba: Askari huyo ambaye kwa sasa ni marehemu na mungu amlaze mahali pema, hakuhudhuria kipindi chuoni hapo kwa vile alikuwa na mapumziko aliyopewa na daktari wa Chuo ( ED ). Baada ya kutafutwa wasiohudhuri vipindi ikaonekana na yeye hakuhudhuria hivyo Afisa mmoja aliyetajwa kwa jina la JB IBRAHIM mwenye Cheo cha Mrakibu mwandamizi (ASP), na ambaye ni Adjutant hapo Chuoni. Afisa huyo bila hata kumsikiliza askari huyo na bila hata kuangalia cheti toka kwa daktari kama kweli amepewa mapumziko. Pamoja na kulalamika kuwa anayo ED bila huruma na bila ubinadamu na bila kutumia busara na bila kutumia akili kama afisa wa polisi mwenye cheo na madaraka makubwa kama hayo. Afisa huyo aliamuru askari huyo awekwe mahabusu kwa kosa hilo. Kitendo cha kuwekwa mahabusu askari huyo kilipelekea afya yake kubadilika ghafla na akiwa ndani ya mahabusu hiyo ni wenzake ambao walitoa taarifa kuwa kuna mgonjwa ndani amezidiwa na ndipo askari waliokuwa zamu wakatoa taarifa na kumkimbiza hospital ambako ndiko alikotwaliwa na Muumbaji na ikwa ndiyo mwisho wake.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi waliopo Chuoni hapo wamehuzunika sana na baadhi yao wamesikika wakisema ni vyema mkuu wa jeshi afanye uchunguzi wa kina wa swala hilo. Inasemekana pia afisa huyo ameonyesha kutokuwa na uelewa wa maamuzi yake katika kila kona ya chuo hicho na kuonekana kama antafuta sifa au kujipendekeza kupandishwa cheo haraka. Pamoja na hayo wameomba kwamba mara mkuu wa polisi atakapofika chuoni hapo wiki hii kuhitimisha mafunzo ni vyema akaondoka na ofisa huyo na kwenda kumpa kazi nyingine huku akifanya uchunguzi wa jambo hilo. Kuendelea kuwepo hapo chuoni ni kuharibu nidhamu ya askari na jeshi zima la polisi. Kitendo cha kumuweka askari mwenzake mahabusu huku akiwa mgojwa na ugonjwa ambao tayari daktari amethibitisha ni kufundisha nini askari ambao watakwenda sasa kuwa karibu na wananchi na endapo watamkamata mwananchi ana kosa na ni mgonjwa je atasalimika. Naomba ndugu zangu hasa waandishi wa habari mlioko humu mnisaidie kupaza sauti ili tukomeshe tabia kama hizi. huyu ni kiongozi ambaye anatoa mafunzo kwa askari wa nchi nzima. je kuna haja ya ofisa huyo kuendelea kuwepo chuoni hapo? Tafadhalini tusaidiane.

nadhani hilo ni somo linalofundishwa huko chuoni kwenu, maana mkitoka huko hata ninyi mko hivyo hivyo
 
ni kweli inahuzunisha, ila nauliza, huyu askari ilikuwaje hadi akawa na hayo magonjwa? Ana muda gani tangu kuwa askari? Na kama alipata maradhi akiwa askari, kwa nini alikubali hiyo hali imfike? Kama aliingia uaskari akiwa mgonjwa, iweje alivuka vizingiti vya vipimo? Tunajua ili uwe askari ni LAZIMA uwe fit na usiwe na magonjwa ya ajabu ajabu. Nanusa tatizo hapa. Uaskari umekuwa ni ajira ya kupeana bila kutazama tena misingi ya KUWA ASKARI. Tupate fundisho sasa.
 
Vifo kama hibyo havikosekani katika kozi za mapolisi huyo sio wa kwanza na hii inatokana na wengi kusingizia ugonjwa wkt hawaumwi.r.i..p polisi feom manyara...ndio uzalendo aliipenda nchi yake mungi ampokeee kwa amani
 
Wana JF acheni hasira....Nina ukaribu fulani na ndg zetu askari tena wa vyeo vya chini hadi Kamishna... Hawawezi kusema kwenye vyombo vya habari lkn wengi wana hasira sana na dhaifu na serekali yake jinsi wanavyowatumia kwa manufaa yao. Hata wanapozungumzia issue ya Mwangosi wanamshangaa alopenda sifa na kumlipua mwangosi na kumuumiza bosi wake huku bosi akiwa keshatoa amri wamwache...hili alinieleza askari mmoja rafiki yangu...Ninachotaka kusema hapa ni kwamba sio askari wote ni wabaya kama wachangiaji wengi wanavyoonekana kuamini na hivyo sio vyema kumhukumu marehemu kwasababu mshamba mshamba mmoja kule Iringa kaamua kutafut sifa/kutumika pasipo kufikiri... Aliyekufa ni Mtanzania mwenzetu, baba wa watoto na mume/mke wa mwenzetu na sio yeye aliyemwuua Mwangosi!
 
Hebu acha kutetea polisi tusijefikiri wewe u mmoja wao. Polisi wa tanzania wana sifa kuu tatu. Ya kwanza ni Uongo, ya Pili kupenda sana Rushwa, na tatu ulevi. Basi. Matatizo wanayotatua wanabahatisha tu!

Wana JF acheni hasira....Nina ukaribu fulani na ndg zetu askari tena wa vyeo vya chini hadi Kamishna... Hawawezi kusema kwenye vyombo vya habari lkn wengi wana hasira sana na dhaifu na serekali yake jinsi wanavyowatumia kwa manufaa yao. Hata wanapozungumzia issue ya Mwangosi wanamshangaa alopenda sifa na kumlipua mwangosi na kumuumiza bosi wake huku bosi akiwa keshatoa amri wamwache...hili alinieleza askari mmoja rafiki yangu...Ninachotaka kusema hapa ni kwamba sio askari wote ni wabaya kama wachangiaji wengi wanavyoonekana kuamini na hivyo sio vyema kumhukumu marehemu kwasababu mshamba mshamba mmoja kule Iringa kaamua kutafut sifa/kutumika pasipo kufikiri... Aliyekufa ni Mtanzania mwenzetu, baba wa watoto na mume/mke wa mwenzetu na sio yeye aliyemwuua Mwangosi!
 
Bora na wao wapate vimachungu kidogo!si wakituua sisi raia wana sema kitu kizito!
 
Kuna watu mmekariri mambo kama maroboti. Yule ni koplo siyo kuruta, naamini anafahamu taratibu zote, kumuumiza askari ili vita ikitokea awe mkakamavu nani kasema?b akirudi mtaani anakuwa raia tu mabia, kitimoto full kitambi.

Nadhani huyo adjutant sio kwamba hakuwa sahihi ila kuna mazingira ya kutoa adhabu na kutotoa adhabu au kuweka adhabu mbadala! Hivyo ni vitu muhimu sana. Sio kukariri tu, kazi haziendi hivyo pamoja ya kuwa yawezekana huyo koplo alikosea lakini kwa hali yake ya ugonjwa angemsikiliza! Mambo ya tekeleza amri malalamiko baadae huwa yanawacost viongozi wengi wa kijeshi, jitahidini kutumuia busara zaidi na sio kukariri PGO iliyotungwa na mkoloni.
Hakuna cha kukariri kama "marobot" hapa, tunazungumzia mambo ya "Kijeshi" kama mada ilivyoletwa. Tatizo lenu mnapenda sana kujiita "Jeshi la Polisi" Bila kutafakari nini haswa maana ya hilo mnaloliita Jeshi. Sasa kama tunajadili makosa yaliyofanyika "kijeshi" narudia tena, Adjutant hakuwa na kosa kabisa na alitekeleza wajibu wake ipasavyo kwani ingekuwa kashfa kubwa "kijeshi" kama askari yule angefia kwenye mabweni au vichakani mnakopenda kujificha ili kukwepa majukumu. Kuna watu wa kuchukuliwa hatua hapa, yule daktari aliyempima na kumwidhinisha askari mgonjwa yule kuhudhuria kozi wenyewe mnayoiita ya "kijeshi" na huyo mmbeya anayetoa siri za "Jeshi" la Polisi kwa ndugu zake kama huyu mleta mada alivyokiri. Unaweza sema hili ni jambo dogo; lakini nakwambia ni kubwa, kwani inadhihirisha jinsi maaskari "weledi" wa Mwema walivyo mahiri kwa kuvujisha siri za kikazi. Hivi ni kozi gani ya kijeshi ambayo hata wagonjwa, tena wa kisukari wanapelekwa kuhudhuria na wakafaulu? Hapa tena unajifunua udhaifu mkubwa ndani ya idara hiyo ya polisi, nao ni wa kuwepo uwezekano wa "kupelekana" kozi ili mradi kuhalalisha fulani apande cheo. Ni wazi kuna rushwa na upendeleo katika kupelekana kozi na kupandishana vyeo; na mara kadhaa wanaopandishwa ni wale wasio na sifa ila wenye uwezo wa kutembeza rushwa! Matokeo yake ndiyo maaskari wa ovyo ovyo waliosheheni ndani ya hilo nyinyi mnaloliita "jeshi" ambalo Bwana Mwema aaliongezea sifa ya utendaji wa weledi! la maaskari wanaopokea amri hata ya mjumbe wa shina wa CCM, wanaotumia silaha nzito za moto hata wanapowakabili wanafunzi wa shule ya msingi au sekondari wanaogomea chakula! Wanaovalia kijeshi mithili ya wanajeshi walioko Iraki au Afghanistan - kumkabili mwandishi mmoja aliyejihami na kamera na note book tu, na askari hao wanaotenda kwa "weledi" kumalizia kwa kumlipua mtuhumiwa na kumsambaratisha kabisa!
Nasema tena; hakuna Proffesionalism katika hilo linaloitwa Jeshi la polisi la sasa ambalo mimi naliona kama kundi la wahuni wanaofanya kazi bila ya mwongozo unaostahili kuitwa wa kijeshi wala nidhamu yoyote. Kundi linaloongozwa na viongozi wasiojua kuwajibika! Ni vigumu kuelewa namna kina Mwema na waziri wake wanavyofikiri hadi kung'ang'ania madarakani baada ya aibu na fedheha zote hizi. Shame on them!!!!
 
Back
Top Bottom