Kashfa nyingine yaibuka kuhusu mashine mpya Muhimbili

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Date::11/25/2008
Kashfa nyingine yaibuka kuhusu mashine mpya Muhimbili
Jackson Odoyo na Zaina Malongo
Mwananchi

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) inadaiwa kukusanya Sh10milioni kwa wiki kinyemela kutokana na gharama ya vipimo kwa kutumia mashine maalumu ya kupima magonjwa inayopiga picha kwa kutumia sumaku (MRI).

Mashine hiyo iliyonunuliwa na Serikali kwa Sh2.6bilioni kutoka Kampuni ya Philips ya nchini Uholanzi inatumiwa kupima wagonjwa 35 kwa wiki.

Kwa muujibu wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya MNH, mashine hiyo ilianza kutumika wiki iliyo pita na kwamba kila siku wagonjwa wanne hadi watano wahupimwa.

“Mashine hiyo inasiku saba tangu ilipoanza kutumika na kila siku wastani wa wagonjwa wanne hadi watano wahupiwa na kila mgonjwa anatozwa Sh400,000 pamoja na dawa na asipoandikiwa dawa zozote anatozwa Sh350,000,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo kingine kilifafanua kwamba sababu za kufanya hospitali hiyo ishindwe kuweka wazi suala la vipimo kwa kutumia mashine hiyo hazijulikani, badala yake wanaendelea kukusanya kiasi cha Sh10milioni kwa wiki.

Chanzo kingine kiliongeza kwamba, baadhi ya wahusika wanadai kwamba bado wako kwenye majaribio, lakini ukweli ni kwamba mashine hiyo imeshatengemaa na badala yake wameanza kuifanyia mradi kwa maslahi yao.

“Kinacho onekana hapa ni mradi na baadhi ya watu wamesha anza kunufaika kupitia mashine hii, kwa sababu hata ukiangalia wagonjwa wanaoletwa hapa, baadhi yao ni vigogo ambao awali walikuwa wanatibiwa katika hospitali ya Agha Kan kwa gharama ya Sh600,000,” kilifafanua chanzo kingine.

Hata hivyo mmiliki wa kampuni hiyo ya Mocas, Mohamed Asham alipofuatwa jana ofisini kwake na waandishi wa habari hii ili azungumzie suala hilo, alikataa na kumuagiza Meneja wa Fedha, Monica Joseph kwamba aeleze kuwa wao hawahusiki na suala hilo.

“Sisi si wahusika na wala si wasemaji kuhusu mashine hiyo bali ni wasambazaji tu, ukihitaji kufahamu undani wa suala hili mtafute Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii viongozi wa MNH,” alisema Joseph.

Naye Afisa Uhusiano wa MNH, Jeza Waziri alipoulizwa juu ya suala hilo alisema yeye si msemaji, bali afuatwe bosi wake, Aminiel Aligaesha ambaye hakuwepo ofisini.

Mapema mwaka huu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilishtukia njama za Hospitali hiyo kutaka kupokea mashine hiyo kinyemela kwa kushirikiana na baadhi ya maofisa wa wizara hiyo na msambaji huyo.
 
Habari haijaeleweka. Hiyo Mocas mbona imetoka out of nowhere? Ni nani hao?
 
Back
Top Bottom