Kashfa mpya serikali ya Kikwete- waziri atishia wananchi bastola

Lazaro is one of huligan, tuliosoma naye tunashangaa madaraka aliyopewa, anyway nchi ya kutupiana pande. WATU TUWE macho na tukumbuke wakuu wa nchi walikuwa wasanii hivi hivi tukapumbazika na mikogo yao, sasa tunalia
 
Hiyo itakua ni Dili Yao na jk.na hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa, Kama unabisha si utaona.
 
Nimependa mtiririko wa kisa na jinsi wananchi hao walivyohangaika huko TRA hadi kumjua "mtu wa kwenye VX"
ni vema wananchi wakakomaa mpaka mwisho wa kisa hicho, kwamba ifahamike hzo nyara ni zipi, zilitoka wapi na je ni kweli huyo waziri alikuwepo na hao watu kwenye gari badala ya kuwa bungeni mda huu?
 
jk.watu ulio wachagua siku zote ndo wanaokuangusha usipokuwa makini kukemea yatakuangusha

Kweli CCM imejaa Majambazi. Sasa naanza kumwelewa yule Gamba aliyependekeza humu jamvini kwamba wamsimamishe Nyari kugombea Ubunge Arusha mjini. Kweli hiki ni Chama Cha Majambazi!
 
Ni mapema mno kusema ni kashfa ya serikali ya JK.....kashfa nyingine si za serikali za mtu binafsi hadi pale itakapothibitishwa serikali imejiingiza officially kumkingia kifua na uhalifu huo kama kweli ulitokea.

Naona waziri wenu wa Magamba anachukua chake mapemaa asivyo na aibu mbele ya wapiga kura wake mkidondokea pua jimbo hilo mtaulaumu upinzani?
 
Katika kile kinachoonekana kuwa ni kitu cha kawaida kwa viongozi wa serikali kuwa wababe (wenye tabia ya kijambazi) na kulindwa na serikali yao. Naibu Waziri wa Viwanda na biashara Lazaro Nyalandu, tarehe 11/04/2012, saa 6:00 Usiku katika Kijiji cha Mwanyonye, Lazaro Nyalandu na watu wengine waliotajwa kuwa nao ni Elia Digha pamoja na Reuben walifika na gari No. T.505 BKM, aina ya VX, walikuta kizuizi kilichowekwa na serikali kwa ajili kukagua mazao ya wanyama na misitu, walishuka na kuwatishia walinzi kwa bastola, wakavunja kizuizi, na kuondoka na taa ambayo walinzi hao waliitumia. Baada ya tukio hilo Wanakijiji wa Mwanyonye walipiga simu kijiji kinachofuata. Kijiji kinachofuata ni Kinyeto, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinyeto na walinzi walijizatiti ili wazuie ile gari itakapofika, walipofika mtu mmoja alishuka kwenye gari haraka akiwa amenyoosha bastola na kuwauliza walinzi mnafungua au hamfungui, walikataliwa, wakavunja kizuizi. haijulikani Nyalandu alikuwa anatorosha nini katika mazingira hayo. Ila walinzi walipopiga picha gari hiyo, na kuchukua namba za usajili, waliripoti polisi mapema kufungua jalada SI/IR/1570/2012 KWA KOSA LA KUTISHIA KUUA KWA BASTOLA. Walinzi na watendaji walienda TRA kuomba umiliki halali wa gari T. 505 BKM, wakazuiliwa mpaka wapate kibali cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, walipewa na walipoenda TRA nao wakathibitisha mwenye gari ni Lazaro Nyalandu. Taarifa za kuaminika inasemekana Nyalandu alikuwa anatorosha Nyara za serikali. Pesa zimemwagwa Singida kuanza kurubuni waandishi wa habari, na maofisa wa usalama wanahaha kusaidia habari hizi zisitoke. Ila kwenye JF Where we dare to talk openly tumeweka jamvini. hii ndio serikali yetu.
Huyu dogo psmojs ns kujifsnys mlokole kote kumbe jambazi; nimeamini ndani ya CCM hakuna msafi hata kidogo
 
Lazaro is one of huligan, tuliosoma naye tunashangaa madaraka aliyopewa, anyway nchi ya kutupiana pande. WATU TUWE macho na tukumbuke wakuu wa nchi walikuwa wasanii hivi hivi tukapumbazika na mikogo yao, sasa tunalia
Wako wengi we unajua kisa cha naibu waziri wa elimu, Filipo Mulugo kupata wadhifa huo ni nini? Nchi hii ina safari ndefu mpaka itoke
 
Hakuna uzalendo nchi hii,mwenzetu kaleta info ni vema tuanze kuzifanyia kazi mara moja kuliko kuendelea kumbeza,rasilimali za nchi ni zetu sote hivyo sote tu walinzi wa rasilimali hizo na wenzetu wamethubutu kupambana kwa uwezo wao so nadhani habari hii ni vema tukafanya jitihada kujua zaidi na kwa nini watu wanamisuse silaha,tuwe na uthubutu wakuu as mwenzetu alivyojitahidi kuifikisha hapa.
 
Mi na hii nchi nimechoka na haya majambazi,majizi ya CCM kujiapiza tuu eti yatatutawala milele naamini wananchi wakiamua hata kufanya maandamano,kupeleka kesi mahakamani kama wakamshitaki kwa kutishia maisha yao
 
Hakuna uzalendo nchi hii,mwenzetu kaleta info ni vema tuanze kuzifanyia kazi mara moja kuliko kuendelea kumbeza,rasilimali za nchi ni zetu sote hivyo sote tu walinzi wa rasilimali hizo na wenzetu wamethubutu kupambana kwa uwezo wao so nadhani habari hii ni vema tukafanya jitihada kujua zaidi na kwa nini watu wanamisuse silaha,tuwe na uthubutu wakuu as mwenzetu alivyojitahidi kuifikisha hapa.
 
Kwa staili hii "Cabinet reshuffle is a must not optional"

na muhusika adhibiwe kisheria
 
Wanataka kupunguza makali ya pesa zao walizohonga kwenye kampeni, waacheni watoroshe hizo nyara, nyingine kwenye ndege, nyingine kwenye magari, n.k.

kusema humu haitoshi kwani si mumwambie mwanaharisi ataitoa then utaona baba faraja atakavofunguka
 
Back
Top Bottom