KASHFA: Mbunge atetea TAKURURU baada ya kufutwa kesi yake ya ufisadi

Si juzi tu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani alikuwa hapa mbona JK hakuthubutu kupinga hilo, na huyo wa TAKUKURU si alikuwepo? Iweje huyu viti maalum awatetee na ilhali wenyewe wameridhika?
 
Wana jamvi,

Mbumbe wa kuteuliwa CCM Munda Tambwe Abdallah ameshauri Watanzania kuachana na mitandao maana inatuchonganisha na kutaka Nchi isitawalike kwa kusema mambo ya uongo ametolea mfano wa wikileak walivyotoa mazungumzo ya siri kati ya Mkurugenzi wa PCCB kuhusu Tanzania na rushwa ya watu wakubwa,kilichonishangaza kusema US wamekaa kimya baada ya PCCB kukanusha habari hizo na hivyo basi ni habari za uongo kwakuwa america ni Taifa kubwa na lenye vyombo makini vya upelelezi hayo ni mawazo mepesi,ukosefu wa uzalendo,unafiki mkubwa sana na hili watanzania wanajua na dunia inajua!

Amesifu PCCB kufungua kesi kubwa nyingi ni zipi hizo za EPA?KAGODA?TICS?TTCL?NBC?IPTL?RICHMOND?DEEP GREEN?DOWANS? wakati tuliona watu walisamehewa wakaambiwa warudishe basi! na hakuna mwenye ushahidi kama walirudisha! na wengine ole wako hata ulalamike haki yako utakamatwa na kuwekwa ndani kama Mbunge yule mama wa cuf na wengine! yote haya Watanzania wanaona na Dunia inajua! kwa hilo nalo katoa mawazo hafifu kabisa mpaka sasa najiuliza hivi ni vigezi gani vinatumika kuchagua wabunge? yaani Mbunge anachangia ukimsikiliza unaona amefisika kabisa kichwani mpaka unabaki unajiuliza ni unafiki au ujinga?


Anaposema tuachane na mitandao nashangaa sana ktk ulimwengu huu ambao sasa ni kama kijiji,technologia ya habari imeleta mapinduzi makubwa sana duniani na Mbunge anapo shauri watu waachane na technologia ya habari anashangaza sana ktk jamii hii ya kimambo leo,mimi leo hii nimemuona huyu mbunge amepitwa na wakati,ni mtu anaeamini mambo ya kale yasiyo na tija!amelala usingizi wa pono wala hajui kinachoendelea ulimwenguni,jamani tusikubali kupotoshwa na watu wa aina hii,wanakula pesa zetu bule,ni wanafiki au wajinga sana hawafai kuingia bungeni ni watu waliofilisika vichwani na hili watanzania wanajua na dunia inajua!

Amezungumzia kuhusu kuvuja kwa siri za serikali,sasa wataanza kuwaonea watu bure,Technologia imekua sana jamani siku hizi kuficha siri sio rahisi na ndio maana baraza la mawaziri lina kaa watu wanakuja nakala ya mambo yaliyo ongelewa na hii nzuri kweli maana tutajua sasa wasiotuonea wananchi huruma na mambo yanayofanyika yasiyo na tija kwa taifa.jamani serikali ibadilike ikumbatie technologia mtajitahidi kuficha lakini kwa hali ya sasa ni vigumu sana hata Pentagon watu wanapata information tu. Ushauri wa kujaribu kifcha siri ni kuachana kabisa na technologia ya digitali.serikli ipige maruku vitu vyote vinavyotumia technologia ya mawasiliano.pili serikali itete maslahi ya wananchi hapo kutakuwa hakuna haja ya kuficha tena maana mnaficha nini au mambo kama ya jando?

Huyu Mbunge ni fisadi anaitwa Munde sio munda kama mwana mwema kajembe alivyoripoti nilibahatika kufanya nae kazi manispaa ya Tabora Mjini mimi nikiwa ni Idara ya Ujenzi yeye akiwa ni Accountant Clerk wa Manispaa ,Mwaka 2001 Yeye (Munde) ,Mweka Azina wa Wilaya Alikuwa Agira Okindo, Pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Mama Alfani walistafishwa kwa manufaa ya Umma baada ya kuifisadi manispaa ya Tabora Mjini na Alishtakiiwa kwa makosa ya Ujumu Uchumi.Wote kwa pamoja walishtakiwa kwa ubadhirifu wa Tshs,832,789,415,fedha za manispaa ya Tabora.Kutokana rushwa kukithiri ktkmahakama zetu pamoja na uhusiano wake wa karibu na Edward Hosea waliachiwa uhuru ( Pasipo na Kifungo )

Mahakama ilamua wastafishwe kwa manufaa ya Umma wasiruhusiwe kushika wadhifa wowote serikalini ,Mama Alfani aliyekuwa Mkurugenzi alifanya Mishe Mishe akarudishwa kwa muajiri wake wa Zamanni Wizara ya Elimu, Agira Okindo Aliekuwa Mweka Hazina wa Wilaya yeye aliamua kufundisha chuo cha uwazili Tabora, Huyu fisadi Munde sijuhi alihibukia wapi hadi akawa mbunge
 
Mh waziri ameonya kuwa nyaraka za serikali ni siri na mtu asiyehusika akikutwa na nyaraka hizi anastahili kuwajibishwa kama sheria za usalama wa taifa zinavyotaka.amewatahadharisha wabunge wanaotumia nyaraka kujengea hoja,wanaweza kuadhibiwa kisheria.

My take:kwa hiyo mh zitto amefanya kosa kisheria kwa kumiliki nyaraka nyeti za baraza la mawaziri.maana yake serikali imemsamehe kwani alistahili kuwajibishwa.
 
Nishamtumia ushaidi kwenye sanduku lake la barua, tuone kama atampeleka mahakamani!!!
 
yule ni mshamba wa ubunge..... na nadhani amepewa kidogo posho ya kutosha....

PCCP hozea siyo huyu alisema dili la radah ni safi .. imekuwaje....

huyu mama hafai kuitwa hata mbunge...
 
Hao ndo wenye chama na serikali pia!! Chenge for Prime Minister in 2015 while EL is the fifth president of URT.
 
CHENGE aseme alizipataje fedha 1 bilioni akiwa mtumishi wa umma?hiyo ni ktk akaunti moja ya nje,jee akaunti zingine zinakiasi gani?
 
nasema hivi, haiwezekani mtu timamu akawa ndani ya chama kile kinachoitwa ccm, hakuna nitajieni nani ? nauliza nani yuko sawasawa, wale woote wanaugua ugonjwa wa maralia ! hakuna mwenye uthubutu wa maswala serious....!
 
Hawa ndio Magamba wana kazi ya kujibeba kila kitu lakn waTz wanajua ukweli wa mambo yote kua Chenge ni mhusika mkuu katika Rada.
 
CHENGE aseme alizipataje fedha 1 bilioni akiwa mtumishi wa umma?hiyo ni ktk akaunti moja ya nje,jee akaunti zingine zinakiasi gani?
CHENGE ANA AKAUNTI PALE NBC YA TAKRIBANI BILLION 25, anaebisha aende pale benki akapeleleze
 
Mi nafikiri zinakuwa siri kabla hazijatoka nje ya kikao cha baraza la mawaziri. Akisha zishika zito na wenziye siyo siri tena. Huyu ni mgojwa wa akili. nasisitaza siri ikishavuja siyo siri tena wajifunze ili siri zisivuje.
 
Inabidi CCM wachekeche na kuvua na haya magamba mengine ya wabunge walioingia bungeni kwa kutumia fedha za wizi ili washitakiwe bola kuoneana haya
 
Huyo Chikawe ni wakukamtwa halafu achapwe vibao kwa ujinga aliouzungumza mbele ya Watanzania na dharau aliolionyesha Taifa
 
  • Thanks
Reactions: FJM
yule ni mshamba wa ubunge..... na nadhani amepewa kidogo posho ya kutosha....

PCCP hozea siyo huyu alisema dili la radah ni safi .. imekuwaje....

huyu mama hafai kuitwa hata mbunge...

haaaaaa! haaaa! umepatia kinoma ni mjumbe kamati ya Nishat na Madini ni miongoni mwa waliopokea Rushwa kutoka wizara ya Nishati na Madini ili wamsaliti January Makamba
 
Hivi Chenge kuonekana Gamba si ni pamoja na hii ishu ya radar au?
Ni hiyo ukiongeza na nyingine nyingi tu.Kila kilichoitwa mkataba wa kimataifa including IPTL, jamaa alihusika
 
CHENGE aseme alizipataje fedha 1 bilioni akiwa mtumishi wa umma?hiyo ni ktk akaunti moja ya nje,jee akaunti zingine zinakiasi gani?

Alishasema kuwa zilikuwa ni "vijisenti" alivyovipata kutokana na kusafiri na Rais huko China.
 
I've always said Tanzania is one of the few select countries in the world where mistakes are always made but by ghosts and phantoms.
 
Masiki Nape Mosses Nnahuye, utazeeka (kama sio kufa kwa BP). Unaona wanavyoanza kukunyofoa roho yako taratibu?
 
Back
Top Bottom