Kasheshe la Mafuta: Dar kimeanza kuwaka, vituo kadhaa vyaanza kutoa mafuta!

Ndugu yangu, siku hizi hakuna Authority. Bunge halina nguvu, watu wanapiga kelele pale , lakini inakuwa kama kelele za kijiweni ambazo hazina impact. Usishangae masaa 24 yakiisha, jamaa hawajauza mafuta na wasichukuliwe hatua yoyote, sanasana wataanza kuwabembeleza kwa kuwaita wajadiliane mezani.Miaka 4 iliyobaki ni kama miaka 100

Hapo pekundu,...umenena mkuu! mbona hii miaka 4 iliyobaki watanzania tutalia vilio vyote...:(
 
Hakuna lolote ni mkwara tu na hawa wafanyabiashara wanajua walitoa rushwa kwenye uchaguzi so no body can touch them wana kiburi cha ajabu. Nyerere alisema unatoa rushwa uingie ikulu then waliokupa rushwa atarudishiaje fedha zao walizokupa?

Habari ndio hiyo.
 
Kwa hapa Arusha, kuna baadhi ya vituo mpaka jana vilikuwa vinauza mafuta, lakini leo vimefungwa.

Nimejiuliza mara mbili mbili, jeuri ya kutunisha misuri wanaipata wapi ukizingatia Waziri husika kapiga mkwara jana Bungeni.
 
Mi nadhani ushauri wa zitto uzingatiwe jeshi litumike vituo na maghala yafunguliwe na mafuta yatolewe bure. La sivyo wananchi tuandamane tuvamie vituo hivyo na kujichotea mafuta kwa nguvu.
HTML:

Na nitashangaa kama polisi watatupiga mabomu kwa hili.
 
Jamani huyo wa kuuza mafuta nani? Mhindi au Mwarabu kwa kumuogopa nani? Kwani wao ni raia wenu kuwa wakigoma mtawafanya nini?

Kwanza wengi wao wana passport za Ulaya na Marekani, Uarabuni na India hivyo sioni sababu ya wao kusurrender amri ya Serikali. Wangekuwa Watanzania hakika sheria hiyo tusingefika huku. Kwa kuwa wangejua kuwa wanahujumu Taifa lao na vizazi vyao.

Mwendo ni ule ule hakuna mafuta hakuna mafuta, tuone kati ya Taifa la Tanzania na wageni nani ni Jeuri.
 
jamani nipo mnazi mmoja, nipo na jamaa wengine watatu, nasubiri mje, njooni tuanze hapa,
 
attachment.php
 
Hv chadema wapo wapi muda kama huu?me sielewi kwann hawajaanda maandamano mpk saiv,zaidi ya siku 7??au wao maandamano wanaandaa kma wakiwa wanataka madaraka tu? Suala la jailo wapo kimya suala la mafuta wapo kimya,jaman mananiangusha chadema,andaeni maandamano jmn tuwashinikize hawa wahuni watoke madarakani,imefika muda tuwe kama watu wa london kwa kuchoma hivi vituo vya mafuta na mali za mafisdi pai

Sio lazima CHADEMA waandae maandamano, hili tatizo linamgusa kila mtanzania pasipo kujali chama, Wewe na mwenzako mkianza kushika mabango na kuingia barabarani wataongezeka watu wakuwapa support bila kujali chama.

Jukumu ni lako.
 
Serikali inajitahidi iwezavyo kuleta maisha bora kwa wananchi wake. Tatizo ni dogo sana yaani watendaji wake kwahiyo susiilaumu sana, ila tuwalaumu watendaji wake.

We nae vp kwani anaye wachagua hao watendaji ni nani ka siyo muuza sura Kikwete
 
Watanzani Washington DC wajipanga kwa maadamano hapo muda mfupi ujao kupinga hali tete ya Tanzania.Je,hapa Bongo vp mazee mbona mko kimya au ndo Ofisi za sisiemu zimewaweka busy for nothing?Tokeni bwana tuikomboe nchi yetu.
 
Hv chadema wapo wapi muda kama huu?me sielewi kwann hawajaanda maandamano mpk saiv,zaidi ya siku 7??au wao maandamano wanaandaa kma wakiwa wanataka madaraka tu? Suala la jailo wapo kimya suala la mafuta wapo kimya,jaman mananiangusha chadema,andaeni maandamano jmn tuwashinikize hawa wahuni watoke madarakani,imefika muda tuwe kama watu wa london kwa kuchoma hivi vituo vya mafuta na mali za mafisdi pai

Ktk hili chadema wapo makini, hii ni ishu inayowagusa wananchi wengi moja kwa moja. Ni jukumu la wananchi wenyewe kujipanga na kuanza maandamano. Yakianzishwa na chadema, wana CCM wanaweza wakashindwa kuunga mkono hata kama na wao ni waathirika.

Ili yawe na nguvu, lazima wananchi wote bila kujali itikadi, kanda au dini waungane kushiriki. Yakianzishwa na chadema itaonekana kama wana uchu wa madaraka na wanataka kutumia tatizo hili kwa manufaa yao binafsi. Maandamano yaanzishwe na mimi na wewe na sio wanasiasa.
 
Hv chadema wapo wapi muda kama huu?me sielewi kwann hawajaanda maandamano mpk saiv,zaidi ya siku 7??au wao maandamano wanaandaa kma wakiwa wanataka madaraka tu? Suala la jailo wapo kimya suala la mafuta wapo kimya,jaman mananiangusha chadema,andaeni maandamano jmn tuwashinikize hawa wahuni watoke madarakani,imefika muda tuwe kama watu wa london kwa kuchoma hivi vituo vya mafuta na mali za mafisdi pai

Madcheda, Hujui kama maandamano yanayoitishwa na chadema yalisababisha viongozi waseme cdm wanataka nchi isitawalike na kwa sasa nia ya kurekebisha sheria ya maandamano imewekwa wazi kwa mwanvuli wa kuwasaidia wanachi waeze kufanya shughuli zao bila bughudha.

However, hiyo nia ya watawala kuwasaidia wananchi kufanya kazi zao bila bughudha inajidhihirisha katika hili la mafuta , usishangae mtu akaibuka kusema ' serikali haina kisima cha mafuta hivyo haina la kuwasaidia wananchi , zaidi ya kuwaomba viongozi wa dini wamwombe muumba aepushe balaa hili.
 
naomba mkutano wa chadema hapa arusha ujumlishe swala la umeme, mafuta,garama za maisha, meya fake...
 
Back
Top Bottom