Kaseja: Sihofii kutemwa Simba

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KIPA wa Simba na timu ya taifa 'Taifa Stars', Juma Kaseja amesema hawezi kuzungumza chochote juu ya suala lolote linalohusu klabu yake au timu ya taifa.

“Nimeamua kufumba mdomo na kuuchunga sana ili nisiongee kwani kuna watu wana mpango wakunichafua kupitia mdomo wangu, kila ninapofungua mdomo kuzungumza wananilisha ya kwao hivyo kwa sasa sihitaji kuzunguza chochote mpaka ligi itakapoanza,”alisema Kaseja.

Msimamo huo wa Kaseja umekuja siku chache baada wadau mbalimbali wa soka nchini kudai mchezaji huyo ameshuka kiwango na kwamba yawezekana akakosa hata usajili katika timu yake ya Simba msimu ujao.

Ingawa Kaseja ni kati ya magolikipa wazuri nchini wenye rekodi nzuri ya kufanya vizuri, lakini kauli na tabia za watanzania za kumzomea mchezaji kila anapofanya kosa uwanjani ndiyo inayomfanya mchezaji huyo abebeshwe lawama kila kukicha.

Wakati huohuo winga wa Taifa Stars, Julius Mrope amesema wachezaji wa Tanzania ni wavivu kiasi cha kushindwa kujituma uwanjani.

Mrope alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu alipoitwa katika timu ya taifa kwa ajili ya kuziba nafasi ya Mrisho Ngassa ambaye ni majeruhi wa paja.

“Wachezaji watanzania hawajitumi kiasi kwamba wamekuwa wavivu ndiyo maana wakipewa nafasi wanashindwa kuzitumia ipasavyo na hii ndiyo sabu Mrisho Ngassa anawazidi na ang'ara kila kukicha,”alisema Mrope.

Alisema yeye binafsi anamkubali Ngassa kwa sababu ni mchezaji mwenye kiwango cha juu kuliko wachezaji wote nchini na sababu ya kuwa juu ni kwa kuwa anajituma kila anapokuwa uwanjani.

Hii ni mara ya pili kwa Mrope kuitwa katika kikosi cha Stars ya Kocha Jan Poulsen, mara ya kwanza aliitwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Palestina iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Stars kushinda bao 1-0 lililofungwa na Ngassa.
 
Kipa chaguo la kwanza wa Simba ya Dar es Salaam, Juma Kaseja amesema kuwa yuko tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayotolewa na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu yake inayotarajiwa kukutana leo jioni, imefahamika.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kaseja alisema kuwa hana hofu na maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na viongozi wake ambao amefanya nao kazi tangu mwaka 2002 akitokea Moro United.
Alisema kuwa katika mpira, mchezaji anapaswa kukubaliana na mazingira yaliyopo, lakini haamini kwamba uwezo wake umeshuka kiasi cha kufikia hatua ya kuona maamuzi ya kuongezwa kwake mkataba yakifikiwa kwa kupiga kura.
"Hivi kweli mimi (Kaseja) nimeshuka kiasi hicho, siamini! Niko tayari kwa lolote, huu ndio mpira wetu wa Tanzania," alisema Kaseja ambaye alikuwa kipa bora msimu wa 2009/ 2010 na kuisadiai Simba kuandika rekodi ya aina yake kwa kutwaa ubingwa huku ikiwa haijawahi kufungwa .
Kaseja aliongeza kuwa yeye bado ana mkataba na Simba ambao unamalizika Juni mwaka huu na kabla ya kufikiria kusaini mkataba mwingine, ni lazima afahamu maslahi yake.
Alisema kuwa kupanda na kushuka kwa mchezaji ni jambo la kawaida na wakati mwingine, hutokana na aina ya wachezaji wanaounda kikosi kinachoshuka uwanjani.
"Ni lazima kwamba uangalie vigezo vingine kabla ya kusema fulani ameshuka kiwango, uzuri wa kila mchezaji huchangiwa na wachezaji wenzake anaoshirikiana nao uwanjani," aliongeza Kaseja.
Hata hivyo, Kaseja aliongeza kwamba amepigiwa simu na mmoja wa viongozi wa juu wa Simba, akielezwa kuwa anatakiwa asichanganwe na taarifa zinazoandikwa au kuzungumwa na watu mbalimbali.
Alisema kuwa kiongozi huyo (jina tunalo) alimueleza kwamba Simba bado inamuhitaji na inaamini kwamba mchango wake unatakiwa ili kufikia malengo waliyoyawekea.
Hata hivyo, habari ambazo gazeti hili inazo ni kwamba viongozi wa Simba bado wanatofautiana kuhusiana na suala la kuachwa kipa huyo, baadhi wakisema kwamba anahitaji kupumzika na ili hilo lifanyike ni lazima wasajili kipa mwingine mwenye kiwango cha juu ili wacheze kwa zamu.
Hivi sasa, Simba pia ina makipa wengine wawili ambao ni Ally Mustapha, 'Barthez' na Kabali Faraji aliyepandishwa kutoka kikosi B cha Simba.
 
namkumbuka MAXIMO alikataa katu kumpanga mtu anayeweza kuhujumu/kuhongwa
WATANZANIA HATUKUMWELEWA
 
Back
Top Bottom