Kaseja amwaga wino Simba

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Somoe Ng`itu
Hatimaye juzi kipa mahiri nchini, Juma Kaseja alisaini fomu za kujiunga na klabu ya Simba kwa ajili ya kuichezea katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
Akizungumza jana kwenye ukumbi wa mgahawa wa Hadees, Kaseja, alisema kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili na anawataka viongozi, wachezaji, wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba kumpa ushirikiano ili aweze kuitumikia vyema timu hiyo.
Kaseja alisema kuwa ameamua kurejea katika klabu yake hiyo ya zamani baada ya kushawishiwa na rafiki yake, Dionis Malinzi na viongozi wa Kamati ya Usajili ya Simba ambayo wote wameridhishwa na uwezo aliokuwa nayo.
"Mimi Juma Kaseja nimesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba, hii imetokana na ushawishi mkubwa wa rafiki yangu Dionis Malinzi ambaye ameshanifanyia mambo mengi makubwa," alisema Kaseja.
Aliongeza kuwa amefanya maamuzi hayo kutokana na uongozi wa Simba kuonyesha kumkubali na anawashukuru viongozi, wachezaji na wanachama wa Yanga kwa ushirikiano waliompatia katika msimu mmoja aliokuwa anaichezea timu yao.
Alisema pia anaamini yeye ni kipa bora na maamuzi yake ya kuondoka Yanga hayatokani na kuogopa ushindani na Mserbia, Obren Curkovic kama inavyotafsiriwa na baadhi ya wadau wa soka nchini.
Kaseja alisema kuwa yeye ndiye kipa aliyecheza mechi nyingi katika timu hiyo msimu uliopita na kuongeza kuwa hatishwi na maneno yanayosemwa na mashabiki kuhusiana na upinzani uliokuwepo katika nafasi hiyo dhidi ya Obren.
Aliahidi kuwa amerejEa kuisaidia Simba kurejesha heshima yake kwa kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Bara na mashindano ya Kombe la Shirikisho mapema mwakani.
NIPASHE
 
Kuna tetesi lengo la Simba ni kumkomoa Juma K, habari ambazo zimepatikana zinadai kwamba viongozi wa Simba na washabiki wao kwa ujumla iliwauma sana baada ya Juma K kusaini Yanga msimu ulopita. Mkakati uliopo ni kuhakikisha katika misimu miwili atakayokuwa Msimbazi Juma K atafanyiwa fitina hadi kummaliza kabisa kisoka ikiwa ni pamoja na kukalia benchi kwa sana.... Time will tell!!!
 
Inaonyesha wewe ndiye ulichukizwa sana kwa Kaseja kwenda Yanga. Soka la sasa ni kazi, mtu anakwenda anapoona kuna maslahi, mambo ya kukaa sehemu hata kama hakuna maslahi yamepitwa na wakati. Wamemsanisha tena kwa sababu Kaseja bado ni Mlinda mlango mzuri na nadhani atawasaidia sana Simba.

Kwahiyo hizo habari za kufikirika sidhani kama zina wakati tena.
 
Yanga msimu huu hata kama mtabebwa vipi ni kipigo tu..Phiri ndaniiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kaseja Karudi tena Simba SC?!..Atulie sasa maana alikuwa(Simba--Yanga--Simba)
Kila la kheri Simba msimu huo ujao!..
 
Timu imekamilika uwanjani sasa....Viongozi wafanye kazi bega kwa bega sasa...hakuna muda wa malumbano.....kila la kheri wana msimbazi
 
Simba: Juma Kaseja, Haruna Ramadhani, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Joseph Owino/Juma Nyoso, Hillary Echesa, Mussa Hassan 'Mgosi', Amri Kiemba, Ema Okwi, Haruna Moshi 'Boban', Uhuru Selemani/Redondo
 
Simba: Juma Kaseja, Haruna Ramadhani, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Joseph Owino/Juma Nyoso, Hillary Echesa, Mussa Hassan 'Mgosi', Amri Kiemba, Ema Okwi, Haruna Moshi 'Boban', Uhuru Selemani/Redondo
Mgosi ameachwa dakika za mwisho mwisho. Source hii HAPA
 
Inaonyesha wewe ndiye ulichukizwa sana kwa Kaseja kwenda Yanga. Soka la sasa ni kazi, mtu anakwenda anapoona kuna maslahi, mambo ya kukaa sehemu hata kama hakuna maslahi yamepitwa na wakati. Wamemsanisha tena kwa sababu Kaseja bado ni Mlinda mlango mzuri na nadhani atawasaidia sana Simba.

Kwahiyo hizo habari za kufikirika sidhani kama zina wakati tena.

Mh, unausemea moyo; pole sana!
 
Mgosi ameachwa dakika za mwisho mwisho. Source hii HAPA

Bila shaka umeona mzee. Mgosi ndani ya nyumba! Ingawa mipango yake ya kwenda Norway imekamilika. Lakini pale hakutakuwa na pengo safari hii. Unajua hapo nilimsahau Danny Mrwanda.
 
Last edited:
Hamna wachezaji hapo, wanaganga njaa.
Kama kuna wachezaji wakacheze soka la kulipwa tuone!!!!.
Kama hawataishia uarabuni na kurudi, na wakiwa masikini.
 
Mwina Kaduguda(Simba wa Yuda) Bado ni katibu simba? Huyu namuona kama kikwazo vile pale.
 
Back
Top Bottom