Karume na ujumbe wake na kauli mbili za jk ambazo ni muhimu ccm na wapinzani wakazikumbuka

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
127
Jana pamoja na kuchoka nilijiibia muda wa kulala ili pamoja na mambo mengine nikapate kumsikiliza Mwenyekiti wa CCM taifa akifunga mkutano mkuu wa 8 wa chama hicho. Badaye sikujilaumu kwa kufanya uamuzi ule wa kuchagua kuwa na CCM katika usiku ule. Mimi si mfurukutwa wa CCM ya leo na pia wakati mwingine napata shida kujituma kuwasikiliza kwani hoja katika mazungumzo yao ni chache kuliko vijembe na maelezo yenye kusengenya na kudhalilisha vyama vya upinzani.

Kwa nini sasa jana ilikuwa ni siku muhimu kwangu kuwasikiliza, kwanza ni kuwa wao ni dola na kwa kiasi kidogo kulikuwa na thamani katika kusikiliza hotuba za viongozi wa CCM na taifa kwa ujumla. Ikumbukwe kuwa wao ni kutoka chama tawala ambao pia wengi wao wako katika timu inayoongoza dola na kwa hiyo kila walinenalo linaathari katika maisha yangu kwa hiyo ni budi kuwasikiliza ili pale nisipokubaliana nao nijiandae kukataa.

Ndugu wana JF nisema wazi mheshimiwa A. A. Karume alinichanganya mara nyingi kuliko nilivyoweza kumuelewa katika maneno yake, kimsingi mimi nilielewa na nitabaki kuelewa hivyo kuwa Karume jana aliishambulia serikali kwa ujumla wake kuwa haizingatii haki za msingi za raia wake. Kwa nini hivo nilianza kuunganisha dots na nikagundua kuwa huenda jana alijivisha joho la wana Uamsho ambao kwa mujibu wa watu wengi kundi hili halijatendewa haki. Tangu lini Karume akawa hodari wa kutetea haki za raia, akahimiza kuheshimiana na kuvumiliana na kwamba kutofautiana katika mitizamo ni afya na wala tusipeane majina ya kudhalilishana. Karume na Kadi ya ASP jana alikusudia kutukumbusha nini? kwamba Zanzibar ni nchi na mfano wa kushindwa kwa CCM Unguja aloutoa ilikuwa ni salaamu tosha kwa CCM kuwa mkileta fyoko CUF watachukua nchi na Zanzibar itakuwa ni Republican???????? kazi kwelikweli wana JF na CCM salamu za mtoto kaanza tambaa huko na huko mama fungua milangoooooooo???????

Jana funga kazi ilikuwa kwa Mwenyekiti kwanza kwa kauli ya kishindo aliwaasa CCM kutokutegemea polisi kuwajibia hoja za kisiasa zinazoelekezwa kwao na vyama vya upinzani. Yes hayo ndio mambo ingawa amechelewa kuitoa kauli hiyo better late than not, hata hivyo ni madhuni yangu kuwa polisi na CCM wamesikia hoja za Rais "no more and no comment"

Kauli ya pili niliihesabu kama ni kauli isiyohitajika kutolewa na kiongozi wa nchi ambaye political statements and presidential comments are hardly inseparable, Katika nchi na mfumo wetu Rais ni chama na Chama ni serikali, na kwa hiyo kauli yake ya 'losing election was not an option', hii ina maana gani kama chama ni dola na dola ni chama? wajumvi wa mambo wanaona kama Rais alitujaza na hofu kwamba tunaichagua ccm au la chama hiki kitachukua dola kwa namna yoyote. Kauli hizi mbili ni mtaji kwa wapinzani zishikieni bango tutafika tu.
 
Back
Top Bottom