Karume, Maalim Seif wateta tena

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana alikutana kwa mara ya tatu na rais wa Zanzibar, Aman Abeid Karume mjini Unguja, katika mkutano ambao unaaminika kuwa ulikuwa wa kuzungumzia matatizo ya uandikishaji wapiga kura.
Hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu mkutano huo wa viongozi hao wa vyama vyenye upinzani mkubwa visiwani hapa ambao walikutana kwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana na baadaye Desemba na kukubaliana kufanya jitihada za kuondoa siasa za chuki.
Mkutano wa kwanza ulisababisha CUF kutangaza kuanza kumtambua Rais Karume na baadaye kupitisha kwa hoja ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliiambia Mwananchi kuwa mkutano wa viongozi hao unaweza kuwa umetokana na malalamiko yaliyoanza kuibuka tena tangu kuanza kwa awamu ya tatu ya uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la kudumu.
Zoezi hilo limekuwa lkiendeshwa kwa matatizo kutokana na wananchi wengi kukataliwa kujiandikisha kwa kukosa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, jambo linalolalamikiwa na wananchi wengi ambao wanadai wananyimwa haki yao ya msingi ya kushiriki katika uchaguzi mkuu.
Wananchi wanawalalamikia viongozi wa serikali za mitaa kuwa wanawanyima vitamnulisho vya ukaazi kutokana na tofauti zao za kisiasa na katika sehemu za kadhaa za uandikishaji wapigakura vurugu zilifumuka wakati wananchi wakizuia wenzao kujitokeza kujiandikisha.
"Wapo wananchi ambao wamekwenda na vielelezo vyao wengie wana vyeti vya kuzaliwa lakini bado vimekataliwa kwa madai kuwa sheha haiwatambui, sasa tunauliza hali hi itaendelea mpaka lini, alihoji Sanani kutoka Pemba.
Wapo masheha huwa wanawaambia watu wetu kuwa hawawatambui au wanawaambia kwa nini mnakuja leo wakati tangazo la watu kutakiwa kuja kuchukua barua ili wapewe vitambulisho ni la muda mrefu... yaani ni yale yale ambayo yalitokea wakati ule ndio yanatokea sasa,aliongeza Sanani.
Tumegundua mchezo mchafu unaochezwa na hawa wenzetu hapa.
Wamekuwa wakiweka maboksi yalioandikwa Micheweni kumbe vitambulisho vilivyomo humo ni vya Konde na boksi lililoandikwa Wawi linaa vitambulisho vya Gando... sasa ukienda kutafuta kitambulisho chako hukioni kumbe kimewekwa katika boksi jingine kwa makusudi, alisema mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi huyo alikariri barua iliotolewa na mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho, Mohammed Juma Ame kwenda ofisi za usajili wilaya ya Januari ya 19/2010 ambayo iliagiza watu hao kupokelewa maombi ya rufaa zao.
Alisema inaonekana afisi za wilaya hazipokei maagizo ya wakuu wao wao na kuwa wao wanakwenda tofauti na maelekezo ya kazi na kusababisha mlundikano wa fomu kwenye ofisi za wilaya wakati zilitakiwa kufika ofisi kuu kwa ajili ya kuwekwa saini na mkurugenzi ili wananchi wapate vitambulisho vyao.
Alisema barua hiyo inaaagiza kupokelewa kwa watu wanaoenda kujaza fomu za rufaa na kwamba kuwarejesha nazo ni kukiuka sheria.
Hata hivyo barua hiyo haikueleza kiundani kuzipokea fomu hizo za malalamiko kiafisi inamaanisha nini lakini watendaji walisema wao wanatakiwa kuzipokea na kuziweka ofisini kwake na sio kuzishughulikia kwa jambo lolote kwani mamlaka ya kutoa vitambulisho ni ya mkurugenzi pekee.
 
Back
Top Bottom