Karume Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano

Wana JF

Kuna tetesi kuwa CCM wanampango wa kumpitisha Rais mstaafu wa Zanzibar katika kugombea urais 2015. Hoja ni kuendeleza mbinu yao ya kutumia udini ili kushinda katika uchaguzi huo pia wataleta ushawishi kuwa ameweza kutuliza ghasia za kisiasa Zanzibar watakapochakachua lengo ni kuwa na Serikali ya umoja wa kitaifa na huku bara. Hii mnaionaje?

Source: Sema usikike
 
Kwa minyukano hii inayoendelea huku bara uwezekano wa Mzanzibari kuwa Rais wa JMT ni mkubwa tu ingawa Zanzibar kwa mabadiliko ya juzi ya Katiba yao ni NCHI kamili na mipaka yake.
 
Kwa minyukano hii inayoendelea huku bara uwezekano wa Mzanzibari kuwa Rais wa JMT ni mkubwa tu ingawa Zanzibar kwa mabadiliko ya juzi ya Katiba yao ni NCHI kamili na mipaka yake.

Ccm ipi itakayo fanya uteuzi huo?
Hivi minyukano yote ndani ya ccm itakuwa bado tu haijafa!
itakuwa ajabu ya nane ya Dunia.
 
Yaani kati yaMABOGA yoote ya ccm ni BORA ya huyu jamaa nadhani atatufaa, ni mzuri ona alivyoibadilisha Zanziabar! MENGINE MABOGA TUU!
 
Zanzibar in nchi kamili kwa sasa.Je tuko tayari kutawaliwa na foreign individuals.ukoloni huo hana chake
 
sura ya katiba mpya kuhusu muungano ndiyo itatupa muongozo wa rais ajaye kwani ha hatujajua tutakuwa na serikali ngapi ..... piga ua galagaza zanzibar iwe na rais wa upande huo wa kwao na bara iwe na rais wa upande wa bara kutokana na mfumo wa muungano utakaokubalika
 
Ccm ipi itakayo fanya uteuzi huo?
Hivi minyukano yote ndani ya ccm itakuwa bado tu haijafa!
itakuwa ajabu ya nane ya Dunia.

Minyukano hii itaendelea sana tu. Hakuna wa kuizima. Nchi imekuwa ya kambale hii ambayo kila mtu ana sharubu hata wanawake! OMBWE la uongozi ni kubwa mno.
 
Loooooooooo!!!!!!!! Muungano ndiyo kushnehi,huyu si ndiye aliyerudisha bendera ya zanzibar,katiba ya zanzibar,zanzibar kuwa nchi kuondoa suala la mafuta kwenye muungano na mengi mengine kuwa please wazanzibari wenzake! na hakika hata Ikulu itahamia zanzibar.
 
Hicho kitakuwa kichekesho cha karne. Haya, hebu tusubiri tuone. Kama waliweza kumfukua Billal huko alikokuwa na kuwa VP, hawa jamaa kweli wanaweza kuja na kituko kingine 2015.
 
Loooooooooo!!!!!!!! Muungano ndiyo kushnehi,huyu si ndiye aliyerudisha bendera ya zanzibar,katiba ya zanzibar,zanzibar kuwa nchi kuondoa suala la mafuta kwenye muungano na mengi mengine kuwa please wazanzibari wenzake! na hakika hata Ikulu itahamia zanzibar.
Atafanikiwa pia kuwarudishieni Tanganyike yenu.
 
Nothing like that...and if so,Im ready to be responsible to my comment.....
 
Back
Top Bottom