Karume Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano

Kuna tetesi kuwa Rais wa Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Abeid Amaan Karume kuwa atapewa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM 2015,habari zimezidi kuelezea kuwa yeye ndie atake kuwa mrithi wa Kikwete baaada ya Mheshimiwa Kikwete kumaliza ngwe yake 2015. Maandalizi ya kumuwezesha Mheshimiwa Karume kukubalika ifikapo mwaka 2015 yameanza na kufanya ziara za mara kwa mara katika mikoa ya Tanzania Bara ili kumjenga kwenye macho ya wananchi.

Hii inasemekana imetokana na utamaduni ambao kuna haja ya kuona unaendelezwa wa kupokezana nafasi ya kiti cha Urais wa Tanzania kwa upande wa bara na visiwani.Baada ya kokosekana wakati alipoondoka Mheshimiwa Benjamin Mkapa.

Pia habari zimezidi kutonya kuwa upo uwezekano wa mgombea huyo kupitia CCM kusimama katika kugombea kiti hicho kwa uchaguzi mkuu ujao 2010 endapo Rais Kikwete akiamua kupumzika, habari za wachunguzi wa mambo ya siasa wameona jitihada za Mheshimiwa Karume kuwekwa mstari wa mbele katika shughuli nyingi za Kichama hapa Tanzania Bara na Chama chake.

Zanzibar imemshinda ataweza jamuhuri ya muungano wa Tanzania?. Pia tumechoka kutawaliwa na baadhi ya familia. Tanzania ina watu zaidi ya 35mil hatuoni sababu ya kuendelea kutawaliwa na karumes, mwinyis, msekwas and the likes. Tunahitaji damu mpya, itikadi mpya,nguvu mpya na mawazo mapya kabisa. Hakuna monarch system ndani ya Tanzania na hatuitaki.
 
Naamini kuwa ally abeid karume ndiye mrithi sahihi wa jkaya 2015. Ndio maana ya kuitaka zenj ili 15 aibebe urt kwa nguvu ya zenj. Wakimnyima huyu jamaa 2010 basi tusubiri mpambano
 
Kuna tetesi kuwa Rais wa Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Abeid Amaan Karume kuwa atapewa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM 2015,habari zimezidi kuelezea kuwa yeye ndie atake kuwa mrithi wa Kikwete baaada ya Mheshimiwa Kikwete kumaliza ngwe yake 2015. Maandalizi ya kumuwezesha Mheshimiwa Karume kukubalika ifikapo mwaka 2015 yameanza na kufanya ziara za mara kwa mara katika mikoa ya Tanzania Bara ili kumjenga kwenye macho ya wananchi.

Hii inasemekana imetokana na utamaduni ambao kuna haja ya kuona unaendelezwa wa kupokezana nafasi ya kiti cha Urais wa Tanzania kwa upande wa bara na visiwani.Baada ya kokosekana wakati alipoondoka Mheshimiwa Benjamin Mkapa.

Pia habari zimezidi kutonya kuwa upo uwezekano wa mgombea huyo kupitia CCM kusimama katika kugombea kiti hicho kwa uchaguzi mkuu ujao 2010 endapo Rais Kikwete akiamua kupumzika, habari za wachunguzi wa mambo ya siasa wameona jitihada za Mheshimiwa Karume kuwekwa mstari wa mbele katika shughuli nyingi za Kichama hapa Tanzania Bara na Chama chake.
Wasituletee siasa za mipasho za Kisiwandui, wakifanya hivyo hata waibe kura zote badoo watashindwa kumsaidia awe Rais, wala wasithubutu.
 
Kuna tetesi kuwa Raisi wa Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Abeid Amaan Karume kuwa atapewa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM 2015.

Kuandaliwa ni suala moja, na kupitishwa ni suala lingine. Unaweza uandaliwe lakini ukifika kwa CC, NEC na Mkutano Mkuu wa CCM usipite. Hivyo mwache aandaliwe, madhali yeye ni mwanachama wa CCM ana haki kama wanachama wengine kugombea kuwa Rais kama wametimiza masharti, sioni kitu kikubwa cha ajabu hapo. Lakini kwa yote hii ni TETESI...
 
Jamani hilo goli la mkono,Wapinzani jiwekeni mkao wa madaraka,Mrema,Mbowe,Lipumba,Mtikila na Mbatia achieni damu changa nafasi. CCM Itabwagwa tu ipende isipende!!Wana CCM Karume anafaa sana msimwachie atasaidia kubadili mwelekeo wa siasa ya Tanzania mpeni kura.
 
Naamini kuwa ally abeid karume ndiye mrithi sahihi wa jkaya 2015. Ndio maana ya kuitaka zenj ili 15 aibebe urt kwa nguvu ya zenj. Wakimnyima huyu jamaa 2010 basi tusubiri mpambano

- Sasa ninaelewa kwa nini Lowassa na kundi lake wapo bize sana na hasa hivi karibuni baada ya kumuweka auntie Sophia, maana kama wagombea wenyewe ndio hawa basi kumbe njia ni nyeupe kwao ya kufikia urais 2015.

- Kwa maoni yangu itachukua muda mrefu sana kabla mgombea wa visiwani hajawa rais tena wa muungano, siamiini kuwa itakuwa ni hivi karibuni.
 
Kwa makundi na mgawanyiko ulioko huku bara wa wana CCM Rais ajae (2015) ni vema atoke Zanzibar. Wamefanya hivyo kwenye UVCCM na pametulia.
 
Sidhani kama sisi wabara tuko tayari kuongozwa na kiongozi wa aina ya Karume. Hoja hapa sio uzanzibari wake, bali uwezo wake yeye binafsi kama Karume.
 
- Sasa ninaelewa kwa nini Lowassa na kundi lake wapo bize sana na hasa hivi karibuni baada ya kumuweka auntie Sophia, maana kama wagombea wenyewe ndio hawa basi kumbe njia ni nyeupe kwao ya kufikia urais 2015.

- Kwa maoni yangu itachukua muda mrefu sana kabla mgombea wa visiwani hajawa rais tena wa muungano, siamiini kuwa itakuwa ni hivi karibuni.

Tuko pamoja mkuu
 
Pengine tunapopoa tunda lilioko mbali wakati lililowiva liko mbele yetu. Harakati hizi zote mnazoziona si za 2015 bali ni za 2010. Makamo wa Rais wa sasa anakwenda kuwa Rais wa Zanzibar na kuvunja usemi wa Wapemba kuwa wanabaguliwa kwenye madaraka. Badala yake Rais Karume anakuwa Mgombea Mwenza wa JK.
Angaalia usuhuba wa JK na Amani unavyojengwa sasa na huku Amani akimwekea kikwazo JK kwa kura ya "BLOCK" iwapo mpango huu hakuupitisha.
Hivyo na sisi Wabara tutaongozwa na huyo mnaefikiri kuwa mbumbumbu akiwa Makamo wa Rais.
 
Kwa taarifa yako, hizo ziara ni za kuaga watu wa bara kwani yeye 2010 anamaliza. Mtu ambaye anaweza kumrithi mkwere labda Dr. Shein.
 
Huyu jamaa hana sifa za kuwa kiongozi hata huko zanzibar walilazimisha tuuu.Si mtu wa kutuongoza watanzania.Hawezi kutufikisha popote zaidi ya kuturudisha nyuma.
 
Pengine tunapopoa tunda lilioko mbali wakati lililowiva liko mbele yetu. Harakati hizi zote mnazoziona si za 2015 bali ni za 2010. Makamo wa Rais wa sasa anakwenda kuwa Rais wa Zanzibar na kuvunja usemi wa Wapemba kuwa wanabaguliwa kwenye madaraka. Badala yake Rais Karume anakuwa Mgombea Mwenza wa JK.
Angaalia usuhuba wa JK na Amani unavyojengwa sasa na huku Amani akimwekea kikwazo JK kwa kura ya "BLOCK" iwapo mpango huu hakuupitisha.
Hivyo na sisi Wabara tutaongozwa na huyo mnaefikiri kuwa mbumbumbu akiwa Makamo wa Rais.

Katika wote walioelezea mawazo yao,nafikiri ya kwako yana nafasi kubwa ya kuwa sahihi. Na kama kuna ushawishi mkubwa wa kuwapa Urais Zanzibar Makamo wa sasa wa Rais anaweza kumrithi Kikwete hapo 2015.
 
Karume hata Urais wa Zbr alipatiwa tu na kuiongoza Zbr kunamshinda Bara itakuwaje?Akimaliza muda wake ni busara akapumzika na kufanya kazi zingine za kusaidia jamii.
 
Huyu jamaa hana sifa za kuwa kiongozi hata huko zanzibar walilazimisha tuuu.Si mtu wa kutuongoza watanzania.Hawezi kutufikisha popote zaidi ya kuturudisha nyuma.
Kwani unahitajika uwe na sifa gani ? Mbona wazee wamemshauri aendelee kwa miaka mingine kumi,huoni kuwa mawazo ya wazee yamewapa mwongozo CCM kwa kuona Karume atafaa awe mgombea wao wa kiti cha Uraisi wa Muungano.Hizi ni fununu lakini Karume anaonekana sana siku hizi katika ziara mbalimbali huko Bara ,Dr Sheini nasikia ni mwaka wake wa mwisho huenda akajiuzulu kuendelea kuwepo katika safu ya uongozi,maana hata katika hesabu hayumo ,anaonekana yumaji !!!
 
Nobody believes a rumor here in Tanzania until it's officially denied so let us wait and c.
Mkuu Mwiba! Acha usanii wa kipemba hapa! Rumours uzianzishe mwenyewe halafu unajifanya kuwa neutral na kusema:"let's wait and c!"
 
naomba huu ubaki kuwa uzushi jamaani!! Huku sasa ni kutafutana ubaya!! Hatuendelei moja kwa sababu hatuna viongozi wenye upeo, sasa Karume si ndio balaa jamaani! Hata uzushi kama huu haufai!!:confused:
 
Aaaaghhhh,, akae huko huko zenji akafunge misuli na kukaa barazani, huyo mdebwedo atamwongoza nani au wanataka ule ukuta wa magogoni tuingie nao? Ohooooooo!!
 
Back
Top Bottom