Karume day ifutwe huku Tanganyika

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Leo ni Karume day ambapo huwa sielewagi umuhimu wake kwa huku Tanganyika hadi kuifanya iwe mapumziko. Naona Rais pia kaamua kwenda kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji ya halaiki huko Rwanda, nadhani ipo haja ya kuifuta hii siku kwa huku Tanganyika kwani inaongeza tu utitiri wa siku za mapumziko.

Swali la kujiuliza ni kuwa hivi huyo Karume hadi tumkumbuke alitufanyia nini hasa Watanganyika?

Rais Magufuli yupo nchini Rwanda akihudhulia maazimisho ya kumbukumbu zoa mauaji ya Kimbali yaliyotokea 1994. Ni kitu kizuri kinachoenesha mshikamano na jirani zetu kuonesha jinsi gani tumeguswa na maafa hayo makubwa.

Ikumbukwe pia leo ni maazimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa hili hayatiMzee wetu mwanamapinduzi Abeid Aman Karume.

Swali kwa Watanzania ni kwamba event ipi ni muhimu Kitaifa kati ya hizo mbili? Je haikuwa muhimu sana kwa Rais kuwa Zanzibar na kushirikiana na Wanzanzibari kuazimisha kifo cha Karume?

Je, ingekuwa kifo cha Nyerere, Magufuli angekwenda Kigali?

Mimi binafsi, msimamo wangu ni kuwa Rais amekengeuka. Natoa hoja.
 
Haiwezi kufutwa kwanza mnakumbuka haikuwepo! Wazanzibari wakalalamika baada kuanzishwa Nyerere day kuwa mapumziko! Nao wanamuenzi Rais wao wa kwanza na Mwenyekiti wa Balaza la Mapinduzi! Ndani ya Muungano siku hiyo haiwezi kufutwa labda zifutwe zote 2.........(Nyerere day)
 
Hapana! Hii haiko sawa i think, mie ni mfuasi mkubwa sana wa utumbuaji wa sikukuu za umma zisizo na tija ila hii naona bora ibaki tu kwa heshima ya Mama Tanzania.

Karume ni founding father wa TANZANIA kama alivyokuwa Nyerere, hakutakuwa na maana kuifuta Karume day alafu tuendelee kuwa Tanzania.

And the last thing, naona kuna hii tabia ya ubaguzi ambayo inazidi kuota mizizi kadri siku zinavyosonga! Ni kwanini tubaguane kwa utanganyika wetu na uzanzibari wetu?! Nyerere tunayemheshimu alikemea hilo kwa nguvu zake zote, kwann tusimuenzi kwa kuliishi hilo?!

Tukianza kuwabagua wazanzibar kwa uzanzibati wao na tukafanikiwa katika hilo basi tujue hatutoishia hapo, tutakuja kwabagua wahindi, wazungu, wachina na watu wa mataifa mengine, tukimaliza hapo tutaingia hadi kwenye makabila, rangi ya ngozi, urefu na ufupi, utajiri na umaskini and it will never end.

Dhambi ya ubaguzi huwa haina mwisho!

Wishing you all happy public holiday.
 
hata mimi hushangaa WAZANZIBARI wanaposherehekea NYERERE day !
for what ?
 
leo ni karume day ambapo huwa sielewagi umuhimu wake kwa huku tanganyika hadi kuifanya iwe mapumziko naona mheshmiwa rais pia kaamua kwenda kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji ya halaiki huko rwanda nadhani ipo haja ya kuifuta hii siku kwa huku tanganyika kwani inaongeza tu utitiri wa siku za mapumziko swali la kujiuliza ni kua hivi huyo karume hadi tumkumbuke alitufanyia nn hasa watanganyika?
Ni kumbu kumbu ya kifo cha Gavana wa kwanza wa Zanzibar.Kumbuka koloni letu TANGANYIKA DAIMA.
 
Kwa nini tusifute na Nyerere day.....? Maana hawa wote ni waasisi wa taifa letu Tanzania
 
Karume day ifutwe sio relevant kwetu kabisa
Karume alikua rais wa Zanzibar na rais wa Zanzibar kwetu hana umuhimu
 
Hata Magufuli ameona ni upuuzi kwenda kusali kwa Kiarabu kwenye kaburi la Karume. Kajitafutia udhuru, Rwanda.

a47ccdda-d31b-43bc-82b9-7f3a2f2b44f6.jpg
 
karume day ifutwe sio relevant kwetu kabisa
karume alikua rais wa Zanzibar na rais wa Zanzibar kwetu hana umuhimu

Karume ni muasisi wa muungano. Karume alikuwa Makamo wa Raisi wa JMT na baadae Makamo wa Kwanza wa Raisi wa JMT mpaka alipofariki. Kwa haya mawili ukitaka kufuta Karume Day lazima ufute Nyerere day labda kama tutakuwa nje ya Muungano.
 
Hapana! Hii haiko sawa i think, mie ni mfuasi mkubwa sana wa utumbuaji wa sikukuu za umma zisizo na tija ila hii naona bora ibaki tu kwa heshima ya Mama Tanzania.

Karume ni founding father wa TANZANIA kama alivyokuwa Nyerere, hakutakuwa na maana kuifuta Karume day alafu tuendelee kuwa Tanzania.

And the last thing, naona kuna hii tabia ya ubaguzi ambayo inazidi kuota mizizi kadri siku zinavyosonga! Ni kwanini tubaguane kwa utanganyika wetu na uzanzibari wetu?! Nyerere tunayemheshimu alikemea hilo kwa nguvu zake zote, kwann tusimuenzi kwa kuliishi hilo?!

Tukianza kuwabagua wazanzibar kwa uzanzibati wao na tukafanikiwa katika hilo basi tujue hatutoishia hapo, tutakuja kwabagua wahindi, wazungu, wachina na watu wa mataifa mengine, tukimaliza hapo tutaingia hadi kwenye makabila, rangi ya ngozi, urefu na ufupi, utajiri na umaskini and it will never end.

Dhambi ya ubaguzi huwa haina mwisho!

Wishing you all happy public holiday.
Kwa maana hiyo huu muungano ni marufuku kwa nchi nyengine kujiunga?ndio maana wazanzibar wanasema Tanzania ndio Tanganyika imejivika koti la muungano kuitawala Zanzibar.
 
Leo ni Karume day ambapo huwa sielewagi umuhimu wake kwa huku Tanganyika hadi kuifanya iwe mapumziko. Naona Rais pia kaamua kwenda kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji ya halaiki huko Rwanda, nadhani ipo haja ya kuifuta hii siku kwa huku Tanganyika kwani inaongeza tu utitiri wa siku za mapumziko.

Swali la kujiuliza ni kuwa hivi huyo Karume hadi tumkumbuke alitufanyia nini hasa Watanganyika?
kijana unataka kuvunja muungano ? maana kwa sasa marehemu wawiili ndio walioshikilia huu muunganiko , walio hai wala hata hawajali kitu .
 
Back
Top Bottom