Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,920
- 31,161
NGUVU ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, imeanza kukitikisa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na sasa kimeahirisha kikao cha Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ili kukabili mmeguko wa wajumbe wa Bara na Visiwani uliosababishwa na ushabiki wa baadhi yao kwa Rais Karume.
Duru za kisiasa kutoka ndani ya Sekretarieti ya CCM inayoandaa vikao hivyo zilisema tayari suala la kutaka Uchaguzi Mkuu Zanzibar uahirishwe ili Rais Karume aongezewe muda limewagawa wajumbe wa NEC. Wanaotoka Visiwani wanaunga mkono hoja hiyo; wajumbe wa Bara wanaipinga.
Kutokana na hali hii, wajumbe wa NEC watokao Zanzibar wamekataa kwenda Dodoma kwenye vikao hivyo, hadi wamalize kikao cha Baraza la Wawakilishi, ambacho pamoja na mambo mengine, kitajadili hoja binafsi ya kumtaka Karume aongezewe muda wa kukaa madarakani.
Hoja hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza hilo, Abubakar Khamis Bakary (CUF), anayetaka uchaguzi mkuu visiwani humo uahirishwe, ili Karume apate muda wa kuandaa mazingira mazuri ya uchaguzi.
Hoja hiyo imeanzishwa na makundi ya wana CCM wa Zanzibar, na sasa imekuzwa na uongozi wa CUF, baada ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, kuibebea bango na kuungwa mkono na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed.
Uongozi wa juu wa CCM umeshtushwa na ushabiki wa ghafla wa CUF kwa Rais Karume na kuleta mtikisiko ambao umeilazimisha Sekretarieti ya CCM kuahirisha kikao cha NEC hadi wajumbe wa Zanzibar watakapokuwa wamehitimisha mjadala juu ya hatima ya urais wa Karume, ambaye ni Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa CCM.
Vyanzo vya habari vimedokeza kwamba uongozi wa juu wa CCM umesema vikao vya CC na NEC haviwezi kufanyika sasa, kulingana na hali ya sasa ya kisiasa, bila Karume na wapambe wake kushiriki.
Kwa sababu hiyo, Sekretarieti ya CCM, chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, akishirikiana na manaibu katibu wakuu, Saleh Ramadhan Feruzi (Zanzibar) na George Mkuchika (Bara), itafanya vikao hivyo kuanzia Februari 7, mwaka huu.
Kabla ya hapo, ratiba hiyo ya awali ilionyesha kuwa Kamati ya Maadili ilipangwa kukutana Januari 23 asubuhi na siku hiyo hiyo mchana, kungekuwa na kikao cha Kamati Kuu, wakati NEC ilitarajia kukutana kwa siku mbili kuanzia Januari 25 na 26.
Wajumbe wengine wa sekretarieti hiyo ni Katibu wa NEC Taifa wa Oganaizesheni, Kidawa Yusuf Himid, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha, Amos Makala.
Ratiba ya awali ilionyesha kuwa tayari sekretarieti imeshaketi kupanga ratiba na ajenda za mkutano huo uliotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
NEC imeahirishwa na sababu kubwa ni kutaka kuhakikisha wajumbe wote kutoka Zanzibar wanashiriki kikamilifu, maana ratiba ya sasa inagongana na vikao vya Baraza la Wawakilishi, alisema mmoja wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Makamba alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu kubadilishwa kwa ratiba ya NEC, alisema yeye ndiye anayepanga ratiba za mikutano na ikifika wakati atawajulisha wananchi.
Hata hivyo alisema hawezi kuzungumzia kwa undani ratiba ya vikao vya NEC kwa vile alikuwa msibani.
Ingawa suala la kutaka uchaguzi Zanzibar uahirishwe halikuwa sehemu ya ajenda ya kikao cha NEC, ni wazi kuwa lingeibuka na kuzua mjadala mzito kutokana na tofauti za mitizamo ya kisiasa.
Vikao hivyo ndivyo vitakavyojadili pia taarifa ya Kamati ya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, iliyoundwa kuchunguza na kuutafutia tiba mgogoro kati ya wabunge wa CCM na serikali yao.
Kwa mujibu wa habari hizo, baadhi ya wajumbe wa NEC wameanza kufanya ushawishi miongoni mwao ili kuwa na msimamo wakati wa kuichambua ripoti ya kamati ya mzee Mwinyi.
Makundi hayo ni lile la wabunge wanaojiita wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi linaloongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta na jingine ni majeruhi wa vita hiyo, akiwamo aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, Edward Lowassa.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa kila kundi linatembea kifua mbele likitamba kwamba haliwezi kuguswa na ripoti hiyo.
Ingawa taarifa ya kamati hiyo imebaki kuwa siri kubwa, baadhi yao wanasema huenda ikaja na mkakati wa kuwajibishana ndani ya CCM kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo za baadhi ya vigogo kuunda mitandao ya kisiasa, kuhusika na vitendo vya ufisadi na wengine kutoa matamko makali nje ya vikao vya chama hicho.
Mambo mawili makubwa yanatarajiwa kujitokeza ndani ya ripoti hiyo. Mosi, vigogo watuhumiwa wa ufisadi kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.
Pili, wenye kutoa kauli kali nje ya vikao vya chama hicho, wakiwamo baadhi ya wabunge kupewa onyo na kutakiwa kuwa makini.
Tayari mkakati huo umeanza kupata upinzani miongoni mwa watu ndani ya CCM na hata baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti, CC na NEC.
Kwa mujibu wa habari zilizotufikia, katika kikao cha sekretarieti hiyo, sehemu kubwa ya wajumbe wanaunga mkono chama kuwawajibisha watuhumiwa wenye kashfa za ufisadi, wakiwamo wanachama wake ambao wanaelekea kuwa mzigo baada ya kuchukuliwa hatua na vyombo vingine.
Lakini wakati hali ikiwa hivyo, inaelezwa kuwa vigogo wa juu serikalini wanaunga mkono uamuzi huo mgumu ili kumtenga Rais Kikwete na chuki zinazoweza kuibuka.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa hali ya kujadiliwa kwa watuhumiwa wa ufisadi wakitajwa kuwa na mikakati yao binafsi ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikikisumbua chama hicho, imewakera na kuwachosha viongozi wengi waadilifu serikalini.
Vyanzo vyetu vya habari vilivyo karibu na viongozi waandamizi nchini vimedokeza kuwa hatua hiyo inachukuliwa ili kuisafisha CCM mbele ya majukwaa ya kampeni baadaye mwaka huu.
Kamati ya Mwinyi inayowashirikisha Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Abdulrahman Kinana, iliundwa na NEC katika kikao chake kilichopita mjini Dodoma ili kutoa mapendekezo ya kumaliza kile kilichotajwa kuwa uhasama miongoni mwa wabunge wa chama hicho pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar waliowahi kupishana kauli na viongozi wa juu wa Serikali ya Muungano.
Mwishoni mwa mwaka jana, Kamati ya Mwinyi iliwahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa imeanza kuparaganyika, ikielezwa kuwa sehemu ya mapendekezo katika taarifa yake ya pamoja kwa ajili ya kuwasilishwa NEC-CCM imevuja.
Katika habari hizo ilielezwa kuwa baadhi ya viongozi wa CCM wamedokezwa kuhusu mapendekezo ya kamati hiyo, yaliyodaiwa kuwa ni pamoja na kuwangoa madarakani baadhi ya watuhumiwa.
Kutokana na mapendekezo hayo ya kungoana, baadhi ya vigogo wanatajwa kuwa na mwelekeo wa kupingana na kamati, kwa madai kuwa hiyo ni hatua kali, bila kujali kuwa wanaotakiwa kuachia madaraka ili wabaki wanachama wa kawaida walikwisha kufanya hivyo kwa kuacha nyadhifa zao serikalini.
Source: Tanzania Daima
My take,
Kunaviashiria CCM bara inapenda mgogoro wa CUF na CCM Zanzibar uendelee kuwepo sijui kwa faida ya nani.Nimekuwa nikijiuliza mara kadha ni kwanini maridhiano ya Maalim Seif na Dr Aman Karume yanawapa taabu sana baadhi ya watendaji wakuu wa CCM huku Tanzania bara.Mwanzoni nilidhani kulikuwa na juhudi hasa kutoka bara kuhakikisha mgogoro uliodumu kwa muda mrefu unamalizwa ili kuipa Tanzania taswira nzuri katika anga za kimataifa.
Nawashauri viongozi wote tuwe makini sana katika maamuzi yetu kwa faida ya vizazi vijavyo,Maalim Seif na Dr Aman Karume wahakikishe makubaliano yao hayakiuki katiba ya Zanzibar na ile ya JMT.