Karudi Baba Mmoja (Toleo Jipya)

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?
 
anayeijua ile story ya sadiki aliyekimbilia mjini kutafuta kazi aiweke hapa wajameni....maisha yalivyomshinda town karudi na viraka vya nguo.

Ubungoubungo, aliyekimbilia town ni sikiri, sadiki yeye alibaki home. Ngoja nikupe mistari michache ninayokumbuka.

Sikiri mi masikini, uvivu wangu nyumbani
nikiwa hapa njiani, nakufa hapa kwa nini

Sadiki sasa ashiba,chakula kingi kwa baba..........

Nakumbuka hayo tu mkuu.
 
UBETI MPYA:

Mwenzetu aliondoka, na pesa zetu za EPA
kimbilia amerika, muhimbili akahepa
akafa tena masika, mkono akatutupa
kama mnataka mali, ibeni na mkimbie!
 
Ahsante sana ndugu zangu hakika mmenikumbusha mbali sana kwa utenzu huu takribani miaka 40 nilipoiacha shule ya mtaro very long time ago sincr the 1970s endelezeni mapambano
 
Ahsante sana ndugu zangu hakika mmenikumbusha mbali sana kwa utenzu huu takribani miaka 40 nilipoiacha shule ya mtaro very long time ago sincr the 1970s endelezeni mapambano

waliianza zamani, moja tisa tisa tano
wakaiba na madini, wakafanya na pambano
babetu katurubuni, miaka kumi na tano
mkitaka umasikini, jaribu utengamano!
 
FISADI SIKIA:

mabeti yamesimama,ukweli uko bayana,
kama kweli wana utu,basi watafanya jema,
watainuia wenzao,pasi kuinua maisha,
wajue tunayo macho,ni siku tu zajisongeza.
 
Akatamka mbaba, nina uchu kweli kweli
Na mwanangu wa la saba,ni mjumbe kwenye meli
Kakaake pia si haba,namkuza asifeli
Na wewe wataka mali? Waweza kua dalali?

Pale kwenye nyumba yao, wameandika kibao
Shamba hili ni la kwao,bisha upigwe dafrao
Mtu hucheza kwao,wa mbali piga miyao
Na wewe wataka mali? Waweza kua dalali?
 
Tanzania bwana. Hatuoni aibu kula hela za umma karibu nusu ya bajeti kwa per diem, workshop na safari? :Lini tutafanya investment kwenye elimu, afya, na miundi mbinu? Au tunasubiri millenium challenge watuokoe kama vile tuna mikono vibutu?
 

KARUDI BABA MMOJA

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
wote wakashangilia, usemi wakakubali,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI"
 
Umesahau ubeti unaosema:
WAKAWANUNUA NG'OMBE MAJIKE KWA MAFAHALI,
WAKAPATA NA VIKOMBE MAVAZI NA BASKELI,
HAWAKUITAKA POMBE, SABABU POMBE SI MALI,
Kama mnataka mali mtayapata shambani.
Safi mkuu, inasisimua beti zimeenda shule sijui alikuwa anatunga nani siku zile!
 
Safi mkuu, inasisimua beti zimeenda shule sijui alikuwa anatunga nani siku zile!

Mashairi mengi alikuwa anatunga baba wa Taifa mwal JK Nyerere, japo yapo mengine ya wataalam wengine.
Umenikumbusha mbali, na shairi hili nilikuwa nalipenda sana, thanks alot bro
 
Umesahau ubeti unaosema:
WAKAWANUNUA NG'OMBE MAJIKE KWA MAFAHALI,
WAKAPATA NA VIKOMBE MAVAZI NA BASKELI,
HAWAKUITAKA POMBE, SABABU POMBE SI MALI,
Kama mnataka mali mtayapata shambani.

Ubeti huu nao mmeusahau wapendwa:

Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili
Wote wakawa tayari, kauli kuikabili
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Umenikumbusha mbali sana-darasa la 4 mwaka 1992. Dah! Asante sana.
 
sungura afahamika, ujanja kajijazia,
wenzake anawacheka, sungura huwazomea,
siku yake ikafika, ya sungura kuumia,
ya sungura kuumia, sungura nakuambia.

endelezeni beti nyingine!!!!!



 
Back
Top Bottom