Karibuni Mtaa wa MANGOMA (MUSIC Boulaverd).....D

Ting a ling..........




Mr. Loverman Shabaaaaaaaaaaaaaa

 
Last edited by a moderator:
Chaka Demus & Pliers...............



Na hiki hapa.....



Hiki je?.....

 
Last edited by a moderator:
Sherehe ya kutukaribisha New commers (First Year) pale Arusha tech. College......

Mzee Issa Mushi ambaye alikuwa Principal wa pale, aliingia na Peogeot yake 504 hadi Parking ya magari ya wageni na kuiweka pale gari yake. Kwa mwendo wa kujiamini na mkewe, aliingia Dining hall, ambayo ilikuwa ikufungwa, inakuwa ni ukumbi mzuri sana na mikutano mingi ilifanyika hapo.

Alikaa kidogo na kutowa mawaidha machache na huyoo akasimama kutufungulia Disco kwa mtindo wa Kiingereza uitwao English WALTS (angalia video) na hao wakaanza kupeperuka uwanjani. Siku hiyo niliona kweli nimefika chuoni..... Kwanza nilichanganywa na wimbo wenyewe na mwisho uchezaji mzuri wa Mzee Mushi na mkewe. Na gauni la mamaa, ilikuwa kama vile walipanga avae nini......., mama na kichwa alikuwa anapatia kwelikweli kwa kukilaza nyuma.



Mtindo wa uchzaji English Walts.....

 
Last edited by a moderator:
Hahahaaa, Shaba Ranks walimuigiza.... hihiiiiii :)



Maadam tupo kwa Shabba yaani Jamaica, basi tumuangalie mtemi wa Roots Reggae anayeishi bado...... Hawa akina mama wapiga midogo ya Bata na Korongo, sijui aliwatowa wapi. Ila kweli wanaipuliza si kawaida.

 
Last edited by a moderator:
Sherehe ya kutukaribisha New commers (First Year) pale Arusha tech. College......

Mzee Issa Mushi ambaye alikuwa Principal wa pale, aliingia na Peogeot yake 504 hadi Parking ya magari ya wageni na kuiweka pale gari yake. Kwa mwendo wa kujiamini na mkewe, aliingia Dining hall, ambayo ilikuwa ikufungwa, inakuwa ni ukumbi mzuri sana na mikutano mingi ilifanyika hapo.

Alikaa kidogo na kutowa mawaidha machache na huyoo akasimama kutufungulia Disco kwa mtindo wa Kiingereza uitwao English WALTS (angalia video) na hao wakaanza kupeperuka uwanjani. Siku hiyo niliona kweli nimefika chuoni..... Kwanza nilichanganywa na wimbo wenyewe na mwisho uchezaji mzuri wa Mzee Mushi na mkewe. Na gauni la mamaa, ilikuwa kama vile walipanga avae nini......., mama na kichwa alikuwa anapatia kwelikweli kwa kukilaza nyuma.



Mtindo wa uchzaji English Walts.....



Nkwingwa................Leo umenifurahisha sana na WALTZ......

Umenikumbusha mbali sana leo......
 
Last edited by a moderator:
250px-Tdkc60cassette.jpg 070820_boombox_12.jpg gramaphone.jpg radio.jpg juke box.JPG philips_22gf403.jpg

Nani anavikumbuka hivi?.......

Picha kwa hisani ya John Kitime....
 
36747_1543603668935_1200297381_31542532_4167289_n.jpg
Kutoka kushoto DJ John Pantalakis(JPP),DJ Nigger J(Masoud Masoud) na Waziry Ally wa Njenje...
 
Salama wakuu?.......

Nawakaribisha katika mtaa wetu huu wa mangoma(music boulaverd).....

Hapa tutajikumbusha mangoma yaliyotamba kipindi kileeee cha miaka ya 80 na 90 mwanzoni(91-92). Tutaaangalia wanamuziki/vikundi vilivyotamba enzi hizo,kumbi za muziki bongo zilizotamba enzi hizo,ma DJ waliotamba enzi hizo pamoja na wacheza Disco waliotamba enzi hizo(ambao walicheza mitindo kama Chacha, Beak Dance, Roboti, Bumping, Michael Jackson Style) ....

Leo nianze na ma DJ waliotamba enzi hizo pamoja na kumbi walizokuwa wakifanya vitu vyao.....

- DJ Chris Phaby "The Lover"- Huyu alikuwa anafanya vitu vyake Mbowe/Margott...
- DJ Ngomely, na DJ Kim(Abdulakim Magomelo),DJ Pop Juice- Hawa walikuwa wakifanya vitu vyao pale Rungwe Oceanic Beach Resort...
- DJ John Peter Pantalakis(JPP), DJ Choggy Sly na DJ Kalikali- Hawa walikuwa wakifanya vitu vyao Silver Sands na baadae wakahamia YMCA..
- DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis- Hawa walikuwa wakifanya vitu vyao pale Keys Hotel....
- DJ Seydou na DJ Yaphet Kotto- Hawa walikuwa wakifanya vitu vyao RSVP Club(RSVP Discotheque) a.k.a Mbowe...
- DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee, DJ Joe Johnson Holela na DJ Young Millionaire- Hawa walikuwa Vision 200 Discotheque...
- DJ Mehboob- Yeye alikuwa Africana....
- DJ Emperor(Joseph Kusaga), DJ Bonny Luv na DJ Jesse(Mawingu Disco)- Hawa alikuwa akifanya vitu vyake pale New Africa Hotel....
- DJ Justin Kusaga - wa Mawingu/Clouds Disco pale Morogoro....
- DJ Nigger Jay(Masoud Masoud) - Yeye alikuwa pale YMCA....

Mimi nawakumbuka hawa kwa sasa,naomba tuendelee kujuzana wakuu wangu....

Karibuni sana kwenye Mtaa wa Mangoma....

Bala.
-

Mkuu hapo kwenye list yako ongeza na:

DJ Deo Composer
 
Unamaanisha John Dilinga?...

Kama ni huyo yeye ni bwa'mdogo mkuu...Alianza kuvuma kati ya mwaka 1996 na 97 nafikiri,yeye pamoja na akina DJ Mike Mhagama,Sos B,Ramkim Ramadhan,Sunday Simba Shomar,Monica Mfumia na wengine waliokuwa Radio One ya enzi hizo

Mkuu Balantanda:

Yuko wapi huyu dada siku hizi?
 
Kitu hiki hapa chini naweza sema ndicho Asili ya muziki wa Bongofleva,Saleh Jabir alikiimba kwa Kiswahili kitu ambacho kilionekana ni kigeni sana...Nakumbuka baadhi ya maneno kama 'Kata kata ngoma za kisasa,kata kata hata kwasakwasa kibao ni chako si cha kuazima hata ukiwa mtu mzima'. 'Kitu kimenikaa moyoni sasa naamua kukitoa mdomoni yooo I don't know kusema mengine naona choo'... 'Niko street nataka mic ya umeme niko kweye stage nayakata madebe..............Ice ice baby oooh oooh'.....
OPP I can explain it Kila moja kwa pembeni kwa kungoja cool S tasema niniO for omba PP for pure penzi Mtoto mweke ndani hakikisha 'naku enzi Vibishoo vya mitaani vyote avyone mshenzi Asijali honda wala marcedes benzi Na kama hii maana nakfanya wewe kushangaa, 'Shangae feri sababu mimi si kichaa Nakupa vyote 'navyotaka kuvijua 'bout Nina kibali kwa naughty by nature. Hiyo ilikuwa OPP ya kiswahili ya saleh jabir. Asante kwa thread kali, umenikumbusha dj peter pantalakis hivi wako wapi hawa wakongwe?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Balantanda:

Yuko wapi huyu dada siku hizi?

Monica Mfumia kwa sasa anaishi Uingereza(sijui anafanya kazi gani hasa).....

Radio One Dream team 1995.jpg
Msatari wa mbele waliokaa toka kushoto ni Charles Martin Hilary Nkwanga, Mikidadi Mahamud , Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Radio One,Julius Nyaisangah (Uncle J).
Waliosimama kutoka kushoto ni Deo Mshigeni, Mike Mhagama, Monica Mfumia, Flora Nducha, Vicky Msina, Aboubakar Liongo, Sunday Shomari, Mmojawapo wa watangazaji wa kike jina simkumbuki na Taji Liundi.
 

Attachments

  • 4139804.jpg
    4139804.jpg
    71.6 KB · Views: 65
Umenikumbusha pia enzi zile za break dance miaka ya 80, kuna jamaa mmoja alikuwa matata sana alikuwa anaitwa abbas alikuwa anakaa k'koo sikumbuki 2nd name, wakati huo tunashindana viwanja vya gymkhana na air india(sea view) , nawakumbuka pia kina usungu (young millionaire) alikuwa anakaa mitaa ya kisutu, nicco scaba scuba - maeneo ya pale mohans, wengine wakina abel siwale(RIP) na mdogo wake makka, chuche, mpeni, umenikumbusha wakati wa YMCA disco toto kiingilio ilikuwa ni shs 10 tu, kiwanja kingine ni Dar institute
 
Chaka Demus & Pliers...............



Na hiki hapa.....



Hiki je?.....



Hapo mkuu umenikumbusha mbali sana,enzi zile nakumbuka tulialikwa "welcome form v part" hapo mjini Azania sec,tukitokea shule fulani jirani.Yaani kama huo bam bam ndio ulikuwa on top kipindi hicho.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom