Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,108
- 37,644
Water Development and Management Institute (WDMI) ama chuo cha usimamizi na maendeleo ya Maji, zamani Water Resources Institute (WRI) kilianzishwa mwaka 1974 kama kitengo ndani iliyokuwa wizara ya maji na nishati mnamo mwaka 1974.
Lengo kuu la uanzishwaji wa chuo hiki ilikuwa kukidhi mahitaji ya wataalamu wa maji wa ngazi ya kati katika uliokuwa mpango mkubwa wa miaka 20 wa program ya usambazaji maji nchini Tanzania kati ya (1971-1991).
Ilipofika mwaka 1980, chuo kilibadilisha jina na kuitwa Taasisi ya Rasilimali za Maji ya Rwegarulila ama Rwegarulila Water resources Institute. Chuo kimelenga katika kuandaa wataalamu mbali mbali wa sekta ya maji kupitia program zake za mafunzo, ushauri na tafiti chini ya sera husika ya wizara ya Maji, kwa sasa chuo kinatambulika rasmi kama Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya Maji, Water Development and Management Institute.
Chuo kinatambuliwa na TCU, kwa sasa chuo kinatoa kozi moja tu ya ngazi ya degree, ambayo wanafunzi wake, wanapata mkopo kutoka HESLB.
Bachelor degree in Water Resources and Irrigation engineering
Chuo ni cha Serikali, chini ya Wizara ya Maji, kozi zote za diploma zinazotolewa na chuo hiki, zinatambuliwa kwa usajili wa NACTE.
1. Diploma in Irrigation engineering
2. Diploma in Meteorology and hydrology
3. Diploma in Hydrology and water well drilling
4. Diploma in water supply and sanitation engineering
5. Diploma in water quality laboratory
Chuo kinatoa kozi mbali mbali za ngazi ya cheti. Chuo kwa kushirikiana na serikali, wanaandaa mkakati ili wanaomaliza masomo yao katika chuo hiki, waajiriwe moja kwa moja na serikali kupitia wizara ya Maji.
Chuo kina scholarship/sponsorship kwa watanzania katika ngazi ya diploma, kupitia WATER TECHNICIAN FUND, ofisi zao zipo ndani ya chuo cha Maji Ubungo.
Chuo kipo Dar es salaam, eneo la Ubungo, kutoka barabara ya Sam Nujuma kuelekea barabara ya chuo kikuu, inayopitia geti Maji.
Karibu Chuo cha Maji Ubungo, Dar es salaam.