Kariakoo kwachafuka, maduka yafungwa...

JoyPeace

Member
Oct 18, 2012
66
49
Vurugu kariakoo..

Ni habari za kweli mi niko ofisini ila kuna mtu ana spouse wake kampigia simu kuwa hali si shwari, mabumu na vya moto tinatembea huko! Mungu atuepushe na nguvu za shetani hizi! maana hapo hakuna uungu ni shetani mwenyewe!!

=================
UPDATES
=================

Kwa picha za matukio maeneo mbalimbali fuatilia: Picha: Yaliyojiri Dar na kwingineko leo mchana

Ni kweli nimepata taarifa tayari kariakoo waislamu wameshakinukisha, kuna mabom na helkopta ya polisi inatanda anga la kariakoo, cha muhimu ni kuchukua Tahadhali hapo ulipo, kuepuka vurugu hizo
Nikiwa maeneo ya Magomeni naziona gari nne aina ya roli zenye wanajeshi wa kutosha wakiwa na silaha za kutosha wakielekea mitaa ya Kariakoo/Jangwani.

Kwa upande wa hapa Magomeni, msikiti wa kichangani wametulia baada ya FFU kupiga mabomu ya machozi matatu na gari la kuwasha limepaki katika mlango wa kuingilia msikitini.
Malori ya Polisi katika picha:
attachment.php


Natimiza haki yangu ya raia mwema,

Jamaa wa JWTZ wanaingia na mafuso mitaa ya Jangwani wakitokea njia ya kigogo. Aidha kuna DCM kama 5 zilizowashusha waislam zinawasubiri

Kipeperushi hiki kimesambazwa maeneo ya Kariakoo na Magomeni kuanzia jana.

attachment.php

Nipo hapa ktk mtaa wa uhuru na msimbazi, hali ni mbaya,mabomu yanapigwa hovyo na police, hali ni ya wasiwasi wanainchi wanakimbia hovyo.

Police wametanda mitaani zaidi ya mabomu 30 ya kutoa machozi yamelipuliwa na bado wanaendelea kupiga.gari la police linapiga kingora kuwasihi raia wote waondoke eneo la kariakoo. Kwa kweli hali ni mbaya, maduka yote yamefungwa.

Kisa ni maandamano ya waisilamu yaliyopangwa kufanyika leo.
 

Attachments

  • jwtz.jpg
    jwtz.jpg
    36.8 KB · Views: 10,993
  • kipeperushi.jpg
    kipeperushi.jpg
    80.9 KB · Views: 6,848
nipo maeneo ya kurasini, kuna helkopta ya polisi imepita katika anga hili muda huu. Sijui inaelekea wapi?
 
Mkuu piga picha hata kama ni simu ya mchina inatosha kutuhabarisha sisi tulio makorongoni kupata news.
 
Mitaa ya Mchikichi, Congo, Msimbazi, Aggrey kute kumenuka.
 
Jamani hapa kariakoo maeneo ya Bigborn kuna FFU wa kutosha. baadhi ya askari walikuwa wanashauri watu wafunge maduka. Duh! hawa watu wanataka kuwa na nguvu zaidi ya polisi sasa. Sijaweza kubaki sana kuona kinachojiri kutokana na usalama wangu.
 
Back
Top Bottom