Karani wa sensa...

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Ni mtu anayefuata kwa ubovu baada ya kichaa, anapata shida sana kutafuta poi la kujitambulisha, espeshale mwenye nyumba anapokuwa amekunja uso wa ndimu.
Anaongoza kwa kuwa na vitu vingi ambavyo havina msaada katika maisha ya kawaida.
Ana kalamu ya risasi aina ya 2HB, ambayo hata yeye hajui kwanini anaitumia, sanasana ukimkazania atakujibu "Ni kwa madhumuni ya sensa."
Teh teh teh... Ana mabegi mawili, wakati moja pekee latosha kuweka mizigo yote aliyonayo.
Anakuwa ameweka chaki mifuko yote, ana makaratasi ambayo hajayapanga kwa utaratibu kiasi kwamba hata yeye mwenyewe hajui lepi limewekwa wapi. Mara nyingi ukimuona ni kama mtu asiyejua mahali anapoenda, akijaribu kugonga mlango huu na ule... Loh!
Mara nyingi amechoka na kukata tamaa, miguu ikiwa na vumbi kama vile anauza bidhaa za promosheni.
Basi tu, karani wa sensa ni mtu wa kumuonea huruma na kumpa ushirikiano wote anaostahili.

8.jpg
 
Pole yao, lakini hao wapemba kwani huwaga wanafanya nini majumbani kwao?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom