Elections 2010 Karagwe: Matokeo kutangazwa?

Niko hapa niulizen mimi polisi utadhan wanao wapiga mabomu ci watz wenzao,inatia aibu.

Tupo pamoja, tunawaombea. Mungu hatawaacha waonevu watawale! Hawa jamaa wanajiona kama miungu vile. Eti wanaamua hatma ya watu bila ridhaa yao.

Tupe maendeleo.
 
Nguvu ya dola imetumika kubwa sana kuwatawanya umati uliokuwa pale, ila watu hawakwenda mbali. mabomu ya machozi, blancoo, na mabomu mengine yenye mlio mkubwa sana.
Wananchi wameamua na nadhani watarudi kuendelea kushinikiza
Naona mtandao wangu ni mbaya, nashindwa kuweka picha. Niki-click kwenye manage attachments, hakuna display inayokuja
Mwandishi wa habari wa radio karagwe aliporipoti mabomu yaliyokuwa yanaendelea kupigwa na kueleza kuwa nguvu imetumika nyingi bila ya sababu polisi walimsikia na kum-arrest, lakini naona waliogopa nguvu ya umma - hawakumweka ndani.
 
Kama kweli Blandes wa ccm ni mzalendo na Mtanzania mpenda amani kwanini asishauriwe ku conceed defeat ni rahisi, akifanya hivyo matokeo yatatangazwa kuwa chadema imeshinda na wananchi watawanyika. Hata mtoto wa kindergaten ata reason hivi. Kwa nini wananchi wafe, damu imwagike kwa ajili ya kuridhisha watu wachache???? Inaonesha ccm wanajali zaidi madaraka kuliko watu wake, ukweli unajionesha.
 
Mawakala wa chadema wasitoe mguu hapo hata ikibidi wasiende ****** au kunywa soda kama mkwere alivyo jibu waandishi huko msoga eti ukidanganywa kwenda kunywa soda huku nyuma wenzio waaaharibu!ha ha haa mkwere kumbe anakubali kweli wana kwiba!
 
Kwa kweli nimewafurahia sana wa Karagwe, Biharamulo etc
Sio wahaya wa Bukoba ambao bado wamelala macho wamefunga u nshomile umewaisha, mji umeingiliwa na watu wa makabila mengi

I guess ni kesho hiyo au sijui lini, jamani wana Karagwe hiyo ni kuonyesha wanajaribu njia zote kubadilisha votes msivunjike moyo:nono:
 
Sasa hivi ni saa 5.50 asubuhi tarehe 3/11/2010, matokeo bado hayajatangazwa. Kuna taarifa kuwa tume imewaita waandishi wa habari ili kuwaeleza kinachoendelea.
 
nimepost kuwataarifu chama cha demokrasia na maendeleo kimeshinda karagwe ila iyo post siioni. Ni habari ya kweli kabisa

matokeo yametangazwa na sherehe zimeanza kuelekea nyumbani kwa mh mbuge uko kituntu!

Mbuge anaitwa mh. Deusdedith kahangwa

du! Tunakushukuru mungu, sijaona majitu makatili kama ya ccm, kama kweli kuna watu waliwapigia kura watakuwa wamerogwa!!!
 
Lete Matokeo kamili Yaliyotanganzwa na mteule wa rais(Mkurugenzi) kwani kazi zao ni kuchakachua,
 
Mawakala wa chadema wasitoe mguu hapo hata ikibidi wasiende ****** au kunywa soda kama mkwere alivyo jibu waandishi huko msoga eti ukidanganywa kwenda kunywa soda huku nyuma wenzio waaaharibu!ha ha haa mkwere kumbe anakubali kweli wana kwiba!


CCM uwepo usiwepo ni sawa tu. Maana wao 1 ni 10000 na 10000 ni 1. Huwajui
 
In short hilo jimbo since 2005 lilibidi liende kwa CHADEMA, but kutokana na wananchi hawakua na mwamko wa kutosha kama hivi sasa, matokeo yalibadilishwa usiku wake. But this time wananchi wa nyumbani karagwe wamesema BIIGG NNNOOOO, hatutaki mpaka kieleweke mshindi wetu tunamjua tumemchagua wa CHADEMA not CCM huyo Blandness.
 
matokeo hatimae yametangazwa; Blandes wa CCM ametangazwa mshindi kwa tofauti ya kura 6,000. Watu wamebaki na mshangao kwa tofauti kubwa hivyo kutoonekana tangu jumatatu!
 
Back
Top Bottom