Elections 2010 Karagwe hapatatosha KAHANGWA ndani ya ulingo

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetupilia mbali pingamizi alilowekewa mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe kupitia Chadema, Deusdedith Kahangwa.

Kwa mujibu wa barua ambayo gazeti hili limeona kivuli chake, mrufani, amerejeshwa rasmi kuwa mgombea halali wa ubunge katika jimbo hilo.

Awali Kahangwa aliwekewa pingamizi hilo na CCM na NCCR Mageuzi ambavyo vilidai kuwa mgombea huyo hakudhaminiwa na chama chake na kuwa alijaza majina yake katika sehemu iliyotakiwa kujazwa na Katibu wa chama hicho.

Madai mengine katika pingamizi hilo ni kutodhaminiwa na wanachama, ambayo yamepuuzwa na Nec kuwa hayana msingi.

“Kama wanachama walirubuniwa kumdhamini, basi walipaswa kupeleka malalamiko yao kwa Msimamizi wa Uchaguzi kabla ya pingamizi kupelekwa kwa msimamizi huyo,” ilieleza barua hiyo ya Nec.

Kuhusu madai kwamba mgombea hakudhaminiwa na wapiga kura, Nec imesema kuwa fomu zinaonesha kuwa Kahangwa amedhaminiwa na wapiga kura 31 na msimamizi wa uchaguzi alithibitisha hivyo.

Kushinda rufaa kwa Kahangwa jimboni humo, kunatazamiwa kuleta chachu ya ushindani wa kisiasa kwani Chadema inaonekana kuwa na nguvu zaidi ya vyama vingine vya upinzani jimboni humo.
 
Yaani hapo umesema ukweli Luteni. Nilipita hapo na msafara wa JK wakati huyo Deusdedith Jovin Kahangwa akiwa bado amefungiwa na msimamizi wa uchaguzi, lakini alishindwa kumnadi mgombea wa Karagwe Gozibert Blandes.
Blandes anakabiliwa na kesi mbaya ya Rushwa ambayo imekamilika kusikilizwa inasubiriwa hukumu. Karagwe pamekucha kwa sababu huyo kijana anatisha akisimama ulingoni.
 
Mimi naomba isiishie tu kuwarudisha, next move ya CHADEMA au chama chochote cha upinzani ambacho kitakubaliwa rufaa yake, waandike barua ya kutokuwa na imani na msimamizi wa uchaguzi kwenye jimbo husika. Kwa mfano, Msimamizi wa Jimbo la Singida Mjini ambaye alidai kwamba hakukagua vyema sehemu ya wadhamini, NEC ikasema hakutoa maelezo kwanini hakukagua sehemu hiyo [huo ni uzembe au alifanya makusudi kwa malengo yake binafsi].

Wasimamizi kama hawa wanakuwa wameishaonyesha kwamba wanaelemea upande gani tangu mwanzo, maana kuna makosa mengine ambayo sioni kama ni ya msingi. Mfano mtu kukosea kujaza tarehe yake ya kuzaliwa sehemu ambayo sio. Ni jukumu la msimamizi kuikagua fomu inaporudishwa ili kama ina mapungufu au makosa, isahihishwe ama kurekebishwa siku inaporejeshwa. Mapingamizi mengi ninayaona ni ya kulengeshana tu na yana ashiria dalili mbaya.
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetupilia mbali pingamizi alilowekewa mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe kupitia Chadema, Deusdedith Kahangwa.

Kwa mujibu wa barua ambayo gazeti hili limeona kivuli chake, mrufani, amerejeshwa rasmi kuwa mgombea halali wa ubunge katika jimbo hilo.

Awali Kahangwa aliwekewa pingamizi hilo na CCM na NCCR Mageuzi ambavyo vilidai kuwa mgombea huyo hakudhaminiwa na chama chake na kuwa alijaza majina yake katika sehemu iliyotakiwa kujazwa na Katibu wa chama hicho.

Madai mengine katika pingamizi hilo ni kutodhaminiwa na wanachama, ambayo yamepuuzwa na Nec kuwa hayana msingi.

"Kama wanachama walirubuniwa kumdhamini, basi walipaswa kupeleka malalamiko yao kwa Msimamizi wa Uchaguzi kabla ya pingamizi kupelekwa kwa msimamizi huyo," ilieleza barua hiyo ya Nec.

Kuhusu madai kwamba mgombea hakudhaminiwa na wapiga kura, Nec imesema kuwa fomu zinaonesha kuwa Kahangwa amedhaminiwa na wapiga kura 31 na msimamizi wa uchaguzi alithibitisha hivyo.

Kushinda rufaa kwa Kahangwa jimboni humo, kunatazamiwa kuleta chachu ya ushindani wa kisiasa kwani Chadema inaonekana kuwa na nguvu zaidi ya vyama vingine vya upinzani jimboni humo.
Safi sana
 
Ngoma inogile . . . moja baada ya nyingine . . . kama gobole livyotungua.

Yote tisa, kumi ni 31st October 2010.
 
Baada ya kurudishwa ulingoni, mgombea wa CCM anasemekana alienda kujikita sehemu inayoitwa bushangaro kwani alishatangaza kuwa hataakiweka koti tu atashinda.
Kahangwa tunamuamini.
 
Back
Top Bottom