KAPUYA ana hali ngumu KALIUA

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,146
884
Mgombea ubunge wa Urambo Magharibi kupitia CCM Prof. Juma Kapuya ana hali ngumu sana katika jimbo la Kaliua, hali ambayo imemlazim kutegemea vyombo vya dola kudhibiti wapinzani. Hakika wananchi hawamtaki kabisa kutokana na tabia ya wafuasi wake kuwapiga wananchi wanapouliza maswali magum kwenye mikutano yake ya kampeni, kwa madai kuwa wananchi hao eti wametumwa. Wiki jana imetokea fujo kubwa sana Kaliua baada ya kijana mmoja kuuliza swali gumu, ambapo Kapuya aliposhindwa kujibu alimtukana "******" ndipo wananchi wakachachamaa na kuanzisha fujo kubwa, polisi wa kaliua wakapiga risasi zaidi ya 10 hewani lakini wapi, ikabidi waombe msaada Polisi Urambo, nao wakaenda wakapiga mabomu na risasi zaidi ya 30 kutisha watu, wananchi wakatawanyika, ikawa sasa mtu yeyote anayeonekana amevaa nguo za CCM ni kichapo tu, hali iliyopelekea watu kutembea vifua wazi kwa usalama wakati wanaelekea makwao, Jana yamepita magari ya Jeshi(JWTZ) yanaenda Kaliua, hali ya hatari imetangazwa hapa kaliua, mwisho wa kutembea ni saa mbili usiku, ukikamatwa unawekwa ndani, Kapuya anatumia ubabe sana, HATAKIWI, anaetakiwa ni mgombea wa CUF Anayeitwa KIRUNGI. hivi jamani hii ni HAKI?
 
Picha tafadhali, unajua mkuuu matukio kama haya ndo yenyewe kwanza yatakuweka juu ktk kumbu kumbuzetu za JF hapa jamvini, kwa hiyo kama una picha za kash kash hizo weka picha hizo hapa. Ahsante kwa taarifa, kapuya hatakiwi muda mwingi sana, apumzike huyo mzee ndo aliyefanya mitihani ya Form Four 1998 ikaliki vibaya sana.
 
haha kapuya alikuwa anajali familia yake tu na baadhi ya watu...sasa wamemstukia
 
Kuwenu kama wanaume wa tarime,musoma moshi mbeya na kwingineko
nguvu na maombi toka mungu vitawaokoa tu.
Lakini kimbia hao askari hakikisha usidondoshe kadi yako ya kura
siku hiyo ndio ummalize huyo kapuya.
 
Siwezi kuweka picha mtanisamehe kwa sababu sina kamera. Habari ni za kweli kwa sababu nilikuwepo kwenye tukio. Hadi sasa mgeni yeyote atakiwi kuingia kaliua, akionekana mtu mgeni anakamatwa na kuhojiwa na vyombo vya dola. Pia mwanae na Kapuya aitwae Baraka imebidi atoroshwe kwa sababu wananchi wakimkamata wataua, yeye pia amekuwa katili sana na kundi lake kupiga watu hovyo na kuchukua wake za watu, mwaka jana aliua watu wawili kwa risasi ambapo ilitokea ghasia kubwa sana kama ya wiki jana, lakini vyombo vya dola vikafichaficha kumlinda, hadi sasa huyu Kijana ni WANTED na wananchi. Haijulikana KAPUYA kamkimbizia wapi. Mwaka huu ama zake ama za wananchi, wameapa wanyonge.
 
Mgombea ubunge wa Urambo Magharibi kupitia CCM Prof. Juma Kapuya ana hali ngumu sana katika jimbo la Kaliua, hali ambayo imemlazim kutegemea vyombo vya dola kudhibiti wapinzani.

Mwisho wa CCM ni tarehe 31 Oktoba
 
Alinufaika na hela za kashfa ya manji na NSSF alipokuwa Waziri wa Kazi na Usitawi wa jamii kabla ya JK kuingia na kumpa uwaziri wa ulinzi ambayo aliiboronga kwa kupiga raha na ndege za jeshi hilo na ununuzi wa helikopta feki zilizokuwa zinaanguka hovyo.

Ni yeye aliyetangaza hivi karibuni kwamba tangu JK aingie madarakani hadi sasa zimepatikana ajira 1.3 milioni. Dr Slaa alimchallenge akihoji hizo ni ajira zipi kwani kuna vijana wanatembea na digrii zao lakini hawana kazi. Alimuomba kapuya aonyeshe orodha ya ajira hizo.

Mie jamani simpendi kabisa Kapuya.
 
Habari za kutia moyo. Hv Kaliua ni kata au? Kama ni kata, vp kwenye kata zingine? Endelea kutujuza. Kapuya ni kati ya mawaziri mbumbumbu licha ya kuwa Prof
 
cuf wazidishe nguvu pale wanapo ona kupata matumaini ili wapate wabunge wengi bara ama sivyo wataambulia madiwani tupu kwa mara nyingine
 
Leo nimepata wasaa wa kuongea kwa kirefu na jamaa yangu anayetokea kijiji cha Vumilia kilicho katikati ya Urambo kwa Samuel Sitta na Kaliua kwa Prof. kapuya kwa kweli huyu Profesa anatumia vibaya madaraka na pesa alizonazo kuwanyanyasa mananchi wa Kaliua waliomfikisha hapo alipo. Jamaa yangu alinieleze jinsi Prof. kapuya na mwanaye Baraka wanavyowanyanyasa wapinzani kwani maji yashawafika shingoni. Wakikuta mikutano ya CHADEMA inafanyika wanawavuruga kwa kutumia polisi na kuwapa vichapo wananchi bila hata huruma. Alieleza kuwa hivi karibuni kuna eneo lililo umbali wa kilometa 64 linalotakiwa kutengwa kama hifadhi ya taifa ambapo askari game walienda na silaha kuwafukuza wananchi wa hapo na ndipo zikatokea vurugu kubwa sana na ikabidi wale askari watumie silaha na waliuua watu zaidi ya 20 na habari hii ikazimwa kimya kimya ila wananchi wa Kaliua wanalifahamu hili fika. Pia mwanaye Baraka yaani yeye ndio yeye huko Kaliua wananchi wananyanyaswa sana na mibangi yake kwani anadiriki hata kuwapiga vibao polisi pindi wanapomsimamisha barabarani na hadi sasa amekwishafanya mauaji ya watu wasio na hatia watatu bila kufanywa chochote. Mwaka juzi alimpiga jamaa mmoja kwenye club yake ya usiku baada ya kutaka kumnyang'anya demu wake jamaa ambaye alikuja kufarika baada ya kulazwa hospitali ya wilaya ya Urambo kwa siku mbili. Kama hiyo haitoshi mwaka jana mwezi September alimuua mwanafunzi aliyekuwa kwenye disco la kumaliza kidato cha nne kwa risasi na ikasingiziwa ni mlinzi wake (yuko ndani hadi sasa). Tukio hilo liliwakasirisha sana wazee wa Kaliua wakamtengeneza jamaa akawa kama chizi, amabapo abbake aliahangaika huku na kule hadi Nigeria kutafuta mganga wa kumtibu na kufanikiwa. Hivi juzi mnamo mwezi July Baraka akitokea ulyankulu kuelekea Tabora alimgonga kwa makusudi mpita njia na kumsababishia kifo pale pale na polisi hawakumfanya kitu.


Hoteli ya Kapuya yashambuliwa, mwanawe chupuchupu


Mtoto wa kapuya na mauaji ya mwanafunzi Tabora


Polisi yamsafisha mtoto wa Kapuya


Sasa nauliza hivi nchi hii wanyonge tutaishia kunyanyaswa hadi lini na wenye madaraka na pesa na je jeshi la polisi linafanya kazi gani kudhibiti wauaaji kama huyu Baraka Kapuya? Iko Siku haya manyanyaso yataisha Inshalllah... Stay tuned more to follow...

I'd rather die as a man than live as a coward -Tupac Amar Shakur (R.I.P)
 
Siwezi kuweka picha mtanisamehe kwa sababu sina kamera. Habari ni za kweli kwa sababu nilikuwepo kwenye tukio. Hadi sasa mgeni yeyote atakiwi kuingia kaliua, akionekana mtu mgeni anakamatwa na kuhojiwa na vyombo vya dola. Pia mwanae na Kapuya aitwae Baraka imebidi atoroshwe kwa sababu wananchi wakimkamata wataua, yeye pia amekuwa katili sana na kundi lake kupiga watu hovyo na kuchukua wake za watu, mwaka jana aliua watu wawili kwa risasi ambapo ilitokea ghasia kubwa sana kama ya wiki jana, lakini vyombo vya dola vikafichaficha kumlinda, hadi sasa huyu Kijana ni WANTED na wananchi. Haijulikana KAPUYA kamkimbizia wapi. Mwaka huu ama zake ama za wananchi, wameapa wanyonge.

Muuaji kwa upanga naye atakufa kwa upanga Mungu yupo
 
Mfunyukuzi Mkuu, ahsante kwa taarifa, mimi najiuliza kuna nini huko Tabora hadi Kapuya akae miaka yote hiyo bungeni, wakati bado hatusikii Tabora imeendelea kiviwanda, kielimu nk. Jamaa wanaonea wananchi sana hawa, pamoja na kusoma kwake hana la kufanyia watu zaidi ya kuwahonga pombe za kienyeji na kufanya uhuni na dada zetu. Kapuya, ng'atuka sasa.
 
Nyamizi,

Kama wewe una habari hizi, basi hizi ni za kweli haswaa. Nilikuwa nasubiri comment zako na sasa nimeziona.

Huko Tabora kwetu huko, ni matatizo matupu. Wanyamwezi wakiamka, nchi italipuka. Heri tubaki tumelala.
Ni kweli kabisa,hata mimi nimeongea na jamaa yangu ambaye yupo huko na kaniambia fujo hizo zilitokea tarehe 11
 
Mfunyukuzi Mkuu, ahsante kwa taarifa, mimi najiuliza kuna nini huko Tabora hadi Kapuya akae miaka yote hiyo bungeni, wakati bado hatusikii Tabora imeendelea kiviwanda, kielimu nk. Jamaa wanaonea wananchi sana hawa, pamoja na kusoma kwake hana la kufanyia watu zaidi ya kuwahonga pombe za kienyeji na kufanya uhuni na dada zetu. Kapuya, ng'atuka sasa.

Umenena mkuu jamaa na Uprofesa wake hafai kabisa na wananchi wa Kaliua wamemchoka sasa
 
Back
Top Bottom