Kapteni anapo omba kutoguswa (immune) ili aokoe “Air Tanzania”

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
128
Abiria wako kwenye ndege ambayo imetekwa nyara na wahudumu (Flight Attendants) wa ndege hiyo. Wahudumu hao wakishirikiana na kapteni (au pengine wamemrubuni kapteni) wamefanikiwa kuiteka ndege hiyo na kuipeleka siko ndiko.

Abiria wanahangaika kutafuta njia ya kujikomboa. Wanawasihi watekaji nyara either wawafikishe salama wanakokwenda au watue chini kwa dharura ili abiria wapate kutafuta kapteni na wahudumu wengine ambao watafaa kuwapeleka wanakotaka kwenda.

Ombi la abiria linaleta mkanganyiko. Mgongano baina ya watekaji nyara (wahudumu na kapteni) unaanza kuleta mgawanyiko kati yao. Zoezi la utakaji nyara linaelekea (au linaonekana kuelekea) njia panda.

Abiria wanazidi kuweka msukumo wa kutaka waachiwe huru….

Kapteni, kwa siri, anapeleka ujumbe kwa abiria. Ujumbe huwa unasema hivi:

"Ndugu abiria, kwanza napenda kuomba msahama kwa adha yote hii mliyoipata toka muda tuliopaa angani. Kwa kweli ninajisikia vibaya sana kuona kwamba, mimi kama kapteni wenu, nimeshindwa kuiongoza hii ndege katika hali inayotakiwa. Badala yake nimeshirikiana na nimeendekeza tamaa za timu yangu ya wahudumu kuiyumbisha safari yenu. Sahamanini kwa hilo."

Kisha ujumbe unaendelea:

"Niko tayari kujirudi. Niko tayari kutumia nguvu zangu za ukapteni na kuiokoa ndege hii. Kwa baraka, rukhsa, na ushirikiano wenu; ningeomba nianze kuwapa adhabu wahudumu wangu hawa ili niweze kuifikisha safari yenu kunakotakiwa."

Ujumbe huo unaendelea tena:

"Nina ombi mmoja kubwa kwenu. Kutokana na mimi mwenyewe kuwa sehemu ya utekaji nyara huu, nina wasiwasi kuwa mfikapo mwishoni mwa safari yenu, mnaweza kuniadhibu na mimi pia. Kwa hiyo, ili niweze kutekeleza uokoaji wa ndege hii kwa usanifu mkubwa, ningeomba mniondolee wasiwasi wa kuniadhibu."

Je watanzania tunaweza kumsamehe JK pindi akiomba ‘immunity' ili aweze kuwashughulikia mafisadi? Je tuko tayari kumlinda kama akiwageuka marafiki zake ambao wanatumia urafiki huo kum-control na kutumia resources zetu kwa manufaa yao binafsi?

Tuko Tayari?
 
Tutamtaka akaungane na kina zombe kule rupango, na immune atapewa na jaji kwenye hukumu itakayoendana sawa sawa na matendo yake
 
Tutamtaka akaungane na kina zombe kule rupango, na immune atapewa na jaji kwenye hukumu itakayoendana sawa sawa na matendo yake

Kwenye hii kesi majaji tutakuwa sisi watanzania wenyewe. Yaani tuwe tayari kuhakikishia sio tu tutamwachia huru, bali pia tutamlinda. Hapo ndipo atapo iokoa Air Tanzania.
 
Kwanza awakamate na kuwashughulika tuone alichokifanya ndio aje kwa abiria msanii huyu atasema nitafanya hiki kisha afanyi bora kesha jihakikishia! Tena msinipe mimi hiyo nchi nakwambia itakuwa hakuna cha msalia mtume eti niliwaambia warudishe pesa za epa kisha nikawasamehe! tena naanzia na che Nkapa kabisa huko!
 
Nadhani bora mkosaji anayejirudi kuliko "anayehalalisha" makosa. Na pia kama gharama ya kuwakamata hao wengi ni kumwachia mmoja, it is worth it, tumpe hiyo "immunity".
 
Je ataaminikia? Je ana nia ya kweli au ni kuzuga? mpaka pale Rubani atakapoweza rudisha imani kwa abiria na wasimhisi kuwa anawadanganya, ndipo anaweza kusameheka kwa kwa urahisi.

Mpelekee huo ujumbe!
 
Nadhani bora mkosaji anayejirudi kuliko "anayehalalisha" makosa. Na pia kama gharama ya kuwakamata hao wengi ni kumwachia mmoja, it is worth it, tumpe hiyo "immunity".

Yeah I guess I can have a change of heart then for the "greater good"!
 
Je ataaminikia? Je ana nia ya kweli au ni kuzuga? mpaka pale Rubani atakapoweza rudisha imani kwa abiria na wasimhisi kuwa anawadanganya, ndipo anaweza kusameheka kwa kwa urahisi.

Mpelekee huo ujumbe!

Of course, pengine abiria watataka kuona vitendo kwanza kabla hawaja grant hiyo immunity.

As much as ninamwona JK ni disaster, ninaamini kuwa anaweza kujirudi. Ninaamini kuwa anaweza kabisa kusimama kidete na kuwaadhibu wale wote (pamoja na marafikiri zake) wanaoiyumbisha Air Tanzania. Kama akiweza kufanya hivyo, basi kwa uhakika atahitaji ulinzi wa hali ya juu. Kwa maana, marejuhi watageuka mbogo....
 
Hana lolote bwanaa....atuachie nchi yetu...Nchi imeshamshinda...Uraisi si rahisi ....
 
Back
Top Bottom