Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
Hivi kumbe bado tunaishi kwa amri za wanasiasa, siyo sheria tena?!
Actually mimi naona kuwa na ringtone ya Mungu Ibariki ni moja ya njia za kuonyesha uzalendo wako kwa nchi yako. Lakini hili lijamaa halioni hilo.....jamaa shamba kweli yaani....
Yaani hili ndio ovyo kabisa, halafu linatoa amri linafikiri tupo jeshini hapa, kero kubwa sana haya majamaa!
Tatizo Watanzania hatuna utamaduni wa kuonyesha uzalendo wetu....sasa mijitu kama hili li Mkuchika inakuwa inapata culture shock ya aina fulani hivi inapoona vijana au watu tu kwa ujumla wanapoanza kuwa patriotic na ku display patriotism kwa njia mbalimbali kwa kutumia teknolojia. Sasa sijui jitu kama hili likiona bikini za bendera ya Tanzania zinauzwa madukani si linaweza likazimia kabisa.....Lol
.....Bora wakatali kuliko kuwa kama wale waliokwenda Mauritius!!!Hivi bado tunayo timu itakayotuwakilisha katika Olimpiki au ni watalii tu?
.....Bora wakatali kuliko kuwa kama wale waliokwenda Mauritius!!!
Uliona wapi wachezaji 10 viongozi wa msafara 20????
... Nimekubali Sikonge,Kipanga,
Tembea uone ndugu yangu. Huko SOMALIA kuna rekodi za aina nyingi tu. Kama ni kuona basi TUMEIONA Tanzania. Na Somalia, kwenye watu WAWILI basi kuna VYAMA VYA SIASA VITATU.
Siku moja nikiwa vichochoroni nchi za watu, ghafla nikaona AFRICA mbele yangu. Yes, jamaa wameibeba Africa nzima. Kuangalia nguo zao nikaona Wakenya. NikawasalimiaHAMJAMBO NYIE WAFUKUZA UPEPO? Jamaa walikuwa wengi aisee. Ila matokeo yake unayaona. Na sisi siku moja mambo yatakuwa MSWANO tu na kupeleka wachezaji 15 na viongozi 17.
Hii naona itakuwa Top topic katika mwezi huu ,dah ,yaani nchi nyengine zina Mawaziri wanazungumza mambo yakaeleweka na wananchi kuyatia akilini lakini hapa Tanzania sijui tumekosa nini kwa Mungu , yaani hata kusema ndio chaguo la Mungu basi naona utakuwa unapata zambi,yaani Mungu ndio katuchagulia watu wa ajabu ajabu kabisa , aisee ,nchi zenye Deokrasia basi huyu Waziri alikuwa ajiuzulu moja kwa moja ,hafai kuwa Waziri ,inaonyesha huyu anaichukia Tanzania ile mbaya ,hapendi kusikia hata huu wimbo wetu wa Taifa ,sasa aulizwe wimbo aliousikia kwenye hizo simu ni wa Africa ya Kusini au Zambia au wa Afrika ?Jamani waandishi na wana habari mtwangeni huyu zezeta hili suali.... Nimekubali Sikonge,
Ngoja warudi usikie nyimbo zao Oohh!!! mara kulikuwa na moshi mwingi vijana wameshindwa kukimbia, mara bara bara zina mashimo mengi, maji ya China sio vugu vugu waogeleaji walikuwa wanasikia baridi mwisho wao utasikia tumeitangaza Tanzania na Mlima K'njaro!!!....Kila mtu ana mabegi 8.....Hivi sio ufisadi huu jamani???