Kapt. Mkuchika na Maagizo yake!

Wataka waandishi wasomi wakati hata hao wanaowaita hawajasoma wakiwauliza maswali muhimu wanabaki kurushiana mpira.
Mwandishi gani aliwahi kuhoji wazi wazi mambo ya EPA,Rochimond,BOT na wenzake....kama si zaidi ya Kubenea na mwanahalisi.....Waandishi wa Bongo Makanjanja wasome wapanue mawazo yao mgando......bravo Mkuchika
 
Unafikiri sababu kubwa ya magazeti serous hayauzi ni hiyo?.....jiulize kwanini vitabu vya kupanua mawazo haviuziki hapa Bongo kuliko vile vya hadithi za Shigongo? hata magazeti kama raia mwema haliuzi sana kama magazeti pendwa kama kasheshe na wenzake

Watu hawataki kuumiza vichwa, wanafuatisha falsafa za Marijani Rajab zenye hekima ya mfalme Suleiman katika wimbo wake (Marijani) "Sikia Mambo"

Anavyosema "kula ugali wako ukalaleee"

Sasa utamwambia mtu hajala hajaenda shule halafu hajawahi kufanyiwa checkup maishani mwake kuhusu muungano na katiba na mageuzi na mambo abstract kama hayo? Wakati hela ya kuweka mambo ya mlo sawa inapiga chenga? Si bora ajidunge na Shigongo tu?
 
Alafu kuna kitu kingine hawa waandika habari wananikera...habari zao hazina uchunguzi na si za kitaalam.....najaribu kuangalia mwandishi gani anaeandika habari za financial sijaona.....huyu kaly Lyimo siku hizi haeleweki....

Huyu Ayubu Lyoba ambae ni mwalimu wa wandishi wa habari nae hana jipya...kipindi chake cha sema usikike hakina la yaani hajakifanya kiwe talk show kama tunazoziona ughaibuni
 
Yoyo unasema ni WEWE...Lakini Yo Yo ninayoifahamu ni ile inayo bounce kadri inavyopigwa..I mean kimwelekeo.
Any ways...Mawazo mazuri...Lakini Agustoos amelielezea vizuri sana...Ndugu yangu ili bounce kama Yo Yo juzi tu ulipodai eti ulinipa ushauri.
Naomba usiwe kigeu geu tena...Ni bora u reserve point kuliko kukurupuka!
Mimi naamini nilionewa...Lakini wewe ukajidai kunigeuka..Uliniandikia PM nilipofungiwa mwanzoni na nilikueleza sioni ni kwanini nilifungiwa.
Kama hatutapata watu wenye PRINCIPLE kwenye mpambano...Watu wa HUSDA....Tanzania haitakombolewa.
 
Vyeti, vyeti, vyeti! Tanzania tunapenda vyeti kama tunavyopenda ulabu na uloda as if it really matters!

Nimelifikiria tamko la Mkuchika kwa upande mwingine si wa kisiasa bali ni wa kielimu.

Nitaanzia hapa ndani uwanja wa fujo. Kila mmoja wetu ana utaalamu wa kuongea, lakini ukiangalia uandishi wa hoja na dataz, unagundua haraka haraka kuwa mtoa hoja, hajafundishika katika suala la uandishi. iwe ni insha au majibu ya kitu, kuna kuchanganya vituo, matumizi mabaya ya herufi kubwa na ndogo, mkazo na maandishi yasiyolingana alimradi mtu kaamua kujiongelea na kutoa maoni.

Sasa kama hapa JF tunatapia hizo hatutumii kanuni tulizofunsishwa tangu shule ya msingi hata kuangalia kuwa maneno tuliyoandika tunayapitia kuyasoma tuyaelewe kwanza sisi wenyewe kabla ya kumpa mtu wa nne ayasome, tunafikiriaje Waandishi wa habari Tanzania watakuwa na tofauti na sisi?

Si sisi wana JF tunaojivuna vifua mbele kuwa tumesoma, tunajua mambo mengi, sasa kama kanuni rahisi za uandishi (writing) zinatushinda, je hao wa Tanzania watakuwaje, wawe wamesoma TSJ Buguruni au UDSM?

Matatizo ya magazeti na Televisheni kuonekana kuwa ni vihiyo si kosa la aliyeajiriwa kama mwandishi, ni makosa ya mwenye mali na mhariri wa idara na mhariri mkuu.

Kama Mkuchika lengo la kutoa kauli yake ni kuhusu uhakiki wa habari kupitia wahariri na wahariri wakuu, ndipo basi kuna haja ya kuwa na waliosomea Taaluma ya Uandishi na wanajua umuhimu wa habari kufanyiwa tahariri na hata wale wanaoajiriwa kama waandishi wa makala, utangazaji au habari kwa ujumla.

Kwa hili la uhakiki na uhariri, nitamuunga mkono Mkuchika, lakini mnalosema wengine hapa kuwa kuandika makala au kutangaza n ilazima uwe na cheti cha TSj, nafikiri huko ni kujidanganya!

Hivi jamani kuna tatizo gani waandishi kusomea?kwani uandishi wa habari na utangazaji sio taaluma?hapa sasa wakuu ndio tunapoidhalilisha hii fani ya habari,fani hii inatakiwa ithaminiwe kama zilivyo taaluma nyingine ili hawa jamaa zetu wanaotundikia habari waweze kuwa na maisha bora,waweze kudai maslahi mazuri kwa waajiri wao,na waweze kufanya kazi kwa umakini hasa investigative journalism. Tukiangalia kwa mfano hawa waandishi wa BBC,VOA,CNN nk mbona wamesoma sana and they are proud of their professional hata maisha yao huwezi kulinganisha na mwandishi wa bongo.
Tunachokosea hapa ni kuona kwamba eti tukisema waandishi wasome tuna maana wote wawe na digrii hapana,elimu ipo ya ngazi mbalimbali,kuna certificate,diploma,higher diploma,first degree,second,na doctorates sasa tunahitaji waandishi katika ngazi zote hizo hapo juu,na maslahi yao yatofautiane kulingana na elimu na performance.
Pia kinachohitajika sasa ni kuwa na professional body ya kusimamia taaluma ya habari,ili kuoanisha mitaala na kusimamia ufundishaji wake kwa vyuo vyote vya serikali na binafsi, tofauti ilivyo sasa ambavyo vyuo vinavyotoa taaluma hiyo haviko coordinated wala supervised na specific body.Mwandishi hajui hata namna ya kujitetea akiandika habari ambayo mwingine anadhani ni defamatory.Sasa inabidi waweze kujua mbali ya kuandika vizuri pia wajue media law,law of tort,abc za katiba na uhuru wao,pia mipaka yao ili kesho na keshokutwa waweze kutetea maslahi yao.

Ni kwa kufanya hivi pamoja na mambo mengine taaluma hii itakua sana,wote hapa wanahusika wahariri na waandishi junior.
 
Alafu kuna kitu kingine hawa waandika habari wananikera...habari zao hazina uchunguzi na si za kitaalam.....najaribu kuangalia mwandishi gani anaeandika habari za financial sijaona.....huyu kaly Lyimo siku hizi haeleweki....

Huyu Ayubu Lyoba ambae ni mwalimu wa wandishi wa habari nae hana jipya...kipindi chake cha sema usikike hakina la yaani hajakifanya kiwe talk show kama tunazoziona ughaibuni

You know how do you get rid of that? Not by college degrees, you can get all the college degrees in the world and still have sloppy journalism.

First the readership must demand better journalism. In my experience of reading newspapers and magazine, I have realized the more respected a newspaper / magazine is, the more critical its readership is.The readres must keep the editors and reporters on their toes.We do not do this.I seldom see a "baraua ya msomaji" setting the record straight or demanding exoneration.

Second the papers must know that they will bear responsibility for every minute detail they publish.Thats why people have courts and lawsuits can be served.

But you cannot do all or any of that without starting with educational and economic and social paradigm shifts, thats what we need above all.

Build a clientelle, some would say a middle class, that can demand better because it will be educated and will have discretionary income to have the purchasing power that comes with the sense of ownership to enable one to demand better.

Tou can't demand better from Alasiri knowing well that all it took is kinyento (sijui shilingui ngapi siku hizi, so substitute it's current tag)
 
Hivi jamani kuna tatizo gani waandishi kusomea?kwani uandishi wa habari na utangazaji sio taaluma?hapa sasa wakuu ndio tunapoidhalilisha hii fani ya habari,fani hii inatakiwa ithaminiwe kama zilivyo taaluma nyingine ili hawa jamaa zetu wanaotundikia habari waweze kuwa na maisha bora,waweze kudai maslahi mazuri kwa waajiri wao,na waweze kufanya kazi kwa umakini hasa investigative journalism. Tukiangalia kwa mfano hawa waandishi wa BBC,VOA,CNN nk mbona wamesoma sana and they are proud of their professional hata maisha yao huwezi kulinganisha na mwandishi wa bongo.
Tunachokosea hapa ni kuona kwamba eti tukisema waandishi wasome tuna maana wote wawe na digrii hapana,elimu ipo ya ngazi mbalimbali,kuna certificate,diploma,higher diploma,first degree,second,na doctorates sasa tunahitaji waandishi katika ngazi zote hizo hapo juu,na maslahi yao yatofautiane kulingana na elimu na performance.
Pia kinachohitajika sasa ni kuwa na professional body ya kusimamia taaluma ya habari,ili kuoanisha mitaala na kusimamia ufundishaji wake kwa vyuo vyote vya serikali na binafsi, tofauti ilivyo sasa ambavyo vyuo vinavyotoa taaluma hiyo haviko coordinated wala supervised na specific body.Mwandishi hajui hata namna ya kujitetea akiandika habari ambayo mwingine anadhani ni defamatory.Sasa inabidi waweze kujua mbali ya kuandika vizuri pia wajue media law,law of tort,abc za katiba na uhuru wao,pia mipaka yao ili kesho na keshokutwa waweze kutetea maslahi yao.

Ni kwa kufanya hivi pamoja na mambo mengine taaluma hii itakua sana,wote hapa wanahusika wahariri na waandishi junior.

Tatizo ni kwamba wanataka kuiguild fani muhimu sana kwa interest za kisiasa, huoni hili?

Mimi naamini katika freedom of expression, hata mjinga naye ana uhuru wa kujieleza ili mradi havunji sheria.Akivunja sheria mpelekeni kortini.Wajinga wa Tanzania wakiamua kuwa na gazeti lao na waandishi wao, wakawaacha wasomi na gazeti lenu, tatizo liko wapi?

Au wanaogopa hawa wajinga si wajinga hivyo?
 
Hivi jamani kuna tatizo gani waandishi kusomea?kwani uandishi wa habari na utangazaji sio taaluma?hapa sasa wakuu ndio tunapoidhalilisha hii fani ya habari,fani hii inatakiwa ithaminiwe kama zilivyo taaluma nyingine ili hawa jamaa zetu wanaotundikia habari waweze kuwa na maisha bora,waweze kudai maslahi mazuri kwa waajiri wao,na waweze kufanya kazi kwa umakini hasa investigative journalism. Tukiangalia kwa mfano hawa waandishi wa BBC,VOA,CNN nk mbona wamesoma sana and they are proud of their professional hata maisha yao huwezi kulinganisha na mwandishi wa bongo.
Mimi nasema wasome na kusoma sio lazima wawe na vyeti vya taaluma yao......kuna waandishi wengi tu maarufu hawajasomea taaluma ya habari lakini wanafanya kazi zao mpaka unapenda.....unaweza kuwa na taaluma ya biashara ukabobea kwenye habari za biashara....
Au ukabobea katika taaluma ya uuguzi na uka base kwenye habari za uuguzi mfano Dr Sanjay Gupta wa CNN....
 
Kwani kawatukana???? Kama waandishi watalalamikia kauli ya Mkuchika basi ni uthibitisho kuwa wao ni makanjanja!!!! Shule si tusi, ni capacity building!!!!

Hapa hamna issue, hawa jamaa warudi shule tu!!!
 
Mimi naamini habari ni zaidi ya taaluma, it is the fourth estate.

Kwa hiyo, kwa kufuatisha uhuru wa vyombo vya habari na demokrasia, kila mtu awe na uwezo wa kuandika na kujieleza.

Juzi nilikuwa nasoma "The Economist" online edition, katika wachangiaji kuna bwana mmoja mwalimu wa art alikuwa analalamika kwamba zile article za uchumi ni nzuri sana lakini zinaandikwa kwa lugha iliyo technical sana na zinakuwa inaccessible.Labda haya ndiyo matokeo ya usomi mwingi, ndiyo sababu magazeti serious hayauzi sana.Labda tunahitaji waandishi wetu wawe respresentative ya population yetu, labda inabidi tuache kuwa condescend watu wasio na degree na stashahada kwani mfumo wetu wenyewe wa elimu ni sandakarawe amina, mwenye kupata apate, mwenye kukosa akose, kipapatikio cha kuku, kuna watu hawajafika chuo kikuu si kwa sababu hawana uwezo wa kishule au hawajafaulu, ila kwa sababu nafasi hamna.

Unaona hapo? Naelewa kuhusu standards na kwa kiasi fulani ninaweza kukubali hili when it comes kujenga madaraja, lakini kuhusu fourth estate this becomes a little bit too much.

It just sounds too much like Mkuchika using some clever guise to stifle freedom of the press.

Pundit
Msomi bora ni yule anayeweza kuifanya jamii yake ielewe kile anachokiandika au kukieleza. Nitakupa mfano mdogo tu,lugha ya sheria ni ngumu sana hata kutafsiri katika kiingereza cha kawaida tu,lakini a good lawyer anahimizwa kuandika kugha nyepesi inayoweza kueleweka kwa common man hasa inapotokea hadhira yake ni common man.Ipo tofautisana mimi kama mwanasheria napowahutubia wanasheria,hapa hata nikitumia lugha ngumu watanielewa tu,lakini napomweleza mtu wa kawaida asiye na taaluma ya sheria nikatumia lugha ngumu mimi ndo nitakuwa bomu.

Katika fasihi zote,fasihi andishi na fasihi simulizi kuna kitu kinaitwa fani na maudhui,fani ndiyo yale madoido na mbinu za uandishi zinazoipamba habari na kumfanya mtu avutiwe kusoma,wakati maudhui ndio ule ujumbe wenyewe. Kazi ya fasihi inatakiwa ibalance kati ya fani na maudhui,maudhui yakizidi kuliko fani watu hawasomi,kama ambavyo watu wachache wanasoma The financial Times hapa ulaya.Lakini tena fani ikizidi sana watu wanasema huu ni udaku wanakuwa hawapti content. Hivyo mwandishi ajitahidi sana kuwianisha vitu hivi japo ni ngumu kuwa 50 kwa 50.Nandio maana utakuta waandishi wa vitabu kama mashimo ya mfamle suleiman,tujifunze lugha yetu.adili na nduguze,Juma na Rosa,Someni kwa furaha.Roho mkononi, nk walifanikiwa sana kuliko waandishi wengi wa sasa ukiacha Shigongo ambaye kwa kweli kazi zake zinajitahidi sana kuwianisha fani na maudhui japo wakati mwingine fani zimezidi sana.

Tunachosema ni kwamba hata kama wanaandika udaku basi taaluma ya uandishi jumlisha kipaji chao huo udaku utakuwa mzuri sana hadi watu tukisoma tutakuwa tunachelewa kazini. Watu wana uhuru wa kutoa maoni,lakini uandishi wa habari ni zaidi ya uhuru wa kutoa maoni,hata kubwabwaja ni uhuru wa kutoa maoni,lakini mwandishi ana hadhi yake kwa jamii hawezi kutoa maoni yake kama mlevi aliyelewa chakari na kuanza kutoa maoni yake usiku wakati anarudi home kwa zile nyimbo zake.

Sema kosa hapa ni la serikali yetu yenyewe haikuthamini wanahabari kama wana taaluma na ndio maana haikujishughulisha kujenga vyuo vya uandishi kama TSJ na uandihi wenyewe ukaishia level ya certificate. Mimi ni mmoja ya watuniliopenda sana kusomea digrii ya habari lakini napotafuta kozi pale udsm nikakuta hakuna digrii ya habari ikabidi nifall kwenye sheria ambako kwa kweli sikuwa na ndoto ya kusomea fani hiyo katika maisha yangu. Since std 6 my ambition was to be a journalist sasa ndoto yangu ikashindwa sababu hiyo.Hata hivyo am still enjoying in the current professional
 
Augustoons,

Kwa hiyo wanaosoma sheria Marekani, amabao inawabidi wasome bachelor somo lingine halafu degree ya sheria ni ya pili, hawawezi ku practise sheria bongo?

A bit off the track but of substantial interest to me nevertheless.

Pundit
Believe me,kama digrii hiyo ya pili ni bachelor of law wataruhusiwa kupractice,lakini kama ni masters they will never practice law katika jamhuri ya muungano wa Tanzania au Kenya au Uganda.Maana sheria zetu za uwakili zinafanana.Hapa kwetu inaitwa ADVOCATES ACT.India pia wao wanaihesabu law kama second degree yaani ili usome law lazima uwe na digrii nyingine kwanza mf.bachelor of art in education ukimaliza ndio unasoma bachelor of law. Kama mtu akisoma kwa mtindo huu ataruhusiwa kupractice hapa home,lakini akisoma eti digrii ya kwanza bachelor of art in education afu akaja akasoma masters of law in e.g.international trade au criminal law.Hata afanyeje hawezi kupractice law hapa kwetu.Hii ndio current legal position in east africa.
 
Mimi naamini katika freedom of expression, hata mjinga naye ana uhuru wa kujieleza ili mradi havunji sheria.Akivunja sheria mpelekeni kortini.Wajinga wa Tanzania wakiamua kuwa na gazeti lao na waandishi wao, wakawaacha wasomi na gazeti lenu, tatizo liko wapi?
Au wanaogopa hawa wajinga si wajinga hivyo?

Nafananisha na kile kisa cha wendawazimu waliokuwa wanasafiri ktk ndege, ambapo muangalizi wao alimuona mmoja katulia akadhani anaweza kuwaangalia wenzake. Yule muangalizi akampatia funguo za "emergency exit door" yule chizi aliyepona kisha akaenda kujipumzisha. Aliporudi hakuona wale wengine, alipomuuliza yule jamaa, akamjibu "NIMEWAFUNGULIA MLANGO, WAPO NJE WANACHEZA"

Kama wajinga wanataka kuendeleza ujinga wao basi si ktk taaluma ya habari!!!! Uhuru wa kujieleza na kuandika habari si vitu vinavyoshabihiana 100%
 
Wanataaluma ndiyo waandishi wazuri wa habari kuliko hata waandishi wasio na taaluma nyingine zaidi ya uandishi wa habari, nionavyo mimi. Hoja ya msingi hapa ni kuwa na programu za kuwaendeleza waandishi wetu ndani ya vyombo vya habari husika. Hilo inawezekana linafanyika kwa vyombo vingi, isipokuwa serikali inaweza kuingilia kati, kwa ajili ya control anayosema Mwanakijiji, kwa kuanzisha mamlaka ya usajili wa waandishi ambapo waandishi watalazimika kufanya some basic courses wakiwa kazini na kutambuliwa na mamlaka baada ya kufuzu.
 
Ninaomba kutofautiana na wewe hapa mkuu, hapa JF tupo wananchi wa namna mbali mbali na kutoka kwenye avenue nyingi na tofauti za maisha, kinachotukutanisha hapa ni uchungu wa taifa letu, na siamini kuwa ili kutoa hoja ikaeleweka ni lazima iwe katika form fulani ya uandishi, au uandishi uliotukuka au ulioenda shule,

Hii comment ninaiona kama ni an insult kwa wale tusioenda shule, au tusioweza kuandika kama unavyotaka wewe kwa maneno yako hapo juu, ninaamini kuwa wananchi wote wanaruhusiwa kuja hapa kutoa maoni yao, bila ya kujali shule zao au uwezo wao kuandika, kwa sababu tukifanya hivyo basi itabidi wengi hapa ambao hatukwenda shule tuondoke,

I mean sina uhakika na the point lakini naona kama you should have been a little bit sensitive na maneno yako hapo juu, sio wananchi wote waliosoma vizuri kama wewe na wengine mnaojua kuandika vizuri, kama ninakuelewa vizuri , waacheni wananchi hapa JF waandike watakavyo na wawezavyo, tukianza hizi hatuwezi kufika mbali maana huu utakuwa ni ubaguzi period, between waliosoma na wanoweza kuandika vizuri na wasioweza, JF tunapswa kuwa bigger than mawazo ya namna hii!


FMES, Agoostoons

Nafikiri hamjanielewa.

Kwa kuangalia mkao wa kisiasa, nimesema tamko la Waziri ni la kikandamizaji. Lakini ukizungumzia kama Taaluma, na hasa Uhariri, ndipo niliposema kuna ulazima wa kuwa na watu wenye fani ya Uandishi ambao kazi yao itakuwa ni kuhakiki kazi.

Nimeongelea tofauti zetu humu ndani (mimi ni kiwa mmoja wapo!) za kuandika bila kuweka vituo, iwe nukta au koma, sentensi kuanza na herufi ndogo au kuchanganya tungo (grammar) iwe kwa kiingereza au kiswahili na nikauliza je hili si somo la awali tunalofundishwa shule ya msingi? Je tuliosoma shule ya msingi mpaka sekondari si kila mwalimu alikuwa akisahihisha kazi zetu kwa kuangalia uzito wa tulichoandika na matumizi mazuri ya lugha sanifu, viuto na hata herufi?

Sasa kama sisi tutasema hakuna ulazima sana kujihakiki katika tunayoandika, iwe hapa JF au kwenye kubeba maboksi, kuna maana gani basi kushupalia kuwa ni lazima waandishi wawe na shahada au kila anayeandika kwenye gazeti awe na shahada ikiwa sisi zile nguzo za msingi wa uandishi (kuandika) hatuzifuatilii?

Suala si kujigamba kuwa fulani ni msomi au najiona msomi. SIna usomi wowote, hivyo kufuata kanuni za uandishi ambazo nakiri bado zanipiga chenga, hakuna maana kuwa najisikia au natukana watu.

Ikiwa tunapuuzia vitu vidogo vidogo kama kanuni za uandishi, kisa ni ghadhabu zetu kukoromea Ufisadi na kutetea maslahi ya Taifa, je tunauhakika tunaweza kufuata na kutii sheria nyingine bila kushurtishwa?

Uandishi wa habari ni fani, kama Uhandisi, Utabibu, Uhasibu, Ualimu, Ubwana Shamba, Mchumi na kazi nyinginezo. Kwa yeyote ambaye anataka kuwa mwandishi wa habari, basi ni lazima awe na uwezo wa kufuata kanuni za uandishi ambazo Augustoon amezitaja.

Tofauti inakuja kwenye kuandika maoni au makala. Haya ni mawazo ya mtu binafsi kutokana na upeo wake, sawa na utenzi wa mashayiri.

Lakini katika gazeti, redio na hata televisheni, ni lazima kuwepo na wataalamu wa fani ya uandishi, ili kuhakiki kazi, kuikosoa na kuiboresha kabla haijalishwa kwa jamii.

Sasa kama tayari tunalalamika udhaifu wa magazeti yetu kutumia lugha za mitaani na hasa Swangish kutoa habari, kosa hili halipaswi kuonyeshwa na kutoa mkazo lazima kuwe na uhakiki wa kuhakikisha kuwa habari au makala inapitiwa kabla ya kuchapwa?

Au kama habari ina mapungufu na walakini, si jukumu la mhariri kuhakiki facts na data kabla hajachapa ili gazeti lidumishe heshima?

Ikiwa kuwa mkweli kujikosoa na kusisitiza haja ya kujisahihisha kati yetu ni kosa la jinai, naombeni wana JF wote radhi.
 
Rev. Umesomea uandishi lakini?

Watakuja mpaka humu na kusema ili kuandika JF inabidi uwe na degree ya Journalism, this is an online forum after all.

Pundit,

Sijasomea uandishi wa habari. Lakini wakati wa kujifunza lugha iwe shule ya msingi, sekondari au ngazi za chuo, kanuni za uandishi (kuandika) ni lazima zifuatwe.

Nilichokuwa nazungumzia ni kanuni za kuandika writing skills, punctuation, capitalization etc. ambazo tumejifunza toka shule ya msingi na kupigwa fimbo au makwenzi tukikosea.

Niliposema suala la usomi na vyeti, ni kutokana na tabia zetu kama jamii na Taifa kutukuza vyeti. Ndiyo maana nikauliza, ikiwa mtu anajitapa kuwa ana cheti na shahada, lakini hata spell check, grammar, punctuation na vikorokoro vingine vinamshinda iwe ni kwenye lugha ya kiswahili au kiapani, je tutasemaje kuwa huyu mtu kaelimika?

Kanuni za uandishi ni rahisi sana, ni sheria za uandishi(kuandika), sasa kama hata hizo nazo tunaziona hazina maana, tunapochekwa na Wakenya tunakasirika kwa misingi gani?

Hapa ndani tuna uhuru wa kuongea, ni online blog, hakuna sheria za punctuation. Lakini logically, it is expected kuwa mtu atatumia kanuni za kuandika anapoandika jambo period, kwa kuwa kajifunza tangu akiandika kwa penseli.
 
Inabidi tufike mahali tuseme ukweli na wazi kabisa kuwa matapeli wasiingie kwenye fani zisizo za kwao, waendelee na utapeli tu. Wasiingie kwenye uandishi wa habari, biashara, siasa au hata michezo
 
Je mwandishi ambaye amesomea na hafuati maadili ya uandishi ni bora kuliko mwandishi anayefuata maadili na ambaye hana cheti cha kuonesha elimu yake hiyo? Je mhasibu aliyesomea lakini hafuati maadili ya kazi ni bora kuliko mtu anayefanya shughuli za uhasibu kwa maadili lakini hana usomi huo?

Je tatizo ni maadili au usomi? Je mtu aweza kujifunza maadili ya kazi bila kupewa cheti cha shahada.
 
Kuhani,
Uandishi na utangazaji ni kipawa. Jennings nasikia alikuwa high school graduate. And he was one of the best.

Mzee mzima mwenyewe Larry King wa CNN hajasomea Fani hiyo, ni High School Graduate tu.

Sasa huyu mkuchika anataka kutuambia nini?

Kwanza yeye mwenyewe ana shule ya kutosha? Imetakata? Au ni sifa za kukimbiza Mwenge wa Uhuru na kujipendekeza kwa wakubwa kwa dizaini ya changu??

Hebu atuondokee hapa na ujinga wake uliojaa uzembe na Uzuzu.
 

Ndugu Wana JF,

Hivi karibuni tutakuwa na sheria itakayoweka viwango vya elimu ya waandishi wa habari. Kwa mtazamo wa wengi, wabunge wakiwamo, kwa muda mrefu baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiipotosha jamii kwa kuandika chini ya viwango. Wanadhani sasa kuwabana kuongeza elimu kutasaidia kuondoa tatizo hili.

Lakini wakati tunaliangalia hili, je tunalizungumziaje suala la wabunge, ambao kazi yao ni kutunga sheria zinazoongoza nchi, kuwa na elimu ya kutosha, badala ya kuweza tu kusoma na kuandika?

Nimelazimika kuanzisha hii thread baada ya kumsikiliza sana Mkuchika juzi, akisisitiza umuhimu wa elimu kwa waandishi, na kuwamo kwenye chombo kitakachowasimamia, huku alitolea mfano wa chama cha madakitari na wahandisi (na hapa tujiulize wao wabunge wana elimu gani na wanasimamiwa na nani kama MCT inasimamia waandishi na vyombo vya habari?)

Karibuni!
 
mbunge kama mtunga sheria kwa mtazamo wangu nafikiri lazima awe na elemu ya kutosha ya kuweza kufahamu jinsi ya kuchanganua sheria inayojadiliwa au inayotakiwa kutungwa.

tatizo ni kuwa ubunge sio profession........na ndio maana, kusema mbunge lazima awe na elimu fulani inakuwa ngumu.

ila kimtazamo wangu nadhani mbunge anahitajika angalu kwa uchache awe amehitimu angalau o-level education.
 
Back
Top Bottom