Kaondoka na shati la blue, karudi na shati la hudhurungi na marashi ya blue lady

malisak

JF-Expert Member
Mar 16, 2006
694
772
Nina jirani yangu alikuja kuomba ushauri kwangu(true story), hakumuona mumewe siku 3 nyumbani na simu haipatikani, bibie pressure juu kibinadamu.

Mwanaume ni fundi mitambo, kawaida huwa anafanya kazi mpaka usiku mwingi hata muda mwengine kwenda mikoani ila kwa taarifa maalum.

Sasa bwana yule siku 3 hajaonekana isistoshe kaondoka na shati la blue akiwa amejipulizia manukato aina ya blue for men,aliporudi amerudi na shati la rangi ya hudhurungi na ananukia perfume ya blue lady shorsty akazimia hapohapo alipomwona na jinsi alivyong'aa.kuzinduka mwanaume amemtumbulia mijicho kama ndubwi kwa tahayuri hata la kusema hana shoga akalianzisha timbwili la haja.

Sasa nikamsahauri asiondoke kwani watoto wake ni wadogo na isitoshe hana japo kibarua kitakachomfanya awatunze na bwana anaendeleza libeneke je nimekosea kumshauri?,ungekua wewe ungefanyaje?.(tukio limetokea leo kama siku ya 5 hv)
 
Men men men men jamani! duh... huyo ndo wale wanaotetea vimada. Mie naona huyo hakuwa na mchezo huo mchafu sasa ndo ameonjeshwa na kapagawa kabisa pum... zake. anasahau hadi kids wake, alaaniwe huyo.
 
Hivi dunia ya sasa kuna kumwamini binadamu mwenzio kimapenzi/ndoa?! huyo nae presha kama hizo ataishia kufa na baada ya matanga mwingine anaingizwa ndani tena kwa ndoa nzito!!..pole yake masikini!!
 
Hujakosea, mwambie azidishe mambo atatulia tu! ikiwezekana abadili badili namna ya kumtunza na kumpa vitu adimu pamoja na lugha nzuri zenye ushwawishi ili akitoka tu langoni anakumbuka ndani kila wakati.
 
Nina jirani yangu alikuja kuomba ushauri kwangu(true story), hakumuona mumewe siku 3 nyumbani na simu haipatikani, bibie pressure juu kibinadamu.

Mwanaume ni fundi mitambo, kawaida huwa anafanya kazi mpaka usiku mwingi hata muda mwengine kwenda mikoani ila kwa taarifa maalum.

Sasa bwana yule siku 3 hajaonekana isistoshe kaondoka na shati la blue akiwa amejipulizia manukato aina ya blue for men,aliporudi amerudi na shati la rangi ya hudhurungi na ananukia perfume ya blue lady shorsty akazimia hapohapo alipomwona na jinsi alivyong'aa.kuzinduka mwanaume amemtumbulia mijicho kama ndubwi kwa tahayuri hata la kusema hana shoga akalianzisha timbwili la haja.

Sasa nikamsahauri asiondoke kwani watoto wake ni wadogo na isitoshe hana japo kibarua kitakachomfanya awatunze na bwana anaendeleza libeneke je nimekosea kumshauri?,ungekua wewe ungefanyaje?.(tukio limetokea leo kama siku ya 5 hv)
Hapo ndio tunaanza kupata watoto wa mitaani,kwa kuwa mwanamke ni golikipa itabidi akae tu hapo maana hana jinsi ya kufanya hata kama akisema aondoke bado tatizo litakuwa kwa watoto.
Kilichobaki ni kutafuta namna ya kumfanya mumewe atulie nyumbani,kina mama wengi magolikipa hawashughuliki kabisa kujiweka wasafi yaani muda wote wapo wapo tu hata hawavutii kuomba mchezo.
 
mhhhh Joseph!!! naona umewadhalilisha kina mama...

kwahiyo huyu bwana hana adabu akiachiwa watoto wake atafanya nini....
 
sijui nisemeje maana hata ingetokea kwangu ghafla hivyo sijui ingekuwaje!
 
Mmmmh hivi kwa nn mtu unasema mkeo ni mama wa nyumbani ina maana hamna hata kashughuli ka ujasiriamali anafanya. Hili ni kosa kubwa sana kwenye ndoa kutomuwezesha mkeo apate shughuli ya kufanya ni tatizo kubwa sana na mwisho wake ndio hayo mtu anashindwa kumhudumia mkewe kutokana na facts kwamba hela yake inashindwa kugawanyika kufanya kila kitu cha kifamilia mwishowe anaishia kusema mama wa nyumbani hawajiweki vizuri kumvutia mumewe, sasa atavutia vp wakati hana kipato cha kumwezesha kuvutia
 
eti mwanamke ni lazima apate tabu na kupoteza maisha yake kwa ajili ya watoto? yani mwanaume yeye hana role yoyote katika maisha ya watoto... mimi hii yakuvumila upuuzi wa mwanaume kwa ajili ya watoto sidhani kama naweza kukubaliana nayo...yani ukisha zaa basi huna life tena....

najua ni very difficult for a woman to live without her kids but if i had no other option i will leave and go to start my own life from scratch.....
 
ajabu mimi namwachia wanawe hata kama ninae mdogo wa miezi 2 yeyey si kidume alee mwenyewe au hawara yake amsaidie pumbavu nazi.
 
Hapo ndio tunaanza kupata watoto wa mitaani,kwa kuwa mwanamke ni golikipa itabidi akae tu hapo maana hana jinsi ya kufanya hata kama akisema aondoke bado tatizo litakuwa kwa watoto.
Kilichobaki ni kutafuta namna ya kumfanya mumewe atulie nyumbani,kina mama wengi magolikipa hawashughuliki kabisa kujiweka wasafi yaani muda wote wapo wapo tu hata hawavutii kuomba mchezo.
Mmmhhh wamama magolikipa hawajipendi?,siamini hilo

Sent from my Hol-U19 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom