Kanusho la habari potofu katika Tanzania Daima - 'JK alinda mawaziri'

jana kikwete hakuwa dodoma..na jana hiyo usiku nilisema kwenye thread ile iliyosema jk atua dodoma...ile thread ilijaza sumu sana na gazeti la tz daima wakatoa habari pale na kuchapicha gazetini


wewe ukweli unaufahamu? kwenye taarifa ya rweyemamu hakuna chochote zaidi ya kanusho. Hivo taarifa ya jana ni sahihi ama vinginevyo. Tusiposikia mawaziri wamajiuzulu hiyo kesho basi tutathibitisha kwamba wewe, kurugenzi ya ikulu ni waongo wakubwa.
 
hvi hii kurugenzi ya mawasiliano kazi yake ni kijibu magazeti tu?kwann isitueleze Rais ansema nn juun ya kashfa za mawaziri wake,yeye kutueleza ndio angekuwa amejibu gazeti,lkn yeye kunyamaza nakutuma vibarua kwenye TV ina maana habari hzo ni zakweli
 
Kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu..........my behind!

kurugenzi ambayo kazi yake ni KUKANUSHA KASHFA TU!!!
kurugenzi ambayo haina TAARIFA ZA MAANA ZA IKULU???

Afadhali hata wangekuwa wanatoa wao zile 'Activity reports' za Kikwete anazotoaga wakati amerudi kutoka ughaibuni........mwenyewe huwa anaziita HOTUBA ZA MWISHO WA (MI)MWEZI!!
 
Hakuna lolote hapo, alikuwa ana-beep kwa msimamo huo ili aone ulimwengu (umma) uta-react vipi! Now that he has seen the reaction, lazima wajifanye kukanusha. Narudia tena, natamani jeshi lichukue hii nchi japo kwa wiki moja tu!
 
Rweyemamu hajasahau kuandika UDAKU tu. Kweli nimegundua njiwa pori hata akifanana na wakufugwa bado hafugiki
 
Ikulu na Kurugenzi yake Kanushi & Propaganda wanazidi kuchemka. Ok wamekanusha lakini ni nini taarifa mbadala ya mada husika? I still will take Tz Daima's info till satisfactorily otherwise proven.
 
Hii ni ngumu kueleweka. Kuonana sawa huenda hawajaonana, hata kuongea kwa simu? Basi hii ni serikali ya mabubu au wenye bifu kama wake wenza.
 
Katika hali iliyonifurahisha ni Pinda kuuzwa na jakaya kiasi hiki, mkubwa katoka kupiga mpunga na maximo mnataka kumletea maluelue ya bunge lenu ili iweje? Kumlilia Kanumba he was very right kama shabiki na mkuu wa inji anaejali, je kwa haya yanayoendelea juu ya pinda na mawaziri wake hayahitaji uwepo na maamuzi yake akiwa mezani ofisini kwake? mi sipendi wanavokuita vasco ila kuna muda naoana wanamaana vile!
 
hawa jamaa wanatuchezea akili ngoja sasa kesho tuwaoneshe kuwa sisi ni m4c, wanatuona sie mabwege ngoja tumtimue huyo mkulima wao, afu tuanze upya.
 
Ukiona hivyo, ujue Pinda hajakubaliana na Jk. Tusubiri hiyo kesho tuone.

Kama kweli walikutana au kuwasiliana kwa njia mmoja au nyingine ,yawezekana Pinda hakukubaliana na Raisi kwa kile kinaitwa mambo yatapoa tu baada ya muda labda Pinda amechoka kutolewa lawama zisizo zake,labda ametishia nae kujiondoa.Ili kuweka mambo sawa taarifa za Ikulu ndio maana zinakanusha.Na kama hali ndio hiyo,Raisi itambidi kufanya mabadiliko katika baraza lake japo cosmetic change.Lakini tusubiri taarifa rasmi.
 
Mchawi wa pinda si mwingine ni jehikehi, yaani anasubiri taarifa ya bunge ina maana huwa hawaongei kwenye simu? Hii ni kusema mukulu wa nchi anakulaga malikizo many times ndo maana mpaka leo anawasiliana kwa fax tu hamwamini mtu
 
siamini kama state house inaweza ikaliogoppa Tanzania Daima kiasi hiki .... je Newsweek au Times
 
Ndg zangu wana jf! Let me teli u something! Kuna m2 wangu wa karibu,mfanya biashara pale kariakoo, ni mchaga mwenzengu, wote tunatoka pale kibosho, yupo karibu sana na waziri Chami, kindungu, na hata kibiashara....baada ya kuzungumza na chami leo asubuhi. Amenihakikishia kwa 100% kwamba hakuna waziri hata m1 atakayejiuzulu. Sababu ni kwamba JK amewakatilia. Inasemekana jk alishauriwa angalao awatose Mkulo na Ngeleja, "kakataa" akidai kuwa wizara ya nishati na madini,tayari ina matatizo kibao. Pale kwa mkulo hakukataa wala hajakubali kumtosa,inadaiwa atapima upepo, kwenye nn!? Sijui poleni sana huo ndo ukweli!
 


SUNDAY, APRIL 22, 2012

KANUSHO LA HABARI POTOFU KATIKA TANZANIA DAIMA AMBALO LEO LINA KICHWA CHA HABARI KISOMEKACHO "JK.ALINDA MAWAZIRI"



download.png



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Tanzania Daima la leo Jumapili Aprili 22, 2012 lina habari katika ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari ‘JK alinda Mawaziri’, inayodai kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

Habari hiyo imedai kuwa Mhe. Pinda anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini, imeendelea kudai habari hiyo, “Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita”.

Tunachukua nafasi hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo hazeti la Tanzania Daima Jumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.

Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma.

Mhe Rais anawasihi wananchi wasiamini habari hizo za upotoshaji zilizomo kwenye gazeti hilo la Tanzania Daima Jumapili.

Pia ametoa rai kwa wanahabari wasitoke nje ya mstari wa weledi katika kutekeleza kazi zao ili kuendelea kulinda heshima zao binafsi, vyombo wanavyofanyia kazi pamoja na taaluma yenyewe.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Aprili, 2012



Hii habari haina sahihi ya huyo mkurugenzi? Nisaidieni wadau au ndivyo matangazo ya ikulu yalivyo?
 
Ndg zangu wana jf! Let me teli u something! Kuna m2 wangu wa karibu,mfanya biashara pale kariakoo, ni mchaga mwenzengu, wote tunatoka pale kibosho, yupo karibu sana na waziri Chami, kindungu, na hata kibiashara....baada ya kuzungumza na chami leo asubuhi. Amenihakikishia kwa 100% kwamba hakuna waziri hata m1 atakayejiuzulu. Sababu ni kwamba JK amewakatilia. Inasemekana jk alishauriwa angalao awatose Mkulo na Ngeleja, "kakataa" akidai kuwa wizara ya nishati na madini,tayari ina matatizo kibao. Pale kwa mkulo hakukataa wala hajakubali kumtosa,inadaiwa atapima upepo, kwenye nn!? Sijui poleni sana huo ndo ukweli!
 
Hii ni mara ya tatu jk anakanushiwa alosema,kumbukeni kumrudisha jairo,posho za wabunge na hii,huwa hajiamini m2 huyu,akisema ki2 akiona negative respond anatumia kurugenzi yake kibogoyo.
 
Hivi wewe umeona jf ndo pa kutoa habari hii, si ulifunge hilo gazeti au kulichukulia hatua za kinidhamu kama wanapotosha umma. Mi naona unapoteza muda watanzania wa leo si wa jana tunashukuru shule za kata na vyuo vya kata kama udom atleast vimeweza kuwatoa ujinga wa tz kinamna fulani so tunaelewa tanzania daima huwa hawakurupuki kama gazeti la ccm uhuru. So tunaiamini hityo habari, there is no way ukatupotosha me nadhani wewe ndo unajaribu kuupotosha umma.
 
Idara ya mawasiliano Ikulu inatia aibu. Sasa siamini kama ina watu makini, wasomi na wenye uelewa. Kama sivyo basi inalengo la kuanika ubovu wa Rais Kikwete na Serikali yake kwa kuonyesha kuwa haina uwajibikaji na haina mawasiliano mazuri baina watendaji wake hata kwenye maswala yenye maslahi kwa Taifa. Nikinukuru sehemu ya taarifa ya Ikulu hapa chini ni wazi kabisa kuwa ama Waziri mkuu Pinda amezidharau kelele au michango ya waheshimiwa wabunge. Km PM aliwadharau wabunge waliongea kwa uchungu basi PM ni mnafiki au hafai au na yeye ni sehemu ya ufisadi au kuna jambo linafichwa. Kama Pinda angekuwa amesikia vilio vya wabunge basi angenyanyua simu na kumpigia Rais kokote aliko na kumwelezea yaliyojiri wakati hayupo. Lakini pia nashindwa kuiamini na kuielewa taarifa ya Ikulu kama ni ya kweli au la kwa maana siamini kama kweli Katibu mkuu wa Rais Bw. Sifue alilazimika kufunga safari akaenda Dodoma kuonana na wenyeviti wa kamati, spika na wabunge wengineo iweje hata yeye asimjulishe Rais walau kwa ufupi tu kiasi kwamba Rais asiwe na taarifa kabisa? Kama taarifa ingesema Rais amepokea taarifa kwa ufupi anahitaji muda wa kupitia ripoti kwa ukamilifu na kisha kutoa taarifa rasmi hapo ningeelewa. Lakini kwa sasa sielewi idara hii ya mawasiliano inaundwa na nani, kama siyo inaundwa na swahiba au watoto wa familia ya kikwete na swahiba wake ambao wanajibu kwa jaziba tu bila hekima. Hata kama Kikwete amewasiri leo kutoka Brazil yaani anafika ofisini asiambie hata yaliyojiri wakati hayupo? Kama ndivyo ilikuaje akajua msiba wa Mwakanjuki hadi akaenda kuaga mwili na asijulishe swala nyeti lililojiri bungeni kwa kweli haiingii akilini kabisa. Jamani hebu soma nukuru ndogo ya taarifa hapa na nyie muone "Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma".
 
Back
Top Bottom