Kama ni kweli, kilichofanywa na hawa madiwani wa CDM ni uhuni. Huwezi kujiorodhesha kwenye mahudhurio baadaye ukataka kufuta jina lako. Bila shaka barua za kuwaalika ziliwajulisha wanakwenda kufanya nini. Wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwani wanatoa picha mbaya kwa chama ambacho watu tumeanza kukiamini.