Kanuni zavunjwa tena Arusha...hii ndiyo bongoland.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
[FONT=Helvetica, sans-serif]Baraza la Madiwani Jiji la Arusha limepitisha bajeti ya zaidi ya Sh. bilioni 48.1 kwa mwaka huu wa fedha wa 2011/ 2012, licha ya madiwani 11 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) kususia kikao hicho kilichofanyika jana kwa kutoka ukumbini. [/FONT]

[FONT=Helvetica, sans-serif]Baraza hilo likiwa na wajumbe 16 kutoka vyama vya CCM na TLP, lililazimika kuendelea na kikao na kupitisha bajeti hiyo, huku baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kutoka vyama hivyo viwili wakishutumu hatua ya madiwani wa Chadema kususia kikao hicho.[/FONT]

[FONT=Helvetica, sans-serif]Awali, baada ya wajumbe wote kuingia katika ukumbi, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomiah Chang’a, alitoa taarifa ya idadi ya madiwani waliokuwa ukumbini wakiwemo wa Chadema, CCM na TLP kuwa ni 25.[/FONT]

[FONT=Helvetica, sans-serif]Alisema idadi hiyo ni zaidi ya akidi ya theluthi mbili ya wajumbe wote 32 wanaotakiwa kuhudhuria kikao hicho. [/FONT]

[FONT=Helvetica, sans-serif]Lakini wakati Meya wa Jiji la Arusha, Mstahiki Gaudence Lyimo, aliposimama kwa ajili ya kufungua kikao hicho, madiwani wa Chadema wakiongozwa na John Bayo wa kata ya Elerai walinyanyuka vitini na kutoka nje ya ukumbi.[/FONT]

[FONT=Helvetica, sans-serif]Hata hivyo, Chang’a, alisema kanuni na taratibu zinaelekeza kwamba iwapo mjumbe yeyote wa kuchaguliwa atapata wito na akaitikia na kufika ukumbini ni dhahiri mjumbe huyo atakuwa amehudhuria kikao hicho na hivyo kuchangia kufikia idadi ya wajumbe wanaotakiwa kufikisha akidi ya kikao ya theluthi mbili hata kama atakuwa ameondoka ukumbini. [/FONT]

[FONT=Helvetica, sans-serif]Mbali na wadiwani wa Chadema kuingia ukumbini na kujiorodhesha katika kitabu cha mahudhurio, Bayo, aliamua kuchukuwa rejesta ya majina na kukatakata majina yao.[/FONT]

[FONT=Helvetica, sans-serif]Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, Diwani wa TLP kutoka kata ya Sokoni One, Maiko Kivuyo, alisema wamepitisha bajeti ya jiji kwa manufaa ya wananchi wa Arusha.[/FONT]
 
Kuna kususia lakini hili la Bajeti halikuhitaji kususiwa - kuna hospitali, mashule, kazi za usafi zote zinategemea bajeti hii ya manispaa.
 
Wakubwa ukihudhuria 2 inatosha kupitisha bajeti?hakuna mda ukifika wajumbe/madiwani wakapiga kura?naomba mnijuze wadau!
 
Madiwani wa CDM wamedhihirisha kuwa hawajui watendalo.

Wanajiorodhesha kisha wanachafua rejesta kwa kufutafuta kwa kalamu.

Sijui hiyo ni njia ya kuondoa ushahidi kuwa hawakuhudhuria?

Kwanini waliamua kuingia na kujiorodhesha? Hawakujua wanachofanyai?

Upuuzi utoto na uhuni wa aina hii mpaka lini?

Ole wao waliowachagua kuwawakilisha ... wameona matokeo ya kudanganywa na wasanii wa siasa .... imekula kwa wapiga kura.
 
Madiwani wa CDM wamedhihirisha kuwa hawajui watendalo.

Wanajiorodhesha kisha wanachafua rejesta kwa kufutafuta kwa kalamu.

Sijui hiyo ni njia ya kuondoa ushahidi kuwa hawakuhudhuria?

Kwanini waliamua kuingia na kujiorodhesha? Hawakujua wanachofanyai?

Upuuzi utoto na uhuni wa aina hii mpaka lini?

Ole wao waliowachagua kuwawakilisha ... wameona matokeo ya kudanganywa na wasanii wa siasa .... imekula kwa wapiga kura.

ushashiba pilau .... mashuzi tuu
 
Madiwani wa CDM wamedhihirisha kuwa hawajui watendalo.

Wanajiorodhesha kisha wanachafua rejesta kwa kufutafuta kwa kalamu.

Sijui hiyo ni njia ya kuondoa ushahidi kuwa hawakuhudhuria?

Kwanini waliamua kuingia na kujiorodhesha? Hawakujua wanachofanyai?

Upuuzi utoto na uhuni wa aina hii mpaka lini?

Ole wao waliowachagua kuwawakilisha ... wameona matokeo ya kudanganywa na wasanii wa siasa .... imekula kwa wapiga kura.
Unadhani CCM wataweza kuongoza jiji wakitumia ujanja ujanja wa kuvizia kolumu kwa miaka yote mitano, itafikia watanyosha mikono wenyewe.
 
Tuache ushabiki madiwani wa CDM wawe na uchungu kwa maendeleo ya wananchi, wataendelea kususia vikao vya madiwani mpaka lini??
 
Kimsingi madiwani wa Arusha inabidi watulie,wawabane vilivyo viongozi wa halmashauri ya Arusha ili maendeleo yapatikane na kwa kuwa Lema ndo mbunge wao,basi wataweza kuongoza hata next time kwenye ubunge na madiwani mwaka 2015.
 
Tunaomba ufafanuzi wa hili kutoka Chadema Makao makuu, kwa nini waingie wajiorozeshe halafu watoke nje, nafikiri wangetakiwa kutofika kabisa ili idadi isifike na kutoa hoja zao kupitia media ili sisi tunaowamini tuwaelewe lakini kwa hili, nahitaji kuelimishwa na wakubwa ni kwanini wamefanya hivyo na lengo lilikuwa nini, na hata kama wangebaki na kupiga kura ya kutopitisha je sheria inasemaje wengi wameshinda au mpaka idadi ifikie pia.
 
Tuache ushabiki madiwani wa CDM wawe na uchungu kwa maendeleo ya wananchi, wataendelea kususia vikao vya madiwani mpaka lini??
Kwani madiwani wa CCM ndio leo wameuona huo uchungu zamani haukuwepo.
 
kwa hapo nami siungani nao hao madiwani wa cdm. ni uhuni sasa. i dont see kwa nini basi waliingia ndani na kuandikisha majina yao, ni dhahiri hawajui taratibu, hata unapokuja kukata majina sijui ndo kufanya nn sasa. hao jamaa hakika wanapotosha dhana nzima ya kuwa mpinzani.
 
hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa chadema choo jitu 11 inataka kusema itazidi ujanja jitu 16. wanafuata mwongozo wa lema. walisaini ili wachukue posho.

hao wajinga wa mwaka unaweka sahihi kisha unaondoka
 
CCM ni mafundi wa kutafsiri sheria na kanuni. Mnakumbuka Bungeni walivyotoa tafsiri ya 'kambi rasmi ya upinzani Bungen?" Hili suala la madiwani kuingia ukumbini, kujiorodhesha majina na halafu kutoka nje na hivyo kutoshiriki mjadala na kupiga kura linaweza kukubalika kwamba quorum ilikuwapo -- kwa tafsiri ya CCM!

Hivi Bungeni inakuwaje? Kama kunatakiwa kupigwa kura inayohitaji quorum, kweli inaweza ikapigwa kwa kusema quorum ilikuwapo kwa kuangalia tu idadi ya majina ya mahudhurio katika rejesta? Na siyo wajumbe halisi waliomo?

Hivi Tanzania tunakwendaje au tunaenda wapi? Mbona tunakuwa kama watu tusiyoweza kufikiri? Au ni kutokana na utawala wa nusu karne wa CCM?

Sishangai Babu anapata mashabiki!
 
Waliingia kuonesha dhamili zao za kuwatumikia wana wa arusha. Walitoka mara baada ya anayeitwa meya kusimama kuonesha hawamtambui kama meya halali wa arusha. Mmeelewa???
 
hao kama wamefika wakajiorodhesha wamukalia Ndugu zanguni ..
Kwanza niwapuuzi kabisa mnasema amhudhurii alafu unakwenda unatka nje Meya fanya kazi achana na hawa pumba UPINZANI LAZIMA MUWE NA UHAKIKA MNACHOKIFANYA ...
 
Back
Top Bottom