Kanuni za Uchaguzi ndani ya CCM, je wanatekeleza wanayoyahubiri?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Ufuatao ndio mwongozo kama ulivyotolewa na Halmashauri Kuu ya CCM mwaka 2005.

KANUNI ZA UCHAGUZI

"Tangu tuingie katika mfumo wa vyama vingi Julai 1, 1992, Viongozi wetu wa kuchaguliwa katika Chama wamekuwa wakifanya kazi za CCM kwa kujitolea ..... Kufanya kazi za Chama kwa kujitolea ndiyo mila inayoendana na mifumo ya vyama vingi duniani kote ..... CCM itahakikisha kuwa msimamo huu wa kujitolea unaimarika, kukubalika na kuenezwa ndani ya Chama."

UTANGULIZI


  • Katika kuimarisha kazi yake ya kuongoza Mapinduzi yetu ya Kijamaa, Chama Cha Mapinduzi hakina budi kuhakikisha kuwa viongozi wake wote, wa kuchaguliwa au kuteuliwa, ni waumini wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na kwamba ni wanamapinduzi wa kweli kweli wasioyumba wala kubabaika.
  • Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Uchaguzi Mkuu wa Chama hufanyika kila baada ya kipindi cha miaka mitano. Kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana kutokana na chaguzi za nyuma tangu CCM izaliwe mwaka 1977 na pia tangu mageuzi ya mfumo wa vyama vingi vya Siasa yafanyike mwaka 1992, CCM inalazimika wakati wa chaguzi zake zote kuwa makini zaidi katika kuhakikisha kwamba inachagua viongozi wenye uwezo wa kuhimili vishindo vya ushindani wa kisiasa katika ngazi zote za uongozi.
  • Ili tuweze kupata ufanisi mkubwa zaidi katika chaguzi zetu sharti tufanye juhudi ya kuepuka kasoro zote zinazogusa maadili ya Chama na zile za utendaji ambazo zinawezesha watu wasiostahili kuchaguliwa waweze kupenya kwenye uongozi ama kwa rushwa au kwa hila. Kwa sababu hiyo lazima Maadili ya Chama yazingatiwe kwa ukamilifu na vikao vyote vinavyochuja na kuteua wagombea. Aidha, pamoja na kuwapo kwa kanuni hizi, Katibu Mkuu wa CCM aweza kutoa miongozo ya ziada kuhusu masuala yanayopaswa kuzingatiwa katika chaguzi za Chama Cha Mapinduzi.

UONGOZI


Uongozi bora katika Chama chetu, una masharti matano yafuatayo:-


  • Kiongozi wa Chama akinai maadili ya Chama, na asiwe mtu wa kuyumba katika masuala ya msingi ya ujamaa wetu.
  • Awe na uwezo wa kazi anayotarajiwa kufanya katika ngazi yake ya uongozi kulingana na wakati uliopo.
  • Awe na uwezo wa kuhimili na kuvishinda vishindo/vitimbi vya wapinzani.
  • Kwa kiongozi wa kuchaguliwa, lazima wanachama wamchague kiongozi wao kwa hiari na uhuru kabisa, na kwa njia ya haki. Vinginevyo tutajenga chama cha wachache tu ambacho wanachama wengi hawana kauli nacho.
  • Muda wa uanachama wa kila mgombea usipungue miaka mitano mfululizo ili Chama kiwe na uhakika na msimamo wake. Hii inawahusu hata wanaorudi CCM baada ya kujiuzulu, kuachishwa au kufukuzwa uanachama. Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ina uwezo wa kuamua kwa kadri itakavyoona inafaa juu ya utekelezaji bora wa sharti hili la Kanuni kwa manufaa ya Chama.

Kamati Kuu imekasimu madaraka yake kwa Kamati za Siasa za Wilaya kuhusu chaguzi za ngazi ya Shina hadi Tawi; na kwa Kamati za siasa za Mikoa kuhusu chaguzi za ngazi za Kata/Wadi na Jimbo.

Katika kitabu cha TANU na Raia (1962) twasoma hivi:

Kila mmoja wetu aliye katika hali ya uongozi, toka President mpaka Chairman wa Kijiji; toka Secretary General mpaka Secretary wa Tawi, hana budi ajiulize: Ikiwa nilichaguliwa kwa kura, hizo kura nilizipataje? Nilizipata kwa hila, kwa rushwa, kwa vitisho au kwa ujanja wa aina yoyote, au nilizipata kwa hiari ya wapiga kura wenyewe?

Asili ya uongozi wetu ni mbili:-


  • Ya kwanza ni WATU. Uongozi wetu hauna budi utokane na watu wa nchi hii, bila hila, bila rushwa, au bila vitisho na bila ujanja wa aina yoyote. Tunapofika katika hali ya uongozi kwa kupitia mlango wa hila, au rushwa, au vitisho au ujanja wa aina nyingine yoyote basi hatukutokana na watu wenyewe.
  • Ya pili ni HAKI. Lakini haki ni haki ya watu, siyo kwa majani au kwa miti. Tunapofika katika uongozi kwa njia yoyote ambayo si ya haki, ni wazi kwamba haiwezekani tuwe tumetokana na watu wenyewe. Watu na Haki ni misingi ya uongozi ambayo haiachani......."

Uongozi bora unaendelea kusisitizwa na kuzingatiwa na maandishi yafuatayo:-


  • Ko kote aliko, mawazo na juhudi ya Kiongozi, fikra na kazi yake wakati wote lazima ziwe mfano mwema na bora wa utekelezaji wa wajibu wake kwa viongozi wenziwe na kwa watu wengine.
  • Msingi wa wajibu wa kiongozi lazima daima utokane na imani ya kutumikia wananchi kwa dhati katika kuwasaidia na kuwaendeleza wainue hali zao za maisha na kuzifanya zilingane.
  • Ni mwiko kwa Kiongozi kutumia wadhifa wake kwa ajili ya hamu yake, kwa upendeleo au kwa chuki na ni mwiko kutumia vyombo vya Chama au Serikali yake kwa kazi yoyote ya binafsi au kwa shughuli yoyote ya binafsi au kwa shuhguli yoyote isiyohusiana na wajibu wake akiwa kiongozi.

My take
- Hayo ndiyo yalikuwa mahubiri ya CCM, je wanatekeleza kwa vitendo wanayoyahubiri? Naamini ni wakati muafaka kwa kila mwananchi mwenye uchungu kwa taifa letu kuutambua ulaghai wanaofanyiwa na chama tawala, CCM, mradi tu iendelee kung'ang'ania kubaki madarakani. Nawakilisha.
 
Mkuu Adharusi, hivi leo mtu yeyote anayeendelea kuitetea CCM na wale wote wanaokesha humu JF wakiitetea CCM nasikitika kusema ni lumbukeni; hawaijui CCM wala historia yake. CCM ya leo iko mikononi mwa wezi, wanyang'anyi, walaghai na wauaji na kwa sababu hizi CCM imekuwa kimbilio la watu wa aina hiyo hiyo toka Kiongozi wake Mkuu hadi wa chini kabisa. Hakuna, narudia hakuna kongozi wa CCM hata moja ambaye ameweza kuukwaa uongozi kwa hiari ya wapiga kura wenyewe bila kutumia hila, rushwa, vitisho au ujanja wa aina yoyote.

Tatizo tulilo nalo kama taifa ni kwamba hali hii kwa sasa imeenea hadi katika mihimili yote rasmi ya dola na isiyo rasmi kama serikalini na vyombo vyake vyote vya dola, mahakamani hadi bungeni. Kuna usemi humu ndani ya JF kwamba kuitetea CCM ni lazima uwe na akili za maiti na kweli Watanzania wengi ingawa tunatembea lakini kiakili na kimaadili tumekufa. Wengi tumekuwa kama mazezeta...pale ambapo kwa akili ya kawaida tungekataa tunaunga mkono, ambapo tungezomea tunashangilia na ambapo tungekemea tunakubali...mradi tunapumua.

Hakuna namna ya kuelezea kwa nini watu wasio na uwezo tunawapa madaraka, wezi tunawapa hela zetu watutunzie, waongo tunawaamini hata pale tunajua wanatudanganya, manyang'au tunawapa ulinzi wa mbuzi wetu na wauaji tumwakabidhi usalama wetu, ptuu...! Kwa kweli tumekufa ingawa tunatembea; hatuoni na hata tunapoambiwa tunakoelekea siko tunaongeza tu mwendo, hatusikii na hata ngurumo za hatari zinavyozidi hatujali, hatuhisi na hata joto linapozidi tunasogea tu penye moto. Tunazidi kuimba wimbo wa CCM na kucheza ngoma ya CCM!

Walafi wamekaa mezani wanazidi kula tu kama nzige bila kushiba huku wengi wetu tukifurahia kunenepa kwa makombo tunayotupiwa chini ya meza tukisifia huruma yao kwa kutukumbuka. Hatujiulizi ni kwa nini chakula tunachokihangaikia juani wale walafi kivulini, viti tulivyovichonga wakalie wavivu, numba tuliyoijenga waishi kupe and the list goes on...! Tumekuwa misukule na hivyo tumebakiwa na jukumu moja tu, kuwatetea hadi mapovu yanatutoka; mifano iko humu humu, wapo Lizaboni, laki si pesa, MSALANI, FaizaFoxy, mjepo na wengine...so sad!
 
Ujamaa umepitwa na wakati hakuna kitu kama hicho kwa sasa Tanzania, ulikufa kabla ya Nyerere.
 
Mag3 hujatuambia mbadala wa CCM,kama hakuna mbadala mimi nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM,nikiwa naamini tatizo si CHAMA bali WATU,leo simba ikifungwa na KAGERA tatizo sio SIMBA bali waliopewa dhamana,dawa kuwabadili Mag3
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom