Kanuni za fizikia ya umeme zimewaamsha wabunge wa CCM kuikataa bajeti ya Ngereja?

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,628
3,155
Inaonekana kila mtanzania anayefatilia habari za siasa za bunge amepatwa na mshangao wa furaha kuhusu kukubaliana kwa wabunge wa CCM na wa Upinzani kuikataa budget ya serikali iliyotengwa kwa ajili ya uendeshaji wa Wizara ya Nishati na Madini. Watu wanajiuliza hivi kwa nini ni katika hili la umeme ambapo wabunge wa CCM wamekubaliana kimtazamo na wabunge wa upinzani kuikataa budget hii? Mbona kuna hoja nyingi sana bungeni zinazozungumzia maslahi ya taifa kama vile kuwajadili na kuwawajibisha watuhumiwa wa ufisadi wa matrilioni ya shilingi za kitanzania walioingizia hasara isiyokokotoleka serikali lakini wabunge wa CCM, kwa kuwa wao ni wengi, wakazikandamiza hizo hoja na kuwasafisha watuhumiwa? Hili la umeme lina nini?


Watu wanaowapongeza wabunge, hasa wa CCM, eti wameamka kwenye masuala ya kitaifa wanasahau kuwa umeme unatii kanuni za asili za fizikia (Laws of Physics). Kama nyumba ya Mbunge wa CCM ipo jirani na ya kwako mlalahoi na mnatumia umeme laini moja; umeme hauwezi kukatika kwako usikatike kwa mbunge. Umeme hauna macho hayo. Kwa hiyo hata wabunge wa CCM makali ya umeme wanayapata. Pia wao wanaudhika wanapokuwa kwenye magheto yao na kuburudika na kiyoyozi kwenye mazingira ya joto kama Dar huku wakiangalia UEFA champions league kwenye Dstv zao mara TANESCO wakachukua chao.


Hivyo tusiwasifie sana wabunge wa CCM. Kwa hili la umeme hata mboni za macho yao zinaguswa. Ni pale tu watakapotetea maslahi ya umma bila kujali kama wao wana maslahi ya moja kwa moja au la ndipo tutakapofahamu kuwa, ah, kumbe wabunge wa CCM nao wanaweza kuwa na mawazo mazuri!
 
Back
Top Bottom