Kanuni za bunge maalum la katiba 2014

NAPITA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
5,076
2,243




View attachment Rasimu kanuni bunge maalum-nyingine.pdfSHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA

SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI
Jina
1.(1) Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Bunge Maalum, Toleo la mwaka
2014.
(2) Kanuni hizi zitaanza kutumika baada ya kupitishwa na Bunge
Maalum.
Matumizi
2.(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria, Kanuni hizi zitatumika kwa mambo
yote yanayohusu utaratibu wa uendeshaji wa Shughuli za Bunge Maalum.
(2) Iwapo jambo au shughuli yoyote haikuwekewa masharti katika
Kanuni hizi, Mwenyekiti ataamua utaratibu wa kufuata katika jambo au
shughuli hiyo, kwa kuzingatia mila na desturi za uendeshaji wa Shughuli za
Bunge Maalum.
(3) Utaratibu utakaowekwa kwa mujibu wa fasili ya (2) utatumika kama
sehemu ya Kanuni hizi katika kuongoza uendeshaji wa Shughuli za Bunge
Maalum
Tafsiri
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama maelezo yanahitaji vinginevyo-
"Akidi" ni idadi ya Wajumbe wa Bunge Maalum inayoruhusiwa kufanya
maamuzi ya Bunge Maalum kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 33(1) ya
Kanuni hizi;
"Bunge Maalum" maana yake ni Bunge Maalum lililoundwa kwa mujibu
wa masharti ya kifungu cha 22(1) cha Sheria;
"Gazeti" ni Gazeti la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
"Hoja" maana yake ni pendekezo mahsusi lililotolewa na Kamati ya
Bunge Maalum au Mjumbe wa Bunge Maalum kwa ajili ya kupata Uamuzi wa
Bunge Maalum kuhusu kuboresha masharti ya Rasimu ya Katiba;
Jamhuri ya Muungano" ni eneo lote lililokuwa ndani ya mipaka ya
Jamhuri ya Tanganyika na eneo lote lililokuwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar kabla ya tarehe 26 Aprili, 1964;
"Kamati" ni Kamati yoyote ya Bunge Maalum iliyoundwa kwa mujibu
wa Kanuni hizi;
1
"Kamati inayopendekezwa" maana yake ni Rasimu ya Katiba
iliyopitishwa na Bunge la Katiba kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
"Katibu" ni Katibu wa Bunge Maalum au Naibu Katibu wa Bunge
Maalum aliyetajwa katika Kifungu cha 24(1) cha Sheria na inajumisha pia
mtumishi mwingine yeyote wa Bunge Maalum aliyeidhinishwa kutekeleza kazi
ya Katibu;
"Kikao" ni kikao cha siku moja cha Bunge Maalum kinachoanza kwa
kusomwa Dua na kumalizika kwa kuahirisha Bunge Maalum hadi siku
itakayotajwa;
"Kitabu cha Maamuzi" ni kitabu cha Kumbukumbu ya maamuzi
mbalimbali ya Mwenyekiti kuhusu suala lolote la utaratibu katika Bunge
Maalum;
"Maeneo ya Bunge" linajumuisha eneo lote la Ukumbi unaotumika
kuendesha Mikutano ya Bunge Maalum, pamoja na ofisi, vyumba, maeneo ya
mahojiano baina ya Wajumbe wa Bunge Maalum na watu wengine, kumbi,
bustani, viwanja na maeneo yote mengine yanayotumiwa kuendesha shughuli
za Bunge Maalum na Kamati zake;
"Mamlaka ya Bunge" ni mamlaka ya Bunge Maalum kama yalivyotajwa
katika kifungu cha 25 cha Sheria;
"Maisha ya Bunge Maalum" ni muda wote unaoanzia tarehe ambapo
Bunge Maalum limeitishwa na Rais likutane kwa mujibu wa masharti ya
kifungu cha 22(4) na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwake kwa mujibu wa
masharti ya kifungu cha 28 cha Sheria;
"Mgeni" maana yake ni mtu yeyote ambaye si Mjumbe, Katibu au
mtumishi yeyote wa sekretarieti ya Bunge Maalum, na ambaye hatekelezi kazi
rasmi zinazohusu Bunge Maalum;
"Mjumbe" ni mtu aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum kwa
mujibu wa masharti ya kifungu cha 22 cha Sheria;
"Mkutano wa Bunge" ni mfululizo wa vikao vya Bunge kuanzia kikao
cha kwanza hadi cha mwisho, vinavyopangwa kwa ajili ya Bunge Maalum
kujadili na kufanya uamuzi kuhusu jambo au hoja mahsusi iliyowekwa kwenye
Orodha ya Shughuli kwa kuzingatia ratiba ya Shughuli za Bunge Maalum
iliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni hizi;
"Mpambe wa Bunge Maalum" ni mtumishi wa Seretarieti ya Bunge
Maalum anayetekeleza majukumu yaliyoainishwa katika Kanuni ya 27 ya
Kanuni hizi;
"Mwenyekiti" maana yake ni Mjumbe wa Bunge Maalum aliyechaguliwa
kuwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum kwa mujibu wa
kifungu cha 23 cha Sheria;
"Mwenyekiti wa Kamati" maana yake ni mjumbe yeyote aliyechaguliwa
kuongoza Kamati au Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge Maalum;
"Mwenyekiti wa Muda" maana yake ni mjumbe wa Bunge Maalum
aliyechaguliwa kuwa Mwenyekliti wa muda kwa mujibu wa Kifungu cha 22A
cha Sheria;
"Mwenyekiti wa Tume" maana yake ni Mwenyekiti wa Tume ya
Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananachi kuhusu mchakato wa mabadiliko
ya Katiba;
2
"Orodha ya Shughuli" ni Waraka mahsusi unaoonyesha mpangilio wa
Shughuli za Bunge Maalum katika kila kikao cha Bunge Maalum;
"Rais" ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
"Rasimu ya Katiba" maana yake ni Rasimu ya Katiba ambayo
imetayarishwa na Tume chini ya Sheria;
"Sekretarieti" ni watumishi wa Sekretarieti ya Bunge Maalum
waliochaguliwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 24(5) na (6) cha
Sheria;
"Sheria" maana yake ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83;
"Siwa" ni alama maalum inayotumika kama kielelezo cha mamlaka ya
Bunge Maalum;
"Taarifa Rasmi" ni taarifa za majadiliano ya Bunge Maalum zilizotajwa
kwenye Kanuni hizi;
"Tume" maana yake ni Tume iliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuratibu
na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba;
"Wimbo wa Taifa" ni wimbo wa Taifa wa Jamhuri ya Muungano.
SEHEMU YA PILI
HAKI, KINGA NA MADARAKA YA BUNGE MAALUM
Bunge
Maalum
4.(1) Bunge Maalum litaitishwa na Rais baada ya kukubaliana na Rais wa
Zanzibar kupitia Tangazo kwenye Gazeti la Serikali ambalo litataja tarehe,
siku, mahali na muda ambao Rais ameliitisha Bunge Maalum kukutana.
(2) Bunge Maalum litakuwa na Wajumbe watakaotangazwa na Rais
kupitia agizo katika Gazeti la Serikali ambao ni-
(a) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
(c) Wajumbe mia mbili na moja walioteuliwa na Rais kwa makubaliano
na Rais wa Zanzibar kama ifuatavyo:

Wajumbe ishirini kutoka Taasisi zisizokuwa za kiserikali;
Wajumbe ishirini kutoka Taasisi za kidini;
Wajumbe arobaini na mbili kutoka Vyama vyote vya siasa
vyenye usajili wa kudumu;
Wajumbe ishirini kutoka Taasisi za elimu ya juu;
Wajumbe ishirini kutoka makundi ya watu wenye
ulemavu;
Wajumbe kumi na tisa kutoka Vyama vya Wafanyakazi;
Wajumbe kumi kutoka Vyama vya Wafugaji;
Wajumbe kumi kutoka Vyama vinavyowakilisha Wavuvi;
Wajumbe ishirini kutoka Vyama vya Wakulima;
Wajumbe ishirini kutoka makundi mengine yoyote
ambayo yana malengo yanayofanana.

3 Mamlaka ya Bunge Maalum
5.(1) Kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria, Bunge Maalum
litakuwa na mamlaka ya-
(a) kujadili na kupitisha Rasimu ya Katiba; na
(b) kutunga masharti ya mpito na masharti yatokanayo na Rasimu ya
Katiba kadri litakavyoona inafaa.
(2) Katika kutekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa fasili ya (1), Bunge
Maalum litazingatia masharti ya Sheria na Kanuni hizi.
Haki na
kinga za
Bunge
Maalum

6.(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, maoni katika mijadala ya Bunge
Maalum na maoniya Mjumbe hayatahojiwa mahakamani au sehemu yoyote nje
ya Bunge Maalum.
(2) Utaratibu wa kuendesha mijadala katika Bunge Maalum utakuwa
kama ulivyowekwa na Kanuni hizi.
(3) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, kila mjumbe wa
Bunge Maalum atatekeleza majukumu yake kwa uhuru, na hatashurutishwa,
hatashinikizwa wala kupokea maelekezo kutoka kwa mtu au chombo chochote.
(4) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria au sheria nyingine yeyote,
Mjumbe yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani
kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge Maalum
linalohusiana na utekelezaji wa mamlaka ya Bunge Maalum.
(5) Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum hatashitakiwa wala kufunguliwa
shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au
alilolifanya katika kutekeleza uamuzi wowote wa Bunge Maalum au wa
Kamati yoyote ya Bunge Maalum.
(6) Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum hatakamatwa kwa sababu ya
shauri lolote la madai, isipokuwa kwa kosa la jinai, ambapo Bunge Maalum
litakuwa na haki ya kutaarifiwa kuhusu kukamatwa huko na sababu zake.
Ukomo
wa
mamlaka
ya Bunge
Maalum

7. Bila ya kuathiri masharti ya kifungu cha 28(2) cha Sheria, Bunge
Maalum litafikia ukomo wake baada ya kupitisha masharti ya Rasimu ya
Katiba, masharti ya mpito na masharti yatokanayo na Rasimu ya Katiba.
SEHEMU YA TATU
MIKUTANO NA VIKAO VYA BUNGE MAALUM
Utaratibu wa
ukaaji ndani
ya Ukumbi
wa Mikutano
ya Bunge
Maalum

8.(1) Kila Mjumbe wa Bunge Maalum kabla ya kuingia katika Ukumbi
wa Mikutano ya Bunge Maalum, na kukaa mahala pake, atatakiwa kuweka
saini katika Kitabu cha Mahudhurio kitakachowekwa kwenye eneo
litakalopangwa kwa ajili hiyo.
(2) Baada ya kuingia Ukumbini, kila Mjumbe atakaa mahala pake, kwa
4
mujibu wa utaratibu maalum wa ukaaji wa Wajumbe ndani ya Ukumbi wa
Mikutano utakaokuwa umewekwa na Katibu.
(3) Wapambe na Watumishi wa Bunge Maalum pamoja na waandishi
wa habari watakaa sehemu ambazo zimetengwa kwa ajili yao.
(4) Wageni wengine wanaweza kutengewa sehemu maalum ya kukaa.
(5) Wageni mashuhuri, Mabalozi na Viongozi wengine watakaa
sehemu maalum kama itakavyopangwa na Katibu.
Mkutano wa
kwanza wa
Bunge
Maalum

9.(1) Mkutano wa kwanza wa Bunge Maalum utaanza tarehe, siku na
mahali ambapo Rais ataagiza kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 22(4)
cha Sheria.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni hizi kuhusu kuanza na kukoma
kwa vikao vya Bunge Maalum, Mkutano wa kwanza wa Bunge utaendelea
kwa muda wowote ambao utahitajika kwa ajili ya kutekeleza na kukamilisha
shughuli zote za Mkutano wa kwanza wa Bunge Maalum.
(3) Kila Mkutano unaofuata wa Bunge Maalum utaanza siku yoyote
itakayopangwa na Bunge lenyewe au siku yoyote itakayopangwa kwa
mujibu wa Kanuni hizi.
Shughuli
za Mkutano
wa Kwanza
wa Bunge
Maalum

10.(1) Shughuli za Mkutano wa Kwanza wa Bunge Maalum zitakuwa
kama ifuatavyo-
(a) kusomwa kwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge Maalum;
(b) uchaguzi wa Mwenyekiti wa muda;
(c) kuandaa na kupitisha Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Bunge
Maalum;
(d) uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti;
(e) kiapo cha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti;
(f) wimbo wa Taifa na Dua ya Kuiombea Nchi na Bunge Maalum;
(g) kiapo cha Wajumbe wa Bunge Maalum;
(h) Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba;
(i) shughuli yoyote nyingine ambayo Bunge Maalum litaona inafaa
kufanywa au kutekelezwa kwa wakati huo.
(2) Mwanzoni mwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa
Bunge Maalum, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano au Katibu wa
Baraza la Wawakilishi, atasoma Tangazo la Rais la kuliitisha Bunge
Maalum.
5
(3) Mara baada ya Tangazo la Rais kusomwa kwa mujibu wa fasili ya
(2), Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la
Wawakilishi kwa pamoja watasimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda
wa Bunge Maalum kwa utaratibu watakaoona kuwa unafaa.
(4) Baada ya Mwenyekiti wa Muda kupatikana, Bunge Maalum
litafanya shughuli ya kuandaa na kupitisha Kanuni za Bunge Maalum
zinazoweka utaratibu wa kuendesha shughuli zake.
(5) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (6), Kanuni zilizopitishwa kwa
mujibu wa fasili ya (4) zitaanza kutumika mara moja kuendesha Shughuli za
Bunge Maalum, baada ya nakala zake kugawanywa kwa Wajumbe.
(6) Toleo la Kanuni za Bunge Maalum litachapishwa kwenye Gazeti la
Serikali.
Utaratibu wa
kumchagua
Mwenyekiti
na Makamu
Mwenyekiti

11.(1) Kutakuwa na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
wa Bunge Maalum utakaofanyika katika Mkutano wa Kwanza wa Bunge
Maalum, mara baada Bunge Maalum kuandaa na kupitisha Kanuni zake.
(2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watachaguliwa kutoka
miongoni mwa Wajumbe wa Bunge Maalum, kwa kuzingatia masharti ya
kifungu cha 23(4) cha Sheria na utaratibu ulioainishwa katika Nyongeza ya
Kwanza ya Kanuni hizi.
(3) Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti utafanyika na
kuendeshwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 23 cha Sheria, masharti
ya Kanuni hizi, na pia kwa kuzingatia utaratibu wa Uchaguzi uliowekwa na
Nyongeza ya Kwanza ya Kanuni hizi.
(4) Endapo ikitokea kuwa Kiti cha Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti ki-wazi, uchaguzi utaitishwa kumchagua Mjumbe wa kuziba
nafasi hiyo, na Mjumbe huyo atatakiwa atoke upande wa Jamhuri ya
Muungano alikokuwa ametokea mtangulizi wake.
Kiapo cha
Mwenyekiti
na Makamu
Mwenyekiti

12.(1) Mjumbe yeyote aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti, kabla ya kushika madaraka yake, ataapa au kula yamini,
vyovyote itakavyokuwa, mbele ya Katibu wa Bunge Maalum, kwa kutamka
maneno yafuatayo yaliyowekwa na Jedwali la Nne la Sheria:
"Mimi...................................................nikiwa nimechaguliwa kuwa
Mwenyekiti/Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum, naapa/nathibitisha
kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano na
kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu na
kufanya kazi zinazonihusu bila upendeleo, na bila ya kukiuka Sheria za
Nchi. Ewe Mungu nisaidie".
6
(2) Wakati wa kuapa au kula yamini, Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti anayeamini kuwa kuna Mungu, atalazimika kushika Biblia au
Kuran au kitabu kingine kitakatifu kinachotambuliwa na imani ya dini yake.
(3) Iwapo Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti haamini kuwa kuna
Mungu, basi hatashika Biblia au Kuran au kitabu chochote kitakatifu au
kutamka maneno "Ewe Mungu nisaidie", bali atalazimika kuinua juu mkono
wake wa kuume.
Wimbo wa
Taifa

13.(1) Baada ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kushika
madaraka yao, Wimbo wa Taifa utapigwa na kuimbwa kuashiria kuanza
rasmi kwa Shughuli za Bunge Maalum, na pia baada ya kikao cha mwisho
cha Mkutano wa mwisho, kuashiria kukamilika kwa Shughuli za Bunge
Maalum.
(2) Wakati Wimbo wa Taifa unapigwa na kuimbwa, kila Mjumbe na
mtu yeyote aliyopo ndani ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum,
atasimama mahala pake kwa staha na utulivu, kama ilivyo mila na desturi ya
kutoa heshima kwa Wimbo wa Taifa unapopigwa na kuimbwa.
Dua ya
kuiombea
Jamhuri ya
Muungano
na Bunge
Maalum
14.(1) Dua ya kuiombea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
kuliombea Bunge Maalum itasomwa na Mwenyekiti, itakuwa na maneno
yafuatayo:-
"Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu, Muumba Mbingu na Dunia,
umeweka Mataifa katika Dunia, ili haki yako itendeke. Twakuomba
uibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania idumishe uhuru, umoja,
haki na amani.
Utujaalie hekima na busara, sisi Wajumbe wa Bunge hili Maalum ili
tuwe na uwezo wa kujadili kwa dhati mambo yatakayoletwa mbele
yetu leo, na kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya watu wote na
ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amina."
(2) Wakati Dua ya kuiombea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
kuliombea Bunge Maalum itakapokuwa inasomwa, kila Mjumbe aliyepo
ndani ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum atasimama kwa staha na
utulivu mahala pake, kama ilivyo mila na desturi ya kutoa heshima kwa Dua.
Kiapo kwa
Mjumbe wa
Bunge
Maalum

15.(1) Kila Mjumbe ataapa au kula yamini mbele ya Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti kwa kutamka maneno yafuatayo:
"Mimi ........................... nikiwa nimeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge
Maalum, naapa/nathibitisha kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu
kwa Jamhuri ya Muungano na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu,
nitatimiza wajibu wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila ya
upendeleo, na bila ya kukiuka Sheria za nchi. Ewe Mungu Nisaidie."
7
(2) Wakati wa kuapa au kula yamini, Mjumbe anayeamini kuwa kuna
Mungu, atalazimika kushika Biblia au Kuran au kitabu kingine kitakatifu
kinachotambuliwa na imani ya dini yake.
(3) Iwapo Mjumbe haamini kuwa kuna Mungu, basi hatashika Biblia
au Kuran au kitabu chochote kitakatifu au kutamka maneno "Ewe Mungu
nisaidie", bali atalazimika kuinua juu mkono wake wa kuume.
(4) Utaratibu wa kuapa au kula yamini utakuwa ni kwa mujibu wa
Orodha ya majina ya Wajumbe iliyoandaliwa kwa kuzingatia mpangilio wa
alfabeti ya kwanza ya jina la kwanza la kila Mjumbe.
Mikutano ya
kawaida ya
Bunge
Maalum

16.(1) Isipokuwa kama itaelekezwa vinginevyo, kila Mkutano wa
Bunge Maalum utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum
ulioandaliwa kwa ajili hiyo.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni zinazofuata za Kanuni hii, kila
Mkutano, isipokuwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge Maalum, utaanza siku,
tarehe na wakati utakaowekwa na Bunge Maalum.
(3) Iwapo manufaa ya Taifa yatahitaji kuwa Bunge Maalum lisikutane
tarehe ile iliyowekwa kwa Mkutano utakaofuata, bali likutane tarehe ya
mbele zaidi au ya nyuma zaidi, basi Mwenyekiti anaweza, baada ya
kushauriana na Kamati ya Shughuli za Bunge Maalum kuliitisha Bunge
likutane tarehe hiyo ya mbele zaidi au nyuma zaidi.
Utaratibu wa
vikao vya
Bunge
Maalum

17.(1) Vikao vya Mikutano ya Bunge Maalum, isipokuwa kikao cha
kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Maalum, vitaanza saa tatu
asubuhi, ila tu kama Bunge Maalum litaamua vinginevyo.
(2) Bunge Maalum litakutana hadi saa saba mchana ambapo
Mwenyekiti atasitisha Shughuli yoyote itakayokuwa inafanyika, hadi saa
kumi jioni:
Isipokuwa kwamba, Mwenyekiti akiona inafaa, Bunge Maalum
linaweza kuendelea kukutana kwa muda usiozidi dakika thelathini, au
kusitishwa wakati wowote kabla ya saa saba mchana, baada ya kuwahoji
Wajumbe.
(3) Hoja ya kubadilisha nyakati za vikao inaweza kutolewa na Mjumbe
yeyote na itaamuliwa kama hoja nyingine yoyote na haitahitaji kutolewa
taarifa.
(4) Bunge Maalum litaendelea kukutana hadi saa mbili usiku, wakati
ambapo Mwenyekiti atasitisha shughuli na kuliahirisha hadi kesho yake au
siku nyingine atakayoitaja.
8
(5) Endapo shughuli zilizopangwa kwa siku hiyo zimemalizika kabla
ya saa mbili usiku, Mwenyekiti ataliahirisha Bunge Maalum bila kuhoji,
lakini iwapo zimesalia dakika kumi kabla ya kufikia muda wa kuliahirisha,
na Bunge au Kamati ya Bunge Zima bado haijamaliza shughuli zake,
Mwenyekiti anaweza kuongeza muda usiozidi dakika thelathini, bila kulihoji
Bunge au Kamati ya Bunge Zima, ili kukamilisha shughuli zilizobaki.
(6) Iwapo wakati wa kusitisha Shughuli umefika na Mwenyekiti
atakuwa analihoji au yupo karibu kulihoji Bunge Maalum, basi hatasitisha
Shughuli hadi hoja iwe imeamuliwa, na baada ya hoja kuamuliwa,
Mwenyekiti ataliahirisha Bunge Maalum hadi kesho yake au siku nyingine
atakayoitaja.
(7) Endapo majadiliano yote ya Bunge Maalum au Kamati ya Bunge
Zima yatasitishwa na Mwenyekiti kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hii,
wakati yatakaporudiwa katika Bunge Maalum au katika Kamati ya Bunge
Zima, yataendelezwa kuanzia pale yalipositishwa, na Mjumbe yeyote
ambaye hotuba yake ilikatizwa na Mwenyekiti, atakuwa na haki ya
kuendelea na maelezo yake katika marudio ya mjadala huo, na endapo
Mjumbe hatoitumia haki yake hiyo, basi atahesabiwa kuwa alikuwa
amemaliza kutoa maelezo yake.
(8) Iwapo shughuli zilizopangwa kwa ajili ya kikao hazijamalizika, na
mjumbe akatoa hoja ya kuahirisha kikao kutokana na dhamira au sababu
nyingine yoyote. Mwenyekiti atalihoji Bunge Maalum kuhusu hoja ya
kuahirisha kikao hicho na baada ya hoja hiyo kuafikiwa, atakiahirisha kikao
hicho hadi kikao kinachofuata ambacho, kama Bunge Maalum halikuamua
vinginevyo, kitakuwa ni siku itakayofuata, isipokuwa tu kama itakuwa ni
siku ya Jumamosi, Jumapili au siku ya mapumziko.
Kuahirisha
Mkutano wa
Bunge
Maalum

18.(1) Isipokuwa kwa Mkutano wa mwisho wa Bunge Maalum, kila
Mkutano wa Bunge Maalum utafungwa kwa kuliahirisha Bunge Maalum
hadi Mkutano utakaofuata.
(2) Endapo Shughuli zote zilizowekwa kwenye Orodha ya Shughuli
kwa ajili ya Mkutano huo zimemalizika, Mwenyekiti atalihoji Bunge
Maalum kuhusu hoja ya kuahirisha Bunge Maalum.
(3) Mara tu baada ya Bunge Maalum kupitisha hoja ya kuahirisha
Mkutano wa Bunge Maalum, Mwenyekiti ataliahirisha Bunge Maalum hadi
siku, muda na mahali atakapopataja:
Isipokuwa kwamba, iwapo kikao hicho kitakuwa ni cha mwisho cha
Mkutano wa Mwisho wa Bunge Maalum, Wimbo wa Taifa utapigwa na
kuimbwa kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Kanuni hizi.
Wajibu wa
Mjumbe
kuhudhuria
Mikutano na
19.(1) Kila Mjumbe wa Bunge Maalum atakuwa na wajibu wa
kuhudhuria Mikutano na vikao vyote vya Bunge Maalum na Kamati zake.
9
vikao vya
Bunge
Maalum
(2) Mjumbe yeyote atakayepata tatizo lolote linalomfanya ashindwe
kuhudhuria Mkutano au kikao cha Bunge Maalum na Kamati zake, atatakiwa
kumwarifu na kumwomba ruhusa Mwenyekiti wa Bunge Maalum na pia
Mwenyekiti wa Kamati husika ya Bunge Maalum kwa maandishi.
(3) Mjumbe yeyote ambaye atashindwa kuhudhuria kikao chochote cha
Bunge Maalum hatalipwa posho ya kikao au vikao alivyoshindwa
kuhudhuria.
(4) Kwa kuzingatia kwamba, kuhudhuria Mikutano na vikao vya
Bunge Maalum na Kamati zake ni wajibu wa kwanza wa kila Mjumbe, mtu
au chombo chochote kitakachomkamata na kumzuia Mjumbe yeyote wa
Bunge Maalum kuhudhuria Mikutano na vikao vya Bunge Maalum
kitalazimika kutoa taarifa ya maandishi kwa Mwenyekiti kuhusu kukamatwa
na kuzuiliwa kwa Mjumbe huyo na sababu zake.


SEHEMU YA NNE
UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM

(a) Viongozi wa Bunge Maalum Mwenyekiti na mamlaka yake
20.(1) Mwenyekiti atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge Maalum, na
majukumu yake yatakuwa ni:
(a) kuongoza Mikutano na vikao vya Bunge Maalum;
(b) kuongoza mwenendo na utaratibu wa majadiliano katika Mikutano
na vikao vya Bunge Maalum;
(c) kutoa uamuzi kuhusu masuala yote ya utaratibu katika Mikutano na
vikao vya Bunge Maalum;
(d) kusimamia amani na utulivu katika Mikutano na vikao vya Bunge
Maalum;
(e) kusimamia uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge Maalum.
(2) Mwenyekiti wa Bunge Maalum atakuwa na madaraka na mamlaka
ya kutafsiri Kanuni hizi, na uamuzi wake kuhusu suala lolote la utaratibu
kwa mujibu wa Kanuni hizi utakuwa ni wa mwisho.
(3) Katika kutekeleza majukumu yake, Mwenyekiti ataongozwa na
Sheria pamoja na Kanuni hizi, na pale ambapo Kanuni hazikutoa mwongozo,
basi ataongozwa na sheria nyingine za nchi, kanuni nyingine zilizopo,
pamoja na mila na desturi za nchi nyingine katika uendeshaji bora wa
Shughuli za Bunge Maalum.
(4) Mwenyekiti atawajibika kusimamia ipasavyo Kanuni zote za
Bunge Maalum, na katika kutekeleza wajibu huo, anaweza kumtaka Mjumbe
10
yeyote anayekiuka Kanuni yeyote au utaratibu uliowekwa na Kanuni hizi
ajirekebishe mara moja.
(5) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (3), wakati wowote ambapo
Mwenyekiti hatakuwepo katika Bunge Maalum, au kwa sababu nyingine
yoyote hawezi kutekeleza madaraka na majukumu ya Mwenyekiti, basi
madaraka na majukumu hayo yatatekelezwa na Makamu Mwenyekiti.
(6) Mwenyekiti atakoma kuwa Mwenyekiti na Kiti cha Mwenyekiti
kitakuwa ki-wazi endapo litatokea tukio lolote kati ya matukio yafuatayo-
(a) atafariki;
(b) atajiuzulu;
(c) atathibitika kuwa amekosa uwezo wa kutekeleza majukumu yake
kwa sababu za kiafya;
(d) atatiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifungo gerezani
kwa muda usiopungua mwezi mmoja; na
(e) atapoteza sifa ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum.
(7) Hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge Maalum
wakati wowote ambapo Kiti cha Mwenyekiti kitakuwa ki-wazi, isipokuwa
uchaguzi wa Mwenyekiti.
Makamu
Mwenyekiti
na
majukumu
21.(1) Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum atashika madaraka
yake kwa mujibu wa masharti ya Sheria na Kanuni hizi.
(2) Makamu Mwenyekiti atakuwa msaidizi wa Mwenyekiti katika
kuliongoza Bunge Maalum na atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa
masharti ya Kanuni hizi.
(3) Wakati wowote ambao Mwenyekiti hayupo katika Bunge au kwa
sababu nyingine yoyote hawezi kutekeleza mamlaka na majukumu yake, basi
mamlaka au majukumu hayo yatatekelezwa na Makamu Mwenyekiti.
(4) Wakati wowote ambao Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wote
hawapo Bungeni, au kwa sababu nyingine yoyote hawawezi kutekeleza
mamlaka na majukumu yao, basi mamlaka na majukumu hayo yatatekelezwa
na Mjumbe yeyote atakayechaguliwa na Wajumbe kwa ajili hiyo.
(5) Makamu Mwenyekiti atakoma kuwa Makamu Mwenyekiti na Kiti
cha Makamu Mwenyekiti kitakuwa ki-wazi iwapo -
(a) atafariki;
11
(b) atajiuzulu,
(c) atathibitika kuwa amekosa uwezo wa kutekeleza majukumu yake
kwa sababu za kiafya;
(d) atatiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifungo gerezani
kwa muda usiopungua mwezi mmoja; na
(e) atapoteza sifa ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum.
Uadilifu kwa 22.(1) Kwa kuzingatia kiapo cha kazi yake kilichowekwa kwa mujibu
viongozi wa wa Sheria, na kwa madhumuni ya uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge
Bunge Maalum, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe yeyote atakayekuwa
Maalum amechaguliwa kutekeleza kazi na majukumu ya Mwenyekiti wa Bunge
Maalum, ataendesha Shughuli za Bunge Maalum kwa kutoa uamuzi kwa
haki, kwa uadilifu na bila chuki wala upendeleo wowote, kwa kuongozwa na
Sheria, sheria nyingine za nchi, Kanuni hizi, Kanuni nyingine zilizopo,
pamoja na mila na desturi za Nchi nyingine katika uendeshaji bora wa
Shughuli za Bunge Maalum.
Katibu na 23. Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum kama walivyotajwa
Naibu katika kifungu cha 24 cha Sheria, kabla ya kushika madaraka yao, kila
Katibu wa mmoja wao ataapishwa na Rais kiapo kilichowekwa kwa mujibu wa kifungu
Bunge cha 24(7) cha Sheria.
Maalum
Kazi na 24.(1) Katibu atawajibika kuhakikisha utekelezaji bora wa kazi na
majukumu majukumu ya Bunge Maalum, na kwa madhumuni hayo-
ya Katibu wa
Bunge
Maalum
(a) atahudhuria au atawakilishwa na mtumishi yeyote wa Bunge
Maalum katika vikao vyote vya Bunge Maalum, vikao vya Kamati
ya Bunge Zima, na vikao vya Kamati nyingine yoyote ya Bunge
Maalum;
(b) ataweka kumbukumbu zote zinazotakiwa ziwekwe kwa mujibu wa
Kanuni hizi;
(c) atatayarisha Taarifa Rasmi za majadiliano ya Bunge Maalum kwa
mujibu wa Kanuni hizi;
(d) atatayarisha kwa utaratibu wa siku hadi siku, kitabu cha Shughuli za
Bunge Maalum na kukihifadhi ofisini kikiwa kinaonesha yafuatayo:
(i) maagizo yeyote yaliyotolewa na Bunge Maalum;
(ii) shughuli zote zilizopangwa kufanywa siku yoyote ya baadaye;
na
(iii) taarifa zote za hoja zilizokubaliwa na Mwenyekiti.
12
(2) Katibu atawajibika kuhakikisha utekelezaji bora wa Shughuli za
Bunge Maalum na kwa madhumuni hayo atatayarisha siku hadi siku, Orodha
ya Shughuli za Bunge Maalum kama itakavyoelekezwa na Mwenyekiti.
(3) Katibu atawajibika kutunza kitabu cha Maamuzi ya Mwenyekiti,
Kitabu cha Shughuli, Taarifa Rasmi za Majadiliano ya Bunge Maalum,
nakala ya Rasimu ya Katiba, nakala ya Katiba, unayopendekezwa na Bunge
Maalum na hati nyingine zilizowasilishwa katika Bunge Maalum.
(4) Mwananchi yeyote anaweza kukagua kumbukumbu zilizoainishwa
katika fasili ya (3) wakati wowote unaofaa kwa kufuata utaratibu
utakaowekwa na Mwenyekiti.
(5) Katibu ataweka kumbukumbu ya Uamuzi wa mara kwa mara wa
Mwenyekiti kuhusu masuala ya utaratibu katika Bunge Maalum.
(6) Katibu atawajibika kuhakikisha kuwa Ukumbi wa Mikutano ya
Bunge Maalum , Kumbi za Mikutano ya Kamati za Bunge Maalum, maeneo
ya Bunge Maalum, huduma kwa Wajumbe wa Bunge Maalum na vifaa
vingine vinavyohusika na Shughuli za Bunge Maaalum viko katika hali nzuri
na inayofaa kuliwezesha Bunge Maalum kutekeleza kazi na majukumu yake
ipasavyo.
Naibu
Katibu na
majukumu
yake
25.(1) Naibu Katibu atashika madaraka yake kwa mujibu wa masharti
ya Sheria na Kanuni hizi.
(2) Naibu Katibu atakuwa msaidizi wa Katibu katika kuhakikisha
utekelezaji bora wa kazi na majukumu ya Bunge Maalum, na katika
utekelezaji wa kazi na majukumu ya Ofisi ya Katibu.
(3) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, wakati wowote
ambao Katibu hatakuwepo au kwa sababu nyingine yoyote hawezi
kutekeleza madaraka na majukumu yake, basi madaraka na majukumu hayo
yatatekelezwa na Naibu Katibu.
(4) Endapo wakati wowote Katibu na Naibu Katibu wote hawapo
Bungeni, au kutokana na sababu nyingine yoyote, hawawezi kutekeleza
madaraka na majukumu yao, basi madaraka na majukumu hayo
yatatekelezwa na mtumishi yoyote wa Bunge Maalum atakayeteuliwa na
Katibu kwa ajili hiyo.
(b) Sekretarieti ya Bunge Maalum
Sekretarieti
ya Bunge
Maalum
26.(1) Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum, watateua watumishi
kuunda Sekretarieti ya Bunge Maalum, kwa mujibu wa masharti ya kifungu
cha 24 cha Sheria.
13
(2) Sekretarieti ya Bunge Maalum itakuwa na watumishi kwa idadi na
nafasi za madaraka ambazo Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum
wataona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa kazi na majukumu ya Bunge
Maalum.
(3) Sekretarieti ya Bunge Maalum chini ya uongozi wa Katibu na
Naibu wa Bunge Maalum itatekeleza kazi na shughuli zote zilizowekwa au
zitakazokuwa ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji bora wa
shughuli za Bunge Maalum kwa mujibu wa masharti ya Sheria na ya Kanuni
hizi.
(c) Uendeshaji wa Shughuli
Shughuli za
kila siku
27.(1) Katibu ataandaa Orodha ya Shughuli za kila siku za vikao vya
Bunge Maalum, kwa mujibu wa maelekezo ya Mwenyekiti baada ya
kushauriana na Kamati ya Shughuli na kugawa nakala kwa kila Mjumbe
kabla ya kikao husika.
(2) Katibu, kwa maelekezo ya Mwenyekiti, baada ya kushauriana na
Kamati ya Shughuli za Bunge Maalum, anaweza kuandaa Nyongeza ya
Orodha ya Shughuli, na kugawa nakala kwa kila Mjumbe, kabla au wakati
wa kikao husika.
(3) Kamati ya Shughuli iliyoundwa kwa mujibu wa Kanuni hizi
itamshauri Mwenyekiti kuhusu uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge
Maalum.
Upangaji wa
muda wa
kutekeleza
shughuli
28.(1) Mwenyekiti kwa kushirikiana na Kamati ya Shughuli atapanga
muda wa majadiliano ya Bunge kwa kila jambo litakalowasilishwa Bungeni
kwa ajili ya kujadiliwa.
(2) Baada ya muda uliopangwa kwa mujibu wa fasili ya (1) kuisha,
Mwenyekiti baada ya kusitisha mjadala, atalihoji Bunge kwa ajili ya kupata
uamuzi kuhusu jambo lililokuwa linajadiliwa.
(d) Mpangilio wa Shughuli
Mpangilio
wa Shughuli
za Bunge
Maalum

29.(1) Shughuli za Bunge Maalum zitaendeshwa kwa kufuata
mpangilio ufuatao:-
(a) kuwaapisha Wajumbe wapya Kiapo cha Utii;
(b) Taarifa ya Mwenyekiti;
(c) mambo yanayohusu haki za Bunge, ikiwa ni pamoja na kuzifanyia
marekebisho Kanuni za Bunge Maalum;
(d) taarifa au hoja za Kamati;
14 (e) shughuli yoyote ambayo Bunge
kushughulikiwa kwa wakati huo.
Maalum
litaona
inafaa
(2) Shughuli za Bunge Maalum katika kila kikao zitatekelezwa kwa
kufuata Orodha ya Shughuli za siku hiyo au kwa kufuata utaratibu mwingine
ambao Mwenyekiti ataagiza ufuatwe kwa ajili ya uendeshaji bora wa
Shughuli za Bunge Maalum.
(3) Baada ya hoja yoyote kuwasilishwa na kujadiliwa, Bunge Maalum
linaweza kuamua kuipitisha hoja hiyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na
Kanuni hizi, au kwamba, hoja hiyo ipelekwe kwenye Kamati ya Bunge
Maalum inayohusika ili ifanyiwe kazi na kupata ushauri wa ziada kuhusu
hoja hiyo kabla ya kuipitisha.
Taarifa ya 30. Wakati wa kikao chochote cha Bunge Maalum, Mwenyekiti
Mwenyekiti anaweza kutoa taarifa yoyote kuhusu Shughuli za Bunge Maalum kadri
atakavyoona inafaa.
Mambo 31.(1) Jambo lolote linalohusu haki za Bunge Maalum litawasilishwa
yanayohusu kwa kufuata mpangilio wa Shughuli za Bunge uliowekwa chini ya Kanuni ya
haki za 30(1) ya Kanuni hizi, baada ya Mwenyekiti kuarifiwa mapema kuhusu jambo
Bunge hilo.
Maalum
(2) Endapo baada ya kupata taarifa mapema, Mwenyekiti ataamua
kwamba jambo hilo liwasilishwe kwenye Bunge Maalum, basi atampa nafasi
Mjumbe anayehusika kuliwasilisha kwa kutoa maelezo mafupi kuhusu jambo
lenyewe na sababu zinazomfanya aamini kwamba linahusu haki za Bunge
Maalum zilizotajwa kwenye Sheria na Kanuni hizi.
(3) Hoja inayohusu jambo linalohusu haki za Bunge Maalum itapewa
kipaumbele katika mpangilio wa Shughuli nyingine zote zilizopangwa kwa
kikao kinachohusika.
(4) Iwapo wakati wa kikao chochote cha Bunge Maalum jambo lolote
linaloonekana linahusu haki za Bunge Maalum litazuka ghafla, Shughuli
zitasitishwa kwa madhumuni ya kuliwezesha jambo hilo kuwasilishwa na
kuamuliwa, isipokuwa tu kama wakati huo kura inapigwa.
(e) Uhalali wa Shughuli
Akidi ya
vikao vya
Bunge
Maalum

32.(1) Akidi kwa kila kikao cha Bunge Maalum, isipokuwa wakati wa
kupitisha Uamuzi wa Bunge Maalum, itakuwa ni nusu ya Wajumbe wote wa
Bunge Maalum.
(2) Mjumbe yeyote aliyehudhuria anaweza kumjulisha Mwenyekiti
kwamba, Wajumbe waliopo ni pungufu ya akidi inayohitajika kwa ajili ya
Shughuli inayoendelea.

15 (3) Endapo Mwenyekiti ataridhika kwamba, idadi ya Wajumbe walio
ndani ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge ni pungufu ya akidi inayohitajika,
basi atasitisha Shughuli za Bunge kwa muda atakaoutaja na atamwagiza
Katibu kupiga kengele.
(4) Bunge Maalum litakaporejea baada ya muda uliotajwa chini ya
fasili ya (3) kukamilika, Mwenyekiti atahakiki kama idadi ya Wajumbe
waliopo inafikia akidi inayohitajika ili kuwezesha Shughuli inayohusika
kuendelea.
(5) Endapo Mwenyekiti ataridhika kwamba bado idadi ya Wajumbe
waliomo ndani ya Ukumbi wa Bunge haifikii akidi inayohitajika, basi
ataahirisha Shughuli inayohusika ya Bunge hadi muda mwingine
atakaoutaja.
(6) Shughuli za Bunge Maalum pamoja na Uamuzi wowote wa Bunge
Maalum hautakuwa batili kwa sababu tu kwamba nafasi yoyote ya Mjumbe
ipo wazi.
(f) Utaratibu wa Kujadili Hoja
Utaratibu wa 33. Mjumbe wa Bunge Maalum atakapoitwa na Mwenyekiti kujadili
kujadili hoja hoja, atasimama mahali pake na kutoa maelezo yake, kwa kuyaelekeza kwa
Mwenyekiti.
Kubadilisha 34.(1) Hoja ikishatolewa ili iamuliwe inaweza kubadilishwa kwa:-
hoja
(a) kuondoa maneno fulani kwa ajili ya kuingiza maneno mengine;
(b) kuondoa maneno fulani bila ya kuongeza mengine;
(c) kuingiza au kuongeza maneno mapya.
(2) Hoja ya marekebisho au mabadiliko ya hoja yoyote,
itawasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Maalum inayohusika, na
endapo haitapitishwa kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi,
hoja hiyo itatenguka na Katibu ataweka kumbukumbu kwenye Taarifa
Rasmi kwamba, kwakuwa hoja au marekebisho au mabadiliko hayo
hayakuungwa mkono, basi hayakujadiliwa.
(3) Iwapo hoja ya mabadiliko inapendekeza kuondoa maneno fulani
na kuingiza meneno mengine, basi mjadala juu ya suala la kufanya
mabadiliko unaweza kuangalia kwa pamoja yale maneno yanayopendekezwa
yaondolewe na maneno ambayo yanapendekezwa yaingizwe.
(4) Iwapo hoja inapendekeza kuondoa au kuingiza maneno, mjadala
utahusu tu uondoaji au uingizaji wa maneno mapya, kadri itakavyokuwa.

16 (5) Hoja ya kufanya mabadiliko katika hoja nyingine ya mabadiliko
sharti ihusiane na hoja ya kwanza ya mabadiliko na itatolewa, itajadiliwa na
kuamuliwa kabla ya ile hoja ya kwanza ya mabadiliko kufanyiwa uamuzi.
Mabadiliko
ya hoja na
kuondoa
hoja ya
mabadiliko

35.(1) Endapo Kamati inataka kupendekeza mabadiliko yafanywe
katika hoja kwa kufuata masharti ya Kanuni hizi, inaweza kutoa hoja yake ya
kufanya mabadiliko wakati wowote baada ya hoja inayotaka kuibadilisha
kutolewa, lakini kabla ya Bunge kuhojiwa liifanyie uamuzi.
(2) Endapo kuna mapendekezo mawili au zaidi ya kubadilisha hoja
moja, Mwenyekiti ataweka utaratibu wa mpangilio atakaoona unafaa, lakini
pia Mwenyekiti anaweza kuelekeza mapendekezo hayo yapelekwe na
kujadiliwa kwanza kwenye Kamati iliyoshughulikia hoja hiyo.
(3) Iwapo mapendekezo yote ya mabadiliko yameamuliwa, Mwenyekiti
ataitoa tena hoja ya awali ili ijadiliwe kama itakavyokuwa imebadilishwa.
(4) Hoja yoyote ya mapendekezo ya marekebisho au mabadiliko
inaweza kuondolewa wakati wowote kabla haijafikishwa Bungeni iwapo
Kamati inayotoa hoja itampelekea Katibu, taarifa ya maandishi ya kuiondoa
hoja hiyo.
(5) Endapo hoja ya mapendekezo ya marekebisho ya mabadiliko
imefikishwa Bungeni, Kamati inayotoa hoja hiyo inaweza tu kuiondoa hoja
yake kwa Mwenyekiti wa Kamati husika kusimama mahali pake na kusema
"Ninaomba ruhusa kuondoa hoja", na papo hapo Mwenyekiti wa Bunge
Maalum ataliuliza Bunge kama inaafiki hoja hiyo kuondolewa na inapotokea
Wajumbe walio wengi watakubali, Mwenyekiti atasema "Hoja inaondolewa
kwa idhini ya Bunge" na hoja hiyo itakuwa imeondolewa, na Bunge
litaendelea na Shughuli inayofuata.
SEHEMU YA TANO
KANUNI ZA MAJADILIANO
Nyakati za
Mjumbe
kusema
Bungeni
36. Kwa idhini ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mjumbe yeyote wa
Bunge Maalum anaweza kusimama na kuchangia Bungeni katika nyakati
zifuatazo:-
(a) wakati wa kuchangia mjadala wa hoja yoyote iliyowasilishwa katika
Bunge Maalum ambayo Kanuni zinaruhusu ijadiliwe;
(b) wakati anawasilisha mabadiliko yoyote ya hoja;
(c) wakati amesimama kutaka kuzungumzia jambo lolote linalohusu
utaratibu;
(d) wakati amesimama kuzungumzia jambo linalohusu haki za Bunge
Maalum.
17
Jinsi ya
kupata
nafasi ya
kusema
Bungeni

37.(1) Mjumbe yeyote akitaka kusema katika Bunge Malaum anaweza-
(a) kumpelekea Mwenyekiti ombi kwa maandishi;
(b) kusimama kimya mahali pake; au
(c) kutumbukiza kadi ya elektroniki.
(2) Isipokuwa kwamba, Mjumbe yeyote hataanza kuzungumza hadi
aitwe na Mwenyekiti kwa jina lake na kumruhusu kusema, na wakati wa
kusema ataelekeza maneno yake kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
(3) Mjumbe akimaliza kutoa maelezo yake atakaa kwenye nafasi yake
na hapo Mwenyekiti atamwita Mjumbe mwingine aliyepeleka ombi la
maandishi au kama Mwenyekiti hakupata ombi lolote la maandishi, basi
Mjumbe mwingine yeyote anayetaka kujadili hoja, anaweza kusimama
mahali pake na kusubiri Mwenyekiti amwone.
(4) Iwapo Wajumbe wawili au zaidi watasimama wakati mmoja,
Mwenyekiti atamwita Mjumbe atakayemwona kwanza.
(5) Endapo maombi ya kuchangia hoja fulani yatakuwa mengi zaidi ya
muda uliotengwa kwa hoja hiyo, Mwenyekiti atatoa nafasi ya kwanza kwa
Wajumbe ambao:-
(a) hawajachangia katika hoja zilizotangulia kujadiliwa katika
Mkutano unaoendelea; au
(b) wamechangia mara chache katika hoja zilizotungulia kujadiliwa.
(6) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (5) Mwenyekiti atahakikisha
kuwa, nafasi za kuchangia zinatolewa kwa uwiano unaofaa baina ya aina
zote za Wajumbe walioomba kuchangia hoja hiyo.
(7) Masharti yaliyotangulia katika Kanuni hii, hayatamzuia Mwenyekiti
kutoa nafasi ya kuchangia kwa Mjumbe mwingine yeyote iwapo ataona
kuwa, taaluma au uzoefu fulani wa Mjumbe huyo utaboresha hoja
inayojadiliwa.
(8) Mjumbe hatasoma maelezo, isipokuwa, kwa madhumuni ya kutilia
nguvu maelezo yake, anaweza kusoma dondoo kutoka kwenye kumbukumbu
zilizoandikwa au kuchapishwa, na anaweza pia kujikumbusha kwa kuangalia
kwenye kumbukumbu alizoziandika.
(9) Kila Mjumbe atazungumzia jambo ambalo liko katika mjadala tu na
hatarudiarudia maneno yake au yale yaliyokwisha kusemwa na Wajumbe
18
wengine, na iwapo itatolewa hoja ya kufanya mabadiliko katika hoja
inayojadiliwa, mjadala sharti uhusu hoja hiyo ya mabadiliko mpaka
imalizike, ndipo mjadala urudie kwenye hoja ya msingi.
(10) Kila Mjumbe atasema akiwa amesimama na atatoa maelezo yake
kwa kutumia vyombo vilivyowekwa kwa madhumuni ya kutafsiri, kukuza na
kurekodi sauti:
Isipokuwa, kwa ruhusa ya Mwenyekiti, Mjumbe yeyote aliye na
ulemavu au ugonjwa anaweza kuzungumza akiwa ameketi.
(11) Endapo Mwenyekiti atasimama wakati Mjumbe yoyote anatoa
hotuba ndani ya Bunge Maalum, au atakuwa amesimama mahali pake
akisubiri kuanza kuzungumza, Mjumbe huyo ataketi mahali pake na Bunge
Maalum litabaki kimya ili Mwenyekiti aweze kutoa maelekezo au taarifa
yake.
(12) Mjumbe hataruhusiwa kuzungumzia hoja iliyokuwa likijadiliwa
baada ya Mwenyekiti kuwahoji Wajumbe na hoja hiyo kutolewa uamuzi.
Mambo
yasiyoru-
husiwa
Bungeni

38.(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi yanayolinda
na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge Maalum,
Mjumbe haruhusiwi:-
(a) kusema uongo ndani ya Bunge Maalum;
(b) kutoa ndani ya Bunge Maalum taarifa zisizokuwa na ukweli;
(c) kuzungumzia jambo lolote ambalo halipo kwenye mjadala;
(d) kuzungumzia jambo lolote ambalo limekwisha kutolewa uamuzi;
(e) kutumia jina la Rais kwa dhihaka au kwa madhumuni ya kutaka
kushawishi Bunge Maalum kuamua jambo lolote kwa namna fulani;
(f) kuzungumzia mwenendo wa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti;
isipokuwa tu kama imetolewa hoja mahsusi ya kumwondoa
Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti madarakani;
(g) kumsema vibaya au kutoa lugha ya matusi kwa Mwenyekiti, au
Makamu Mwenyekiti, au Mjumbe au kwa mtu mwingine yeyote;
(h) kutumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha watu wengine;
(i) kutoa kauli za dhihaka au zinazoshutumu mwenendo wa Mwenyekiti
au Makamu Mwenyekiti au Mjumbe au mtu mwingine yeyote;
(j) kufanya jambo lolote ambalo linaathiri heshima ya Bunge Maalum au
mwenendo bora wa Shughuli za Bunge;
19
(k) kufanya jambo lolote ambalo linakiuka masharti ya Sheria na Kanuni
hizi.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (1), ni marufuku kwa Mjumbe
kusema uongo ndani ya Bunge Maalum, na Mjumbe yeyote anapokuwa
anasema Bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au
maelezo ya ukweli kuhusu jambo analolizungumzia.
(3) Mjumbe yeyote anapokuwa akisema ndani ya Bunge Maalum
hatachukuliwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya andiko la
kitabu au utafiti kuhusu jambo fulani au habari kuhusu jambo hilo
iliyotangazwa au iliyoandikwa na vyombo vya habari.
(4) Mjumbe mwingine yeyote anaweza kusimama mahali pake na
kutamka "kuhusu utaratibu" na baada ya kuruhusiwa na Mwenyekiti kudai
kwamba, Mjumbe aliyekuwa anasema kabla yake ametoa maelezo ya uongo
kuhusu jambo au suala alilokuwa analisema Bungeni.
(5) Mjumbe anayetoa madai kwa mujibu wa fasili ya (4) ya Kanuni hii
atakuwa na wajibu wa kutoa na kuthibitisha ukweli kuhusu jambo au suala
hilo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge Maalum.
(6) Bila ya kuathiri masharti ya fasili zilizotangulia za Kanuni hii,
Mwenyekiti au Mjumbe yeyote, baada ya kutoa maelezo mafupi ya ushahidi
unaotilia mashaka ya dhahiri kuhusu ukweli wa kauli au usemi au maelezo
kuhusu jambo au suala ambalo Mjumbe amelisema ndani ya Bunge Maalum,
anaweza kumdai Mjumbe huyo atoe uthibitisho wa ukweli wa kauli au
maelezo yake na kama atashindwa kufanya hivyo, afute kauli au usemi au
maelezo yake hayo.
(7) Mjumbe aliyetakiwa kuthibitisha ukweli wa kauli au maelezo yake
aliyoyatoa katika Bunge Maalum, atawajibika kutoa uthibitisho huo kwa
kiwango cha kuliridhisha Bunge Maalum, papo hapo au katika muda
atakaopewa na Mwenyekiti kwa ajili ya kufanya hivyo.
(8) Endapo Mjumbe aliyetakiwa kuthibitisha kauli au maelezo yake
aliyoyatoa katika Bunge Maalum atashindwa kufanya hivyo, anaweza
kujirekebisha kwa kufuta kauli au maelezo yake papo hapo au katika muda
atakaokuwa amepewa na Mwenyekiti kwa ajili ya kuthibitisha kauli au usemi
au maelezo yake.
(9) Endapo hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, Mjumbe
aliyetakiwa kutoa uthibitisho wa ukweli wa kauli au maelezo yake aliyoyatoa
Bungeni atakataa au atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha
kuliridhisha Bunge Maalum na kama atakataa kujirekebisha kwa kufuta kauli
au maelezo yake, basi Mwenyekiti atamwadhibu kwa kumsimamisha
Mjumbe huyo asihudhurie vikao vya Bunge Maalum visivyozidi vitatu.
20
Muda wa
kusema
ndani ya
Bunge
Maalum

39. Isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo kwenye Kanuni hizi au
Mwenyekiti ameelekeza vinginevyo:-
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
atakapokuwa anawasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge
Maalum atasema kwa muda ambao Mwenyekiti wa Bunge
Maalum ataona unafaa kwa ajili hiyo;
(b) Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Maalum anayewasilisha
hoja na maoni ya Kamati atawasilisha kwa muda usiozidi
dakika thelathini.
(c)
Kusema
zaidi ya
mara moja
(a) kila Mjumbe anayejadili hoja, ataruhusiwa kusema kwa
muda usiozidi dakika kumi.

40.(1) Isipokuwa tu kwa idhini ya Mwenyekiti, Mjumbe yeyote
hataruhusiwa kusema zaidi ya mara moja kuhusu hoja, ila tu kama:-
(a) anatumia haki yake ya kujibu;
(b) anasema kuhusu utaratibu; au
(c) anasema kuomba kupata ufafanuzi wa jambo mahsusi linalohusu
hoja inayojadiliwa ndani ya Bunge Maalum.
(2) Mjumbe ambaye amezungumza kuhusu hoja anaweza kuzungumza
tena kuhusu hoja ya kufanya mabadiliko katika hoja aliyoisemea.
(3) Wakati wa kujibu, mtoa hoja atapaswa kujibu mambo yale tu
yaliyozungumzwa na Wajumbe waliochangia hoja yake na hataruhusiwa
kutoa maelezo yoyote mapya, isipokuwa kama maelezo hayo ni ya lazima
kwa madhumuni ya kufafanua jambo lililochangiwa na Wajumbe.
(4) Mjumbe yeyote hataruhusiwa kusema ndani ya Bunge Maalum
kuhusu jambo baada ya Mwenyekiti kuwahoji Wajumbe na kura ya uamuzi
ya aina yoyote kupigwa kuhusu jambo hilo.
Staha
ndani ya
Bunge

41.(1) Wakati wa Vikao vya Bunge Maalum, Mwenyekiti anapokuwa
anaingia au kutoka katika Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum,
Wajumbe na wageni wote waliopo kwenye Ukumbi huo watasimama kwa
utulivu mahali pao na kubaki kimya hadi Mwenyekiti atakapokuwa ameketi
katika Kiti chake au atakapokuwa ametoka kwenye Ukumbi wa Mikutano ya
Bunge Maalum.
(2) Mjumbe aliyepo Bungeni wakati wa mjadala atatakiwa:
21
(a) kuingia au kutoka kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bunge
Maalum kwa staha na atainamisha kichwa kuelekeza kwa
Mwenyekiti kwa heshima kila mara Mjumbe huyo atakapokuwa
akienda au kutoka mahali pake;
(b) kutulia na kukaa kwa heshima mahali pake, na hatatangatanga
kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum;
(c) kutopita kati ya kiti cha Mwenyekiti wa Bunge Maalum na
Mjumbe anayesema;
(d) kutosoma kitabu chochote, gazeti au barua, isipokuwa nyaraka
zinazohusu shughuli za mjadala unaoendelea wakati huo.
(3) Mtumishi wa Bunge Maalum na mgeni yeyote aliyepo kwenye
Ukumbi wa Mikutano ya Bunge na kwenye baraza za Ukumbi huo wakati wa
mjadala atatakiwa:
(a) (b) kutulia na kukaa kwa heshima mahali pake, na hatatangatanga
kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum;
(c)
Mamlaka ya
Mwenyekiti
kukatiza
majadiliano
kuingia au kutoka kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bunge
Maalum kwa staha na atainamisha kichwa kuelekeza kwa
Mwenyekiti kwa heshima, kila mara anapotoka au anapokwenda
kukaa mahali pake;
kutosoma kitabu chochote, gazeti au barua, isipokuwa nyaraka
zinazohusu shughuli za mjadala wa Bunge Maalum unaoendelea
wakati huo.

42.(1) Mwenyekiti anaweza kulihutubia Bunge Maalum wakati wowote
na kwa ajili hiyo, anaweza kumkatiza Mjumbe yeyote anayezungumza.
(2) Endapo Mwenyekiti atasimama wakati wa mjadala, na kuanza
kuzungumza, Mjumbe yeyote ambaye atakuwa anazungumza wakati huo au
ambaye atakuwa amesimama mahali pake akisubiri kuanza kuzungumza,
ataketi mahali pake, na Bunge Maalum litabaki kimya ili Mwenyekiti aweze
kutoa maelekezo au taarifa yake.
Haki ya
kuomba na
kupata
ufafanuzi

43.(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, Mjumbe
yeyote atakuwa na haki ya kuomba na kupata ufafanuzi wa jambo lolote
mahsusi linalohusu hoja inayojadiliwa ndani ya Bunge Maalum.
(2) Katika kutumia haki ya kuomba na kupata ufafanuzi kwa mujibu wa
masharti ya fasili ya (1), Mjumbe analazimika kufuata utaratibu wa jinsi ya
kupata nafasi ya kuitumia haki hiyo uliowekwa na Kanuni hizi, na muda wa
kusema utakuwa ni dakika mbili.
22
(3) Haki ya Mjumbe kuomba na kupata ufafanuzi kwa mujibu wa
masharti ya Kanuni hii itapewa kipaumbele cha kwanza dhidi ya haki ya
Mjumbe ya kusema Bungeni.
(4) Mjumbe yeyote anayekusudia kuomba na kupata ufafanuzi kwa
mujibu wa Kanuni hii, atasimama mahala pake na kusema "kuhusu
ufafanuzi", akielekeza maneno hayo kwa Mwenyekiti.
(5) Baada ya kuitwa na Mwenyekiti kwa jina na kuruhusiwa kusema,
Mjumbe aliyesimama kwa ajili ya kuomba na kupata ufafanuzi ataeleza kwa
kifupi jambo hilo mahsusi analoliombea ufafanuzi, na wakati wa kusema
ataelekeza maneno yake kwa Mwenyekiti.
(6) Baada ya kuhitimisha maelezo yake, Mjumbe mhusika ataketi
mahali pake, na kama kuna Mjumbe mwingine aliyesimama kwa ajili ya
kuomba na kupata ufafanuzi wa jambo lingine, Mwenyekiti atamwita jina na
kumruhusu kusema; na kama hakuna Mjumbe mwingine, Mwenyekiti atatoa
ufafanuzi ulioombwa na Mjumbe kabla ya kuruhusu mjadala wa hoja
kuendelea
(7) Endapo Wajumbe wawili au zaidi watasimama wakati mmoja
kuhusu jambo la ufafanuzi, Mwenyekiti atamwita Mjumbe atakayekuwa
amemwona kwanza, na atafuatiwa na yule mwingine; na iwapo idadi ya
Wajumbe waliosimama itakuwa ni zaidi ya wawili, basi Mwenyekiti atawaita
kwa mpangilio atakaouona unafaa.
(8) Bila ya kuathiri masharti yaliyotangulia ya Kanuni hii, jambo lolote
la ufafanuzi litashughulikiwa kwanza na Mwenyekiti kabla ya kuruhusu
mjadala wa hoja inayohusiana na jambo linaloombewa ufafanuzi kuendelea.
Taarifa
kuhusu
utaratibu na
Mwongozo
wa
Mwenyekiti

44.(1) Mjumbe yeyote atakuwa na haki ya kuhoji kuhusu jambo lolote
la utaratibu katika Bunge.
(2) Mjumbe anayetaka kuhoji kuhusu jambo la utaratibu anaweza
kusimama wakati wowote na kusema maneno "kuhusu utaratibu", ambapo
Mjumbe yeyote ambaye wakati huo atakuwa anasema atanyamaza na kukaa
chini na Mwenyekiti atamtaka Mjumbe aliyedai utaratibu ataje Kanuni au
sehemu ya Kanuni iliyokiukwa.
(3) Mjumbe aliyedai utaratibu atalazimika kutaja Kanuni au sehemu ya
Kanuni ya Bunge iliyokiukwa na muda wa kusema hautazidi dakika moja.
(4) Baada ya kutaja Kanuni au sehemu ya Kanuni iliyokiukwa, Mjumbe
aliyesimama kuhusu utaratibu, ataketi mahali pake kusubiri uamuzi wa
Mwenyekiti kuhusu suala hilo la utaratibu.
(5) Mwenyekiti anaweza, ama papo hapo kutoa uamuzi wake kuhusu
jambo la utaratibu lililotajwa au kuahirisha uamuzi ili alifikirie zaidi jambo
23
hilo na kutoa uamuzi baadaye au kutoa uamuzi, baadaye kutoa sababu za
uamuzi huo, vyovyote atakavyoona inafaa.
(6) Katika kufikia uamuzi, Mwenyekiti anaweza kuitaka Kamati ya
Kanuni na Haki za Bunge Maalum au Kamati nyingine yoyote ya Bunge
Maalum impe ushauri kuhusu jambo husika.
(7) Mjumbe aliyekuwa anazungumza wakati jambo la utaratibu
lilipohojiwa anaweza kuendelea na hotuba yake baada ya Mwenyekiti kutoa
uamuzi juu ya jambo hilo au baada ya kuahirisha uamuzi juu ya jambo hilo.
(8) Hali kadhalika, Mjumbe anaweza kusimama wakati wowote
ambapo hakuna Mjumbe mwingine anayesema na kuomba "Mwongozo wa
Mwenyekiti" kuhusu jambo ambalo limetokea Bungeni mapema, ili
Mwenyekiti atoe ufafanuzi kama jambo hili linaruhusiwa au haliruhusiwi
kwa mujibu wa Kanuni na taratibu za Bunge Maalum na majibu ya
Mwenyekiti yatatolewa papo hapo au baadaye, kadri atakavyoona inafaa.
(9) Uamuzi wa Mwenyekiti kuhusu suala lolote la utaratibu katika
Bunge Maalum utakuwa ni wa mwisho.
Hoja ya
kuahirisha au
kusitisha
mjadala

45.(1) Mjumbe yeyote anaweza kutoa hoja kwamba mjadala
unaoendelea Bungeni uahirishwe au usitishwe hadi wakati wa baadae.
(2) Mjumbe anayependa mjadala unaoendelea kuhusu hoja yoyote
uahirishwe hadi wakati wa baadaye, anaweza kutoa hoja "Kwamba mjadala
sasa uahirishwe" na atataja mjadala huo uahirishwe hadi wakati gani, na pia
atalazimika kutoa sababu kwa nini anataka mjadala uahirishwe.
(3) Kama Mwenyekiti atakuwa na maoni kwamba kuwasilishwa kwa
hoja hiyo ni kinyume cha uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge, atakataa
kuitoa ili iamuliwe; vinginevyo, papo hapo atawahoji Wajumbe kuhusu hoja
hiyo kadri atakavyoona inafaa.
(4) Endapo hoja iliyowasilishwa haitapata kibali cha Bunge, mjadala
kuhusu hoja iliyoko mbele ya Bunge utaendelea.
(5) Mjumbe yeyote hataruhusiwa kutoa hoja ya kufanya mabadiliko
katika hoja iliyotolewa kwa mujibu wa Kanuni hii.
Hoja ya
kufunga
mjadala

46.(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya Kanuni hii, Mjumbe yeyote
anaweza kutoa hoja ya kufunga mjadala.
(2) Utaratibu utakaotumika ni kutoa hoja ya kufunga mjadala wakati
ambapo bado kuna Wajumbe wanaopenda kuzungumza juu ya jambo lililoko
katika mjadala, lakini muda uliotengwa umekwisha, au pale ambapo Bunge
limewekewa kiwango cha juu cha muda wa kujadili hoja inayohusika na
muda huo bado haujaisha.
24
(3) Hoja ya kufunga mjadala inaweza kutolewa baada ya hotuba yoyote
kukamilika au ikiwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum ataruhusu hoja ya
kufanya mjadala mara tu au muda mfupi baada ya hoja hiyo kutolewa ili
iamuliwe.
(4) Mjumbe anayetoa hoja ya kufunga mjadala, anaweza kusimama
mahali pake na kutoa hoja "Kwamba mjadala unaondelea sasa ufungwe".
(5) Endapo Mwenyekiti ataona kuwa hoja ya kufunga mjadala inakiuka
mwenendo bora wa Shughuli za Bunge Maalum au inavunja haki za
Wajumbe wa Bunge Maalum, basi ataikataa.
(6) Iwapo hoja "Kwamba mjadala unaoendelea ufungwe" itakubaliwa,
basi Mwenyekiti atawahoji Wajumbe ili kuamua hoja hiyo.
Vikao vya
faragha vya
Bunge
Maalum

47.(1) Kwa kuzingatia hali na mazingira ya mjadala unavyoendelea
ndani ya Bunge Maalum, Mwenyekiti wa Bunge Maalum anaweza kuamua
mjadala husika uendeshwe katika kikao cha faragha cha Bunge Maalum.
(2) Hakuna mtu yeyote asiyekuwa Mjumbe au mtumishi wa Bunge
Maalum atakayeruhusiwa kuwepo katika sehemu yoyote ya Ukumbi wa
Mikutano ya Bunge Maalum wakati kikao cha faragha cha Bunge Maalum
kikiendelea, isipokuwa watu maalum watakaokuwa wameruhusiwa na
Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
(3) Utaratibu utakaotumika katika kuendesha mjadala kwenye kikao
cha faragha cha Bunge Maalum utaamuliwa na Mwenyekiti wa Bunge
Maalum.
(4) Mwenyekiti wa Bunge Maalum anaweza kutoa taarifa fupi kwa
wananchi kupitia vyombo vya habari, kuhusu majadiliano na uamuzi
uliofanywa na Bunge Maalum katika kikao chake cha faragha, kama
atakavyoona inafaa.
(5) Endapo Bunge Maalum litaona kwamba inafaa taarifa za mwenendo
wa majadiliano katika kikao cha faragha zitolewe hadharani, Mwenyekiti wa
Bunge Maalum ataagiza taarifa hizo zichapishwe katika taarifa rasmi za
Bunge Maalum.


SEHEMU YA SITA
KAMATI ZA BUNGE MAALUM
Kamati za Bunge Maalum
48.(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, Bunge
linaweza kuunda Kamati za Bunge Maalum za namna mbalimbali, kwa kadri
litakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa kazi na mamlaka yake.
25
(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (1), kutakuwa na Kamati za
Bunge Maalum zifuatazo:-
(a) Kamati ya Shughuli za Bunge Maalum;
(b) Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum;
(c) Kamati ya Uandishi;
(d) Kamati Namba Moja;
(e) Kamati Namba Mbili;;
(f) Kamati Namba Tatu;
(g) Kamati Namba Nne;
(h) Kamati Namba Tano;
(i) Kamati Namba Sita;
(j) Kamati Namba Saba;
(k) Kamati Namba Nane;
(l) Kamati Namba Tisa;
(m) Kamati Namba Kumi;
(n) Kamati Namba Kumi na Moja;
(o) Kamati Namba Kumi na Mbili;
(p) Kamati Namba Kumi na Tatu;
(q) Kamati Namba Kumi na Nne;
(r) Kamati Namba Kumi na Tano;
(s) Kamati Namba Kumi na Sita;
(t) Kamati Namba Kumi na Saba.
(3) Majukumu ya Kamati za Bunge Maalum zilizoundwa kwa mujibu
wa masharti ya fasili ya (2) yatakuwa kama yalivyoainishwa katika Kanuni
hizi.
Muundo wa
Kamati za
Bunge
Maalum

49.(1) Kamati za Bunge Maalum zitaundwa na Mwenyekiti wa Bunge
Maalum kwa namna ambayo itawezesha kila Mjumbe wa Bunge Maalum
kuteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati mojawapo.
(2) Wakati wa kufanya uteuzi wa mjumbe kuwa Mjumbe wa Kamati
yoyote ya Bunge Maalum, Mwenyekiti wa Bunge Maalum atazingatia
yafuatayo:
26
(a) kwa kadri inavyowezekana, idadi ya wajumbe inalingana kwa kila
Kamati.
(b) uteuzi wa wajumbe katika kila Kamati utazingatia-
(i) uwiano wa Wajumbe wa Bunge Maalum kutoka pande zote za
Muungano; na
(ii) idadi ya kila aina ya Wajumbe wa Bunge Maalum ilivyo katika
Bunge Maalum.
(3) Katibu wa Bunge Maalum tahakikisha kuwa Wajumbe wote wa
Bunge Maalum wanapewa orodha inayoonesha jinsi walivyopangwa katika
Kamati mbalimbali.
(4) Ujumbe katika Kamati za Bunge Maalum utadumu kwa kipindi
chote cha uhai wa Bunge Maalum.
(5) Bila ya kuathiri masharti mengine ya Kanuni hizi, wajumbe wa kila
Kamati ya Bunge Maalum watamchagua Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti wa Kamati kutoka miongoni mwao, ambao kwa muda wote
watakaokuwa Wajumbe, wataendelea kushika nafasi hizo kwa kipindi chote
cha uhai wa Bunge Maalum.
(6) Kutakuwa na Sekretarieti ya kila Kamati ya Bunge Maalum
itakayoundwa na watumishi kutoka katika Sekretarieti ya Bunge Maalum.
(7) Sekretarieti ya kila Kamati ya Bunge Maalum itakuwa na Wataalam
wa masuala ya kibunge, Sheria, uandishi wa Sheria, utafiti na fani zingine za
utaalam kwa ajili ya kuiwezesha Kamati kutekeleza ipasavyo majukumu
yake, na itafanya kazi zake chini ya usimamizi wa Katibu wa Bunge
Maalum.
(8) Bila ya kuathiri masharti ya fasili zilizotangulia za Kanuni hii,
Katibu wa Bunge Maalum atateua mtumishi yeyote wa Sekretarieti ya Bunge
Maalum kuwa Katibu wa Kamati ya Bunge Maalum, kwa ajili ya kutekeleza
majukumu yafuatayo:-
(a) kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Kamati; na
(b) kuratibu shughuli za Kamati.
(9) Kwa ajili ya kutekeleza wajibu wake wa usimamizi kwa mujibu wa
fasili ya (7), Katibu wa Bunge Maalum atakuwa na haki ya kuingia katika
kikao chochote cha Kamati au Kamati Ndogo yoyote ya Kamati ya Bunge
Maalum na kutoa maelekezo au ushauri kwa Katibu wa Kamati au mtumishi
yeyote wa Sekretarieti ya Kamati husika ya Bunge Maalum kuhusu utaratibu
unaotakiwa kufuatwa katika uendeshaji wa kikao kinachohusika cha Kamati.
27
Utaratibu wa
mikutano,
vikao na
akidi katika
Kamati za
Bunge

50.(1) Masharti ya Kanuni hii yanayoweka utaratibu wa kuendesha
Mikutano, vikao na shughuli za Kamati yatatumika kwa Kamati zote za
Bunge Maalum.
(2) Mwenyekiti wa Kamati ataongoza vikao vyote vya Kamati ya
Bunge Maalum na endapo hayupo kwenye kikao, Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ataongoza shughuli za kikao hicho, na ikiwa Mwenyekiti na Makamu
wote hawapo, wajumbe waliohudhuria watamchagua mmojawapo miongoni
mwao kuongoza kikao hicho.
(3) Kamati ya Bunge Maalum itakutana kila itakapoagizwa kukutana na
Mwenyekiti wa Bunge Maalum au Mwenyekiti wa Kamati baada ya kupata
idhini ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
(4) Vikao vya kawaida vya Kamati za Bunge Maalum vitafanyika
katika maeneo ya Bunge au katika maeneo mengine yaliyo nje ya maeneo ya
Bunge Maalum yaliyoandaliwa kwa ajili hiyo.
(5) Kila Kamati ya Bunge Maalum itafanya vikao vyake kwa
kuzingatia ratiba ya Shughuli za Bunge Maalum iliyowekwa kwa mujibu wa
Kanuni hizi.
(6) Akidi ya vikao vyote vya Kamati ya Bunge Maalum itakuwa nusu
ya wajumbe wote wa Kamati.
(7) Mambo yote yatakayojadiliwa na Kamati ya Bunge Maalum
yataamuliwa kwa theluthi mbili ya wajumbe wa Kamati waliohudhuria na
kupiga kura.
(8) Bila ya kuathiri masharti yaliyotangulia ya Kanuni hii, kila Kamati
ya Bunge Maalum itajiwekea utaratibu wake, na inaweza kuwaruhusu
Wajumbe ambao si wajumbe wa Kamati au watu ambao si wajumbe
kuhudhuria na kushiriki katika shughuli za Kamati, lakini hawatakuwa na
haki ya kupiga kura.
(9) Shughuli za kawaida za Kamati ya Bunge Maalum zitaendeshwa
kwa uwazi ambapo Kamati kama itaona inafaa, inaweza kumwalika mtaalam
yeyote ili kupata maoni na ushauri kwa ajili ya kuboresha jambo ambalo
litakuwa linajadiliwa na Kamati hiyo.
(10) Mtu yeyote atakayealikwa kutoa maoni na ushauri wa jambo lolote
kwenye Kamati ya Bunge Maalum kwa mujibu wa fasili ya (9)-
(a) atastahili haki na kinga zilizowekwa na Sheria na Kanuni hizi
kuhusiana na maoni na ushauri atakaoutoa kwenye Kamati ya Bunge
Maalum;
28
(b) atavaa vazi la heshima na pia atapaswa kuwa na nidhamu na kutii
maelekezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Maalum.
(11) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (9) ya Kanuni hii, shughuli zote
za Kamati ya Bunge Maalum zinazohusu kuandaa na kutoa mapendekezo ya
kuwasilishwa katika Bunge Maalum zitafanywa kwa faragha.
(12) Mwenyekiti wa Kamati yoyote ya Bunge Maalum atakuwa na
mamlaka ya kuhakikisha kuwepo kwa amani na usalama, na pia nidhamu
inayohitajika kwa ajili ya uendeshaji bora wa kazi na shughuli za Kamati; na
kwa ajili hiyo, Mwenyekiti huyo anaweza kuchukua hatua za kinidhamu
atakazoona zinafaa dhidi ya mjumbe yeyote wa Kamati atakayevuruga au
atakayejaribu kuvuruga mwenendo bora wa kazi na shughuli za Kamati.
Vikao vya
faragha vya
Kamati za
Bunge
Maalum

51.(1) Kwa kuzingatia hali na mazingira ya mjadala unavyoendelea
katika kikao cha Kamati, Mwenyekiti wa Kamati yoyote ya Bunge Maalum
anaweza kuamua mjadala husika uendeshwe katika kikao cha faragha cha
Kamati.
(2) Hakuna mtu yeyote asiyekuwa mjumbe wa Kamati au mtumishi wa
Sekretareti ya Kamati atakayeruhusiwa kukaa katika sehemu yoyote ya
Ukumbi wa mikutano ya Kamati wakati kikao cha faragha cha Kamati
kinaendelea, isipokuwa watu maalum watakaokuwa wameruhusiwa na
Mwenyekiti wa Kamati.
(3) Utaratibu utakaotumika katika kuendesha mjadala kwenye kikao
cha faragha cha Kamati ya Bunge Maalum utaamuliwa na Mwenyekiti wa
Kamati.
Muundo na
majukumu
ya Kamati ya
shughuli za
Bunge
Maalum

52.(1) Kutakuwa na Kamati ya Shughuli za Bunge Maalum ambayo
itakuwa na Wajumbe wafuatao:-
(a) Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambaye atakuwa Mwenyekiti wa
Kamati;
(b) Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambaye atakuwa Makamu
Mwenyekiti wa Kamati;
(c) Wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum; na
(d) Katibu atakuwa Katibu wa Kamati.
(2) Majukumu ya Kamati ya Shughuli za Bunge Maalum yatakuwa
kama ifuatavyo:
(a) kujadili na kuamua kuhusu mambo yote yanayohusu uendeshaji
bora wa Shughuli za Bunge Maalum na Kamati zake;
29
(b) kujadili na kupanga ratiba ya utekelezaji wa Shughuli za Bunge
Maalum; na
(c) kujadili na kufanya uamuzi kuhusu masuala yatakayohitaji
usuluhishi na maridhiano.
Majukumu
ya Kamati
ya Kanuni
na
Haki za
Bunge
Maalum

53.kuwa na Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum
itakayotekeleza majukumu yafuatayo:-
(a) kujadili mapendekezo ya kuzifanyia marekebisho au mabadiliko
Kanuni za Bunge Maalum yaliyopelekwa kwenye Kamati hiyo na
Mwenyekiti wa Bunge Maalum, na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti
wa Bunge Maalum;
(b) kujadili na kutoa taarifa ya ufafanuzi, mwongozo au utaratibu
kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum kuhusu jambo lolote la
kikanuni litakalopelekwa kwenye Kamati hiyo na Mwenyekiti wa
Bunge Maalum;
(c) kuchunguza kuhusu masuala yote ya haki, kinga na madaraka ya
Bunge Maalum yatakayopelekwa kwenye Kamati hiyo na
Mwenyekiti wa Bunge Maalum, na kutoa mapendekezo na ushauri
kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum kuhusu hatua zinazofaa
kuchukuliwa;
(d) kujadili na kumshauri Mwenyekiti wa Bunge Maalum kuhusu
utekelezaji bora wa haki, kinga na madaraka ya Bunge Maalum; na
(e) kushughulikia suala lolote linalohusiana na nidhamu ya Mjumbe
yeyote wa Bunge Maalum lililopelekwa kwenye Kamati hiyo na
Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
(2) Bila ya kujali masharti ya Kanuni hii, wajumbe wa Kamati hii
wanaweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Kamati nyingine zilizoundwa kwa
mujibu wa Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati ya
Uandishi


54.(1) Kutaku
wa na Kamati ya Uandishi itakayotekeleza majukumu
yafuatayo:-
(a) kuandaa Rasimu ya Katiba, kama ilivyopitishwa na Bunge
Maalum kutokana na uamuzi wa Bunge Maalum kuhusu taarifa za
Kamati Namba Moja hadi Namba Kumi na Saba za Bunge
Maalum; na
(c) kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, Rasimu ya Katiba iliyotajwa
katika aya ya (a) ili ipigiwe kura ya mwisho na kupitishwa na
Bunge Maalum kwa ujumla wake.
30
Majukumu
ya Kamati
Kamati
Namba
Moja
55. Majukumu ya Kamati Namba Moja yatakuwa ni:-
(a)
kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b)
Majukumu
ya Kamati
Namba
Mbili
kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Kwanza ya Rasimu
ya Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni
hizi.
56. Majukumu ya Kamati Namba Mbili yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura ya Pili ya Rasimu
ya Katiba na kutoa taarifa kwenye Bunge Maalum kwa
mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Tatu
57. Majukumu ya Kamati Namba Tatu yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura ya Tatu ya Rasimu
ya Katiba na kutoa Taarifa Bungeni kwa mujibu wa masharti
yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba Nne

58. majukumu ya Kamati Namba Nne yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura ya Nne ya Rasimu
ya Katiba na kutoa Taarifa Bungeni kwa mujibu wa masharti
yaliyowekwa na Kanuni hizi.
31
Majukumu
ya Kamati
Namba Tano

59. Majukumu ya Kamati Namba Tano yatakuwa ni:
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura ya Tano ya
Rasimu ya Katiba na kutoa Taarifa Bungeni kwa mujibu wa
masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba Sita

60. Majukumu ya Kamati Namba Sita yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura ya Sita ya Rasimu
ya Katiba na kutoa Taarifa Bungeni kwa mujibu wa masharti
yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Saba
Majukumu
ya Kamati
Namba
Nane

61. Majukumu ya Kamati Namba Saba yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura ya Saba ya Rasimu
ya Katiba na kutoa Taarifa Bungeni kwa mujibu wa masharti
yaliyowekwa na Kanuni hizi.

62. Majukumu ya Kamati Namba Nane yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura ya Nane ya
Rasimu ya Katiba na kutoa Taarifa Bungeni kwa mujibu wa
32
masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba Tisa

63. Majukumu ya Kamati Namba Tisa yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Tisa ya Rasimu ya
Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Kumi

64. Majukumu ya Kamati Namba Kumi yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Kumi ya Rasimu ya
Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Kumi na
Moja

65. Majukumu ya Kamati Namba Kumi na Moja yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura zote za Rasimu
kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Kumi na Moja ya
Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na
Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Kumi na
Mbili

66. Majukumu ya Kamati Namba Kumi na Mbili yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine
ya Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya
kuzingatiwa;
33
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Kumi na Mbili ya
Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na
Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Kumi na
Tatu

67. Majukumu ya Kamati Namba Kumi na Tatu yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine ya
Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye Kamati
ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya kuzingatiwa;
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Kumi na Tatu ya
Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na
Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Kumi na
Nne

68. Majukumu ya Kamati Namba Kumi na Nne yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine ya
Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye Kamati
ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya kuzingatiwa;
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Kumi na Nne ya
Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na
Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Kumi na
Tano

69. Majukumu ya Kamati Namba Kumi na Tano yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine ya
Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye Kamati
ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya kuzingatiwa;
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Kumi na Tano ya
Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na
Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Kumi na
Sita

70. Majukumu ya Kamati Namba Kumi na Sita yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine ya
Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye Kamati
ya Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya kuzingatiwa;
34
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa
kuhusu mambo yaliyomo katika Sura ya Kumi na Tatu ya
Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na
Kanuni hizi.
Majukumu
ya Kamati
Namba
Kumi na
Saba

71. Majukumu ya Kamati Namba Kumi na Saba yatakuwa ni:-
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika Sura zote za Rasimu na
kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu ya
Katiba na endapo linahitaji kuzingatiwa na Kamati nyingine ya
Bunge Maalum, basi italiwasilisha jambo hilo kwenye Kamati ya
Bunge Maalum inayohusika kwa ajili ya kuzingatiwa;
(b) kujadili na kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, taarifa kuhusu
mambo yaliyomo katika Sura ya Kumi na Tatu ya Rasimu ya
Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Upangaji wa
ratiba ya
utekelezaji
wa kazi na
majukumu
ya Bunge
Maalum
Sura 83

72.(1) Katika kipindi cha siku saba baada ya Kanuni hizi kupitishwa, Bunge
Maalum kupitia Kamati ya Shughuli za Bunge Maalum itaandaa ratiba ya
utekelezaji wa kazi na majukumu ya Bunge Maalum na Kamati zake, kwa
kuzingatia muda uliowekwa na Sheria.
(2) Ratiba ya utekelezaji wa kazi na majukumu ya Bunge Maalum
iliyoandaliwa kwa mujibu wa fasili ya (1) ambayo itaitwa "ratiba ya
Shughuli" itatekelezwa kama sehemu ya Kanuni hizi.
(3) Endapo itatokea haja ya kuifanyia marekebisho, pendekezo la
kuifanyia marekebisho ratiba hiyo ya shughuli litajadiliwa na kufanyiwa
uamuzi na Kamati ya Shughuli ya Bunge Maalum.
Kazi za
Kamati na
utekelezaji
wake

73.(1) Kabla ya kuanza kutekeleza kazi na majukumu yake yaliyowekwa
kwa mujibu wa Kanuni hizi, kila Kamati ya Bunge Maalum itaandaa orodha
ya kazi na majukumu yanayotakiwa kutekelezwa na Kamati husika, pamoja
na ratiba kwa ajili ya utekelezaji wa kazi na majukumu hayo.
(2) Orodha ya kazi na majukumu ya kila Kamati ya Bunge Maalum
ikiambatana na ratiba ya utekelezaji wake iliyoandaliwa kwa mujibu wa
fasili ya (1), vitawasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati husika katika kikao
cha Kamati ya Shughuli ya Bunge Maalum kwa ajili ya kujadiliwa na
kuzingatiwa katika ratiba ya Shughuli za Bunge Maalum itakayowekwa na
Kamati ya Shughul ya Bunge Maalum.
Utaratibu wa
kufanya
uamuzi
katika
Kamati za
Bunge

74.(1) Maoni ya Kamati ya Bunge Maalum yatakuwa ni yale
yaliyokubaliwa na theluthi mbili ya wajumbe wa Kamati waliohudhuria na
kupiga kura, na yatawasilishwa kwenye Bunge Maalum na Mwenyekiti wa
Kamati au mjumbe mwingine wa Kamati ya Bunge Maalum.
35
(2) Mjumbe yeyote wa Kamati ya Bunge Maalum hataruhusiwa
kuzungumzia hadharani maoni ya Kamati kuhusu jambo lolote litakalokuwa
linashughulikiwa na Kamati kabla maoni hayo hayajawasilishwa rasmi
kwenye Bunge Maalum.
(3) Kamati yoyote ya Bunge Maalum inaweza kuunda Kamati Ndogo
kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli zake, kadri itakavyoona inafaa, na
kila Kamati Ndogo itapangiwa kazi zake na Kamati ya Bunge Maalum
inayohusika.
(4) Kila Kamati ya Bunge Maalum itakuwa na jukumu la kujadili
maudhui ya Rasimu ya Katiba kuhusiana na mambo yaliyo chini ya mamlaka
yake na kuandaa taarifa ya Kamati itakayowasilishwa katika Bunge Maalum
kwa ajili ya kujadiliwa.
(5) Bila ya kujali iwapo umepangwa muda maalum au la kwa ajili ya
Kamati ya Bunge Maalum kujadili maudhui ya Rasimu ya Katiba,
Mwenyekiti wa Kamati anaweza kuufupisha mjadala huo endapo ataona
unarefushwa bila sababu ya msingi wala tija yoyote.
(6) Baada ya kukamilisha kazi yake, itakuwa ni lazima kwa kila Kamati
ya Bunge Maalum kuwasilisha kwenye Bunge Maalum taarifa ya mambo
ililokuwa inayafanyia kazi, kwa madhumuni ya kujadiliwa na kupata uamuzi
wa Bunge Maalum.
(7) Taarifa ya Kamati ya Bunge Maalum itakayowasilishwa kwenye
Bunge Maalum kwa mujibu wa fasili (1), itawasilishwa kama hoja ya
Kamati.
(8) Mwenyekiti wa Bunge Maalum ataweka utaratibu wa kujadili
taarifa za Kamati za Bunge Maalum ambapo taarifa ya Kamati ya Bunge
Maalum inapowasilishwa katika Bunge Maalum, itajadiliwa kwa kufuata
mpangilio wa Shughuli za Bunge Maalum.
Wajibu wa
Mjumbe
kuhudhuria
vikao na
ukomo wa
Kamati

75.(1) Utakuwa ni wajibu wa kwanza kwa kila mjumbe wa Kamati ya
Bunge Maalum kuhudhuria vikao vya Kamati kwa wakati uliopangwa.
(2) Mjumbe yeyote ambaye hatahudhuria vikao vitatu mfululizo vya
Kamati bila sababu zozote za msingi, atapewa onyo na Mwenyekiti wa
Kamati, na endapo ataendelea mara mbili au zaidi kutohudhuria vikao vya
Kamati baada ya kupewa onyo, Mwenyekiti wa Kamati atalipeleka jina lake
kwa Mwenyekiti wa Bunge ili aliwasilishe katika Kamati ya Kanuni na Haki
za Bunge Maalum kupata ushauri wa hatua za kinidhamu zinazofaa
kuchukuliwa dhidi yake.
(3) Mjumbe ambaye jina lake litapelekwa kwenye Kamati ya Kanuni na
Haki za Bunge kwa mujibu wa fasili ya (2) anaweza kupewa adhabu au
36
kuchukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu itakayopendekezwa na Kamati
hiyo.
(4) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa fasili ya (2), mjumbe yeyote wa
Bunge Maalum mwenye udhuru, atalazimika kutoa taarifa ya maandishi kwa
Mwenyekiti wa Bunge na nakala kwa Mwenyekiti wa Kamati na Katibu wa
Bunge kuhusu kutohudhuria kwake, na taarifa hiyo itahifadhiwa na Kamati
kwa ajili ya kumbukumbu.
(5) Kamati za Bunge Maalum zilizoundwa kwa mujibu wa Kanuni hizi
zitakoma baada ya maisha ya Bunge Maalum kufikia ukomo wake.


SEHEMU YA SABA
UTARATIBU WA KUWASILISHA, KUJADILI NA KUPITISHA MASHARTI
YA RASIMU YA KATIBA
Utaratibu wa kuwasilisha Rasimu ya Katiba sura ya 83

76.(1) Rasimu ya Katiba itawasilishwa katika Bunge Maalum na
Mwenyekiti wa Tume, kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 20(3) cha
Sheria.
(2) Hakutakuwa na mjadala wowote utakaofanyika wakati wa Rasimu
ya Katiba itakapowasilishwa kwenye Bunge Maalum.
(3) Baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa kwa mujibu wa fasili ya
(1), Mwenyekiti wa Bunge Maalum ataliahirisha Bunge kwa muda atakaoona
unafaa kwa ajili ya kuwawezesha Wajumbe kupata muda wa kuisoma
Rasimu ya Katiba.
(4) Bunge Maalum litakapokutana tena baada ya kuahirishwa kwa
mujibu wa fasili ya (3), Mwenyekiti wa Bunge Maalum atatangaza majina ya
wajumbe wa kila Kamati ya Bunge Maalum, na kila Kamati itatekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
Rasimu ya
Katiba
kupelekwa
kwenye
Kamati

77.(1) Mwenyekiti atapeleka nakala za Rasimu ya Katiba katika Kamati
za Bunge Maalum, na kila Kamati ya Bunge Maalum itajadili Rasimu hiyo
kwa mujibu wa mgawanyo wa majukumu ya Kamati za Bunge Maalum
uliowekwa na Kanuni hizi.
(2) Baada ya Kamati ya Bunge Maalum kukamilisha kazi ya kujadili
Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa masharti ya fasili ya (1), Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge Maalum atamjulisha Mwenyekiti wa Bunge Maalum kwa
maandishi kwamba, Kamati imemaliza kazi ya kujadili Sura ya Rasimu ya
Katiba inayohusika nayo.
(3) Baada ya kupokea taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
Maalum kwa mujibu wa fasili ya (2), Mwenyekiti wa Bunge ataagiza taarifa
ya Kamati iwekwe kwenye Orodha ya Shughuli kwa ajili ya kuwasilishwa na
37
kujadiliwa katika Bunge Maalum kama hoja ya Kamati kwa mujibu wa ratiba
ya shughuli, ili kupata Uamuzi wa Bunge Maalum.
Uwasilishaji
wa hoja ya
Kamati

78.(1) Isipokuwa kama Kamuni hizi zimeelekeza vinginevyo, hakuna
mjadala wowote utakaoendeshwa Bungeni ila tu mjadala unaohusu shughuli
iliyoingizwa kwenye Kitabu cha Orodha ya Shughuli za Bunge na kuwekwa
kwenye Orodha ya Shughuli z akikao hicho.
(2) Hoja zote zitaingizwa kwenye Kitabu cha Shughuli za Bunge
Maalum kitakachoandaliwa na Katibu, na zitawekwa kwenye Orodha ya
Shughuli ya kikao cha Bunge Maalum kulingana na maelkezo ya
Mwenyekiti.
(3) Siku ambayo taarifa ya Kamati kuhusu Sura ya Rasimu ya Katiba
imepangwa katika Orodha ya Shughuli, Mwenyekiti wa Kamati husika ya
Bunge Maalum husika au mjumbe wa Kamati hiyo aliyeteuliwa na
Mwenyekiti wa Kamati kwa ajili hiyo, atawasilisha hoja kwamba, Taarifa ya
Kamati hiyo Isomwe na kujadiliwa Bungeni.
(4) Hoja ikishawekwa kwenye Orodha ya Shughuli itawasilishwa na
kuamuliwa Bungeni kwa utaratibu kwamba, baada ya Mwenyekiti wa
Kamati iliyopelekewa hoja hiyo kuwasilisha maoni na ushauri wa Kamati,
Mwenyekiti wa Bunge ataelekeza hoja hiyo ijadiliwe.
(5) Hoja yoyote ya Kamati itakayowasilishwa katika Bunge Maalum
kwa mujibu wa Kanuni hii itawekwa katika lugha ambayo italiwezesha
Bunge kufanya uamuzi ambao ni bayana.
(6) Mwenyekiti wa Kamati husika ya Bunge Maalum au mjumbe
mwingine wa Kamati hiyo aliyeteuliwa kwa ajili hiyo, atasoma kwa ufupi
taarifa ya Kamati kuhusu Sura ya Rasimu ya Katiba na kutoa hoja kwamba
taarifa hiyo ijadiliwe Bungeni.
(7) Hoja ya taarifa ya Kamati Kusomwa na kujadiliwa Bungeni
itakuwa kama ifuatavyo:-
"Kwamba, taarifa ya Kamati Namba........ sasa isomwe na kujadiliwa
na Bunge Maalum, naomba kutoa Hoja."
(8) Baada ya hoja ya Kamati kutolewa katika Bunge Maalum na
Mwenyekiti wa Bunge Maalum kuelekeza hoja hiyo ijadiliwe, mjadala
kuhusu taarifa ya Kamati utaanza.
(9) Mwenyekiti wa Bunge Maalum kwa kushauriana na Kamati ya
Shughuli, atapanga muda utakaotumika kujadili taarifa ya kila Kamati ya
Bunge Maalum, kwa kuzingatia muda uliowekwa na Sheria, pamoja na ratiba
ya shughuli iliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni hizi, kwa ajili ya Bunge
Maalum kutekeleza majukumu yake.
38
(10) Wakati wa mjadala huo, Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum
anaweza kushauri na kutoa mapendekezo ya marekebisho au mabadiliko kwa
ajili ya kuboresha masharti yaliyomo katika Sura ya Rasimu ya Katiba
inayohusika na taarifa ya Kamati iliyowasilishwa Bungeni.
(11) Mwenyekiti wa Bunge Maalum hataruhusu hoja yoyote
inayokiuka Sheria au masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
(12) Kila hoja itawekwa kwenye Orodha ya Shughuli ikiwa kama
ilivyowasilishwa au kama ilivyofanyiwa marekebisho au mabadiliko.
Masharti
kuhusu
mapende-
kezo ya
Kamati

79.(1) Bila kujali masharti mengine yaliyowekwa na Kanuni hizi,
Bunge Maalum halitashughulikia pendekezo lolote la Kamati ambalo
linahusu jambo ambalo lipo nje ya mamlaka ya Bunge Maalum.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (1), mapendekezo yoyote ya
marekebisho au mabadiliko hayatakubaliwa iwapo:
(a) yanapendekeza kufuta au kuondoa misingi mikuu ya kitaifa
iliyowekwa na kifungu cha 9(2) cha Sheria; au
(b) yanakiuka au kwenda kinyume na uamuzi wa Bunge Maalum
uliokwishafanyika awali.
Utaratibu wa
majadiliano
wakati wa
kujadili
taarifa ya
Kamati

80.(1) Kwa kuzingatia mamlaka ya Bunge Maalum ya kujadili na
kupitisha Rasimu ya Katiba yaliyowekwa na Sheria, msingi wa majadiliano
ya Bunge Maalum utakuwa ni mapendekezo yatakayowasilishwa na
Kamati ya Bunge Maalum inayohusika kupitia taarifa ya Kamati
itakayowasilishwa katika Bunge Maalum kama hoja ya Kamati.
(2) Mwenyekiti wa Bunge Maalum atakuwa na mamlaka ya kuamua
kama pendekezo lolote la Kamati ya Bunge Maalum au la Mjumbe yeyote
wa Bunge Maalum linakubalika au halikubaliki kwa mujibu wa masharti
yaliyowekwa na Kanuni hizi, na uamuzi wake utakuwa ni wa mwisho.
(3) Mjumbe wa Bunge Maalum baada ya kuitwa na Mwenyekiti wa
Bunge Maalum kujadili hoja, atasimama mahali pake na kutoa maelezo yake,
kuhusu hoja hiyo kwa kuyaelekeza kwa Mwenyekiti.
(4) Katika kujadili taarifa au hoja ya Kamati, kila Mjumbe wa Bunge
Maalum atakayepata nafasi ataelekeza maelezo yake kwenye hoja au jambo
mahsusi linalojadiliwa kwa wakati huo, na endapo Mjumbe yeyote ataanza
kujadili au kutoa maelezo ambayo hayahusiani na hoja au jambo mahsusi
linalojadiliwa
kwa
wakati
huo
au
anarudiarudia
maelezo
yaliyokwishatolewa na Mjumbe au Wajumbe wengine, Mwenyekiti wa
39
Bunge Maalum atamwamuru Mjumbe huyo akatishe maelezo yake na kukaa
chini.
(5) Mjumbe wa Bunge Maalum aliyeamriwa na Mwenyekiti wa Bunge
Maalum kukatisha maelezo yake na kukaa chini kwa mujibu wa fasili ya (4)
atatii amri ya Mwenyekiti bila ukaidi wowote, na iwapo atakaidi,
ataadhibiwa na Mwenyekiti papo hapo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo
ya kusimamia Kanuni hizi na pia uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge
Maalum.
(6) Endapo wakati mjadala unaendelea ndani ya Bunge Maalum na
Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum anahitaji kupata ufafanuzi wa jambo
lolote linalojadiliwa, anaweza kuomba na kupata ufafanuzi huo kutoka kwa
Mwenyekiti wa Bunge Maalum bila mjadala wowote, kwa mujibu wa
utaratibu wa kuomba ufafanuzi uliowekwa na Kanuni hizi.
(7) Wakati wa kujadili taarifa au hoja ya Kamati ya Bunge Maalum,
Mwenyekiti wa Kamati inayohusika au mjumbe mwingine wa Kamati hiyo
ndiye atakayewajibika kutoa maelezo ya ufafanuzi na kujibu hoja
mbalimbali zitakazotolewa na Wajumbe wa Bunge Maalum wakati wa
mjadala.
(8) Endapo majibu au ufafanuzi kuhusu hoja zilizojitokeza wakati wa
mjadala wa hoja ya Kamati ya Bunge Maalum hautatolewa kwa kiwango
cha kuliridhisha Bunge Maalum, Mwenyekiti wa Bunge Maalum
ataliahirisha Bunge Maalum na kuelekeza Kamati husika ijadili na kupata
majibu ya hoja zilizojitokeza, kabla ya kurejea tena kwenye Bunge Maalum
kwa ajili ya kuwasilisha tena majibu ya hoja hizo katika siku na muda kama
Mwenyekiti atakavyoelekeza.
Utaratibu wa
kupiga kura
kupitisha
mapende-
kezo ya
marekebisho

81.(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, mapendekezo
ya marekebisho au mabadiliko yaliyokidhi matakwa na masharti ya Kanuni
hizi yatajadiliwa na kupigiwa kura kwanza kabla ya Sura au Sehemu au Ibara
inayohusika ya Rasimu ya Katiba kupigiwa kura na kupitishwa.
(2) Mapendekezo ya marekebisho au mabadiliko yaliyowasilishwa kwa
mujibu wa fasili ya (1) yatajadiliwa na kupigiwa kura moja baada ya jingine,
isipokuwa kwamba, pale ambapo marekebisho au mabadiliko hayo yanahusu
jambo moja, Mwenyekiti anaweza kuelekeza yapigiwe kura kwa pamoja.
(3) Pale ambapo mapendekezo ya marekebisho au mabadiliko
yatakubaliwa, basi Sura, Sehemu au Ibara inayohusika ya Rasimu ya Katiba
itahesabiwa kuwa imepitishwa pamoja na mabadiliko yake:
Isipokuwa kwamba, pale ambapo mapendekezo ya marekebisho au
mabadiliko yatakataliwa, Sura, Sehemu au Ibara inayohusika ya Rasimu ya
Katiba itahesabiwa kuwa imepitishwa bila marekebisho au mabadiliko.
40
Utaratibu
wa kufanya
uamuzi

82.(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, utaratibu wa
Bunge Maalum kufanya uamuzi utakuwa ni kwa Mwenyekiti kulihoji Bunge
Maalum na kupata Uamuzi wa Bunge Maalum utakaotokana na wingi wa
idadi ya Wajumbe kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi:
Isipokuwa kwamba, ili Rasimu ya Katiba iweze kupitishwa katika
Bunge Maalum itahitaji kuungwa mkono kwa wingi wa theluthi mbili ya
idadi ya Wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar.
(2) Iapo jambo lolote linahitaji kuamuliwa au kutekelezwa na Bunge
Maalum, basi jambo hilo halitahesabiwa kuwa limeamuliwa au
limetekelezwa ipasavyo, ila mpaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na
Bunge Maalum kwa kuzingatia masharti na utaratibu uliowekwa na Sheria
pamoja na Kanuni hizi.
(3) Kwa madhumuni ya Kanuni hii, utaratibu utakaotumika kupata
uamuzi baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum kutoa swali la kulihoji
Bunge Maalum utakuwa ni kwa:
(a) kura ya siri, au
(b) Kura ya kielektroniki.
(4) Mwenyekiti wa Bunge Maalum anaweza kutumia mojawapo ya
utaratibu wa kura iliowekwa na masharti ya fasili ya (3) kwa kuzingatia
jambo husika lilivyo, kwa kadri atakavyoona inafaa.
(5) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (4), Mjumbe yeyote wa Bunge
Maalum anaweza kutoa hoja kupendekeza mojawapo ya utaratibu wa kura
uliowekwa na fasili ya (3) utumike, kwa kuzingaia mazingira ya jambo
husika, na pia uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge Maalum.
(6) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, wakati wa
kupata umauzi wa Bunge Maalum kuhusu kupitisha Rasimu ya Katiba,
Bunge Maalum litapiga kura ya siri, ambayo kwa madhumuni ya Kanuni hii,
itaitwa "kura ya mwisho".
(7) Hoja iliyowasilishwa na Kamati ya Bunge Maalum katika Bunge
Maalum itaamuliwa kwa kuungwa mkono kwa wingi wa idadi ya theluthi
mbili ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum kutoka Tanzania Bara na theluhi
mbili ya idadi ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum kutoka Tanzania
Zanzibar.
(8) Wakati amekalia kiti cha Mwenyekiti wa Bunge Maalum,
Mwenyekiti wa Bunge Maalum hatakuwa na kura ya kawaida bali atakuwa
na kura ya uamuzi endapo kura ya "Ndiyo" na "Siyo" zitalinga.
Kura ya
siri

83.(1) Wakati wa kupiga kura ya siri, kila Mjumbe atapiga kura ya
"Ndiyo" au "Hapana", kwa kutumia karatasi za kupigia kura zitakazokuwa
zimeandaliwa na Katibu wa Bunge Maalum kwa ajili hiyo.
41
(2) Upigaji kura utakuwa ni kwa Mjumbe baada ya kupewa karatasi ya
kupigia kura, kuweka alama ya √ kwenye moja ya kisanduku kilichopo sanjai
na maneno "Ndiyo" na "Hapana", kwa jinsi yeye binafsi anavyoona inafaa.
(3) Mjumbe ambaye kwa bahati mbaya ataharibu karatasi yake ya
kupigia kura atairudisha karatasi hiyo iliyoharibika kwa Makatibu Wasaidizi
na atapewa karatasi nyingine ya kupigia kura.
(4) Mjumbe ambaye atakuwa na mahitaji maalum au atakuwa anahitaji
usaidizi katika zoezi la kupiga kura, atapatiwa mahitaji hayo na usaidizi huo
kwa utaratibu ulioandaliwa na Sekretarieti ya Bunge Maalum kwa ajili hiyo.
(5) Baada ya kila Mjumbe aliyehudhuria kikao kupiga kura, kura hizo
zitakusanywa na kuwekwa kwenye masanduku ya kura na kupelekwa
kwenye chumba maalum kitakachokuwa kimeandaliwa kwa ajili ya
kuhesabu kura.
(6) Baada ya kura kuhesabiwa, Katibu wa Bunge Maalum atatangaza
matokeo ya kura, na matokeo hayo yataingizwa katika taarifa rasmi za Bunge
Maalum.
Kura ya
kielektroniki

84.(1)mpigaji kura kwa elektroniki utatumika pale ambapo
Mwenyekiti au Mjumbe yeyote atapendekeza, na Bunge kukubali kwamba
utumike.
(2) Pale ambapo utaratibu huo wa upigaji kura umeamuliwa utumike,
lakini kutokana na matatizo ya kiufundi utashindwa kutumika, basi upigaji
wa kura utafanyika kwa utaratibu wa kura ya siri.
(3) Endapo utaratibu wa kura ya kielektroniki utatumika, basi
kumbukumbu za matokeo ya kura hiyo zitahusu idadi ya kura za "Ndiyo" au
"Hapana", kwa tarakimu bila majina.
Utaratibu wa
kupiga kura
na kupitisha
masharti ya
Rasimu ya
Katiba

85.(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya Kanuni hizi, utaratibu
utakaotumika kwa ajili ya Bunge Maalum kutumia mamlaka yake ya kujadili
na kupitisha masharti ya Rasimu ya Katiba utakuwa kama ifuatavyo:-
(a) kujadili na kupigia kura marekebisho au mabadiliko ya kuboresha
Rasimu ya Katiba yaliyowasilishwa na Kamati za Bunge; na
(b) kujadili na kupiga kura ya mwisho kwa ajili ya kupitisha Rasimu ya
Katiba kwa ujumla wake.
(2) Endapo taarifa ya Kamati ya Bunge Maalum inayohusika
haitapendekeza marekebisho yoyote ya kuboresha Rasimu ya Katiba, basi
masharti ya Sura inayohusika ya Rasimu ya Katiba yatachukuliwa kwamba
yamepitishwa kama yalivyo bila ya marekebisho au mabadiliko yoyote.
42
(3) Kupiga kura kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hii itakuwa ni
wajibu na haki ya msingi ya kila Mjumbe wa Bunge Maalum, na kila
Mjumbe atapiga kura kwa binafsi yake:
Isipokuwa kwamba, Mjumbe ambaye anahitaji usaidizi au nyenzo
maalum kwa ajili ya kupiga kura mwenyewe, atapatiwa usaidizi au nyenzo
hiyo kwa ajili ya kumwezesha kupiga kura.
Utaratibu wa
kupitisha
Rasimu ya
Katiba

86.(1) Baada ya Bunge Maalum kukamilisha shughuli ya kujadili na
kupitisha mapendekezo ya Kamati zote za Bunge Maalum ya kuboresha
Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi,
Mwenyekiti wa Bunge Maalum ataiagiza Kamati ya Uandishi ya Bunge
Maalum kuandaa nakala ya Rasimu ya Katiba kama ilivyopitishwa na Bunge,
wakati wa kupitisha mapendekezo hayo ya Kamati za Bunge Maalum.
(2) Baada ya Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum kukamilisha kazi
yake kwa mujibu wa masharti ya fasili ya (1), Mwenyekiti wa Kamati hiyo
atamwarifu kwa maandishi Mwenyekiti wa Bunge kuhusu kukamilika kwa
kazi hiyo.
(3) Baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum kupokea taarifa
iliyowasilishwa kwa mujibu wa fasili ya (2), ataagiza Rasimu ya Katiba
iliyoandaliwa kwa mujibu wa masharti ya fasili ya (1) iwekwe kwenye
Orodha ya Shughuli kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum na
kupitishwa kwa kuzingatia masharti ya Kanuni ya 81(2).
Hoja ya
kuwasilisha
Rasimu ya
Katiba

87.(1) Hoja ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalum
kwa mujibu wa fasili hii itakayowasilishwa Bungeni na Mwenyekiti wa
Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum itakuwa katika maneno yafuatayo:-
"Kwamba, Rasimu ya Katiba, kama ilivyopitishwa Sura kwa Sura na
Bunge Maalum, sasa ijadiliwena kupitishwa kwa ujumla wake "
(2) Baada ya hoja ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa
fasili ya (1) kutolewa, Bunge litaanza mjadala wa jumla kuhusu Rasimu hiyo,
na katika hatua hii, mjadala utahusu ubora wa misingi na maudhui ya Rasimu
hiyo tu; ambapo mijadala kuhusu Sehemu, Sura au ibara za Rasimu, wala
mapendekezo ya marekebisho yoyote katika Rasimu hiyo hayatakubaliwa.
(3) Baada ya majadiliano wa jumla kwa mujibu wa fasili ya (2)
kukamilika, Rasimu ya Katiba itapitishwa na Bunge Maalum kwa mujibu wa
masharti ya Sheria pamoja na masharti ya Kanuni hizi.
(4) Baada ya kupitisha Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa fasili ya (3),
Bunge Maalum litapitisha Utangulizi na Jina la Rasimu ya Katiba.
43
Kufanya 88. Mwenyekiti anaweza kumuagiza Katibu wa Bunge Maalum
masahihisho kuifanyia masahihisho Rasimu ya Katiba iliyopitishwa na Bunge Maalum,
ya kuondoa kwa ajili ya kuondoa makosa ya uchapishaji, kabla ya saini za Wajumbe wa
makosa ya Bunge Maalum kuambatanishwa kwenye Rasimu hiyo.
uchapishaji
katika
Rasimu ya
Katiba
Ridhaa ya 89. (1) Rasimu ya Katiba kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum,
Bunge itaidhinishwa kwa kuwekwa saini na kila Mjumbe wa Bunge Maalum na
Maalum na kuthibitishwa na Katibu wa Bunge Maalum, na Mwenyekiti wa Bunge
hifadhi ya Maalum ndani ya siku saba, atawasilisha kwa Rais Katiba Inayopendekezwa.
Rasimu ya
Katiba
(2) Katibu wa Bunge Maalum atahifadhi nakala mango na tete za
Rasimu ya Katiba iliyopitishwa na Bunge Maalum kwa ajili ya
kumbukumbu.
(3) Bunge Maalum litaandaa Shughuli maalum ya kitaifa katika tarehe
na siku ambayo Mwenyekiti wa Bunge Maalum atakabidhi kwa Rais Katiba
Inayopendekezwa.


SEHEMU YA NANE
UTARATIBU WA KUTUNGA MASHARTI YA MPITO NA
MASHARTI YATOKANAYO
Utaratibu wa kutunga masharti ya mpito na masharti yatokanayo

90.(1) Mamlaka ya Bunge Maalum ya kutunga masharti ya mpito na
masharti yatokanayo yatatekelezwa kwa Bunge Maalum kujadili na kupitisha
masharti hayo kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hii.
(2) Mara baada ya Bunge Maalum kukamilisha kazi ya kujadili na
kupitisha Katiba Inayopendekezwa, Mwenyekiti wa Kamait ya Masharti ya
Mpito na masharti Yatokanayo atawasilisha hoja ya kutunga masharti ya
mpito na masharti yatokanayo kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa na
Bunge Maalum kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Kanuni ya 75 hadi 78
ya Kanuni hizi.
(3) Kwa madhumuni ya Kanuni hii, "masharti ya mpito" na "masharti
yatokanayo" maana yake ni masharti yaliyowekwa katika Sura ya Kaumi na
Saba ya Rasimu ya Katiba.
(4) Baada ya masharti ya mpito na masharti yatokanayo kujadiliwa na
kupitishwa na Bunge Maalum, Katibu wa Bunge Maalum atawasilisha
nakala ya masharti hayo, kama yalivyopitishwa na Bunge Maalum, kwa Rais
ili Rais atoe kibali chake kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 97(1) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
44
(5) Nakala halisi ya Sheria ya Masharti ya Mpito na Masharti
Yatokanayo iliyopata kibali cha Rais kwa mujibu wa fasili ya (4)
itahifadhiwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

SEHEMU YA TISA
AMANI NA UTULIVU BUNGENI
Mamlaka ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum kusimamia utaratibu

91.(1) Mwenyekiti wa Bunge Maalum atakuwa na mamlaka na wajibu
wa kuhakikisha kuwa, utaratibu bora unafuatwa katika Bunge Maalum na
uamuzi wa Mwenyekiti kuhusu jambo lolote la utaratibu utakuwa ni wa
mwisho.
(2) Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum atakayekiuka utaratibu
uliowekwa na Kanuni hizi anaweza papo hapo kutakiwa na Mwenyekiti
afuate utaratibu, na vilevile Mjumbe mwingine yeyote anaweza kusimamia
na kumfahamisha Mwenyekiti wa Bunge Maalum kuhusu ukiukwaji wa
utaratibu na katika kufanya hivyo, atalazimika kutaja Kanuni ya Bunge
Maalum iliyoweka utaratibu uliokiukwa.
Adhabu
zinazoweza
kutolewa na
Mwenyekiti
kwa
ukiukwaji
wa Kanuni

92.(1) Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum atakayekiuka Kanuni yoyote
ya Kanuni hizi au atakayezungumzia jambo au mambo ambayo hayaruhusiwi
na Kanuni hizi, anaweza kuamriwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum
ajirekebishe mara moja na kama atakaidi Mwenyekiti atamwamuru akatishe
maelezo yake na kukaa mahali pake.
(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (1), Mwenyekiti wa Bunge
Maalumanaweza kumpa onyo Mjumbe yeyote aliyefanya kosa la kukiuka
utaratibu uliowekwa na Kanuni hizi, au kosa la kuvuruga majadiliano
kwenye Bunge Maalum au uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge Maalum.
(3) Endapo Mjumbe yeyote atatumia maneno au lugha isiyotakiwa
Bungeni, yaani lugha ya matusi, usafihi, uchokozi au lugha ya maudhi, na
akitakiwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum kujirekebisha kwa kufuta
maneno au lugha hiyo akikataa kufanya hivyo, Mwenyekiti anaweza
kumwamuru Mjumbe huyo atoke mara moja nje ya Ukumbi wa mikutano ya
Bunge Maalum na abaki huko nje kwa muda wote uliosalia wa kikao cha
siku hiyo.
(4) Endapo Mjumbe yeyote aliyeamriwa na Mwenyekiti wa Bunge
Maalum kutoka nje ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum atakaidi
amri hiyo, Mwenyekiti atamwamuru Mpambe wa Bunge Maalum na askari
waliopo wamtoe Mjumbe huyo nje ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge
Maalum na kutokana na kukaidi amri ya Mwenyekiti hatahudhuria vikao
vitatu vya Bunge Maalum vinavyofuata.
45
Adhabu
zinazoweza
kutolewa na
Bunge kwa
ukiukaji wa
Kanuni

93.(1) Mwenyekiti wa Bunge Maalum anaweza kutaja jina la
Mjumbe yeyote kwamba amedharau Mamlaka ya Mwenyekiti na kupeleka
jina hilo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum ikiwa:-
(a) kwa maneno au vitendo, Mjumbe huyo anaonesha dharau kwa
mamlaka ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge
Maalum;
(b) Mjumbe huyo kwa makusudi atafanya kitendo chochote cha
kudharau Shughuli za Bunge Maalum au kuvuruga mwenendo wa
Shughuli za Bunge Maalum.
(2) Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum itajadili suala hilo, na
ikithibitika kuwa Mjumbe husika ametenda kosa, inaweza kushauri kwamba:
(a) ikiwa ni kosa lake la kwanza, Mjumbe huyo asihudhurie vikao vya
Bunge Maalum visivyozidi vitatu; au
(b) ikiwa ni kosa lake la pili au zaidi, Mjumbe huyo asihudhurie vikao
vya Bunge Maalum visivyozidi vitano.
(4) Bunge linaweza kuzingatia ushauri mwingine wowote utakaotolewa
na Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum kuhusu adhabu
anayostahili kupewa Mjumbe aliyetenda kosa kwa mujibu wa masharti ya
Kanuni hii.
(5) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (4), Bunge Maalum linaweza
kumchukulia hatua nyingine za kinidhamu Mjumbe yeyote aliyetenda kosa
chini ya Kanuni hii, kwa mujibu wa mapendekezo ya Kamati ya Kanuni na
Haki za Bunge Maalum.
(6) Adhabu yoyote itakayotolewa kwa Mjumbe aliyekiuka masharti ya
Kanuni hii itatolewa kupitia Azimio la Bunge Maalum ambalo litataja
adhabu hiyo pamoja na sababu zake.
(7) Mjumbe aliyeadhibiwa kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hii,
atatoka mara moja katika Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum, baada ya
adhabu yake kutolewa.
Mamlaka
maalum ya
Mwenyekiti
ya
kuhakikisha
amani na
utulivu
Bungeni

94. Endapo Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum atavunja au atajaribu
kuvunja utaratibu au amani na utulivu kwenye Bunge Maalum au ataonyesha
tabia za vurugu kwa kutumia nguvu na mabavu ndani ya Ukumbi wa
Mikutano ya Bunge Maalum, Mwenyekiti wa Bunge Maalum ataamuru
Mpambe wa Bunge Maalum amtoe mara moja Mjumbe huyo nje na
asihudhurie vikao vya Bunge Maalum na Kamati zake kwa muda wa siku
kumi.
46
Masharti 95. Mjumbe wa Bunge Maalum aliyesimamishwa kuhudhuria vikao
kwa Mjumbe atatoka katika Bunge na hataingia tena katika sehemu yoyote ya Ukumbi wa
aliyesimami- Mikutano ya Bunge Maalum na maeneo ya Bunge na pia hatahudhuria vikao
shwa kazi vyovyote vya Kamati za Bunge kwa muda wote atakapokuwa
amesimamishwa, na hatalipwa posho nyingine yoyote isipokuwa posho ya
kujikimu.
Mamlaka ya 96. Bila ya kujali masharti yaliyowekwa na Sehemu hii, endapo
msamaha ya Mjumbe aliyeadhibiwa ataomba radhi kwa makosa aliyoyafanya,
Mwenyekiti Mwenyekiti anaweza kumsamehe baada ya kuzingatia maoni ya Wajumbe
kupitia Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge.
Udhibiti wa 97.(1) Kwa madhumuni ya kudhibiti fujo endapo itatokea ndani ya
fujo Bungeni Ukumbi wa Bunge Maalum na iwapo Mwenyekiti wa Bunge Maalum ataona
kuwa kuna haja ya kutumia nguvu, basi anaweza kuahirisha Shughuli za
Bunge Maalum bila ya hoja yoyote kutolewa, au anaweza kusitisha kikao
kwa muda atakaoutaja, ili fujo hiyo iweze kudhibitiwa na Mpambe wa Bunge
Maalum.
(2) Baada ya utulivu kurudia, Mwenyekiti wa Bunge Maalum
atalipeleka kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum suala
ambalo lilisababisha kutokea kwa fujo ikiwa ni pamoja na jina la Mjumbe au
majina ya Wajumbe waliohusika na fujo hiyo ili Kamati hiyo iweze
kuzingatia suala hilo na kulishauri Bunge Maalum hatua za kuchukua.
Wajibu wa
Mjumbe
kutunza
amani na
utulivu
Bungeni

98.(1) Kutunza amani na utulivu ndani na nje ya Ukumbi wa Mikutano
ya Bunge Maalum utakuwa ni wajibu wa kila Mjumbe wa Bunge Maalum.
(2) Bila kujali masharti mengine yaliyowekwa na Sehemu hii, Mjumbe
yeyote wa Bunge Maalum atakayefanya kosa la kutotekeleza wajibu wake
wa kutunza amani na utulivu kwenye Bunge Maalum, anaweza kuadhibiwa
na Mwenyekiti wa Bunge Maalum au na Bunge Maalum.
SEHEMU YA KUMI
WAGENI
Ruhusa ya
wageni
Bungeni

99.(1) Wageni wanaweza kuruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi wa
Mikutano ya Bunge Maalum katika sehemu yoyote ya Ukumbi huo ambayo
itatengwa kwa ajili hiyo.
(2) Wageni wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum
watalazimika kufuata na kuzingatia masharti yafuatayo:-
(a) watakaa kimya na kwa heshima inayostahili hadi watakapotoka nje
ya Ukumbi huo;
47
(b) wanapaswa wawe wamevaa mavazi ya heshima;
(c) wataingia na kutoka Ukumbini kwa staha;
(d) wasisome kitabu chochote, gazeti, barua au hati nyingineyo ambayo
haihusiani na Orodha ya Shughuli za Bunge;
(e) wasiandike wala kurekodi jambo lolote linalozungumzwa,
isipokuwa tu kama ni wawakilishi wa vyombo vya habari;
(f) inapolazimu kuzungumza, wasizungumze kwa sauti ya juu;
(g) wasivute sigara au kiko wakati wowote wakiwa ndani ya Ukumbi
wa Mikutano ya Bunge Maalum au mahali popote nje ya Ukumbi
huo ambapo kuna sehemu ya kukaa wageni;
(h) wazime simu zao za mkononi na kutozitumia kwa namna yoyote
wakati wote;
(i) wasiingie na kamera wala kupiga picha;
(j) wasishangilie wala kuzomea wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge
Maalum; na
(k) wasifanye jambo au kitendo chochote ambacho kinaweza kuvuruga
amani na utulivu ndani ya Bunge Maalum.
(3) Mwenyekiti wa Bunge Maalum anaweza kumwamuru mgeni yeyote
atoke nje ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum endapo atavunja sharti
lolote kati ya masharti yaliyotajwa katika fasili ya (2) ya Kanuni hii.
Ruhusa kwa
Waandishi
wa Habari

100.(1) Katibu wa Bunge Maalum anaweza kutoa ruhusa maalumu au
ya jumla kwa mwakilishi wa chombo chochote cha habari kuhudhuria vikao
vya Bunge Maalum.
(2) Ruhusa yoyote itakayotolewa na Katibu wa Bunge Maalum inaweza
kuwekewa masharti yafuatayo:
(a) chombo husika kitoe maombi rasmi; na
(b) chombo husika kiteue Waandishi wenye sifa na maadili ya kuweza
kuandika habari za Bunge Maalum.
(3) Katibu anaweza wakati wowote kuondoa ruhusa aliyotoa kwa
mwakilishi wa chombo chochote cha habari, iwapo chombo hicho kitatoa
taarifa yoyote kuhusu Shughuli za Bunge ambayo, kwa maoni ya Bunge,
inapotosha ukweli au vinginevyo inakiuka Kanuni, taratibu au haki za Bunge
Maalum.
48
Mamlaka ya
kuwaondoa
wageni
Bungeni

101.(1) Mwenyekiti wa Bunge Maalum anaweza kuamuru wageni
watoke nje ya sehemu yoyote ya Ukumbi wa mikutano ya Bunge Maalum na
maeneo yake, na anaweza pia kuamuru milango ya Ukumbi wa Mikutano ya
Bunge Maalum ifungwe.
(2) Endapo wakati wa kikao chochote cha Bunge Maalum Mjumbe wa
Bunge Maalum atatoa hoja kuwa wageni watoke nje, Mwenyekiti wa Bunge
Maalum atalihoji Bunge papo hapo na hoja itaamuliwa bila ya mjadala au
mabadiliko yoyote, wakati wowote atakapoona inafaa kufanya hivyo.


SEHEMU YA KUMI NA MOJA
USALAMA WA MAENEO YA BUNGE MAALUM
Utaratibu wa kuingia maeneo ya Bunge

102.(1) Mwenyekiti wa Bunge Maalum ataweka utaratibu wa kutoa
vitambulisho kwa Wajumbe wa Bunge Maalum, watumishi wa Bunge
Maalum, watumishi wa Serikali na kwa mtu mwingine yeyote anayeingia
kwenye Ukumbi wa Mikutano au maeneo mengine ya Bunge Maalum.
(2) Katibu wa Bunge Maalum atatoa vitambulisho vya aina tofauti kwa
ajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum, watumishi wa Bunge Maalum,
watumishi wa Serikali na wageni wanaokaribishwa katika Ukumbi wa
Mikutano na maeneo mengine ya Bunge Maalum.
Ukaguzi

103.(1) Kutakuwa na utaratibu wa kumkagua mtu yeyote anayeingia
katika maeneo ya Bunge Maalum kwa kuzingatia:
(a) staha na heshima; na
(b) tofauti ya jinsia.
(2) Mtu yeyote anayeingia maeneo ya Bunge atalazimika kuacha
kwenye eneo la ukaguzi simu yake ya mkononi, vifaa vyote vya kielektroniki
na vifaa vingine vyovyote ambavyo kwa asili yake vina uwezo wa kurekodi
na kuchukua picha.
(3) Endapo katika kufanya ukaguzi mtu yeyote atapatikana na kifaa
ambacho kwa asili yake ni cha hatari, mtu huyo atakiacha kifaa hicho kwa
walinzi waliopo mlangoni.
(4) Mjumbe, mtumishi au mgeni yeyote atakeyekataa kukaguliwa au
kukabidhi kitu chochote ambacho walinzi wataona kwamba kinazuiliwa,
hataruhusiwa kuingia ndani ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge au maeneo
ya Bunge.
49


SEHEMU YA KUMI NA MBILI
MENGINEYO
Lugha Rasmi Bungeni Stahili za Wajumbe na Watumishi wa Bunge Maalum
104.(1) Shughuli za Bunge zitaendeshwa katika lugha ya Kiswahili.

105.(1) Kila mtu aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum
atalipwa posho na malipo mengine kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha
29(2) cha Sheria.
(2) Katibu na Watendaji wa Bunge Maalum watalipwa kwa kuzingatia
Sheria, Kanuni na taratibu kwa namna ambayo Rais ataamua.
Taarifa
Rasmi za
Bunge

106.(1) Taarifa Rasmi ya Majadiliano Bungeni, ikiwa katika lugha
iliyotumiwa na msemaji, yakiwa ni maneno halisi aliyotamka, itatayarishwa
chini ya usimamizi wa Katibu kwa kufuata maagizo yatakayotolewa na
Mwenyekiti kwa ajili hiyo.
(2) Kila Mjumbe aliyetoa hotuba Bungeni atapewa nakala ya hotuba
yake mapema iwezekanavyo, ili aweze kusahihisha makosa ya uchapaji,
kama yatakuwepo, lakini hataruhusiwa kubadilisha maana halisi ya maneno
aliyoyasema Bungeni.
(3) Mjumbe yeyote atakayefanya masahihisho kwa mujibu wa fasili ya
(2) atarejesha masahihisho hayo kwa Katibu ndani ya kipindi cha saa ishirini
na nne.
Mavazi
Rasmi

107.(1) Mjumbe anayeingia kwenye Ukumbi wa mikutano ya Bunge au
ukumbi mwingine wowote ambao kikao cha Kamati ya Bunge kinafanyika,
atawajibika kuvaa mavazi nadhifu na yenye kuhifadhi heshima yake, hadhi
ya Bunge na utamaduni wa nchi, na yasiwe na alama au rangi inayoashiria
Chama chochote cha Siasa.
(2) Vazi Rasmi kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge
litakuwa ni joho lenye kuonesha rangi za Bendera ya Taifa na Nembo ya
Taifa lililoshonwa maalumu kwa ajili hiyo, ambalo litavaliwa juu ya vazi
lake.
(3) Vazi rasmi la Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum na
Makatibu Wasaidizi wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge Maalum litakuwa
kama ifuatavyo:-
(a) Kwa Makatibu wanaume
(i) suti kamili ya kiafrika au suti ya safari, yenye ukosi au shingo
ya mviringo na mikono mirefu au mifupi ya rangi nyeusi au
bluu na joho maalum la Makatibu Mezani.
50
(ii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi nyeusi au bluu na shati jeupe
na tai na joho maalum la Makatibu Mezani.
(b) Kwa Makatibu wanawake
suti ya rangi nyeusi au ya bluu na shati jeupe na tai na joho
maalum la Makatibu Mezani.
(4) Mpambe wa Bunge na Wasaidizi wake ndani ya Ukumbi wa
Mikutano wa Bunge watavaa mavazi rasmi ambayo yataamuliwa na
Mwenyekiti.
(5) Mwenyekiti anaweza kwa sababu maalum, kumruhusu mtu yeyote
anayehusika na Shughuli za Bunge kuvaa vazi ambalo sio rasmi.
(6) Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum anaweza kutoa taarifa kwenye
Bunge Maalum au kwenye Kamati ya Bunge Maalum iwapo Mjumbe
mwingine wa Bunge Maalum ataingia kwenye Ukumbi wa Mikutano ya
Bunge Maalum au Ukumbi wa Kamati ya Bunge Maalum akiwa amevaa vazi
linalovunja au kukiuka masharti ya Kanuni hii.
(7) Mwenyekiti wa Bunge Maalum au Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge Maalum atakaporidhika kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum
aliyetolewa taarifa kwa mujibu wa fasili ya (6) ya Kanuni hii hajavaa vazi
rasmi, ataamuru Mjumbe huyo atoke nje ya Ukumbi wa Bunge au Ukumbi
wa Kamati.
(8) Mjumbe wa Bunge Maalum aliyetolewa nje kwa mujibu wa fasili
ya (7) ya Kanuni hii, hataingia ndani ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge
Maalum au Ukumbi wa Kamati ya Bunge Maalum hadi pale atakapokuwa
amevaa vazi rasmi.
Ufafanuzi
kutoka Tume
ya
Mabadiliko
ya Katiba

108.(1) Bila ya kujali masharti ya kifungu cha 20(4) cha Sheria, Bunge
Maalum na Kamati yoyote ya Bunge Maalum inaweza kuomba kupata
maelezo ya ufafanuzi kutoka Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu jambo
lolote katika utekelezaji wa majukumu na mamlaka ya Bunge Maalum.
(2) Ufafanuzi kwa mujibu wa fasili ya (1) unaweza kutolewa na
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba au Mjumbe yeyote wa
Tume.
Utaratibu
baada ya kifo
cha Mjumbe
109. Endapo Mjumbe atafariki wakati Bunge likiwa katika shughuli
zake, Mwenyekiti ataahirisha Shughuli za Bunge kwa siku hiyo kwa ajili ya
maombolezo.
51
Maoni na 110.(1) Endapo jambo lolote linalohusu Kanuni za Bunge Maalum
ushauri wa litahitaji ushauri wa kisheria, Katibu atalipeleka jambo hilo kwa Mshauri wa
kisheria Sheria katika Sekretarieti ya Bunge Maalum ili alitolee maoni na ushauri wa
kuhusu kisheria.
Kanuni za
Bunge
Maalum
Kutengua 111.(1) Kwa idhini ya Mwenyekiti, Kanuni yoyote inaweza
Kanuni kutenguliwa kwa madhumuni mahsusi baada ya Mjumbe yeyote kutoa hoja
kwa ajili hiyo.
(2) Bila kujali masharti yaliyotangulia ya Kanuni hii, maoni na ushauri
wa kisheria kuhusu masuala ya kikatiba na kanuni zake unaweza kuombwa
kwa wataalam wengine wa sheria kutoka nje ya Bunge Maalum, kama
ambavyo Mwenyekiti wa Bunge Maalum, baada ya kushauriana na Katibu
wa Bunge Maalum ataona inafaa.
(2) Maelezo ya hoja ya kutaka kutengua Kanuni yoyote itakuwa ni
pamoja na maelezo kuhusu madhumuni ya kutaka Kanuni hiyo itenguliwe.
(3) Kanuni hiyo itatenguliwa kwa madhumuni yaliyokusudiwa tu na
siyo kwa madhumuni mengine yoyote.
Matumizi ya 112 Ukumbi wa Mikutano ya Bunge Maalum hautatumika kwa
Ukumbi wa shughuli nyingine yoyote, isipokuwa kwa shughuli ya uendeshaji wa
Mikutano ya Mikutano na vikao vya Bunge Maalum na Kamati zake, na pia shughuli
Bunge nyingine za Bunge Maalum.
Maalum
Kufanya 113.(1) Bunge Maalum linaweza kuzifanyia mabadiliko au
mabadiliko marekebisho Kanuni hizi kwa Azimio litakalowasilishwa Bungeni na
au Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge.
marekebisho
katika
Kanuni
(2) Endapo Mjumbe yoyote wa Bunge Maalum ataona kuna haja ya
Kanuni fulani kufanyiwa mabadiliko au marekebisho, anaweza kuwasilisha
mapendekezo yake pamoja na sababu zake, kwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Kanuni na Haki za Bunge ili yafanyiwe kazi na Kamati hiyo, na kama
yataonekana yanafaa, yatawasilishwa Bungeni kwa mujibu wa fasili ya (1).
52
____________
NYONGEZA YA KWANZA
___________
KANUNI ZA UCHAGUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI
[Chini ya Kanuni ya 11(4)]
___________
SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI
Jina 1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum, 2014.
Matumizi 2. Kanuni hizi zitatumika katika mchakato wa Uchaguzi wa Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Tafsiri 3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale ambapo maelezo yatahitajika
vinginevyo-
"Mgombea" ni Mjumbe wa Bunge Maalum aliyejitokeza au
aliyependekezwa na Mjumbe mwingine au Wajumbe wengine wa Bunge
Maalum kuwa mgombea wa Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum;
"Msimamizi wa Uchaguzi" ni Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
na Katibu wa Baraza la Wawakilishi ambao kwa mujibu wa Kanuni hizi,
wamepewa mamlaka ya kuendesha na kusimamia mchakato wa Uchaguzi
wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum;
"Mwenyekiti" ni Mjumbe wa Bunge Maalum aliyechaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa Bunge Maalum kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha
23(1) cha Sheria;
"Mwenyekiti wa muda" ni Mjumbe wa Bunge Maalum aliyechaguliwa
kwa mujibu wa kifungu cha 22A cha Sheria awe Mwenyekiti kwa ajili ya
kusimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum;
"Nafasi" ni nafasi iliyo wazi ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum;
"Nafasi ya nasibu" ni nafasi iliyo wazi ya Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum isiyotokana na kuundwa upya kwa Bunge
Maalum;
"Siku ya uteuzi" ni siku ambayo imetangazwa na msimamizi wa
uchaguzi kwamba ni siku ya mwisho ya kupokea majina ya wagombea wa
nafasi ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum;
"Uchaguzi" ni Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum.
53

SEHEMU YA PILI
USIMAMIZI WA UCHAGUZI NA UWASILISHAJI WA JINA LA MGOMBEA
Uendeshaji 4. Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge
na Maalum utaendeshwa na kusimamiwa na Mwenyekiti wa muda wa Bunge
usimamizi Maalum, kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge Maalum,
wa uchaguzi pamoja na Kanuni hizi.
wa
Mwenyekiti
na Makamu
Mwenyekiti
wa Bunge
Maalum
Kuwasilisha 5.(1) Mara baada ya kukalia kiti, Mwenyekiti wa muda atawaalika
jina la Wajumbe wa Bunge Maalum wenye sifa ya kuwa wagombea wa uchaguzi
mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum na Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum kuwasilisha majina yao kwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
(2) Kila jina la mgombea wa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa
Bunge Maalum, atatakiwa kujaza fomu iliyoandaliwa kwa ajili hiyo ambayoi
itakuwa na majina ya Wajumbe ishirini wa Bunge Maalum wanaounga
mkono mgombea husika, kwa idadi ya Wajumbe kumi kwa kila upande wa
Jamhuri ya Muungano.
(3) Fomu za Wagombea wa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum kwa mujibu wa masharti ya fasili
ya (2) zitawasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi, ofisini kwake, kabla ya
saa nne asubuhi ya siku ya uteuzi.
(4) Baada ya kupokea majina ya wagombea kwa mujibu wa masharti ya
fasili ya (3), Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza
la Wawakilishi wataandaa karatasi za kura zinazoonyesha majina na
wagombea wote wa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum, waliotimiza masharti yaliyowekwa na
Kanuni za Bunge Maalum, pamoja na masharti ya Kanuni hizi, na wakati wa
kupiga kura, atatoa karatasi moja tu ya kura kwa kila Mjumbe wa Bunge
Maalum.

SEHEMU YA TATU
UPIGAJI WA KURA
Kujitoa
katika
uchaguzi
6. Muda mfupi kabla ya uchaguzi, mgombea yeyote anaweza kutoa
taarifa ya maandishi kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuwa anajitoa kugombea,
na Msimamizi wa Uchaguzi atawasilisha jina hilo kwa Mwenyekiti wa muda
ambaye atatangaza jina hilo kwamba limefutwa kutokana na sababu ya
kwamba mgombea ametoa taarifa ya kujitoa katika uchaguzi huo.
54
Upigaji wa
kura
7.(1) Kila mjumbe atatakiwa kupiga kura ya siri kwa kuweka alama ya
vyema "(√)" kwenye kisanduku kilichopo pembeni mwa jina la mgombea
anayemtaka awe Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum na
kutumbukiza karatsi hiyo katika sanduku maalum la kura lililoandaliwa kwa
ajili hiyo.
(2) Baada ya kuridhika kwamba Wajumbe wote wamepiga kura na
kutumbukiza karatasi zao za kupigia kura kwenye masanduku ya kura,
Katibu atayakusanya masanduku yote na kuyapeleka kwenye chumba
maalum cha kuhesabia kura, na kura zitahesabiwa mbele ya Wawakilishi
walioteuliwa na wagombea, mmoja kwa kila mgombea.
(3) Mgombea yeyote atakuwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum kama atapata zaidi ya nusu ya kura
za Wajumbe wote, na iwapo hakutakuwa na mgombea aliyepata zaidi ya
nusu ya kura hizo, uchaguzi utarudiwa:
Isipokuwa kwamba, ni wagombea wawili tu watakaokuwa wamepata
kura nyingi zaidi ndio watakaopigiwa kura, na katika hatua hiyo, mgombea
atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa kuwa ndiye mshindi.
(4) Endapo wagombea wawili au zaidi watapata kura sawa, basi
wagombea hao tu ndio watakaopigiwa kura, na mgombea atakayepata kura
nyingi zaidi atatangazwa kuwa ndiye mshindi.
(5) Iwapo wagombea wawili au zaidi watapata kura sawa katika nafasi
ya pili na yule wa kwanza hakupata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa, basi
wagombea hao wawili pamoja na yule wa kwanza ndio watakaopigiwa kura,
na mgombea atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa kuwa ndiye mshindi.
(6) Endapo awamu ya pili ya upigaji wa kura itashindwa kumpata
mshindi, basi Mwenyekiti wa muda atapiga kura yake ya uamuzi ili mshindi
apatikane.
(7) Endapo kutakuwa na mgombea mmoja tu, basi mgombea huyo
atapigiwa kura ya "Ndiyo" au "Hapana", na atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge
Maalum iwapo atapata kura za "Ndiyo" za idadi ya zaidi ya nusu ya kura za
Wajumbe wote.

SEHEMU YA NNE
KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI NA KUAPISHWA
KUSHIKA MADARAKA
Kutangaza
matokeo ya
uchaguzi
Sura 83
8. Mara baada ya mshindi kupatikana, Msimamzi wa Uchaguzi
atamtangaza Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum
aliyechaguliwa, na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti huyo Mteule ataapa
55
viapo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Bunge Maalum.
Mwenyekiti/
Makamu
Mwenyekiti
kula yaamini
/kiapo
Sura 83
9.(1) Muda wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mteule kuapishwa
utakapowadia, Mwenyekiti wa muda atamwita Mwenyekiti wa Bunge
Maalum Mteule apite mbele ya Bunge Maalum ili ale yamini au aape viapo
vinavyomhusu.
(2) Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum aliyechaguliwa kuwa
Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum, kabla ya kushika
madaraka yake ataapa mbele ya Bunge Maalum Kiapo cha Utii na Kiapo
cha Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti vilivyowekwa na Sheria na
Kanuni za Bunge Maalum.
(3) Bila ya kuathiri masharti yoyote ya Kanuni hizi, Uchaguzi wa
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum utaendeshwa kwa utaratibu ule ule
unaotumika kumchagua Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
56

FOMU YA KUPENDEKEZA JINA LA MGOMBEA
[Chini ya Kanuni ya 5(2)]
__________
KUPENDEKEZA MGOMBEA
[Ijazwe na Mjumbe anayependekeza]
________________
Kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwenyekiti/Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Mimi....................................................... nikiwa Mjumbe wa Bunge Maalum,
nampendekeza ........................................................... ambaye ni Mjumbe wa
Bunge Maalum kuwa mgombea wa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti/Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Taarifa muhimu kuhusu mgombea ninayempendekeza ni kama ifuatavyo:-
1. Jina Kamili la Mgombea:.....................................................................
2. Umri wake: ....................................................................................
3. Jinsia: .............................................................................................
4. Kiwango cha Elimu:...........................................................................
5. Anuani yake: ....................................................................................
Jina la Mjumbe anayependekeza: ................................................
Saini yake: ...........................................................................
Pendekezo hili linaungwa mkono na Wajumbe wafuatao:-
A:
Wajumbe Kumi kutoka Tanzania Bara
Jina
Saini
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
57
................................................... ................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
...................................................
B:
...................................
...................................
Wajumbe Kumi kutoka Tanzania Zanzibar
Jina
Saini
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
................................................... ...................................
58
59
 
Kanununi hizi naona azina tofauti sana na zile za Bunge la kawaida kwa kanuni hizi kwa maoni yangu mtu sahii wa kuzisimamia kama Mwenyekiti SITTA anafaa kama hatakuwa amebadilika.
 
Ni nzuri hasa kipengele cha mjumbe asipohudhuria kikao posho hakuna hii safi sana,na mwenyekiti na makamu wake wanaoweza kusimamia hizi kanuni ni MH Sitta na Tundu Lisu
 
Back
Top Bottom