Kanuni ya CCM iliyommaliza SUMARI

Ina maana waliosimamia uchaguzi hawakuijua hiyo kanuni?

Hiyo kaka haifanyi kazi. Angalia mfano wa jimbo la Kigamboni 2010:
Kwamujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana jioni, Kigamboni: Dk. Faustine Ndugulilealishinda kwa kura 4,251, Issa Mangungu kura 2,420 na Mariam Kambi kura 2,377.
 
KAULI YA NAPE MARA BAADA YA USHINDI WA SIOI: Source: HABARI LEO

Ushindi wa Siyoi: Wakati huohuo, Katibu wa Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, amesema utaratibu wa kuteua mgombea aliyepata asimilia 51
ya kura za maoni bado haujaanza kutumika rasmi CCM.

Alifafanua kuwa bado chama hicho kina nia ya kufanya mabadiliko katika mfumo wake wa kura za maoni, ili kifike mahali mgombea anayetoka chama hicho, awe amechaguliwa kwa asilimia 51 ya kura zote.

Alisema hayo alipohojiwa na gazeti hili kuhusu ushindi wa kura za maoni katika jimbo hilo kwa Siyoi Sumari ambaye idadi ya kura zake ni pungufu ya asilimia 50 ya kura zote.

Katika uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika juzi Arumeru kwa ajili ya kupatikana mgombea wa CCM, Siyoi (30) aliibuka na ushindi kwa kura 361 kati ya kura 1,034 za wajumbe wa chama hicho.

Wagombea wengine walikuwa William Sarakikya (259), Elirehema Kaaya (205), Elishiria
Kaaya (176), Anthony Msani (22) na Rishiankira Urio aliyeambulia kura 11.

Akizungumzia taarifa hizo, Nape alisema hakuna
ushahidi wowote unaothibitisha taarifa hizo,
hivyo hawezi kuisemea hali hiyo ina athari gani
kichama katika uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa
kufanyika Aprili mosi.
Uchaguzi huo unatokana na kifo cha aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo, Jeremiah Sumari (CCM)
aliyefariki dunia mwezi uliopita.
Imeandikwa na John Mhala,Arusha na Halima
 
Back
Top Bottom