Kanuni ya CCM iliyommaliza SUMARI

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Utaratibuwa kuhesabu kura na kutangaza matokeo

21 (a) Kazi ya kuhesabu kura itafanyika tu wakati ambapo kuna mwanga wakutosha na wa kuaminika na mahaliambapo kuna ulinzi na usalama madhubuti.

(b) Kiwango cha kura katika kufikiauamuzi wa mshindi katika uchaguzi usio wakundi ni zaidi ya nusu ya kura zote halali zilizopigwa. Kura halali zilizopigwa nikuondoa kura zilizoharibika.

Katika uchaguzi wakujaza nafasi nyingi kwa pamoja (Uchaguzi wakundi) ushindi utahesabiwa kwa kufuata wingi wa kura alizopata mwombaji.

Source: Kanuni za Uchaguzi za CCM, Toleo la Februari 2010.
 
Utaratibuwa kuhesabu kura na kutangaza matokeo

21 (a) Kazi ya kuhesabukura itafanyika tu wakati
ambapo kuna mwanga wakutosha na wa
kuaminika na mahaliambapo kuna ulinzi na
usalama madhubuti.

(b) Kiwango cha kura katika kufikiauamuzi wa
mshindi katika uchaguzi usio wakundi ni zaidi
ya nusu ya kura zote halalizilizopigwa. Kura
halali zilizopigwa nikuondoa kura zilizoharibika.
Katika uchaguzi wakujaza nafasi nyingi kwa
pamoja (Uchaguzi wakundi) ushindi utahesabiwa kwa kufuata wingi wa kura alizopata mwombaji.

Source:Kanuni za Uchaguzi za CCM, Toleo la Februari 2010.

Kwa hiyo wamevunja kanuni eeh chama gani kisichokuwa consistent?
 
Kwa hiyo wamevunja kanuni eeh chama gani kisichokuwa consistent?
Sarakikya alikuwa ahamie CHADEMA na sasa wakaona Wiliam ana kubalika ndani ya chama na kama atahamia Chadema kutatokea mgawanyiko mkubwa ndani ya chama cha magamba.....ndani ya CCM hata kijana mdogo kama Sarakikya kafanikiwa kuwayumbisha mpaka wameamua kunyonga demkrasia....Hongera Sarakikya
 
Safi sana CCM wengine hadi leo wana kigugumizi cha kumpata mgombea! Hongereni CCM kwa demokrasia pana zaidi
 
Kwa nini serikali ya CCM iliifuta kanuni hii kwenye katiba ya JMT kwenye uchaguzi wa Rais ambayo ni muhimu na ya maana zaidi kwa TAIFA? Sasa hivi Rais wetu anapatikana kwa kura zozote zile ilimradi kawazidi wagombea wenzake hata kwa tofauti ya kura moja.
 
Ni ukora wa CCM baada ya kuona cha moto katika uchaguzi wa mwaka 1995, wakajitabiria kuwa Mkapa kwa kuwa alipata kura chini ya 60% basi huenda mwaka 2000 angepata chini ya 50%. Hivyo wakabadili sheria hiyo kwa matakwa hayo tu. Vinginevyo, sheria/kanuni/ibara hii, kama ilivyo kwenye kanuni zao, inapaswa irudishwe kwenye katiba ya JMT.
 
Mbona hiyo Kanuni hatukuiona kwenye uchaguzi wa 2010 wa kuwapata yagombea ubunge wa CCM?
Dr, Kigwangalah alikuwa wa TATU na bado akachaguliwa kupeperusha bendera ya CCM. Kama wanampenda
sana huyo William aliyetishia kuhamia CDM kwanini wasipe yeye kuliko kupindisha katiba yao?
CCM mabingwa wa kuhamisha post wakati mchezo ukiwa dk 45 tayari (read half time)
 
Mmeona jinsi wezi wanavyoogopa kuibiwa? Angalia kanuni hiyo 20(a)! Wao hapa ndipo wanapopata ushindi:
1. Kura zinahesabiwa usiku, hususan vijijini ambapo hakuna umeme.
2. Jeshi la polisi mara nyingi humpendelea anayewapa "kitu kidogo", hivyo CCM hufaidika kutokana na udhaifu huo. Vilevile vyama vya upinzani hukosa mawakala katika baadhi ya vituo.
 
Mbona hiyo Kanuni hatukuiona kwenye uchaguzi wa 2010 wa kuwapata yagombea ubunge wa CCM?
Dr, Kigwangalah alikuwa wa TATU na bado akachaguliwa kupeperusha bendera ya CCM. Kama wanampenda
sana huyo William aliyetishia kuhamia CDM kwanini wasipe yeye kuliko kupindisha katiba yao?
CCM mabingwa wa kuhamisha post wakati mchezo ukiwa dk 45 tayari (read half time)
Kimsingi wanahangaika na jinamizi na kivuli cha Lowasa. Mara nyingi tu wamechukua hadi mshindi wa tatu kwenye kura za maoni kama walivyofanya kwa Dr Kigwangala na wengine wengi.
 
Safi sana CCM wengine hadi leo wana kigugumizi cha kumpata mgombea! Hongereni CCM kwa demokrasia pana zaidi

CCM inatapatapa. Mara mseme kanuni ilivunjwa, mara ooooh Sumari siyo raia wa Tanzania (Ajabu baba yake alikuwa Raia na alipofariki alizikwa kwa heshima za kitaifa na viongozi magamba walihudhuria = mtoto si raia)

Mara ooooooooo tunarudia uchaguzi mshindi wa kwanza na wa pili. Na hii yote ni kutaka kumuweka pembeni Sumari kwani wameshaona kuna hatari ya kutopata kura.

na bado mbona mtakereka sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Nape na mlioko CC ya CCM:
Rudisheni nguvu ya Taasisi hii muhimu katika nchi yetu toka mikononi mwa akina Lowasa. Acheni kuchezea RUZUKU yetu kwa kiwango hiki. Ngoja niwashauri wale wote waliogombea na mliowateua bila kuzingatia kanuni hii waende mahakamani kupinga ushindi wao batili.
 
Siku zote mwizi akiibiwa hujisikia kuzimia mkuu.Kati ya wanadamu wanaoogopa kuibiwa na huwa wanajiskia vibaya zaidi wanapoona wanaibiwa ni wezi

CCM wamebaki na maamuzi ya dharura,naamini hata mchakato wao wa 2015 utategemea na utashi wa ki-dharura dharura tu.Jenerali ulimwengu aliita mipangilio ya uongozi,ni dili....leo tumeshudia mipangilio Arumeru
 
Utaratibuwa kuhesabu kura na kutangaza matokeo

21 (a) Kazi ya kuhesabu kura itafanyika tu wakati ambapo kuna mwanga wakutosha na wa kuaminika na mahaliambapo kuna ulinzi na usalama madhubuti.

(b) Kiwango cha kura katika kufikiauamuzi wa mshindi katika uchaguzi usio wakundi ni zaidi ya nusu ya kura zote halali zilizopigwa. Kura halali zilizopigwa nikuondoa kura zilizoharibika.

Katika uchaguzi wakujaza nafasi nyingi kwa pamoja (Uchaguzi wakundi) ushindi utahesabiwa kwa kufuata wingi wa kura alizopata mwombaji.

Source: Kanuni za Uchaguzi za CCM, Toleo la Februari 2010.

Ina maana waliosimamia uchaguzi hawakuijua hiyo kanuni?
 
Back
Top Bottom