Kanuni ya 64 vis-à-vis hoja Binafsi ya Mhe. MNYIKA

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
412
90
Binafsi nimeguswa sana na hoja ambayo Mnyika anatazamia kuiwakilisha Bungeni kwani zaidi ya yeye kupata ufafanuzi wa anayohitaji naamini Watz tulio wengi ambao hoja hiyo hatukuweza kuielewa kwa undani wakati huo basi tunawezapata undani wa hoja hiyo lakini vile vile inaweza ikasaidia kuwatendea haki wale ambao ama walionewa kwa kuwasilishwa kwa hoja au kuchafuliwa majina yao na kuonekana wenye dhambi katika jamii na mwisho tutaweza kuona ni jinsi gani baadhi ya watu hufanya vitu kizindaki na kinafki kwa ajili ya ubinafsi wao na kuishia kujiita wapambanaji.

Pamoja na nia nzuri hiyo ya Mh. John hizi Kanuni za Kudumu za Bunge hasa Kanuni ya 64 inayozungumzia "Mambo yasiyoruhusiwa Bungeni" kama vile inaleta mizengwe hasa ile fasili ya (1) (c) naomba ninukuu

"............ Mbunge hatazungumzia jambo lolote ambalo lilijadiliwa na kutolewa maamuzi kwenye Mkutano uliopo au uliotangulia.........; isipokuwa kwa kutoa hoja mahususi inayopendeza kuwa uamuzi huo uangaliwe upya"

Sasa hii Kanuni imekaa kimtego mosi ni kwamba ina Claw back Clause lakini pili mwisho inamalizia kuwa labda Mbunge atoe hoja MAHUSUSI of which mimi nadhani ili iwe mahususi au lah itakuwa ni discreation ya Spika kuamua hivyo mi napata shaka kidogo juu ya Kanuni hii inaweza tumika kudismiss hii hoja unless Mh Mnyika awe naye amejipanga vizuri.....

Naombeni ushauri wenu juu ya hili la Kikanuni. Je kama kweli watatumia Kanuni hii je Mnyika atakuwa na Haki Kikatiba kutumia Ibara ya 18???
 
Mnyika has only a year ahead before his eminence begins to diminish and subsequently follow Zitto's trend. It's undeniable fact that no any young politico's vigor has ever come closer to Zitto's vitality as he was able to capture public and media attention but all of his punch came to an end abruptly.
 
Back
Top Bottom