Kanumba: Sipigi kura, 2015 nitagombea ubunge

Kama namuona Kanumba, anavyocheka kwenye tangazo la Star time..hahahahahaha..umeniletea zawadi yangu ya sikukuu! Hahahahaha!
 
sioni tofauti kubwa kati ya sugu na kanumba,tofauti ndogo ni kwamba kanumba sharobaro,sugu mgumu
 
Huyu Kanumba nilishaulizia Profile yake baada ya kusuff kwenye Blog yake na kuikosa! Safi tu wacha agombee aingie mjengoni akatengeze movie na akina Anne Makinda.
 
mnashangaa nini? cha msingi akubalike tu na wapiga kura wake. Mbona hamshangai yule mwimba kwaya na msinziaji mkuu mjengoni? wabunge wachapakazi hata 50 hawafiki kwenye bunge letu, wengine ni njaa ya posho mpaka siku wasomi wetu watakapokubali kurudi majimboni kugombea vinginevyo kuna siku mtawapata hata kina kaole - zecomidi wakawatungie sheria zenu.
 
Kama kweli basi mimi namshauri agombee majimbo ya hapahapa Dar kwa sababu;
1. Makazi yake yapo dar hivyo anazifahamu vizuri kero za jiji hili.
2. Ili kuthibitisha kuwa yuko compitent na si kwa kuwa anauza sura kideoni maana watu wa dar kidogo wana uwezo wa kuwapima wagombea.

n.b; Binafsi siwez kumhukumu moja kwa moja huyu bwana kwa sababu kwa mujibu wa katiba ana uhuru wa kufanya hivyo ILA(natumia simu, siwez ku-bold hilo neno) sijamuona kama ni type ya watu tunaotaka ili walikomboe taifa hili, watu kama Mnyika, Kafulila, Lema, n.k. Kwa maana hiyo ningeshauri agombee kupitia kwa magamba ili afe nao!
Kama Kanumba ameshindwa kutetea haki za wenzake wachache(wasanii) anawezaje kutetea wananchi?
Kama kanumba ameshindwa kuwa mbunifu katika kazi zake na baadala yake anarudia filamu hiyo hiyo na kuona kuwa filamu ni kubadilisha badilisha majumba, magari na mavazi( kwa kifupi kuuza sura), anawezaje kubuni mbinu za kumuondoa Mtanganyika katika lindi la umasikin ilhali nchi yake ni tajiri kuliko maelezo?
 
Acha achukue. Ila kuhusu posho bana mi naona kazoea starehe sana. Sasa cjui ndoo kutumaliza au? Cjui bwana. Let him get in!
 
Anataka kushindana na mh masele au anataka kuleta maendeleo, alete malengo na matarajio yake ambayo yanapingana ama yenye tofauti na masele tutampigia kura.. Je anaweza kushawishi wawekezaji wakachangia maendeleo ya jimbo la shinyanga. Pamoja kuisimamia serikali kusukuma maendeleo? Yote haya hayahitaji usanii
 
Habari wanajamvi nilikua napita mnara wa voda eneo maarufu kwa mafundi vitanda ambapo pembeni kuna ofisi za CHADEMA Shy mkoa nkakuta tetesi kuwa msanii Steven Kanumba atarudi kugombea 2015 kupitia chadema against Masele wa CCM hebu tusaidiane je ina logic? Source mi

Anaweza akachukua jimbo
Vile vile ana haki kikatiba akiwa ni mtanzania aliye vuka umri wa miaka 18 na akijua kusoma na kuandika
 
kazi imeanza, haya ndio yanafanya jf idharauliwe

acha mawazo hayo, kwa lipi idharaulike? kwa hili la hii post au lipi hasa. Nakuuliza wewe ivi mkamia si ame kuwa mbunge? beti mkwasa si mkuu wa wilaya? ivi wakati bety ni mtangazaji ungejua kama atakuwa mkuu wa wilaya? kule senegari anayejipanga kugombea kupitia upinzani si mwana mziki? au Madagascar siinaongozwa na Dj? au kwa kusikia jina Kanumba ndio yeye umemuona hana haki ya kuchaguliwa? hapa la msingi kama anakubalika kwa wananchi na wananchi wakawa na matumaini naye kuwa atawawakilisha basi mie sioni tatizo. Hata hao wengine ambao wewe unadhani wanafaa wamesoma sana hawaigizi ni yepi mazuri kwa professional zao wameyafanya? wote ni full kaputi kutuibia kwa kwenda mbele.
 
Inawezekana na safi sana kama atakuwa mtu makini.

Inaanza kutia furaha kuwa watu wanaanza bila woga kugombea kupitia vyama vingine vya upinzani bila woga.

Kanumba jipange vizuri mdogo wangu na anza kuchukua busara za watu kama Dr. Slaa na wazee wengine wengi hata kama ni wa CCM ila wale tu wanaheshimika.

Wasanii wengi wameanza kuingia kwenye siasa baada ya hawa wajiitao WASOMI kushindwa kazi kabisa.

Haiti, sasa hivi Rais wao ni huyu jamaa alikuwa zamani anaitwa Sweety Mickey.



Hapo njiani tumeshaona DJ kutoka Madagascar, King George Weah, Mcheza film Ronald Reagan, mpiga jazz Bill Clinton........

Na mwingine yupo njiani anaitwa Youssou Ndour kutoka Senegal ambaye ni mwanamuziki maarufu sana duniani na ukiacha u-wanamiziki, jamaa amekuwa mbele sana kwenye kusaidia hujuma za jamii nchi kwake. Nasikia pana wakati alimshangaa Koffi Olomide kwamba hajafanya kitu chochote kwa watu wa Congo hadi leo hii....
 
Last edited by a moderator:
sioni tofauti kubwa kati ya sugu na kanumba,tofauti ndogo ni kwamba kanumba sharobaro,sugu mgumu

Sugu na kanumba wana tofauti kubwa,labda akigombea magamba anashabihiana nao
kumbuka sugu ni mpambanaji na alishakataa kukandamizwa
Huyo K hana tofauti na Kapten Komba ama yule mwanamama aliyeimba wanawake na maendeleo
usitegemee jambo jipya hapo....ila kwa ujinga wa watz kushobokea mtu anayeonekana luningani utashangaa anaweza kumdondosha mpinzani wa maana
 
huyu jamaa alikuwa mpambe wa karibu sana kumnadi shigongo kipindi cha kura za maoni ccm. CDM kaingia vipi na lini?
 
Habari wanajamvi nilikua napita mnara wa voda eneo maarufu kwa mafundi vitanda ambapo pembeni kuna ofisi za CHADEMA Shy mkoa nkakuta tetesi kuwa msanii Steven Kanumba atarudi kugombea 2015 kupitia chadema against Masele wa CCM hebu tusaidiane je ina logic? Source mi

usiwe uanaandika mambo yako ya mautumbo hapa
 
ni haki yake kugombea
kama cantona anafikiria kugombea uraisi wa ufaransa kwanini kanumba asifikirie ubunge wa shinyanga......

mimi nawashauri wale ambao wanamwona hafai wampigie kura yule ambae wanamwona anafaaa, kama wagombea wote anawaona hawafai then itakuwa vizuri nao wakachukue fomu kwa ajili wao wanafaa

mbna yule mwmbji wa senegal pia anatka kugombea urais na 7 leaver sema kapewa stashahada tena ya muziki2 naankubalika?wapo weng 2 ma celeb kina wyclif jean,kina george weah,tuacha dharau,mbna wasira ni mbunge na waziri?
 
Tanzania ni nchi ya majaribio''if u fail 2 make t here u wil never make t anywhere''
 
Back
Top Bottom