Kanumba ndani ya Big Brother House 2009

jana nilistuka sana baada ya kuangalia bba na kumkuta kanumba, maana sikumbuki alichaguliwa lini?? ila yule ni msanii ataharibu tu pale hapamfai, tatizo la wasaniii wetu wa bongo wanajifanya kutumia sana vipaji ambavyo vingine ni vy kulazimisha, wenzao wanasomea, hapa mtu akiigiza tu kidogo eti naye ni msanii....mara eti pia ni director....come on guyz ndio mana kazi zao zinaboa wakati mwingine...
 
Safi sana Kanumba umetuwakilisha vizuri wasukuma na watanzania...! teh teh teh

Wasukuma na Kiingereza chao wakati mwingine kinafurahisha. Unakuta Ngosha anasema "I am comingi furom Jamayika". Kali ni yule alikuwa alienda Urusi pale kusoma na siku moja akiwa anataka kuwasha jiko la Gesi, akaona dada wa Kizambia akitaka kuzima jiko, ngosha akaruka "Don't put it off, i'm cooking ON HIM".
 
Wasukuma na Kiingereza chao wakati mwingine kinafurahisha. Unakuta Ngosha anasema "I am comingi furom Jamayika". Kali ni yule alikuwa alienda Urusi pale kusoma na siku moja akiwa anataka kuwasha jiko la Gesi, akaona dada wa Kizambia akitaka kuzima jiko, ngosha akaruka "Don't put it off, i'm cooking ON HIM".

teh teh teh unajua Msukuma yeyote anayeimba taarabu! Lugha ni issue kwa kweli....nakumbuka mwalimu wa English darasa la tano pale Ilolanguzu primary, alikuwa anachanganya kisukuma na kiingereza sasa huo mchanganyiko ni balaa hasa pronunciation!
 
Wasukuma na Kiingereza chao wakati mwingine kinafurahisha. Unakuta Ngosha anasema "I am comingi furom Jamayika". Kali ni yule alikuwa alienda Urusi pale kusoma na siku moja akiwa anataka kuwasha jiko la Gesi, akaona dada wa Kizambia akitaka kuzima jiko, ngosha akaruka "Don't put it off, i'm cooking ON HIM".

Hahahahahaha bila shaka mkuu Yo Yo na swaum yake dah....
 
jana nilistuka sana baada ya kuangalia bba na kumkuta kanumba, maana sikumbuki alichaguliwa lini?? ila yule ni msanii ataharibu tu pale hapamfai, tatizo la wasaniii wetu wa bongo wanajifanya kutumia sana vipaji ambavyo vingine ni vy kulazimisha, wenzao wanasomea, hapa mtu akiigiza tu kidogo eti naye ni msanii....mara eti pia ni director....come on guyz ndio mana kazi zao zinaboa wakati mwingine...

Mkuu acha kubeza, Kanumba ni 'actor' tena anaiweza kazi yake. Nani kama Kanumba Tanzania? hawa wengine akina Single Mtambalike, JB, Richard nk wanafuata nyayo tu. Waliofyeka njia ya film/movies ni akina Kanumba, Ray, Magali nk. Lakini ktk hao wote staa wao ni Kanumba. Tembelea tovuti yake upate mengi zaidi hapa:http://kanumba.com/

Swala la kwenda BBA hakujipeleka, bali BBA kwa utafiti wao wamemwona kuwa ni moja ya celebs wakubwa Africa, ndo maana akaitwa kule. Pia kumbuka kwamba BBA siyo serious thing, is just fun shows. So, unaweza kufanya chochote ilimradi kinawavutia watazamaji na kuiingizia pesa mnetafrica.

Kanumba anastahili heshma kwa kutangaza movie za bongo mpaka sasa wasanii wanaweza kujiajiri ktk fani hiyo.
 
Masa na Fidel,
Tuache utani pembeni. Nikiwa Mazengo kulikuwa na mwalimu wa Fizikia akifundisha High School akiitwa NYANDA. Pia nilishakutana na kijana anaitwa B. Shija. Hawa jamaa wawili ingawa hawafahamiani walikuwa na kitu incomon. Wote wakiongea Kiswahili utafahamu kuwa ni Wasukuma pure. Ila wakianza kuongea Kiingereza, utaamini wametoka UK. Kisukuma kinapotea na anaanza kuongea kiingereza safi kabisa hadi unashangaa.
Mnyonge mnyonge ila haki yake mpeni. Kuna wengine wameharibiwa kabisa na kisukuma kama Francophones na wale wanaoweza kukificha. Nilibahatika kukutana na mwanamuziki Sekou Keita (alishakuwa kwenye Sauti za Busara Zanzibar) na huwezi amini anatoka Senegal. Kiingereza saafi kabisa.
 
Waveja sanaa....

Hapana, wenyewe tunasema "wabhejja" au siyo hivyo ndugu yangu Sikonge; kuna watu wanachezea lugha yetu ati.

Halafu kwa kuongezea kiingereza cha wasukuma (na wanyamwezi pamoja); kuna ndugu mmoja alisema kuwa kwao Tabora hupikia kuni na kinyesi cha ng'ombe lakini akatamka kuwa "at Tabora we cook for firewood and cow dung." Kwetu unyamwezini kweli tuna mambo!! Ndiyo maana spika anatakiwa afanye kazi ya ziada.


Halafu hivi hii kitu inaitwa "John Wayne International Awards" aliyopata Kanumba mwaka 2007 huwa inatolewaje? Sijawahi kuisikia mahali popote mpaka pale ndugu yetu Kanumba alipoinyakua na baada ya hapo sijaisikia tena. ........
 
Mtoa mada sio wote wenye ving'amuzi majumbani kwao,hebu fafanueni ni kweli yumo au hayumo msiwe mnatuzingua.! kama yupo mjengoni au hayupo basi ijulikane.
Du! Mpaka saa hii mtoa mada hajatokea. Naona yamemfika makubwa huko aliko
 
Mkuu acha kubeza, Kanumba ni 'actor' tena anaiweza kazi yake. Nani kama Kanumba Tanzania? hawa wengine akina Single Mtambalike, JB, Richard nk wanafuata nyayo tu. Waliofyeka njia ya film/movies ni akina Kanumba, Ray, Magali nk. Lakini ktk hao wote staa wao ni Kanumba. Tembelea tovuti yake upate mengi zaidi hapa:http://kanumba.com/

Swala la kwenda BBA hakujipeleka, bali BBA kwa utafiti wao wamemwona kuwa ni moja ya celebs wakubwa Africa, ndo maana akaitwa kule. Pia kumbuka kwamba BBA siyo serious thing, is just fun shows. So, unaweza kufanya chochote ilimradi kinawavutia watazamaji na kuiingizia pesa mnetafrica.

Kanumba anastahili heshma kwa kutangaza movie za bongo mpaka sasa wasanii wanaweza kujiajiri ktk fani hiyo.

Mkuu kama umeenda shule ya kimagharibi, basi shule haikukaa, ulifaulu tu upate cheti.

Kama huajenda hiyo shule wala sioni ajabu.

Hata kama ni show ya kuchekesha lazima ueleweke unaongea nini. Wakati wenzake wanaongea maneno ya kawaida yeye anacheka, akiulizwa maswali anasema YOUR WORDS IS DIFFICULT.

Ndugu yangu ni aibu. Labda wewe tu huoni ila kwenye kila shemu bongo jana ni gumzo.

Ukiwa hujui kuongea kiingereza kuanzia jana unaitwa KANUMBA.

Kama kafanikiwa na shule hana, na wewe umeenda shule, umeshindwa nini kumshauri ajifunze kiingereza? ni muhimu sana kwa kazi yake ndugu yangu.
 
  • Tarehe Mon Sep 07, 04:09:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Bwana mithupu,ametesa nini na ze english not reachable anacheka cheka tu hovyo hata hailewi wenzie wanacheka nini?

    Tarehe Mon Sep 07, 04:10:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Jamani Kanumba kajitahidi alisoma wakati no st.school enzi hizo so nampa big up Kanumba mwaya achana na wabeba mabox!

    Tarehe Mon Sep 07, 04:13:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Anko nanihii, naomba usiibane hii comment, Jana nilikuwa naangalia hiyo Big Brother, Kwakeli Kanumba alituangusha sana kwenye kuongea kiingereza, yaani hadi aibu, Kila swali aliloulizwa na Big Brother yeye anajifanya ajasikia vizuri, na mbaya zaidi hata kusema rudia swali hawezi, yeye ni ehe!, na alikuwa anacheka tu hata pasipo na sababu ya kucheka

    Tarehe Mon Sep 07, 04:13:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    ngonolists......poa wakamue sana haooo...watamu saaana

    Tarehe Mon Sep 07, 04:26:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    msimu wa kuonesha nyuchi unawadia

    Tarehe Mon Sep 07, 04:28:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    mdau sijakusoma vizuri hapo ,,inamaana hizo picha umepiga kwenye tv yako leo hii????
    inamaa jamaa toka jana hajabaddilisha nguo???

    unamaanisha nini unaposema anatesa wakati haongei kitu chochote cha maana,,
    english kwake ni tatizo kubwa ,,alipoitwa na Big brother ktk diary room alikuwa anajiuma sana ,mpaka mamam wa watu anacheka a,aibu tupu kujionyesha mbele ya watu eti huyo kaendas kutuwakilishia ma celebrity wa bongo ,kwa kweli kama uliangalia jana the show utakubaliana na mimi lakini kama wewe ni shabiki tu wa kawaida ilimradi umeona kuwa jamaa kaonekana the all afreica na duniani basi ur right ,
    kama mtu hajui nini anaulizwa kwa just a simle english anajing;ata ng'ata tu ,kwa kweli nilijisikia aibu sana ,na ikabidi nibadilishe channel kila inapofika zamu yake kuongea especial kwenye dinner table pale ,
    folk kushika mzozoz ,jamani jamani
    GOD BLESS TANZANIA GOD BLESS TOLLYWOOD ARTISTS

    MDAU

    awadhi
    DAR

    Tarehe Mon Sep 07, 04:58:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Jamani kwa yaliyotokea jana kwa Kanumba kushindwa hata kuelewa maswali ya kiingereza, ni bora tuwachukue tu hao vijana/mabinti wa Masaki, Oysterbay bin Mbezi Beach kama sio Upanga. Duuuuhhh...!!! That aibu, I don't wish kuipata as Mtanzania anymore. Ya jana inatosha...!!!

    Tusilete u-mkoa hapa, leteni watu wanajua ngeli, wana-exposure ya kutosha, that's what we need kwa mwakilishi wa nchi yetu kwenye BBA. Hakuna Taasisi ya Kiswahili kule, huwezi ongea lugha yako mle ndani, you have to be an entertainer, watu hawaangalii sura au umetoka wapi, wanaangalia how you entertain them na hata IQ + exposure yako. Sasa unamtoa mtu kama Kanumba ambaye even a single word like "strategy" linampa shida na kuishia kudai kuwa ni complex word...!!!...!! Then ndio ulete mtu katoka huko Bush anajua kilugha chao na kiswahili, kiingereza cha kuunga....!!!

    Let's be realistic..!!!

    Tarehe Mon Sep 07, 05:33:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Kaka michuzi kweli hii inaonesha ni jinsi gani watanzania tu wavivu wa fikira; lugha yetu ya Taifa ni kiswahili kwa hiyo kanumba kutokujua kingereza sio ishu.huu ni wivu tu kwani mataifa mangapi raia wake hawajui kingereza na wanawasiliana na ulimwengu pia wanafanya biashara kubwa na kingereza chao cha kuchechemea? Mfano wachina, wahindi n.k. Kwani walemavu(bubu) mbona huwasiliana na mwisho wa siku watu huelewana? Mi naona cha msingi ni kuelewana mwisho wa siku.Mtu anayemponda Kanumba naye wawezakukuta kingereza kinamgonga.Big up Kanumba.

    Tarehe Mon Sep 07, 06:23:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Watu wengine bwana eti Kanumba hajui kiingereza! kwani kiingereza si ni lugha tu ya kawaida kama kilivyo kichina,kijita, kihaya, kigogo n.k hahahahaaaaaaaaa! Utumwa wa akili kweli kazi

    Tarehe Mon Sep 07, 06:46:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    si mpenzi sana wa mambo hayo...lakin watanzania tuache majungu jamaa...kiingereza ni lkugha tu...si kitu cha ajbu...tumcheke kama hajui kiswahili ...sio cha watu....jaman tupende vya kwetu....mi nipo huku nabeba box...hakuna mtu bora na vitu bora kuliko vya kwetu jamaa ..tusishobeke.....ANELKA mcheza mpira yupo uk toka an miak 17 mpaka sasa ana 31..bado anjiumauma sembuese kanumba...tuache uzembe...tusiongee ili tufurahishe baraza...tuchangie ya maana tujenge jamaa....WANGU MTAZAMO TU WAOSHA VINYWA MSIJENGE CHUKI

    Tarehe Mon Sep 07, 06:51:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    jamani mambo mengine ni bora kuelimishana, sasa kama mtu kachemsha au amekosea asiambiwe? Kanumba kweli lugha mzozo, na sio mtu mzima hivyo, yeye ni yankee, yani kijana mdogo anaakiwa kujua international languages hasa kiingereza. Na hatuwezi kufananisha kiswahili na kichina au sijui kijapani, wenzetu wameendelea sana na hata wana-program vitu vyao kwenye lugha yao, wabongo bado sana, na mpaka kufikia huko sijui miaka mingapi ijayo

    Tarehe Mon Sep 07, 07:05:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Jamani huyu kanumba kama ni celebrity kama anavyojiita basi at least ajifunze lugha, halafu awe na uelewa wa mambo ambayo ni basic. Hata kama akijibu swali basi ajibu sahihi hata kama kiingereza ni kibovu. yaani jana niliboreka mpaka basi, kwa kifupi niliona aibu sana, nilikuwa na washkaji wawili wakenya na mmoja mganda na mwingine mnamibia, nilijiona mimi m-tz ndo naabika na wala si kanumba. sasa nashindwa kuelewa kama alikuwa haelewi kabisa kingereza au alikuwa hajui cha kujibu? mi namshauri kanumba na wenzake wakina kigosi watumie nafasi waliyonayo kujiendeleza kidogo at least wasiwe wanatuaibisha kila siku. Ni hayo tu kaka michuzi na wadau wengine hapo juu.

    Tarehe Mon Sep 07, 07:24:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    ujanja wa kanumba ni kuigiza kwa lugha ya kiswahili tu nasio kuongea kingereza.

    bwana unatutia aibu Watanzania

    Tarehe Mon Sep 07, 07:31:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    kwa anaye mtetea Kanumba kuhusu kuto kujua kingereza ni mjinga. Kama msanii nilazima aweze kuwa na kingereza hata cha kuombea maji na kama aelewi mtu anaposema kitu sio kucheka, anatakiwa kuuliza.

    kama kwe kanumba anataka kwenda Hollywood basi anatakiwa ku-rise his game in language ili Director and other crew member wa mwelewe anapo pewa maagizo ya nini cha kufanya.

    so Kanumba nenda English couse pale St ann Kimara.

    Tarehe Mon Sep 07, 09:07:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Mkuu Michu hebu tuwekee hiyo clip ya kijana wetu, kiingereza si lazima lakini kama ndio lugha inayotumika basi hao waliompeleka wangetuma na mkalimani!

    Tarehe Mon Sep 07, 09:28:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Hamna utumwa wa akili,kutokujua kiingereza si kosa ila ya nini kwenda kurepresent TZ wakati hujui lugha ya mawasiliano uendapo.Tena kanumba is innocent yeye alitaka kuonekana tu huko blame it on wahusika waloruhusu aende

    Tarehe Mon Sep 07, 10:10:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    sikupata nafasi ya kuangalia nini kiliendelea coz niko nje ya nchi ila kutokana na majority ya comments zilizo tolewa inaonyesha ni jinsi gani Tanzania tumeaibika sasa kama hajui lugha mbona kwenye movie wanajianya wanakiongea sana kiingereza ?
    simpondi kwasababu hakuna mtu anajua kilakitu lakini nashauri awe kama yeye kama movie ni ya kingereza aongee kingereza na kama niya kiswahili aongee kiswahili..

    Tarehe Mon Sep 07, 11:06:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Jamani mbona wa TZ hamjiamini? kwani Inglishi ni nini?
    Kwa mtu kama Kanumba aliye soma Jitegee or sijui Makongo kwa ujielezaji alio jieleza juzi ni kajitahidi sana , kwakweli nampa hongera sana ka kusingatia Inglish ni lugha ya pili na hajasoma hivyo viji accademy vyenu.
    Kujua KIngereza kama second language ni kitu kiumu haswa unapo sima lugha ukiwa ume shapita miaka 15 , ina bidi uwe mdadisi zaidi ili uweze kuimaster lugha mpya .
    Wengi wetu hatuwezi kuwa fluent in Inglish sababu shule tulizo soma tume soma Kingereza tukiwa akubwa , pale tunapo ingia secondari, Elimu ya Msingi kwa kingereza peke ni ngumu sana kuweza ku ongea lugha iyo, wengi tuna uwezo mkubwa wa kuisikia ila kuiongea ni ngumu.

    Nashnidwa kuwaelewa kanini mnaona ni jambo la aibu kutojua Kingereza , mbona Mshiriki wa Angola alikuwa ana vunja kiingereza vibaya sana na Mbaka Richard alikuwa ana mcheka live ,lakini hatukusema kitu .

    Hongera kanumba , wewe ni a victim wa mfumo wa elimu wa Tanzania , sio kosa lako.

    Tarehe Mon Sep 07, 11:15:00 PM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Tuwache masihara english ni muhimu,fikilia kama ungekuwa wewe ndio umo ndani ya jumba lile ungejisikiaje?kama tuna lugha yetu ya kiswahili kila nchi inalunga yake!!Mizengo yuko Korea kuomba Michuzi anaongea Kiswahili kule?Eti ni lugha kama lugha nyingine what?????

  • Tarehe Tue Sep 08, 12:16:00 AM, Mtoa Maoni:
    anon16-rounded.gif
    Anonymous

    Nyie anoni wa sept7, 5:33PM na 6:23PM hamna tofauti na huyo Kanumba wenu, tumuonee wivu kwa kitu gani alichonacho, acheni ujinga na ubabaishaji hapa. Issue pekee sio lugha kwa Kanumba ni upeo wake wa kuelewa mambo pia ni mbovu, hana idea na lolote, jamaa has no clue na hata mambo ya kawaida tu yaani yupo kwenye giza, sasa nyie mnaosema eti asiambiwe ni wivu what exactly is your point here, wivu na mtu hata general knowledge tu hana wapi na wapi bwana, acheni tabia ya kuwapamba hawa mastaa wa bongo ni kuwajaza ujinga, wanabidi wafanye kazi kweli kweli, na huyo mwingine hapo juu anaedai eti TZ lugha yetu si English kwa hiyo watu waridhike ridhike tu nakuonea huruma na wewe, ni juzi tu nilitoa comment kuhusu topic ya Ray na blog yake kuwa wasanii wa bongo bado wanahitaji lugha ya kiingereza ili ku exhale kwenye mambo yao ya usanii, watu wakaponda, leo angalieni aibu anayowapa huyo kanumba wenu, ndio haya mambo yanayozungumziwa kila siku na nyie kazi yenu kutetea ujinga, it's an embarassment to TZ na hatutaki kutiwa aibu na watu kama kina kanumba eti kwa kuwa ni mastaa wakati kuna watu wenye better profile hapo hapo bongo.
    -Mdau Mnoko.
http://issamichuzi.blogspot.com/2009/09/kanumba-atesa-big-brother-africa-iv.html#comments
 
Kanumba.jpg

mm_spacer.gif

Biography.gif

Steven Charles Kanumba is my name, i was born in a Christian family of 2 girls and i happen to be the last born and the only boy to Mr. & Mrs. Charles Meshark Kanumba. I was given birth on january 8th 1984. I originate from Shinyanga region in Tanzania. I am Sukuma by Tribe. I completed my Primary Education in Bugoyi Primary School in Shinyanga. After Completing my primary education i started my secondary education right away in Mwadui Seminary Secondary School in shinyanga where by i shifted to Dar-es-salaam Christian Seminary Secondary school here in Dar-es-salaam when i was still in form II and complete my O-Level Education there. Thereafter i moved to Jitegemee Sec. School to complete my A. Level Education.
Growing up, acting has always been something that i really liked to do. Apart from that i also liked singing and that made me grave to be an artist while i was still in teens, still in school ie. i started acting in church a lot of people told me i had a talent so i decided to join Kaole Sanaa Group which delt with Acting. After joining Kaole Sanaa Group i met different Teachers from Bagamoyo and other College who helped me to build up my career of Acting for a period of 1 year, after that i got a special Training from University of Dar es salaam Under Doctor Nyoni for about 3 months therefore i was sure to go to work and indulge myself in Soap Operas/Series. i then took acting as my career. Little by little i got to win peoples' attention which made me work even harder and become successful.
After all the hard work that i kept in series i decided to play a part in movies so i took a step forward and associate myself in film industry. i happen to do a lot of movies that did very well in the market and i'm still doing movies up today and it just get better day by day. in addition to this i archieved a lot through my hard work that is prestigious awards, travel across different countries, working with people from different part of the world meeting different people and learn new things and experiencing different life.
I also got to get to work with Nollywood in Nigeria where by i did more than five movies with famous actors from Nolllywood, it was the wonderfull experience. I also got a chance to Visit The United States of America and there is where i got the experience of a lifetime i got visit Hollywood, Warner Bros Pictures, Universal Studios and Disney Land, i learnt a lot i met people who work there so i got to ask alot of Quaestions and gained a lot of knowledge.
Speaking about me as Steven Kanumba i'm a very down to earthguy i like hanging out with my friends and i like to associates myself with people, i love children with all my life, i'm just a simple guy, i'm not outgoing a lot, i love going to movies and just be chilled out and relaxed places. I'm not married for the time being but i am in a commitment in the name of God i hope that one day we will get married.
I would like to end with my most sincerly appreciation, first and foremost i would like to thank God Almighty for giving and Blessing me a beautiful talent cause apart from acting being my Job, it also happen to be something i love doing and when i am at it i do it with passion. I would also like to thank my whole family but special appreciation goes to the most beautiful woman in the whole world that happened to be my mother (I Love you Mom) would also like to thank Game 1st Quality Tanzania Limited and again special thank to my brother, my executive Producer and my Advicer Mr. Mtitu G. Game and His Wife. I Would like to thank all the Artist, Producers and Directors i have worked with. Also my special Thanks to my sister Sharifa Kalala in USA and Sanura Hussein in Denmark. Most Importantly, i would lastly like to thank all my fans from different part of the world, thank you all very much for supporting me, I LOVE YOU all and God bless you.​

signature.gif



................................


Steven Kanumba.

http://www.kanumba.com/Biography.html
 
Wasukuma na Kiingereza chao wakati mwingine kinafurahisha. Unakuta Ngosha anasema "I am comingi furom Jamayika". Kali ni yule alikuwa alienda Urusi pale kusoma na siku moja akiwa anataka kuwasha jiko la Gesi, akaona dada wa Kizambia akitaka kuzima jiko, ngosha akaruka "Don't put it off, i'm cooking ON HIM".

Wanaongeaga lugha ya Taifa na kukandamizaga maneno vile wanavyoongeaga. Kiingereza ni mashokolo mageni kwa watanzania. Hatuongeagi mara kwa mara,sisi tunaongeaga inapotubidi tu.
 
Kiingereza sio our mother tongue, tangu tunazaliwa tunazungumza kama si lugha ya baba na mama, basi ni kiswahili kwa kwenda mbele. Hapa ni vyema waandaaji wakaangalia vyema vigezo vyao vya mwakilishi katika shindano hilo, ila kwa ninavyowafahamu wabongo atagangamala mpaka kitaeleweka tuu.

Mkuu hii excuse ni outdated!!?
Hatuwezi kutumia sababu hii kila mara, kwani yule Methiopia mbona anaongea kiingereza kizuri tu wakati hata shuleni Ethiopia wanasoma kwa Ki-Amaharikh??
Kanumba anashindwa kuconverse na wenzake badala yake anabakia akicheka na kujifanya yuko curious kuangalia vitu?? Too bad!!

Kigezo kilichotumika kumpata Kanumba sina uhakika kilizingatia nini, enewei we can just relax and see the others fight cos m sure huyu mtu wetu ni nothing...
 
Mkuu kama umeenda shule ya kimagharibi, basi shule haikukaa, ulifaulu tu upate cheti.

Kama huajenda hiyo shule wala sioni ajabu.

Hata kama ni show ya kuchekesha lazima ueleweke unaongea nini. Wakati wenzake wanaongea maneno ya kawaida yeye anacheka, akiulizwa maswali anasema YOUR WORDS IS DIFFICULT.

Ndugu yangu ni aibu. Labda wewe tu huoni ila kwenye kila shemu bongo jana ni gumzo.

Ukiwa hujui kuongea kiingereza kuanzia jana unaitwa KANUMBA.

Kama kafanikiwa na shule hana, na wewe umeenda shule, umeshindwa nini kumshauri ajifunze kiingereza? ni muhimu sana kwa kazi yake ndugu yangu.

Tatizo lako ni kudharau watu, wewe unaelimu gani ya kujidai nayo? Wewe unaelimu gani mpaka kunidharau hivyo? Ni taarifa yako shule ninayo, tena ya juu sana. Zungumza mengine siyo hizi pumba zako juu yangu, wala hunijui. Yaani suala la Kanumba liwe kipimo cha elimu ya mtu bwa ha ha ha...

Kuhusu Kanumba, yeye amefanya kwa sehemu yake. Acheni kujifanya msivyo, kingereza cha Watanzania wengi ni kibovu mno na kunasababu ya hilo. Ndo maana BBA wanaenda half-castes (Mwisho, Richard, Lutoya).

Kwani mmejua leo kuwa Kanumba anakingereza kibovu? mbona website yake: www.kanumba.com inakingereza kibovu sana (mfano: 'movies i've wrote') sasa si mngeanza kumsahihisha hapa?

Mimi nilichokuwa nimeongea ni juu ya ustaa wake na mchango wake ktk sanaa ya maigizo nchini kwetu. Nchi za wenzetu wala hawahangaiki na kingereza kizuri. Nimetembelea nchi mbalimbali za Ulaya mashariki na Asia nimejionea mwenyewe english inavyowapiga. Lakini wanaongea hivyohivyo na maendeleo yao ni makubwa. Wanatumia lugha zao na english ni second language kama sisi.

Napenda mtu tunae tofautiana huku tukiendelea kuheshimiana siyo kudharauliana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom