Kanisa nililosali jana na changamoto zake

Mie hivi vyeo vyao tu ndo naishiwa hamu kabisaaaaaaaaa! Kuna mshikaji alikuwa mwalimu wa kwaya tu huku na kule akapelekwa marekani miezi 3 kurudi nasikia anaitwa APOSTLE mweh!

ni neno la kawaida tu ambalo hata mtu asiyeenda shule anaweza kulielewa...na ni upungufu wa kusoma na kuielewa Bible kuhusu categories za watumishi wa Mungu kulingana na vipawa ambavyo Mungu amewachagua/tuma...ukielewa hivyo, utaelewa ni kwanini huyo unayemdharau anaitwa apostle...unaonekana kama una allergy na maandishi ya Bible mkuu....
 
Tufuateni biblia wala sio wahubiri kama hawa, weeengi watamwita Bwana! Bwana! Naye atawaambia ondokeni siwajui! Huyo atakua Tapeli. Afadhali aanzishe bendi ya mndundiko!!!!
 
Jana nilienda kusali kwenye kanisa moja mitaa ya kati.
Huko mhubiri alikuwa bize kuuponda mchezo wa soka kuwa ni wa kishetani uliotawaliwa na uongo na hila.
Akasema mchezaji anapompiga chenga mwenzake anakuwa amedanganya, maana anakuwa anamdanganya kuwa anaenda kulia wakati anaenda kushoto.
Akaendelea kusema wanapoangushana na kuchezeana faulo wanakuwa wanavunja amani na wanafanya uadui.
Pia akasema wachezaji wanapojiangusha kutafuta penalt wanasema uongo.
Akatoa kali zaidi kwa kusema fifa na kombe vya dunia viliundwa na shetani mwenyewe na akavileta duniani ili kuwapofusha watu.
Watu wawe busy na mpira na kumsahau mungu.
Akawashauri waumini wake waache kabisa kufuatilia michuano ya kombe la dunia inayoendelea afrika ya kusini.

najaribu lakini sipati picha huyu mchungaji alikuwa anaongea na watu wa namna gani? maana kuna mahali pengine watu wangetoka nje na unamaliza mahubili huoni mtu.
 
Nilikiona cha mtema kuni

Ungeinuka tu katikati ya mahubiri yake na kuondoka....ungempa nafasi ya kukuchambua inaelekea nimemgusa huyu jamaa sijui yeye ni mchezaji au mpenzi tu? lol! na maneno mengine chugu nzima....kwani hata kama tunafuata neno la Mungu haturuhusiwi kuwa na furaha hata kidogo kwa kuangalia vitu vile tunavyovipenda hasa kama kufanya hivyo hatukiuki neno la Mungu!? Hawa wahubiri wengine ndiyo wanakuwa sababu ya waumini kutohudhuria kwenye nyumba za ibada.
 
Humu makanisani kuna vituko sana.
Mitaa ya sinza shule ya Mapambano, kuna kisehemu walikuwa wanauza bia na kitioto, wakaja Wakenya, wamepanunua na kuweka chuo cha Biblia.
Wanasoma muda mfupi tu, kisha wanapewa vyeo mbalimbali.
Sifa za kujiunga na chuo hicho ujue kusoma na kuandika..
Kwa mradi huu hawa watumishi wenye ufinyu wa fikra hawataisha kamwe
Ungeinuka tu katikati ya mahubiri yake na kuondoka....ungempa nafasi ya kukuchambua inaelekea nimemgusa huyu jamaa sijui yeye ni mchezaji au mpenzi tu? lol! na maneno mengine chugu nzima....kwani hata kama tunafuata neno la Mungu haturuhusiwi kuwa na furaha hata kidogo kwa kuangalia vitu vile tunavyovipenda hasa kama kufanya hivyo hatukiuki neno la Mungu!? Hawa wahubiri wengine ndiyo wanakuwa sababu ya waumini kutohudhuria kwenye nyumba za ibada.
 
Vp mzee, bado unaendelea kwenda kanisa hilo au ndy umeshakacha?
Unatakiwa umsaidie huyo mchungaji, endelea kwenda kanisani kisha utafute muda umhubirie aokoke........kwani inaonekana kashadanganywa na shetani na kufuata miungu ya uwongo! MUNGU ANA MAKUSUDI YAKE KUKUPELEKA KTK KANISSA HILO.........MRUDISHE KUNDINI HUYO PASTA!!
 
kweli ya Mungu haitoki kwa mchungaji, bali i ndani ya Biblia tu
shetani pia hutumia watu kupotosha kweli ya Mungu
katika hili haijarishi wewe ni nani, hata ukiwa mchungaji usiye jua
hila na njia za mwovu ibilisi, utatumika tu, maana yeye hucheza na fahamu
za watu ili kuwapotosha na kweli ya Mungu,
 
Hii huduma ya kiroho naona imeingiliwa na mdudu sasa ndio mafundisho gani haya? Dini imekuwa biashara siku hizi, haya yetu macho...!!!
Wachunga kondoo wa mungu nendeni darasani kidogo mpate kujua nini cha kuhubiri na nini si cha kuhubiri sio mnakaa kutudanganya tu na hadithi zenu za kutunga. Dini na mpira vinahusiana nini kama si kudanganyana tu.. GO WORLD CUP..raha jipe mwenyewe tutatubu siku ikifika!!
 
Jana nilienda kusali kwenye kanisa moja mitaa ya kati.
Huko mhubiri alikuwa bize kuuponda mchezo wa soka kuwa ni wa kishetani uliotawaliwa na uongo na hila.
Akasema mchezaji anapompiga chenga mwenzake anakuwa amedanganya, maana anakuwa anamdanganya kuwa anaenda kulia wakati anaenda kushoto.
Akaendelea kusema wanapoangushana na kuchezeana faulo wanakuwa wanavunja amani na wanafanya uadui.
Pia akasema wachezaji wanapojiangusha kutafuta penalt wanasema uongo.
Akatoa kali zaidi kwa kusema fifa na kombe vya dunia viliundwa na shetani mwenyewe na akavileta duniani ili kuwapofusha watu.
Watu wawe busy na mpira na kumsahau mungu.
Akawashauri waumini wake waache kabisa kufuatilia michuano ya kombe la dunia inayoendelea afrika ya kusini.

Bujix2, huyo mhubiri lazima ni wa kijijini, hajasoma na kama amesoma theology alifeli vibaya sana. Ningekuwa mimi ningetumia World Cup kuhubiri injili yangu badala ya kuiponda world cup. Nionavyo mimi amekaa mimaslahi zaidi anaono uchungu wa kiasi ambacho watu wanatoa kununua bia wakati wanaangalia mpira.Akumbuke kuwa waumini wake wana matatizo mengi sana ambay hayatokani na chenga za world cup, wala kujiangusha kwa wachezaji au faulo za wachezaji Mpira unachezwa dakika tisini tu, hivyo kama kumsahahu mungu watu wanansahau kwa dakika tisini katika 1440 za siku. Akumbuke kuwa World cup inachezwa mara moja kwa miaka 4, hivyo miaka mitatu na miezi 12 ambapo hakuna world cup watu wanamkumbuka mungu sana.alitakiwa ajue kuwa tatizo kubwa ni viongozi wa nchi hao ndio mashetani wakubwa ambao wanadanganya, wanaua kwa kutopeleka dawa hospitali wakati hela zipo, kwa kusaini mikataba mibovu etc. Muumini mwenye njaa hata siku moja hawezi kumkumbuka mungu.
 
Nadhani hukuangalia sawasawa katika kuta za kanisa hilo, naamini kabisa kuwa kuna maandishi yanayosema..UYAONAYO NA KUYASIKIA HUMU YAACHE HUMUHUMU..!!!
 
Back
Top Bottom