Kanisa laanzisha hifadhi ya wanyamapori

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
43
KANISA la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mkoa wa Mbeya, limeanzisha mradi wa hifadhi ya wanyamapori kwa ajili ya kuendeleza sekta ya utalii nchini.


Mchungaji wa kanisa hilo, Markus Lehner ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Chuo cha Ufundi Mbalizi alisema mradi huo upo katika hatua za mwisho kukamilika.


Alisema kanisa lao limeamua kuuendeleza utalii mkoani hapa kutokana na sekta hiyo kuonekana kuwa na manufaa makubwa kwa taifa
.....Endelea http://mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=6702

Wadau hii imekaaje? Kwenye Secular Government yetu yakubalika Hii?
 
Huo ni wizi mwengine na ufisadi ukiwa na sura na rangi ya aina yake ,vipi kama mambu hayo yangeanzishwa na msikiti au kutumika jina la madhehebu ya Kiislamu hivi ingekuwaje na katiba nayo ingeongezea vipi ? Na mapadire na makasisi nao wangechoma nini ?
 
Kuanzisha hifadhi za wanyama au mazingira hakuna maana kuwa taasisi binafsi au za kidini zisijihusishe na shughuli za uzalishaji mali.

Infact kama kuna jambo ambalo jumuiya ya Kikristo duniani kupitia makanisa inalifanya sasa hivi ni kujishirikisha katika uzalishaji mali ili kuinua ubora wa binadamu.

Utalii ni chimbuko la mapato, kama eneo hili ambalo kanisa inamiliki litashamiri, basi huduma za maendeleo kwa jamii kama Shule, Hospitali, maji, na mengineyo yatapatikana kwa urahisi kwa kutumia mtaji unaotokana na mapato ya uzalishaji mali na si kusubiri misaada au sadaka.

Soma Times magazine kuhusiana na Mchungaji Rick Warren anachojaribu kukifanya kuboresha maisha ya binadamu. Soma makala ya Bill Gates ya Creative Capitalism, ugundue ni vipi wenzetu wanapiga hatua na kuachana na kutegemea Serikali.

Falsa ya Kanisa kujiingiza katika huduma za jamii na hata biashara, si kujipataia fedha bali ni kutoa huduma na kushirikisha jamii.

Hii nguzo yake ni ile hotuba ya Yesu maarufu kama sermon on the mountain ambapo aliuliza nilikuwa mgonjwa, ukanitibu, nilikuwa na njaa, ukanilisha, nilikuwa uchi ukanivisha nguo, nilikuwa sina pa kulala ukanipa pango n.k.
 
Huo ni wizi mwengine na ufisadi ukiwa na sura na rangi ya aina yake ,vipi kama mambu hayo yangeanzishwa na msikiti au kutumika jina la madhehebu ya Kiislamu hivi ingekuwaje na katiba nayo ingeongezea vipi ? Na mapadire na makasisi nao wangechoma nini ?

There is nothing wrong with a religious institution to participate in social and community services. The problem arises when there is discrimination and unfairness!
 
Chuma,Rev.Kishoka,Mwiba,

..hiyo article haiku clear. inavyoelekea mradi wanaouzungumzia ni wa ZOO.

..nadhani tumezoea kuona kanisa na taasisi nyingine za dini zikitoa huduma tu, badala kuwa washiriki ktk miradi ya uzalishaji na uchumi.

..Taasisi za kidini Afrika inabidi zitafute mbinu za kuweza kujitegemea. muda si mrefu misaada toka kwa wakubwa itakoma. kwa mfano Kanisa Katoliki USA lina wakati mgumu sana kifedha kutokana na mambo machafu yaliyokuwa yakifanywa na mapadri.
 
Back
Top Bottom