Kanisa la matapeli, Mlima wa Matumaini

Nawashukuru wote walionipa mawazo mazuri sana. Kwa Pdidy na drphone nasikitika kuona mnaanza kunishutumu bila kuniuliza zaidi. Mimi ninaishi ughaibuni kwa miaka mingi (zaidi ya ishirini), lakini kila mwaka ninakuja Tnazania mara mbili au tatu, kwa hiyo siyo kweli kuwa sijui thamani ya pesa na siwasaidii wazazi. Na baba mzazi ni mdhaifu, kila mwaka ninamchukua anakuja kutibiwa ughaibuni na kumrudisha. Hata mwaka jana alikuwa huku. Kinachosikitsha tu ni hicho cha kuuza nyumba na kutaka kuuza ya pili. Zile milioni moja na laki saba zilizotolewa kanisani, zilitokana na mzigo niliotuma mimi, wao wakaupokea na kuuza kwa milioni kumi na saba. Wakanijulisha wenyewe (mama) kuwa wameuza na wamepata milioni kumi na saba, wamechukua milioni moja na laki saba wamepeleka kanisani. Wakati mimi nilitaka wakiuza, waweke pesa bank, ili ziweze kutumika kununua dawa za baba, na zingine iwe nauli yao wakija huku kutibiwa nisiwe na lazima ya kutuma pesa za nauli. Hakuna neno kubwa kwani zilizobaki niliambiwa ziliwekwa bank. Kasheshe ikaja wakati miezi michache baada ya hapo naombwa nitume laki tatu za dawa!!!!

Nimeshaanza kulishughulikia kutokana na ushauri mzuri niliopewa na wanajamvi wengine wengi. Ninatanguliza shukrani zangu za dhati. Safari hii nitajizatiti mpaka kieleweke. Kwa wale wasiotaka kuamini kuwa kuna watu wanaotumia dini kuwalaghai wazee, msishangae hata ninyi yakiwafika!

pole sana mkuu atujakushutumu bali tumejibu kutokana na maelezo yako maana ata mm naishi mbali na familia na mzazi wangu afanyi jambo lolote achilia mbali kama hlo la kuuza nyumba bila ya kutushirikisha kabisa wote na huu ni utamaduni wa wazazi wengi wenye watt pole kama majb yangu yalikukwaza ila na mm nilikwazika pia na kichwa cha habari na maelezo yako yasiyokamilika maana unahisi kama mtumishi wa mungu ni tapeli lakini unauhakika na mahakama pekee ndio inamtia mtu hatiani si mtetei hapana bali hili naongelea kwa yyote tuwaheshimu watumishi wa mungu naamanisha wote wa kikristo na wakiislam.
kama uliwapa wazazi wako wauze bidhaa ya 17m hyo walopeleka linaitwa fungu la kumi wenye ufahamu wanaelewa kwamba kila sehemu ya kumi ya kipato chako si chako ni cha mungu
 
kuna mama anasali EFATHA alipewa mtaji na mtoto wake wa duka sh 5m basi kabla ya duka kuanza kuzalisha akapeleka laki 5 eti fungu la kumi kwa mwingira!jamaa ana lalama mpaka leo hana hamu na dini hizi za unyonyaji
 
Tatizo liko hapa; Fungu la Kumi, hii ni Zaka kwa mujibu wa mafundisho ya misahafu. Jambo ambalo wachungaji hawawaelimishi waumini wao; (inawezekana wanaacha makusudu), zaka haitolewi kwenye mtaji bali ni kwenye faida baada ya kuondoa gharama. Waumini wengi huishia kumaliza mitaji yao na kubakia masikini lakini baadhi yao; baada ya kuona staili ya maisha ya wachungaji, huamua kuacha kutoa na wakati mwingine kuhama makanisa.

Sina hakika kama kuna msaada wowote wa kisheria katika hili, na kwa vile linahusu imani za watu, serikali yetu haitapenda kuonekana inaingilia masuala ya dini.
 
Nawashukuru wote walionipa mawazo mazuri sana. Kwa Pdidy na drphone nasikitika kuona mnaanza kunishutumu bila kuniuliza zaidi. Mimi ninaishi ughaibuni kwa miaka mingi (zaidi ya ishirini), lakini kila mwaka ninakuja Tnazania mara mbili au tatu, kwa hiyo siyo kweli kuwa sijui thamani ya pesa na siwasaidii wazazi. Na baba mzazi ni mdhaifu, kila mwaka ninamchukua anakuja kutibiwa ughaibuni na kumrudisha. Hata mwaka jana alikuwa huku. Kinachosikitsha tu ni hicho cha kuuza nyumba na kutaka kuuza ya pili. Zile milioni moja na laki saba zilizotolewa kanisani, zilitokana na mzigo niliotuma mimi, wao wakaupokea na kuuza kwa milioni kumi na saba. Wakanijulisha wenyewe (mama) kuwa wameuza na wamepata milioni kumi na saba, wamechukua milioni moja na laki saba wamepeleka kanisani. Wakati mimi nilitaka wakiuza, waweke pesa bank, ili ziweze kutumika kununua dawa za baba, na zingine iwe nauli yao wakija huku kutibiwa nisiwe na lazima ya kutuma pesa za nauli. Hakuna neno kubwa kwani zilizobaki niliambiwa ziliwekwa bank. Kasheshe ikaja wakati miezi michache baada ya hapo naombwa nitume laki tatu za dawa!!!!

Nimeshaanza kulishughulikia kutokana na ushauri mzuri niliopewa na wanajamvi wengine wengi. Ninatanguliza shukrani zangu za dhati. Safari hii nitajizatiti mpaka kieleweke. Kwa wale wasiotaka kuamini kuwa kuna watu wanaotumia dini kuwalaghai wazee, msishangae hata ninyi yakiwafika!

pole sana mkubwa,vipi una hati yoyote ya hizo nyumba? huna advocate unaemfahamu? nimekuelewa kuwa hela walizotoa kanisani sii zao kwa hivo hazipo kwenye fungu la kumi la wao kutoa manake sio jasho lao.naamini wachungaji wengi wanakipaji cha kupambaza watu na wengi wao wamenunua uchawi nigeria tena kama ni mkongo ndo usiseme kabsa.hawahubiri injili wanahubiri utajiri.OK kama unamfahamu advocate wasiliana nae mara moja kama anaweza kuweka caveat in case hiyo nyumba ni yako na kama hati ina jina lako, na pia unaweza kumwomba akamweka mpelelezi ambae ni polisi atakaejifanya muumini atawakamata tu na pia polisi huyo huyo atafuatilia hili kanisa na uhalali wa hao jamaa nahisi hawana kibali cha kukaa tanzania. yupom moja alishafungiwa Tabata ni mkenya anaitwa Peter Nyaga alipewa na mahakama hukumu ya nje miezi sita akakaidi akafungwa miezi 6.UKimwangalia ana jeuri kiburi na pia ana tatooo za kutisha mwili mzima...
 
@lokisa unapotoa ushauri soma maelezo vzuri hzo nyumba ni zawazazi wake ndomana alipohoji aliambiwa azikuhusu na mtume peter nyaga yupo anachapa injili je kuna swali la nyongeza
 
jamani toeni ushauri badala ya kumwaga chuki zenu mlizokuwa hamna pa kuzitolea! Inashangaza badala ya mtu kutoa ushauri wa maana wanaingiza mambo hata yasiyo ya msaada kwa OP, badala yake wanamwaga sumu ya chuki zao. Kiwi, be careful na michango ya uzi huu!
 
Pole ndgu KIWi, hiyo ni "KIWI YA MACHO" kwa wazazi wako kwa kutojua dini ya kweli. Makanisa yote ni ya kitapeli yanashirikiana na matapeli wa ndani na nje ya nchi. Mfano "DECI" nk. Msaada kwako; nielekeze kwa wazazi wako nikawafundishe juu ya dini ya kweli na mwenyeezimungu hakuzaa wala hakuzaliwa, hana mwanzo wala mwisho na anamiliki siku ya mwisho na maajabu ya mwzmungu ni huu usiku na mchana tulionao. Na si maajabu ya kichawi ya akina kakobe, mzee wa upako, kibwetere nk. Kwa msaada huo tutakunusuru wasiuze vitu zaidi.
 
Duh wakuu haya makanisa siku hizi yamekuwa biashara nzuri.mdogo wangu wa kiume amejiingiza kwenye kanisa moja nasikia kiongozi wake anajiita nabii/mtume anaishi maeneo ya Mianzini.Bwana mdogo akipokea mshahara anaukimbiza kwa nabii/mtume, rafiki zake wa karibu wakanitonya nikaaza kuchunguza kupitia kwa mke wake hadithi niliyoipata sikuamini masikio yangu.Hati ya kiwanja chao tayari ilikuwa mikononi mwa Nabii/Mtume vitu vingine vidogo vidogo sikushughulika navyo nikaamua kumvaa Nabii/Mtume alipona nimeshajua janja yake akanitishia atanifanyia maombi ya nguvu nife nikamwambia ata yeye atakufa bila kufanyiwa maombi ila lazima arejeshe hati kwa namna yoyote.

Hati ya kiwanja nikaichukua ikabidi kikao cha familia kikae kwa madhumuni ya kumwakoa bwana mdogo mikononi mwa matapeli wasiomjua Kristo achilia mbali Biblia yenyewe.
 
Mimi ni mtu wa karibu sana na hili kanisa na hawa wachungaji, naomba niweke wazi mambo yafuatayo;
1. Kanisa linaitwa Mlima wa Mabadiliko na SIO Mlima wa Matumaini.
2. Mtumishi Ni Apostle Mary Lutumba na Mumewe Papaa David or Jonas Lutumba ni Mchungaji hapo.
3. Kwa maelezo yako nahisi hao wazazi wako nawafahamu, kwa sababu hiyo hela ilipotolewa kanisani ilitangazwa na wazazi wako waliitoa kama fungu la kumi.
4. Kanisa sasa hivi limehamia Tua Ngoma, unashukia kituo kinaitwa Yatima karibu na ile waterpark mpya iliyofunguliwa maeneo ya Kigamboni/Tuangoma.
5. Kwa jinsi ninavyowajua hawa Wachungaji wawili hawana mtoto, kwa hilo la nyumba yenu kuuziwa mtoto wao ninalitilia shaka zaidi.
6. Mara nyingi kila mtu anapotoa hela kanisani kwa huyu mama, huwa anatangaza. Na wakati ule na hata sasa wanajenga kanisa kwa hiyo watu wamekuwa wanatoa sana tu. Na mimi sioni tatizo kwa hili kwa sababu Makanisa mengi tu huwa wanachangisha kwa ajili ya Ujenzi.
7. Kukata Mzizi wa fitina namba za hao wachungaji ni hizi hapa, wapigie simu, fanya appointment nao then shoot all that you want to ask.
Apostle Mary Lutumba +255 655 680122 or 0755 209727
Papaa David Lutumba 0718 680122
 
Nenda kawawekee court injuction sisi yalitutokea huko kwetu baba yetu alikuwa na nyumba yaani two in one mbele bar nyuma guest ya vyumba 35 wote tumesoma private wa kike na wakiuma hata enzi hizo wazazi walipokuwa hawajali sana elimu ya wasichana lakini akajibinda kutusomesha siku ya mwaka akaanza kuwa mzee wa ushauri wa hao walokole mmoja katoka malawi na mwingine MTZ akataka kusukuma mji wote majirani wakatutonya tukaenda mahakamani kwa sababu ni matrimonial property ilichukua mda ana kumalizika hadi kesi kumalizika alikuwa kesha badili nia kwani alizinduka ,wabaya hao ukiweza wababee fimbo kwneda kuwatisha unaenda immigration watakukomaa ( wanachofanya ni mind manupulation kama akina kakobe,mwingira,fenardus ,lwaktare na wengine wengi matapeli tuu hao
 
Mimi ni mtu wa karibu sana na hili kanisa na hawa wachungaji, naomba niweke wazi mambo yafuatayo;
1. Kanisa linaitwa Mlima wa Mabadiliko na SIO Mlima wa Matumaini.
2. Mtumishi Ni Apostle Mary Lutumba na Mumewe Papaa David or Jonas Lutumba ni Mchungaji hapo.
3. Kwa maelezo yako nahisi hao wazazi wako nawafahamu, kwa sababu hiyo hela ilipotolewa kanisani ilitangazwa na wazazi wako waliitoa kama fungu la kumi.
4. Kanisa sasa hivi limehamia Tua Ngoma, unashukia kituo kinaitwa Yatima karibu na ile waterpark mpya iliyofunguliwa maeneo ya Kigamboni/Tuangoma.
5. Kwa jinsi ninavyowajua hawa Wachungaji wawili hawana mtoto, kwa hilo la nyumba yenu kuuziwa mtoto wao ninalitilia shaka zaidi.
6. Mara nyingi kila mtu anapotoa hela kanisani kwa huyu mama, huwa anatangaza. Na wakati ule na hata sasa wanajenga kanisa kwa hiyo watu wamekuwa wanatoa sana tu. Na mimi sioni tatizo kwa hili kwa sababu Makanisa mengi tu huwa wanachangisha kwa ajili ya Ujenzi.
7. Kukata Mzizi wa fitina namba za hao wachungaji ni hizi hapa, wapigie simu, fanya appointment nao then shoot all that you want to ask.
Apostle Mary Lutumba +255 655 680122 or 0755 209727
Papaa David Lutumba 0718 680122

mmmmhh, sidhani tatizo la mtoa mada ni kwamba watu wasichangie makanisa. nadhani hapa, tatizo kubwa ni kwamba wachungaji wa kilokole ni matapeli. hudanganya waumini wajitolee kila kitu, including family property. kama kweli unakumbuka mama yake alitoa kiasi kikubwa hicho cha pesa na unajua kwamba nyumba iliuzwa. basi ukiri kuna mchezo uchafu ulifanyika, kwa jina la yesu!
 
stupid people speak language of generalization! Mara wachungaji wa kilokole matapeli mara makanisa yote ya kitapeli...phew! Mtamwaga chuki zenu zote leo. Hahaaaaah! Bwana kiwi namba ndio hizo, nafikiri ni vema ukaongea nao ujue ukweli wa mambo unayoyataka. Hapa kuna watu wamekuja kumwaga sumu za chuki, wana wa ibilisi!
 
kiwi umefikia wapi?umeongea na wachungaji?Nakushauri usiongee nao wewe mwenyewe,tafuta mpelelezi akaongee nao kwa karibu atakutumia report ya findings zake and what legal actions to take so to secure your family property from illegal sale etc.
naweza kukutumia number ya mtu who can do it for you.
 
Ndugu Pole sana, mimi nawafahamu hawa "manabii wa uongo" waliondikwa kwenye biblia. Nitakupatia mfano wa kweli. Mke wa mjomba wangu alianza kwenda kusali huko. Akawa brainwashed akaanza kuuza mali, mshahara wake wote akawa anapeleka huko. Baada akamushauri mjomba wangu naye akasali huko. Lakini yeye akakataa matokeo yake mama akadai talaka. Wakaachana, wakagawana mali (nusu bin nusu) lakini mbaya zaidi mama akakazania nyumba waliokuwa wamejenga nayo waiuze. (Walikuwa na watoto watatu) Nyumba akiuzwa, ajabu yule mama mali yote aliyogawana na mjomba wangu akapeleka yote kanisani. Sasa hivi anaishi kwenye chumba kimoja cha kupanga. Mjomba wangu naye anaishi nyumba ya kupanga amerudi nyuma hatua 100, ametafuta tena kiwanja anaanza kujenga upya na pia anasomesha watoto pekee yake amewapiga marufuku wasiende kwa mama yao wasije wakawa brainwashed. Bahati nzuri huku Tanzania hatuna custody kama USA.

Moral of the story. Kama kweli wazazi wako wanasari huko na wameshakuwa brainwashed I swear in the name of Jesus Christ watauza kila kitu kuanzia vidani, gari hata nyumba na mwisho watabaki mafukara wa kutupwa Mark my words.

Sometimes it is better to break some eggs to make an omlette. Fanya kila lilo katika uwezo wako hata ikibidi kukosana na wazazi wako BTW itakuwa temporaly uwatoe huko, vinginevyo finally itakuwa mzigo wako na wakati huo watakuwa hawana kitu kabisa hata glass ya kunywea maji. Itabidi uwatunze wewe.

Mimi siongei SIASA naongea ukweli kulingana na experience iliyompata mjomba wangu na mke wake. Unaweza kutochukua ushauri wangu lakini utanikumbuka siku moja wakati huo itakuwa TOO LATE.
 
kiwi umefikia wapi?umeongea na wachungaji?Nakushauri usiongee nao wewe mwenyewe,tafuta mpelelezi akaongee nao kwa karibu atakutumia report ya findings zake and what legal actions to take so to secure your family property from illegal sale etc.
naweza kukutumia number ya mtu who can do it for you.

I would also like to help. Mimi ni mwathirika wa hawa matapeli wanaotumia imani za dini kuibia waumini halafu wanatia familia na hata pengine ukoo kwenye umasikini na ugonvi. Hadi leo ninabeba mzigo wa watoto wa ndugu yangu baada ya Wanaijeria walioanzisha kanisa la Winners kumtapeli ndugu yangu nyumba wakati akiwa mgonjwa na kisha akafa. By then, ilikuwa mwaka 2002 na sikuwa na uwezo wa kufanya chochote lakini nina hasira nao kweli kweli.

Please PM me if you need any assistance
 
Back
Top Bottom