Utingo
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 10,270
- 8,031
kikwete ni gamba tu,
ajivue au tumvue?
kikwete ni gamba tu,
rais ana orodha yake mwaka wa tano huu,nafikiri anawaombea balaa kwa mungu.
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Pentecost Church (TEC) la mjini Mbeya, William Mwamalanga, amesema wanatarajia kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, kutaja hadharani orodha ya vigogo wanaoshiriki katika biashara ya dawa za kulevya.
Kauli ya mchungaji huyo imekuja siku moja baada ya Ofisi ya Rais (Ikulu) kuwataka maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kuacha kutoa saa 48 kwa Rais Jakaya Kikwete kutaja majina ya viongozi wanaouza dawa za kulevya bali yeyote anayejishuku ajisamilishe au atajwe.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mwamalanga alisema kundi la viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali wamepanga kukutana kwa ajili ya kutaja majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo.
Alisema wanatarajia kutaja majina yote, si ya viongozi wa dini ya Kikristo pekee, bali hata wale waliopo nje ya Ukristo, ambao taarifa zao zimefika hadi kwa Rais Kikwete.
"Si kwamba tutataja majina ya maaskofu na wachungaji pekee, bali tutataja hadi wale waliomo ndani ya Ofisi ya Rais, ambao wanafanya biashara hiyo, wabunge pamoja na mawaziri," alidai mchungaji huyo.
Alisema wana taarifa kamili ya viongozi wa dini ambao wanatumia makanisa kama vivuli na kujificha, kumbe wanaendesha biashara hiyo haramu inayoangamiza taifa.
Mchungaji Mwamalanga alisema lengo ya kutaja majina hayo hadharani ni kutaka kumsaidia Rais Kikwete na kuisafisha nchi iondokane na uingizaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya.
"Kwa sasa tupo Dodoma na leo tunatarajia kutaja majina hayo ambayo Rais Kikwete anashindwa kuyataja, ili kumsaidia …maana taarifa za orodha hiyo tuliwahi kumfikishia katika ofisi yake mwaka 2006," alisema.
Alisema viongozi wa dini wanaotumia makanisa kama vivuli huku wakiendesha biashara hiyo wanafahamika wazi, lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua.
Aliongeza kuwa wanategemea kuwa orodha hiyo ikiwekwa hadharani wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwachunguza.
Alibainisha kuwa kama vyombo vya dola vitapuuzia orodha hiyo watakayoitaja, kamwe mapambano dhidi ya dawa za kulevya hayawezi kuzaa matunda.
Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Rais Kikwete akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Killian katika sherehe ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo, kuwa askofu wa Jimbo la Mbinga, alikaririwa akisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya.
Kauli hiyo iliwafanya maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kumpa Rais Jakaya Kikwete saa 48 kuwataja kwa majina viongozi wa dini wanaojihusisha na dawa za kulevya.
Baada ya tamko hilo, juzi Ofisi ya Rais Ikulu iliwakosoa viongozi hao kwa kutoa tamko la kusikitisha, ambalo ililiita kuwa halikustahili kutolewa nao.
Ikulu iliweka bayana kuwa viongozi wa dini si malaika au watakatifu hapa duniani, kwani wanaweza kutumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa katika jamii.
Source: Tanzania Daima ya Leo
Kanisa kutoa orodha ya wauza ‘unga'
Jamani hebu tusaidia
Unajua mtu ukisoma kwa mara ya kwanza hii habari unajua TEC na CCT wamekaa na kuandaa haya.... ati kanisa kutoa orodha, ni bora wangesema kanisa la pentekoste mbeya kutoa orodha
i think it is an intentional move by the media to magnify bullshit na kuendelea kugombanisha wakristu na wanasiasa
sijui inatufikisha wapi hii fooking move
Mtamsaidiaje huyo mjinga hana maamzi hata siku moja ya ni mwanamke kwa lugha nyingine uanaume wake nipale anapokuwa amevaa nguo za kiume mimi sioni haja ya kulumbana au kutaja maana kila kitu anajua kama majina anayo anataka msaada wa nini?Mi JK ananishangaza sana................
Ile orodha ya waharibifu wa bandari anayo.......... lakini hajafanya kitu.......
Orodha ya wahusika wa mishahara hewa ................. anayo hajafanya kitu.............
Meremeta................ hata muwasulubishe hawafanyi kitu...................
Huyo askofu kasema orodha ya wauza unga unayo toka 2006............ hujafanya kitu..........
Mafisadi orodha unayo........................... umewashindwa..................
JK....... KUISHIA KUFAHAMU ORODHA TU HAKUTAKUSAIDIA KITU KATIKA HIZI HARAKATI ZA KUVUANA MAGAMBA.....................KWENYE HILI LA MADAWA MMENIKUMBUSHA AMINA CHIFUPA
Hpana sister,waache waendelee na harakati hizo,kwa kuwa kauli ya rais ina utata mkubwa sana!!mmmh tutasikia mengi..na nyie viongozi wa dini hebu fanyeni kazi ya mungu huko na mzidi kuwaombea kondoo wenu sio madawa madawa :shut-mouth:
na Betty Kangonga
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Pentecost Church (TEC) la mjini Mbeya, William Mwamalanga, amesema wanatarajia kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, kutaja hadharani orodha ya vigogo wanaoshiriki katika biashara ya dawa za kulevya.
Kauli ya mchungaji huyo imekuja siku moja baada ya Ofisi ya Rais (Ikulu) kuwataka maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kuacha kutoa saa 48 kwa Rais Jakaya Kikwete kutaja majina ya viongozi wanaouza dawa za kulevya bali yeyote anayejishuku ajisamilishe au atajwe.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mwamalanga alisema kundi la viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali wamepanga kukutana kwa ajili ya kutaja majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo.
Alisema wanatarajia kutaja majina yote, si ya viongozi wa dini ya Kikristo pekee, bali hata wale waliopo nje ya Ukristo, ambao taarifa zao zimefika hadi kwa Rais Kikwete.
Si kwamba tutataja majina ya maaskofu na wachungaji pekee, bali tutataja hadi wale waliomo ndani ya Ofisi ya Rais, ambao wanafanya biashara hiyo, wabunge pamoja na mawaziri, alidai mchungaji huyo.
Alisema wana taarifa kamili ya viongozi wa dini ambao wanatumia makanisa kama vivuli na kujificha, kumbe wanaendesha biashara hiyo haramu inayoangamiza taifa.
Mchungaji Mwamalanga alisema lengo ya kutaja majina hayo hadharani ni kutaka kumsaidia Rais Kikwete na kuisafisha nchi iondokane na uingizaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya.
Kwa sasa tupo Dodoma na leo tunatarajia kutaja majina hayo ambayo Rais Kikwete anashindwa kuyataja, ili kumsaidia maana taarifa za orodha hiyo tuliwahi kumfikishia katika ofisi yake mwaka 2006, alisema.
Alisema viongozi wa dini wanaotumia makanisa kama vivuli huku wakiendesha biashara hiyo wanafahamika wazi, lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua.
Aliongeza kuwa wanategemea kuwa orodha hiyo ikiwekwa hadharani wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwachunguza.
Alibainisha kuwa kama vyombo vya dola vitapuuzia orodha hiyo watakayoitaja, kamwe mapambano dhidi ya dawa za kulevya hayawezi kuzaa matunda.
Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Rais Kikwete akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Killian katika sherehe ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo, kuwa askofu wa Jimbo la Mbinga, alikaririwa akisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya.
Kauli hiyo iliwafanya maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kumpa Rais Jakaya Kikwete saa 48 kuwataja kwa majina viongozi wa dini wanaojihusisha na dawa za kulevya.
Baada ya tamko hilo, juzi Ofisi ya Rais Ikulu iliwakosoa viongozi hao kwa kutoa tamko la kusikitisha, ambalo ililiita kuwa halikustahili kutolewa nao.
Ikulu iliweka bayana kuwa viongozi wa dini si malaika au watakatifu hapa duniani, kwani wanaweza kutumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa katika jamii.
Source: Tanzania Daima.
Angalizo langu: Ni mpambano kati ya Kanisa na Rais. Nafuu itakuwa kwa sie walalahoi kwani wauza unga wanaiharibu jamii na kama ni watu wenye nguvu basi nafikiri mahakama ya umma inawatosha kuwahukumu. Nawapa hongera sana maaskofu kwa ujasiri wenu watajeni jamii iwahukumu!!!!
Waki mchifupa tutataka zaidi kikwete awataje! Si alishapewa orodha? Hapa anasaidiwa, wanaomsaidia wakichifupwa yeye ataisaidia polisi, maana wauaji lazima wawe toka hiyo orodha! Lakini subiri kidogo! Hivi kumbe Bongo hatuna polisi.. Mwena ni mkuu wa kitengo cha usalama cha ccm...Aangalie wasijewaka mchifupa kabla hajawataja