Kanisa Katoliki yaanzisha kampeni kupima ukimwi waumini wake Tanzania

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Na Mwandishi Wetu
KANISA Katoliki nchini limeanzisha kampeni ya kupima virusi vya ukimwi kwa waumini wake ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini alisema, kanisa limeamua kuanzisha mpango huo kwa malengo makuu matatu, kutokomeza ukimwi, kuondoa unyanyapaa na kuhamasisha upimaji afya kabla ya ndoa.

``Tunataka kutokomeza ukimwi miongoni mwa waumini wetu, pamoja na unyanyapaa na kuhamasisha hali ya upimaji wa afya kabla ya ndoa ili vijana wetu wasiingie kwenye hatari wanapofunga ndoa,” alisema Kilaini.

Alisema mpango huo wa kanisa umesambazwa katika majimbo yote ya Kanisa Katoliki na kwamba kila jimbo limeweka utaratibu wake wa kutekeleza maelekezo ya Baraza la Maaskofu kuhusu kutokomeza ukimwi.

``Hatutatumia mapadri na makatekista kupima virusi vya ukimwi, ila tutatumia wataalamu wetu chini ya mpango wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS in Dar es Salaam Archdiocese (Pasada), katika kupima na kutoa ushauri nasaha kwa waumini na wasio waumini kabla ya kupima,” alisema.

Askofu huyo alisema kuwa jimbo lake tayari kazi hiyo imeanza katika parokia tatu za Manzese, Sinza na Tandale pamoja na vituo vingine vya afya vinavyomilikiwa na kanisa.

Akifafanua jinsi kanisa hilo litakavyoendesha kampeni yake kwa mafanikio, Askofu Kilaini alisema, wataalamu kutoka Pasada wamekuwa wakipewa fursa katika makanisa baada ya misa/ibada kutumia muda huo kuwaelimisha waumini kuhusu umuhimu wa kupima afya zao.

``Hakuna muumini atakayelazimishwa kupima virusi vya ukimwi, ila tutatumia wataalamu ambao wataweza kuwashawishi waumini kupima afya zao na kujitambua; na kujua waishi maisha gani baada ya kupima na kufahamu kuhusu afya zao,” alisema Kilaini.

Aidha, askofu Kilaini alisema kuwa watakaokuwa wanawapima sio watu wanaowafahamu kwa maisha yao ya kila siku, na suala la kupima watakwenda siku ambayo wamejisikia kufanya hivyo.

”Tukitoka kanisani hatusemi haya sasa waumini nendeni mkapime, hapo sasa kinakuwa ni kitu binafsi, maana wanaopima sio mapadri,” alisema Kilaini.

Alisema mpango huo uliridihiwa na Baraza la Maaskofu kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Jimbo la Bukoba, ambalo limeufanya Mkoa wa Kagera kurudi nyuma katika takwimu za maambukizo ya ukimwi ukilinganisha na mikoa mingine, kwa kuwa wanaotaka kuoana wanalazimika kupima virusi vya ukimwi.

Askofu Kilaini alisema, mpango wa Jimbo la Dar es Salaam kuamua kuwatumia mapadre kulizungumzia suala la kupima VVU baada ya misa litasaidia maana waumini wanaamini kile wanachoambiwa na viongozi wao wa kiroho.

Kanisa Katoliki hapa nchini litakuwa ndio taasisi pekee ya dini ambayo imeamua kuingilia kinagaubaga suala la kupima virusi vya ukimwi miongoni mwa waumini wake, ukiondoa mpango wa serikali wa kupima wananchi wote uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kupima yeye na mkewe Salma.
Mwananchi
 
Safi! Bado kuhamasisha mipira mambo yaende vizuri zaidi.
 
Na Mwandishi Wetu
KANISA Katoliki nchini limeanzisha kampeni ya kupima virusi vya ukimwi kwa waumini wake ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini alisema, kanisa limeamua kuanzisha mpango huo kwa malengo makuu matatu, kutokomeza ukimwi, kuondoa unyanyapaa na kuhamasisha upimaji afya kabla ya ndoa.


hiyo kauli mbiu waliyonayo eti kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wakishapata data za waathirika na wanaweza kuibadili na kuwa waumini sasa mtumie kondomu kwa jinsi dat zitakavyowastua.


hilo la pili kwamba mpango huu utasaidia kutokomeza ukimmwi sio kweli kwani kama kwa kanisa katoliki tu kufanya hivyo ndio ukimwi utokomee ungekuta hata mpango wa taifa wa kutokomeza ukimwi umeshafanikiwa siku nyingi ,
labda hili la kusaidia kuondoa unyanyapaa maana kaiaka makanisa siku hizi kuna nyanyapaa wa aina nyingi na huu wa watu wwnye vvu ukiwa mmoja wao kwamfano ni ile dhana ya kususia mazishi huu ni unyanyapaa yaani wanatoa hukumu utafikiri miungu. ili la uhamasishaji upimaji kabla ya ndoa ndilo litakalowashangazisha kabisaa maana fasheni ya siku hizi ni mimba kwanza ndio tufikirie ndoa sasa hapo kanisa litaishiwa nguvu kwani na ndoa ngapi tunaziona zinafungwa huku bibi harusi akijifunika kama mwali huku akisikia kichefuchefu na wengine kushindwa hata kusimama kanisani maana wengine utafikiri wanataka kujifungulia kanisa.

hii dunia kweli imebadilika sana

siupingi mpango hou ila najaribu tu kuangalia maanma haohao waumini si ndio raia wa tanzania kama nguvu zote za serekali kupambambana na ukimwi wameshindwa kuzizingatia watakuwa wanafki sana kuzingati hizi za makanisa maana kama ni ingewezekana basi leo hii magereza uwenda wangelikuwako wapagani tu

ni mtizamo wangu tu
 
Back
Top Bottom