Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

Maandiko yote hayo, hakuna sehemu Kanisa limekanusha, linasema tu, "leta ushahidi".

Inanikumbusha Kikwete alipotakiwa kupeleka ushahidi wa kanisa kujihusisha na madawa ya kulevya, alipokamatwa mchungaji. Likakaa kimya.

Kanisa liseme nini kilimuondoa Slaa katika uongozi wa kanisa?

Kanisa katoliki ni kwamba linaongozwa na KANUNI na katiba ya Kanisa. Siyo Kanisa lililoanzishwa kienyeji tu. Na ndio maana ni Kanisa lililoenea DUNIANI na lina uongozi Mkuu Ulimwenguni (PAPA, MAASKOFU, MAKADINARI, MAPADRE, MASISTA, WALEI)

Hivyo ieleweke kuwa ni kanisa lenye utaratibu wake katika kutoa madaraja ya Utumishi wa Kanisa na pia kuna utaratibu wa mtumishi kuacha Utumishi wake. Huwa wanaweka NADHIRI za utumishi wao.

Hivyo kwa Dr. Slaa kutokuendelea na UPADRE ni kutokana na kanuni na katiba za kanisa Katoliki; na ndio maana RAISI wa Baraza la MAASKOFU ametoa kauli hii ya kutaka ushahidi kwa hili.

Kama upo basi uwasilishwe ili hata na mimi niweze kuujua.

WEKENI USHAHIDI HAPA JF TUONE, ACHENI KUKURUPUKA NA KUSIKILIZA MANENO YA VIJIWENI. ni aibu KWA KIONGOZI WA JUU KAMA WASSIRA KUTOA TAMKO KUTOKANA na MANENO YA VIJIWE VYA WANYWA KAHAWA.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Tujikumbushe msemo wa Eleanor Roosevelt:
"Great minds discuss ideas;
Average minds discuss events;
Small minds discuss people." -

Unamweka wapi Waziri wako Mheshimiwa Stephen Wasira?
 
Kauli ya Wasira ni kauli ya serikali, kwani Waziri akitoa kauli maana yake serikali imetoa kauli.

Pia Wassira ndiye waziri anayeshulika na masuala ya mahusiano ikiwemo makanisa na misikiti, hivyo mzee huyu katoa kauli kama waziri wa mahusiano na si mpiga debe wa CCM.

Jamani hawa Magamba sasa wamekosa gia ya kuingilia Arumeru na kuanza kutafuta marumbano yasiyokuwa na tija, kazi kwelikweli!!!!
 
Hii dhambi ya ahadi za uongo na siasa za maji taka zitawatafuna ccm milele.
 
nivigumu sana kuamini kuwa wasira hana ushaidi wowote wa aliyo yazungumza kama ni kweli kuwa kayatunga haya mambo kichwani kwake basi tanzania inakaribia kuingia vitani Mungu nakuomba uitoe tanzania huko
 
Kwa heshima na taadhima namwomba Dr wa Ukweli awaelekeze wanasheria wake wafungue kesi ya kashfa dhidi ya Wassira ambaye kila siku anazungumza maneno ya hovyo. Kanisa limeshakanusha hivyo taarifa na madai yake ni ya uongo hivyo atakiwe aombe radhi kupitia vyombo vya habari la sivyo apelekwe court au angalao baraza la habari ili lizee hili liumbuke. Mod plz naomba uiache thread yangu ili Dr aupate ushauri wangu
 
Tujikumbushe msemo wa Eleanor Roosevelt:
"Great minds discuss ideas;
Average minds discuss events;
Small minds discuss people." -

Unamweka wapi Waziri wako Mheshimiwa Stephen Wasira?

Bila shaka mtaalamu wa uongo na bingwa wa kulala bungeni Mheshimiwa sana Stephen Wasira ana fit kwenye category ya "Smallest minds discuss people."
 
Kwa heshima na taadhima namwomba Dr wa Ukweli awaelekeze wanasheria wake wafungue kesi ya kashfa dhidi ya Wassira ambaye kila siku anazungumza maneno ya hovyo. Kanisa limeshakanusha hivyo taarifa na madai yake ni ya uongo hivyo atakiwe aombe radhi kupitia vyombo vya habari la sivyo apelekwe court au angalao baraza la habari ili lizee hili liumbuke. Mod plz naomba uiache thread yangu ili Dr aupate ushauri wangu

Utawashitaki wangapi mpendwa na una mangapi ya kufanya. Ila amwambie Wasira aombe radhi awaambie wananchi wa Arumeru mashariki na watanzania wote kuwa ilikuwa siasa ya majukwaani (Platform politics) na haina ukweli.
 
“Mimi
nilishazungumza
na
yakaandikwa
kwenye
vyombovya
habari,hii
leosiyo
habari.” huyu kweli hakukosewa kuitwa Wassira.

Rais wa TEC mie naona kanisa katoliki liende mbele zaidi yakumwomba Wassira atoe ushahidi. Kwa namna ya maneno ya wassira mkiishia kuomba ushahidi na msimpeleke mahakamani kwa kushindwa kuthibitisha ataendelea kudanganya watz. kwa kumpeleka mahakamani mtafundisha kwa vitendo kuwa uongo kwa wanasiasa dhidi ya watz haufai na kanisa litabaki salama. Wassira huyuhuyu kaendelea kusema vicent Kiboko nyerere si mtoto wa ukoo huo hali madaraka kashasema ni mdogo wao. Jamii ya kikristo hata huko kwingine makoita wenzenu makfri mnawaruhusije watu kama kuendelea kuabudu kwenye nyumba zetu za ibada?
 
DSN na Wana JF,
Mkuu comments yako haiendani na Mada au hoja ya muhusika, ungesoma mada yote ndio u-comments, labda nimekuelewa vingine, kiujumla upo nje ya mada, labda ufafanue una maana gani.
Nawakilisha

Ok nimeona nikujibu japo kwa great thinker ingekuwa aibu mimi kumjibu kwa kuwa tayari maana yangu iko wazi.Haya mada yako wewe inaangalia muhusika alipoaanguka yani Kanisa kutupiwa madongo na wanasiasa ambayo si ya kweli.Lakini kanisa alikutazama limejikwaa wapi na wanasiasa mpaka likafikiwa kutungiwa uongo dhidi yake na muumini wake aliyepata kuwa Padri kama wito wake na wito huo ulipokwisha kwa sababu zake binafsi ambazo si wengine hatuna sababu ya kuzijua kwa kuwa wito ni mambo binafsi na ni kati ya kanisa na muumini wake binafsi.Sie raia wengine tena watu wazima kuingilia mambo binafsi ya kanisa na muuumini wake ambae kwa hadhi alifika kuwa padri ni sawa na kuingilia ndoa ya mtu na mkewe.Ndoa ikishafungwa wenye uwezo wa kuingilia migongano ya ndoa ni viongozi wa dini na hata wao pia si waamuzi wa mwisho muamuzi kwa ndoa za kikristo ni Mungu.

Hivyo kwa kanisa kutokuangalia aina ya viongozi wa kisiasa na serikali wanaofika kwenye shughuri zake na kuwajibika kama daraja na wananchi,imekuwa ni ugonjwa uliofikisha Kanisa kufika sehemu kutoheshimika kama nyumba muhimu ya kiimani na kuwa wanaotakiwa kukaribia kanisa lazima wawe ni wanasiasa wenye heshimika kwenye jamiii. Matokeo ya kubeba wanasiasa wasio na maadili ndio chanzo cha wao kuona kanisa kama nyumba ya kishikaji na sio nyumba ya Mungu.

Kanisa limekuwa likiwazoeza kuhalika viongozi kwenye shughuri zake kiasi kuwa imekuwa ni sehemu yao ya kuja kutolea madongo kwa wengine,yani membali za kanisa zimekuwa ndio sehemu ya kufikishia madongo kwa wanasiasa wenzao,hivyo basi nao wanasiasa wengine wameona kanisa kama ni washikaji na kumbe kanisa ni Nyumba ya imani muhimu sana ya maisha ya wanadamu.Tizama wamemualika EL Ifakara kafika uko kalusha kijembe kwa Serikali ya Kikwete,pata picha wasaidizi wa Serikali ya kikwete wako njiani kutoa tamko la Lowasa la Kanisa la Roaman Cathoric Ifakara Morogoro,sio tamko la Lowasa jimboni kwake Monduli sharehe za shule za kata Kata alizoshadadia zijengwe enzi yake.Hivi unapata picha gani inayokwenda kwenye baadhi ya viongozi wakuu na wasaidizi wao dhidi ya Lowasa na Kanisa Katoliki Tanzania

Viongozi wenyewe ndio kama hawa wenye matamko haya nimemnukuu Pakajimmy
Aibu kubwa hii kwa ccm!
Kauli zote za kimasaburi!
1.Dr Slaa aliiba fedha za ziara ya Papa.......................... .............................. ...........Wassira
2.Vicent Nyerere si mtoto wa Familia ya Nyerere....................... .............................. .MkaaHapa
3.Mpeni kura Sioi ili mumfute machozi na aweze kulea Familia....................... ...............Mbunge wa Mtera ccm
4.Vicent Nyerere aende kwao Musoma, anatafuta nini huku kwa Wameru na Wamaasai....Olesendeka

Hivyo ukitizama unaona kuwa kwa picha hii,kanisa linapaswa kuita watu waadilifu,kama hawapo liaache kabisa kuita watu wa kada ya kisiasa na utawala.Hivi pata picha umualike mtu kama Joseph sinde ni heshima gani utakuwa umetoa kwa kanisa au Mtu kama Salim Mohamed Salim,kiasi kuwa wanasiasa wasio waadilifu watasikia tu membali za kanisa na hivyo kanisa kuonekana ni sehemu ya heshima na hata wageni wake ni watu waheshima kwenye jamii ambao hawana madoa ya kutiliwa shaka.Wakikosekana wale ambao ni waadilifu Serikalini na wastaafu basi wako hata wataalamu kama Pro Shivji au Pro Baregu.
 
Haya ndo madhara ya kukurupuka toka usingizini na kuanza kulopoka
 
Haya ndo madhara ya kukurupuka toka usingizini na kuanza kulopoka
Usikute kaamshwa tu akaambiwa ni zamu yake kupanda stejini, sasa alipopewa kipaza akiwa stejini hakujua hata kilichokuwa kikiongewa pale ni nini. Akaamua kusema chochote. Aibu kabisa.
 
Usikute kaamshwa tu akaambiwa ni zamu yake kupanda stejini, sasa alipopewa kipaza akiwa stejini hakujua hata kilichokuwa kikiongewa pale ni nini. Akaamua kusema chochote. Aibu kabisa.

Huyu alikuwa anasinzia ilivyo fika zamu yake kwa vile alikuwa anaota kaanza kulopoka ooh Dr. Slaa alikula pesa za ziara ya Papa ndo maana akafukuzwa upadre kumbe jamaa lilikuwa linaota
 
DSN na Wana JF,
Mkuu comments yako haiendani na Mada au hoja ya muhusika, ungesoma mada yote ndio u-comments, labda nimekuelewa vingine, kiujumla upo nje ya mada, labda ufafanue una maana gani.
Nawakilisha

Kama nimemwelewa vyema mtoa hoja amehusisha kauli za viongozi wa kisiasa dhidi ya kanisa na utamaduni uliojengwa na viongozi wa dini wa kuwaalika wanasiasa wachafu kwenda kwenye shughuli zao mbali mbali ambapo hutumia majukwaa ya kanisa kuongea mambo ya kisiasa. Matokeo yake wanasiasa hawa hawaoni soni kuongea mambo ya uongo yanayolichafua kanisa kwenye majukwaa ya kisiasa. Amemalizia kwa kusema anategemea next time Wasira au mwanasiasa mwingine atakuwa mwalikwa rasmi kwenye jukwaa la kanisa kwenye shughuli iliyoandaliwa na kanisa.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Mi Mungu Mungu ameanza kuwafichua waongo, labda Watanzania muendelee kumng'ang'ania tu shetani na siyo hamkuona wala kuambiwa.
 
Back
Top Bottom